Sunday, 20 March 2022

UFUGAJI WA NGURUWE (KISASA)

UFUGAJI WA NGURUWE (KISASA)

Upate wapi Nguruwe wa Kufuga
Nunua nguruwe wa kufuga kutoka kwenye mashamba au watu binafsi wanaoaminika ukizingatia yafuatayo.
• Usizalishe nguruwe wanaotokana na ukoo mmoja yaani ndugu kama kaka na dada. Nunua dume najike toka mahali   tofauti.
• Tumia ushauri wa wataalamu kuchagua Nguruwe bora

Sifa za kuangalia kwa nguruwe bora wa mbegu:
• Nguruwe wa mbegu awe na sifa ya kukua haraka na asiwe na ulemavu wa aina yeyote, na hasa wa miguu kwa dume.
• Mama mzazi wa nguruwe awe na historia ya kuzaa watoto 10 hadi 12 kwa mzao mmoja
• Jike awe na chuchu zaidi ya 12.
• Dume awe na sehemu za kiume yaani korodani na uume unaoonekana sawa sawa. Pia awe na hamu ya kupanda majike.

Mbinu za uzalishaji
Matunzo ya dome la uzalishaji
• Chagua dume la mbegu bora, lisilokuwa na kilema au ugonjwa wowote. Tenganisha dume na majike iii kuepusha kupandwa kusiko na kumbukumbu. Dume la nguruwe halipaswi kunenepa, kwa hiyo usimlishe chakula kingi na mpatie mazoezi ya kutosha asije akawa mvivu
• Nguruwe dume anaanza kupanda majike akiwa na umri wa miezi 4 hadi miezi 9. Dume liruhusiwe kupanda mara moja tu kwa kila juma. Anapofika miezi 10 anaweza kupanda mara mbili hadi mara tatu kwa wiki. Akiwa na mwaka mmoja na zaidi anaweza kupanda kila siku kwa majuma mawili hadi matatu, kisha apumzike kwa majuma mawili. Ni vizuri nguruwe dume mmoja apande majike 15 hadi 20 kwa mwaka.
• Madume madogo yapande majike madogo, dume kubwa likimpanda jike dogo anaweza akamletea maradhi ya mgongo. Ni muhimu kupandisha dume kabla hajala chakula, na asitumiwe mara tu baada ya chakula ili asiwe mvivu.

Utunzaji nguruwe mwenye mimba
• Mimba ya nguruwe huchukuwa miezi mitatu (3) wiki tatu(3) na siku tatu(3) yaani siku 114
• Nguruwe mwenye mimba apewe chakula cha kutosha kiongezwe polepole tokea posho ya kawaida hadi kilo 3 - 3.5 kwa siku.

Matayarisho ya nyumba kabla ya  kuzaa
• Osha banda la kuzalia kwa maji na kuliacha likauke
• Tandika nyasi kavu mara baada ya nyumba kukauka
• Ongeza taa ya chemli au umeme kama uko mikoa yenye baridi kwenye sehemu ya vitoto.
• Tengeneza sehemu ya kuzalia kwa mbao au mabomba

Kumuandaa nguruwe mama kabla ya  kuzaa
• Mpe  dawa ya minyoo siku 10 kabla ya kuzaa
• Mogeshe mama nguruwe kwa sabuni ya mkono na brashi
• Muhamishie katika churnba cha kuzalia siku 7 kabla hajazaa
• Mpunguzie lishe siku 2 kabla  ya kuzaa
• Siku ya kuzaa mpe nguruwe maji ya kunywa na chakula kidogo ili kuepusha kula watoto

Matunzo ya vitoto vya nguruwe
Vitoto vya nguruwe vinyonye maziwa ya mama siku zote hadi wakifikisha siku 56.

Tuesday, 19 March 2019

JUICE YA TANGO

🥒🥒JUICE YA TANGO🥒🥒

🥒Mahitaji:-
Matango 2
juice ya ndimu/limao 1/4 litre
sukari kadiria
Maji 1/2 litre

🥒🥒changanya vitu vyote then usage ukipenda unaweza kuchuja. au ukainywa hivyo hivyo.

🥒🥒juice hii inaondoa kitambi, mafuta mabaya.
inasafisha kibofu, pressure n.k
   enjoy

*AINA ZA NGOZI NA JINSI YA KUZITUNZA*

*1⃣ NGOZI YA KAWAIDA*

Kama ngozi yako si ya mafuta wala si kavu,iko nyororo,vitundu vyake viko kawaida,haina harara wala misukosuko yoyote,basi ngozi yako ni ya kawaida  yaani normal skin

➡Na kwa sababu hiyo bidhaa unazopaswa kutumia ni za kutunza tu ngozi kuipa unyevunyevu na kuzuia isiharibiwe na jua.

*2⃣ NGOZI YA MAFUTA*

Kama ngozi yako ina ng'aa kila wakati,unapata chunusi,madoa,matundu yake ni makubwa yanaonekana wewe ngozi yako ni ya Mafuta   yaani oily skin

Bidhaa unazopaswa kutumia ni zile za kubalance mafuta,kuzuia chunusi,kuondoa madoa lakini ni lazima bidhaa hizi ziwe hazikukaushi mafuta

Si kweli kwamba ukiwa na uso wa mafuta ni vibaya na kwamba mafuta hayatakiwa usoni mafuta ni muhimu lakini yana kiasi chake

*3⃣ NGOZI KAVU*

Huwezi toka bila kupaka mafuta,unapauka yaniuso unakuwa na mabaka mabaka,ngozi inafifia,haing'ai basi ukiona hivi ujue ngozi yako ni Kavu yaani Dry skin

Mtu wa ngozi kavu anahitaji bidhaa za kurudishia ngozi yake unyevunyevu

Lakini muhimu sana sana kuilinda isiharibiwe na jua kwa kutumia cream maalum za kuzuia ngozi isiungue.

*4 NGOZI NYETI*

Kama ukipaka kitu chochote usoni unapata irritation,au ngozi yako huwa inawasha,wakati mwingine unaona wekundu kama kuungua basi wewe ngozi yako ni sensitive

Mtu mwenye ngozi hii anapaswa kuwa makini sana na aina ya bidhaa anazotumia

Usipende kubadili badili bidhaa, epuka kutumia bidhaa zenye chemikali na ni vizuri ukapata ushauri kwa mtaalam wa maswala ya ngozi kwanza.

*5 NGOZI MCHANGANYIKO*

Kuna watu ambao baadhi tu ya sehemu usoni ndipo anakuwa na mafuta,sehemu zingine mkavu,anapata pia chunusi japo si nyingi na ni sehemu zile zenye mafuta.

Tunaweza sema sehemu zile zenye mafuta uso unakuwa na tabia za ngozi ya mafuta wakati seheme zenye ukavu zinakuwa na tabia za ngozi kavu

Mtu huyu ngozi yake ni mchanganyiko au Combination Skin

NJIA ASILI ZA KUONDOA WEUSI KWAPANI NA MAPAJANI

➿➿➿➿➿➿➿➿➿➿



*🍇Njia asili za kuondoa weusi kwapani na mapajani🍇*

🍇Msuguano kati ya sehemu mbili kwa muda mrefu, unene kupita kiasi, matumizi ya deodorant, spray, matumizi ya dawa za kunyolea, matumizi ya vipodozi vikali na ugonjwa wa kisukari ni baadhi ya visababishi kwa maeneo kadhaa ya mwili kupata weusi hasa katika mapaja na kwapa.

🍇hii ni kwa wanaume na wanawake kwasababu matumizi ya vitu hivyo huchangia seli kufa kwa kiasi kikubwa na kutengeneza weusi.

🍇Ifahamike kwamba weusi mapajani au makwapani sio ugonjwa bali ni mabadiliko tu ya ngozi ambayo huwapata wengi na kuwafanya wasiwe na raha pindi wawapo na waume zao

🍇Zifuatazo ni baadhi ya njia za asili ambazo mhanga wa tatizo hili anaweza kuzitumia kuondokana nalo ambalo limekuwa changamoto kwa watu wengi

🍇2.Njia nyingine ni matumizi ya mafuta ya nazi, mafuta haya ni tib anzuri sana kutokana na uwepo wa vitamini E yansaidia kusafisha na Kung’arisha ngozi.

🍇Unachotakiwa kufanya ni kupaa mafuta hayo sehemu ya mwili iliyoathirikana weusi kwa muda wa dakika 10 hadi 20 kisha osha eneo hili kwa maji ya vuguvugu, fanya hivyo kila siku mpaka utapoona mabadiliko.

🍇3.Matumizi ya Tango pia ni muhimu kwa kusaidia kuondoa weusi sehemu za mapajani na kwapani.

🍇Unachotakiwa kufanya, kata vipande kadhaa vya tango jipake kwapani na mapajani au lisage kisha paka ukishapaka kaa kwa muda wa dakika 10 hadi 20.

🍇4.Majani ya Aloevera, chukua utomvu wa jani la Aloevera, Paka kwenye sehemu yenye weusi na kisha acha ule utomvu kwa muda takribani nusu nasaa kisha osha na maji ya uvugu vugu,  Fanya hivi mara moja hadi mbili kwa siku ili kuweza kupata matokeo haraka.

🍇5.Viazi ulaya/mbatata

menya viazi kata vipande jipake makwapani yale maji yake yakiingia kwenye ngozi yanatoa rangi nyeusi au unaweza kuponda kikiwa kibichi na kujipaka kwa dk 10-20 utanawa utafanya hivyo mara 2 kwa siku mpaka weusi utakapoisha

🍇6.Sukari -chukua brown sugar changanya na olive oil paka  badaa ya mda osha

🍇7.Baking soda-inasaidia kutoa dead cells kwa urahisi .

changanya baking soda na maji iwe nzito nzito paka kwapani acha kwa dk 10 osha na jikaushe fanya hivyo mar 2-3 kwa wiki ,endelea na zoezi mpaka utakaopona umeridhika na mabadiliko

🍇Zoezi hili linaweza chukua mda mchache ukaona mabadiliko makubwa au ikachukua mda mrefu kuona  mabadiliko inategemea kila mtu na ngozi yake .

🍇Zingatia kutumia dodoki la kuogea usugulie sehemu hizo husika na hakikisha hukai na nywele ndefu.

🍇Tumia hand shaver isiwe kiwembe, na iwapo umetumia njia hizi kwa miezi 1-2 na hakuna mabadiliko mwone daktari.

🍇Kuna baadhi ya creams au deudorants nazo zinasaidia kutoa weusi.

*Tutaishia hapa, ni matumaini yangu mmenufaika*

➿➿➿➿➿➿➿➿➿➿

Monday, 18 March 2019

MBAAZI ZA NAZI

MBAAZI ZA NAZI

Mbaazi kavu nusu kg
Kitunguu maji 1 kikubwa
Tomato fresh 1 kubwa au 2 za kiasi
Pilipili boga/cupsicum kiasi
Bizari nyembamb/cumin powder 1 tablespoon
Pilipili manga /black pepper 1 teaspoon
Kitunguu saum/garlic 1 tablespoon
Tangawizi mbichi 1 teaspoon
Chumvi
Vegetable maggi /kidonge cha supu 1 (sio lazima)
Tui la maji vikombe 5 (3 tui jepesi na 2 tui zito )
Bizari ya mchuzi/tumeric kiasi
Chemsha mbaazi kwa maji mpaka ziwive, zikauke maji au zibaki na maji kidogo sana, kata kata kitungu, tomato, pilipili boga ndogo ndogo na uweke kwenye sufuria ya mbaazi, add na vitu vyote vilobaki isipokua tui/nazi,
tia nazi/tui jepesi na uwache zichemke, tui jepesi litaivisha vitu vyote, vikishawiva na tui limekaribia kukauka, tia tui zito, funika wacha zichemke mpaka iwe size unayotaka, angalia chumvi na spices kama ziko epua na ENJOY kwa mikate maandazi au wali, zangu mm mekula na 

Bamia robo kg
Kitunguu maji 1 kikubwa
Kitunguu saum kijiko 1 cha chakula
Tangawizi mbichi kijiko 1 cha chai
Chumvi kiasi
Bizari nyembamba /cumin powder 1 tsp
Mafuta ya kupikia 3 tbsp
Pilipili manga kiasi
Tui/Nazi ya maji kikombe 1

Kosha bamia zikate kate ndogo ndogo, kata kata Kitunguu maji, changanya na bamia zisage, kama unatumia blender tia na tui la maji  nusu kikombe, saga pamoja mpaka zinakua laini kiasi, zitoe

Weka sufuria kwenye moto, tia mafuta ya kupikia, tia kitunguu saum, tangawizi, bizari nyembamba na pilipili manga, wacha zipate moto kidogo, tia ile bamia uliyoisaga na kitunguu, ipike kwa dakika 5 malizia tui nusu kikombe tia chumvi , wacha lichemke mpaka iwive pamoja na kitunguu,

Kama uliposaga ulitia tui ni sawa, kama uliposaga hukutia tui , vile linachemka litie tui lote kikombe 1,  wacha lichemke mpaka liwe zito na kila kitu kiwe kimewiva, unaweza kuweka pilipili ya kuwasha ukipenda.

PILAU YA SAUCE YA SOYA NA MBOGA

PILAU YA SAUCE YA SOYA NA MBOGA

VIPIMO

Kuku (mkate mkate vipande) 1

Mchele wa Basmati (rowanisha) magi 3

Mdalasini  mchi 1                     

Vitunguu maji (vilivyokatwa vyembamba) 6

Mchanganyiko wa mboga za barafu (karoti, mahindi, njegere) - Magi 1

Kabichi (iliyokatwa katwa nyembamba) magi 1

Pilipili mbichi (iliyosagwa) 3

Pilipili boga iliyokatwa vipande vidogo vidogo 1

Pilipili manga kijiko cha chakula 1

Chumvi kijiko cha chakula 1

Sosi ya soya (soy sauce) vijiko vya chakula 5

Kotmiri iliyokatwa katwa magi 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa vijiko vya chakula 2

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1.  Tia mafuta ndani ya karai. Yakipata moto kiasi, mimina vitunguu maji na mdalasini 1 mzima kaanga. Itachukua muda kidogo. Kaanga mpaka viwe rangi ya hudhurungi (brown). Viepue na uweke kando.

2.  Ndani ya sufuria kubwa, mimina kuku, chumvi, thomu na tangawizi, sosi ya soya, pilipili manga, pilipili mbichi, chemsha mpaka kuku awive na maji yakauke.

3.  Changanya vitunguu  ulivyokaanga, kabichi, pilipili, mboga, kotmiri, mchanganyiko wa mboga za barafu na weka kwa muda wa dakika tano au kumi. Tia na mafuta kidogo uliyokaangia vitunguu .

4.  Chemsha mchele na chumvi uwive kama kawaida ya kupika wali wa kuchuja. Ukishauchuja umwagie katika masala ya kuku.

5.  Nyunyizia mafuta kidogo uliokaangia vitunguu.

6.  Weka moto mdogo mpaka wali ukishawiva.  Uchanganye ukiwa tayari kwa kuliwa.

KIDOKEZO:

Unaweza kuupika wali huo ndani ya jiko, yaani badala ya kutia masala kwenye sufuria ukayatia katika bakuli au treya ya jiko (oven), kisha ukamwagia wali uliouchuja humo na kuupika kaitka moto wa 400-450 Deg kwa muda wa dakika 15-20.

Enjoy!

COCONUT HALWA / HALUA YA NAZI

COCONUT HALWA / HALUA YA NAZI :

Mahitaji:

Tui zito –kikombe  1+1/4
Maziwa – 2/3 kikombe
Sukari – 2/3 kikombe
Nazi ilokunwa  – 1/4 kikombe
Siagi isokuwa na chumvi – vjk 2 vya kula
Lozi na Pistachios – kiganja kwajili ya kupambia

Maelekezo:

1. Bandika sufuria jikoni moto wa kiasi.
2. Tia tui zito na maziwa.
3. Acha ichemke.
4. Tia sukari na nazi ilokunwa.
5. Koroga hadi ishikane.
6. Tia siagi, koroga kisha epua.
7. Tandaza kwenye sahani ilopakwa mafuta ipate kupoa.
8. Mwagilia lozi na pistachios ukipenda.
9. Kabla haijapoa kabisa kata vipande.
10. Andaa.

Thursday, 14 March 2019

UTENGENEZAJI WA MISHUMAA YA KUUA MBU

*UTENGENEZAJI WA MISHUMAA YA KUUA MBU*

*MALIGHAFI*
1.PARAFFIN WAX
2.STERINE
3.BORIC ASID
4.MOULD(MAUMBO)
5.UZI (UTAMBI)
6.RANGI KAMA UKIPENDA
7.JIKO
8.SUFURIA

*MAANDALIZI*
andaa maumbo ya mshumaa kwa Jinsi unavopenda unaweza kutumia bati

andaa utambi kwa kuchukua boric asid vijiko vitano vya chakula changanya Na maji vijiko vinne vya chakula ,koroga kwa muda wa dakika tano, KISHA toa Na ANDIKA ili ukauke,sababu ya kufanya hivi ili utambi usiishe haraka wala kutoa moshi. Na hii ndio Kazi kubwa ya boric asid

*UANDAAJI WA MSHUMAA*

baadavya kuwa umeandaa maumbo Yako ya mshumaa chukua utambi wako Na uweke katikati ya mould Yako KISHA funga utambi wako juu ya chombo chako kwa kushikiza Na kijiti .kijiti kitakusaidia ili utambi usikae pembeni

Washa jiko Lako Na weka sufuria Yako jikoni chukua paraffin wax kilo moja ,sterine vijiko vinne,rangi kijiko kimoja cha chai, perfume kama ukipenda kijiko kimoja cha chai

wakati mchanganyiko wako unayeyuka koroga taratibu mpaka uchanganyike vizuri

Epua mchanganyiko wako Na anza kuweka kwenye maumbo Yako uliyoandaa kwa kuweka utambi ndani yake

weka sehemu ya kivuli ili mshumaa wako upate kuganda kwa urahisi ukisha ganda utoe taratibu kutoka katika hayo maumbo yake *BAADA YA HAPO MSHUMAA UTAKUWA TAYARI KWA MAUZO NA MATUMIZI YA NYUMBANI*

*NB:* SIMPRONELLA/CITRONELLA hii ni perfume Na pia ni dawa ya kuua mbu ko kama ukipenda mshumaa wa kuua mbu basi sehemu ya kuweka perfume weka aina hii

Saturday, 9 March 2019

UJASIRIAMALI* YATAKAYOKUWEZESHA KUJIAJIRI MWENYEWE NA KUTIMIZA NDOTO ZAKO.                                              *Masomo 80

*UJASIRIAMALI* YATAKAYOKUWEZESHA KUJIAJIRI MWENYEWE NA KUTIMIZA NDOTO ZAKO.
                                             *Masomo 80
1:SABUNI YA MAJI NZITO(AINA NNE)
2:SABUNI YA MKAA- CHUNUSI.
3:SABUNI YA MCHELE - USOFT
4:SABUNI YA NYANYA.
5:SABUNI YA MAZIWA & ASALI.
6:SABUNI YA KIAZI- MAKOVU.
7: *JIKI.*
8:SHAMPOO.
9:LEMON SOAP.
10:MANJANO SOAP.
11:MISHUMAA/CANDLES.
12: *CHAKI/CHALKS.*
13:SABUNI YA MCHE/LAUNDRY BAR SOAP.
14: *SABUNI YA MAGADI.*
15:SABUNI YA MLONGE.
16:SABUNI YA TANGO.
17:SABUNI YA ALOVERA.
18:SABUNI YA MAJIVU.
19:SABUNI YA UKWAJU
20:SABUNI YA PAPAI.
21:SABUNI YA SULFUR/ NGOZI YA MAFUTA NA CHUNUSI.
22:TILES) SINK CLEANER.
23:SABUNI YA MWAROBAINI.
24:SABUNI YA KUNAWIA MIKONO.
25:MAZULIA/CARPETS.
26:SHAMPOO YA ALOVERA.
27:SHAMPOO YA TANGO.
28:SABUNI YA TANGAWIZI.
29:SABUNI YA  MAWESE NA ASALI.
30:SABUNI YA  CHUNGWA.
31:MITO/PILLOWS.
32:BATIKI TIE & DIE  TONE LA MAJI.
33:BATIKI YA MUHURI.
34:MASHUKA/BEDSHEETS.
35:BATIKI TIE & DIE  CRANCKE. PARTERN.
36:BATIKI YA CHAPA{printing}
37:BATIKI YA KUCHUBUA{Bleach.}
38: *VIATU*
39:BATIKI PUBBLE PRISM.
40:BATIKI TIE & DIE NYOTA.
41:BATIKI TIE & DIE UPINDE  WA MVUA.
42:BATIKI TIE & DIE  DOUBLE SPYRAL.
43:BATIKI ZA MSHUMAA.
44: *MIKOBA/HANDBAGS*
45:MAZIWA YA SOYA.
46:SOYA MASALA.
47:SIAGI YA KARANGA.
48:MAZULIA/CARPETS.
49:CRIPS ZA VIAZI.
50:JUISI YA DUKANI.
51:KARANGA ZA MAYAI.
52:TOMATO SAUCE.
53:CHILI SAUCE.
54:UBUYU WA VIMTO.
55:UFUTA
56:KASHATA ZA KARANGA.
57:ICE CREAM ZA UBUYU.
58:MKAA.
59:UNGA WA LISHE.
60:VIBANIO VYA MAPAZIA.                                                                                                                                                 61: *KEKI NA UPAMBAJI WAKE.*
62:MAFUTA YA KAROTI.
62:AIR FRESHENER.
63:DAWA YA KUUA WADUDU.
64:ICE CREAM YA MAZIWA.
65:LEMON ICE CREAM.
66:BISKUTI.
67:FUDGE AINA ZOTE.
68: *UPAMBAJI WAKUMBI ZA SHEREHE.*
69: MAFUTA YA MNYONYO{Castor oil}
70: *ANTI AGING LOTION*
71:HAND WASHING GEL.
72:MAFUTA YA NAZI.
MAFUTA YA MGANDO.
73:MAFUTA YA NGOZI{MAKUNYANZI}
74:JUISI ZA MATUNDA.
75:SABUNI YA
78: *LEMON OIL.*
79:ALOE VERA GEL.
80:SABUNI YA UNGA

Tuesday, 5 March 2019

JINSI YA KUTENGENEZA MASK KWA AJILI YA NGOZI ZA AINA ZOTE

*JINSI YA KUTENGENEZA MASK KWA AJILI YA NGOZI ZA AINA ZOTE*

*NGOZI YENYE CHUNUSI*

*Mahitaji*

🍇Kungumanga🌰
🍇Asali🍯
🍇Maziwa 🥛

*Jinsi ya kufanya*

Changanya mahitaji yote kwenye bakuli safi mpaka uhakikishe umepata mchanganyiko mzuri

Safisha uso kisha paka na ukae nayo kwa muda wa nusu saa kisha osha vizuri na maji ya uvugu kisha malizia na maji baridi

Futa na taulo laini uso wako kisha jipe unyevu kama kawaida

*NGOZI YA MAFUTA*

*Mahitaji*

🍇Unga wa ngano🍚
🍇Mtindi 🥛
🍇Manjano

*Jinsi ya kufanya*

Changanya mahitaji yote mpaka uhakikishe imechanganyika vizuri

Safisha uso kisha paka paste yako na uiache kwa muda wa nusu saa kisha osha kwa maji ya uvugu ukifuatisha na maji baridi

Futa uso kwa taulo safi kisha paka moisturizer kama kawaida

*NGOZI YENYE MIKUNJO*

*Mahitaji*

🍇Aloe vera gel🌿
🍇Asali 🍯
🍇Mafuta ya nazi

*JINSI YA KUFANYA*

Changanya mahitaji yote mpaka uhakikishe imechanganyika vizuri

Safisha uso kisha paka paste yako na uiache kwa muda wa nusu saa kisha osha kwa maji ya uvugu ukifuatisha na maji baridi

Futa uso kwa taulo safi kisha paka moisturizer kama kawaida

*NGOZI KAVU*

*Mahitaji*

🍇Ndizi mbivu🍌
🍇Asali🍯

*JINSI YA KUFANYA*

Changanya mahitaji yote mpaka uhakikishe imechanganyika vizuri

Safisha uso kisha paka paste yako na uiache kwa muda wa nusu saa kisha osha kwa maji ya uvugu ukifuatisha na maji baridi

Futa uso kwa taulo safi kisha paka moisturizer kama kawaida

JINSI YA KUTENGENEZA COFFEE SCRUB

*JINSI YA KUTENGENEZA COFFEE SCRUB*

*Mahitaji*

🍇¼ kikombe ya kahawa iliyosagwa

🍇½ kikombe ya mafuta ya nazi/olive oil extra virgin

🍇2 Tbs ya mdalasini wa unga au manjano

*JINSI YA KUFANYA*

Changanya mahitaji yote kwenye bakuli safi.

Osha mwili wako kwanza ili kuondoa uchafu kwenye ngozi kisha jikaushe na taulo

Sugua ukitumia scrub yako kwa kufuata mduara

Iache kwa dakika 15 kisha osha vizuri

Kama una sensitive skin hakikisha unasugua taratibu sana

Coffe ni kama exfoliator ambayo inasaidia kuondoa dead cells na itaiacha ngozi yako ikiwa laini ya kupendeza...

Mafuta ya nazi /olive yataipa unyevu ngozi yako na kuiacha ikiwa na afya na yenye mng'ao

Manjano na mdalasini vitaondoa bacteria wanaosababisha chunusi na kuiacha ngozi yako na ikipendeza zaid

JINSI YA KUTENGENEZA LOTION ASILIA KWA NGOZI NYORORO YENYE MNG'AO (NATURAL)

*JINSI YA KUTENGENEZA LOTION ASILIA KWA NGOZI NYORORO YENYE MNG'AO  (NATURAL)*

*Chagua moja kati ya lotion zifuatazo*

*Mahitaji*

🍇Vitamin c powder/unga1 Tbs

🍇Vitamin e Capsule/oil matone 5

🍇Rose water 1Tbs🌹

🍇Glycerin 1 Tsp

🍇Shea butter au Vaseline lotion/Lotion yoyote uipendayo 100ml

*Jinsi ya kufanya*

Tia rose water kwenye bakuli safi kisha tia kijiko kimoja cha unga wa vitamin C

Changanya vizuri na ukoroge kwa muda wa dakika 5 mpk vitamin c iyeyuke kabisa kisha ongezea glycerin na vitamin e na uchanganye vizuri

Tia lotion yako ya vaseline ujazo wa ml 100 ama shea butter ama cream yoyote uipendayo mwenyewe kisha changanya vizuri hadi ichanganyike

Weka kwenye chupa safi tayari kwa matumizi

Hii itafanya ngozi yako kua laini na kuondoa ukavu wa ngozi pamoja na kuiacha ikipendeza zaidi na zaidi

Unaweza kupaka kwenye mwili hata usoni na ni salama kabisa haina sumu

Lotion ya pili

*Mahitaji*

🍇Mafuta ya nazi
🍇Aloe Vera gel
🍇Rose water
🍇Glycerin
🍇Vitamin e Capsule/oil

*Jinsi ya kufanya*

Weka kwenye bakuli safi kijiko kimoja cha chakula cha aloe vera gel (ya dukani iwe 100% natural)

Ongeza kijiko kimoja cha chakula cha mafuta ya nazi pamoja na glycerin na rose water kisha ongezea na vitamin e kama ngozi yako ya mafuta tumia capsule kama kavu unaweza kutumia vitamin e oil

Changanya vizuri mpaka ichanganyike na uone imekua na rangi ya kupendeza na ipo laini kisha hifadhi kwenye kichupa safi tayari kwa matumizi

DAWA YA KUKUZA NA KUNYOOSHA NYWELE,KUONDOA WEUSI MAKAPANI,VIDOLENI,MAGOTI

Utengenezaji  dawa ya kukuza nywele/kuondoa michirizi kwapani,vidole,magoti,kunyoosha nywele

      Mahitaji

1*mafuta ya mzaituni

2*mdalasini ya unga

3*asali

Uandaaji

Andaa sefuria jikon na acha ipate moto

Baada ya kupata moto weka mafuta ya mzaituni nusu Lita acha yachemke (kupata moto )

Baada ya kupata moto weka mdalasini kijae kikombe kimoja cha chupa ya chai acha jikon ukiwa unakoroga

Koroga hadi kuona inaacha kuchemka yani kupata moto sana maana haichemki kama mboga😁

Acha usikoroge na kusubiri hadi ibadirike rangi na kua kahawia nyeusi ipua na subiri kupoa

Baada ya kupoa weka asali vijiko 10 vya chakula kisha koroga tena

Baada ya kuweka asali na kukoroga mafuta yapo tayar kwa matumizi

Matumizi

Paka kichwa kuanzia kwenye ngoz ya kichwa (utosi) hadi juu ya nywele

Nb isikae kichwani zaidi ya robo Saa (dakika 15 )

🍉🍅na kuondoa weusi makwapani,vidoleni na magotini🍒
changanya mchuzi wa limao au ndimu ,na asali au sukari alafu jisugue sehemu husika kila siku kabla ya kuoga.baada ya kujisugua kaa dkk 10 then nawa au oga kama kawaida

♥DAWA YA MICHILIZI
🌷🌷@umbo_la_asili
Mahitaji⤵
🔹limao 1
🔹olive oil vijiko 5
🔹kahawa vijiko 4
🔹sukari vijiko 2

♥♥NJIA♥♥♥
Weka kahawa ktk bakuri ongeza mafuta ya olive oil  vijiko 5 pamoja na sukari vijiko 2
Koroga ongeza na limao ktk mchanganyiko
Paka sehemu za michirizi km unasugua.fanya hiv kwa mda km dkk mbili.acha kusugua kaa kidogo km dkk 20
Baada ya hapo kaoge kisha paka mafuta ya nazi hasa mafuta ya naz ya minara.🌷🌷🌷🌷🌷♥♥♥♥♥♥♥
@umbo_la_asili

KUNYONYOKA KWA  NYWELE
wale walio na tatizo la kunyonyoka kwa nywele,wanaweza kupaka kichwani uji wenye mchanganyiko wa mafuta ya mzeituni yaani olive oil,asali kijiko kimoja cha chakula,mdalsini kijiko kimoja cha chai kabla ya kuoga na kuuacha kichwani kwa muda wa dk 15 na kisha kuosha kichwa.hii husaidia kurudisha nywele

Thursday, 28 February 2019

JINSI YA KUTENGENEZA PIPI TOFI (TOFFEE)

*JINSI YA KUTENGENEZA PIPI TOFI (TOFFEE)*

1/2 kikombe unsalted butter- siagi (ambayo haina chumvi)
1 kikombe sukari
1/2 kijiko cha chai Chumvi
1/4 Kikombe maji au maziwa
1 kijiko cha chakula vanilla au radha yoyote ile
100g Cooking Chocolate (sio lazima)

Zabibu zilizokaushwa, vipande vya Lozi, korosho au karanga

Namna:

Paka siagi sinia yako weka pembeni.
Ktk sufuri weka sukari, siagi, chumvi na maji-maziwa. Chemsha kwa moto mdogo kwa dakika 8 (angalia usiunguze), huku unakoroga utaona inaaza kubadilika rangi kuwa kahawia. Hakikisha mchanganyiko wako unaaza kuwa mzito sana. Weka lozi au karanga ktk mchanganyiko wako koroga.

Yeyusha cooking chocolate kwa mvuke au microwave weka pembeni.

Mwagia tofi ktk sinia ulikwisha tayarisha, tandaza acha ipoe kidogo. Halafu mwagia ila cooking chocolate juu ya tofi acha ipoa kiasi, kata tofi ktk vipande. Tayari kuliwa.

Kikombe kilichotumika ni ´measuring cups´.

Wednesday, 27 February 2019

DAWA YA KUONDOA MICHIRIZI YA UNENE AU MISTARI YA UZAZI

Dawa ya kuondoa michirizi ya unene au mistari ya uzazi

Mahitaji

1*magadi soda

2*limao

   Matumizi

Anda bakuli la kawaida kisha weka magadi soda vijiko 2

Baada ya hapo kata limao utoe vipande 2 kisha chukua kipande kimoja chovya katika bakuli la magadi soda na usugue sehem ya mistari

Tumia hadi kupata matokeo

Monday, 25 February 2019

WHAT IS YOUR REASONS TO LIVE??.

WHAT IS YOUR REASONS TO LIVE??.

"Your reasons to live, gives you the reasons to die".......Katika uumbaji wa Mungu kila kitu na kila mtu alimuumba kwa sababu maalum.....Ile sababu ambayo ilimfanya Mungu akuumbe ndiyo inatakiwa iwe sababu yako ya kukufanya uishi na iwe ndo sababu ya kukufanya uwe tayari kufa kwa ajili ya hiyo.

Miongoni mwa kitu kitakachkokufanya ufanikiwe kirahisi kwenye maisha yako ni kuitafuta sababu ya wewe kuishi na ambayo utakuwa tayari kufa kwa ajili ya hiyo pia.

Kila mtu aliyefanikiwa kuipata sababu muhimu ya kumfanya aendelee kuishi na ambayo alikuwa tayari kufa kwa ajili ya hiyo basi alifanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu sana na watu wa aina hii waliacha alama kubwa duniani ambazo zimefanya ulimwengu usiwasahau!!

Martin Luther King Jr aliwahi kusema “If you haven’t found something worth dying for, you aren’t fit to be living.”.....Alimaanisha kuwa "Kama hujapata sababu ambayo uko tayari kufa kwa ajili ya hiyo basi hustahili kuendelea kuishi".

Martin Luther King Jr alishafariki miaka mingi iliyopita lakini bado anaishi kutokana na mambo aliyoyafanya enzi za uhai wake, kutokana na uthamani wa maisha aliyoishi, kutokana na sababu iliyokuwa inamfanya awe tayari kufa. JE SABABU YAKO YA KUISHI NI NINI?? NA JE UPO TAYARI KUFA KWA AJILI YA HIYO??

Inatakiwa ifike hatua uishi ukiwa na STRONG REASON ya kuishi kiasi kwamba hata kama Mungu akiamua kupunguza watu wanaoishi maisha ya ilimradi akiisikia Sababu yako awe na kila sababu za kukuacha uendelee kuishi!! JE, MUNGU AKIAMUA KUWAONDOA WATU WASIO NA SABABU MUHIMU ZA KUISHI, WEWE UTAKUWA KUNDI GANI??

Fid Q kwenye moja kati ya nyimbo zake aliwahi kusema "JE, UNAISHI ILI ULE AU UNAKULA ILI UISHI??".

Kama Unaishi Ili ule, uwe na Magari au na Majumba au tajiri BASI NAKUPA POLE SANA NA NAKUONEA HURUMA SANA KWANI HUJAJUA NI KWA KIASI GANI UNAMHUZUNISHA ALIYEKUUMBA!!

Na kama UNAKULA ILI UISHI, Basi kuna Sentensi mbele unatakiwa kuimalizia " UISHI ILI UFANYE NINI??".....Kama jibu lako linaishia kwenye "KULA ILI UISHI TU" basi hauna utofauti na yule mtu wa kwanza ambaye ANAISHI ILI ALE!!

Ungana na kundi la watu ambao wamejitoa kuifanya dunia kuwa sehemu nzuri kuishi, Ishi kufanya kile Mungu alikuumba kufanya, Ishi kuweka thamani kwenye maisha ya wengine.

Dr. Myles Munroe alikuwa anapenda kusema "DON'T JUST MAKE A LIVING, BUT LIVE TO MAKE A DIFFERENCE"

Ukifika hatua ukapata kitu ambacho utakuwa tayari kufa kwa ajili ya hicho basi jua kuwa itakuwa ndo mwanzo wako wa kufanya mambo ya ajabu duniani na utafanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu and you will be UNSTOPPABLE!!

JE UPO TAYARI KUFA KWA AJILI YA NDOTO YAKO?? Kama Jibu ni HAPANA basi jua kuwa HAUNA PASSION NA NDOTO YAKO NA JUA KUWA HILO ENEO SIYO ENEO LAKO SAHIHI.
"Ndoto ya kweli ni ile ambayo upo tayari kufa kwa ajili ya hiyo".......Maranyingi huwaga nasema " Ili ufanikiwe ni lazima ukubali kuingia kwenye mapambano ya kufa na kupona" Sasa huwezi kufanya mapambano ya kufa na kupona kwenye ndoto yako kama haupo TAYARI KUFA KWA AJILI YA NDOTO YAKO!!

"FIND YOUR REASON TO DIE THAT WILL GIVE YOU THE REASON TO LIVE"
Martin Luther King Jr alipata sababu ya kupinga ubaguzi wa rangi   ambayo alikuwa tayari kufa kwa ajili ya hiyo,.... Mwalimu Julius Nyerere alipinga ukoloni na alikuwa tayari kufa kwa ajili ya kupambana dhidi ya ukoloni.....Nelson Mandela alipingana na ukoloni na ubaguzi kiasi kwamba ilimpelekea kukaa jera miaka 27 alikataa kila ofa ya cheo, pesa, magari na kila kitu cha kumfanya ayafurahie maisha, alikubali kuendelea kuteseka kwenye chumba ambacho kilikuwa kifupi kuliko yeye ili tu asimamie Kusudi lake na sababu yake ya kuishi......Mahatma Gandhi aliwaambia Wakoloni wakizungu kuwa hatakula chakula wala kunywa maji mpaka afe kama hawatawaachia wananchi wake, WHAT A SPIRIT??

Unaikumbuka Sababu iliyompleta YESU duniani?? Na Je, Unakumbuka Sababu iliyomfanya auawe??
TAFUTA SABABU YAKO YA KUISHI!!

Live Your Dream!!

HAKIKISHA MAPAMBANO YAKO YANAENDANA NA NDOTO YAKO

HAKIKISHA MAPAMBANO YAKO YANAENDANA NA NDOTO YAKO.

Kuna msemo mmoja unasema "The big the dream, the higher the grinding"...... Yaani "Ndoto inapokuwa kubwa basi lazima mapambano yawe makubwa".

Ili malengo yaitwe malengo na ndoto iitwe ndoto ni lazima sifa ya kwanza kabisa malengo au ndoto iwe ni kubwa kuliko level uliyopo sasa na kiwe ni kitu ambacho kita ku-challenge.....Sasa kitu unachotakiwa kukijua ni kuwa kadri unavokuwa na ndoto kubwa au malengo makubwa ndivyo ambavyo mapambano yako ni lazima yawe makubwa zaidi.....Kwa mfano: Mwamafunzi kwenye malengo ya kupata Division One, hawezi kupiga msuli sawa na mwanafunzi mwenye malengo ya kupata Division Three, Mwenye Malengo ya Division One lazima akubali kuumia zaidi ya mwenye malengo ya Division Three....AU, Mtu mwenye ndoto za kuwa Rais ni lazima akubali kuumia sana na zaidi kuliko kijana mwenye malengo ya kuwa Diwani.

Sasa Miongoni mwa swali unalotakiwa kujiuliza mara kwa mara ni hili "JE, MAPAMBANO YANGU YANAENDANA NA NDOTO AU MALENGO YANGU??"........Kama Jibu ni YES basi keep grinding, yaani endelea na Mapambano kwa style hiyohiyo bila kupunguza.....Lakini kama jibu ni NO basi unatakiwa kuongeza Mapambano.

Sasa ili kijiweka kwenye level ya Mapambano kuendana na ndoto au malengo yako basi ni lazima uzingatie na uhakikishe unajifanyia self assessment kwenye maeneo yafuatayo:

Je, Unautumia muda wako sawa na ukubwa wa ndoto yako??

Je, Discipline yako na Commitment na Bidii yako inaendana na ukubwa wa ndoto yako??

Je, Tabia zako za kila zinaendana na ukubwa wa ndoto yako??

Je, Marafiki Unaoambatana wanaendana na ukubwa wa ndoto yako??

Je, kiwango cha Maarifa Uliyonayo sasa yanaendana na ukubwa na ndoto yako na Je, speed yako ya kutafuta Maarifa yakukupeleka kwenye ndoto yako inaendana na ukubwa wa ndoto yako??

Je, Maamuzi unayoyafanya kila siku kwenye maisha yako yanakupeleka kwenye ndoto yako kubwa??

Kimsingi ni kuwa kama una ndoto kubwa lazima na standards zako ziwe kubwa kwenye kila eneo......Eneo muhimu kabisa kupima kiwango cha mapambano yako ni kujiangalia kiwango cha discipline, commitments, hard working yako,marafiki unaoambatana nao, kiwango cha Maarifa Uliyonayo na mambo mengine mengi, kwenye maeneo haya ni lazima uhakikishe standards zako zinakuwa kubwa kama ndoto yako ni kubwa.....Lakini pia ni muhimu ukajua kuwa haya mambo yote kama vile Discipline, Hard working, kiwango cha Maarifa, Marafiki vimejikita kwenye namna unavotumia muda wako...... Kama unatumia muda mwingi Kufanya mambo ambayo hayahusiani na ndoto yako basi jua kuwa mapambano yako hayaendani na ndoto yako, hapa kama kweli upo serious na ndoto yako basi ni lazima ubadili style...... Kumbuka kuwa you are not alone mwenye ndoto kama yako, kuna wengine wana  ndoto ya kuwa Rais kama wewe, kuna wengine wana ndoto ya kuwa best singer in Tanzania kama wewe, kuna wengine wana ndoto ya kuwa wanasiasa mashuhuri kama wewe...... Sasa input ndogo unayoiweka usidhanie hata siku moja kama utashindana na mtu ambaye 24/7 anapambana dhidi ya ndoto yake na ameweka standards za hali ya juu kwenye ndoto yake, ambaye muda wote anajifua ili kuwa bora zaidi na kujiweka sehemu nzuri zaidi ya kutimiza ndoto yake......Yaani haijalishi umejaaliwa uwezo au kipaji kikubwa kiasi gani kama wenzako wenye ndoto kama yako wanafanya zaidi ya wewe unavofanya na wanapambana zaidi yako basi jua kuwa utashika mkia na utaishia level za wakaida sana!!
KUMBUKA YOU ARE IN THE RACE....YOU ARE IN THE COMPETITION!! HAUPO PEKEYAKO UNAYEKITAKA HICHO KITU!! RAISE YOUR STANDARDS!!

Live Your Dream!!

Friday, 22 February 2019

JINSI YA KUTENGENEZA MISHUMAA

*JINSI YA KUTENGENEZA MISHUMAA*

*Malighafi na Vifaa*

Mafuta ya taa waxi/ Nta (Paraffin wax)
Asidi boriki na Stearine
Rangi (ukipenda)
Pafyumu (ukipenda)
Utambi / uzi
Umbo (mould) ya mshumaa
Jiko  la  mafuta  ya  taa/ mkaa na sufuria na vijiko vya chakula
Vifungashio vyenye lebo

*Utengenezaji*

Utambi
Changanya asidi boriki vijiko 5 vya chakula na maji vijiko 4 vya chakula
Koroga kwa dakika 5
Tumbukiza utambi ukae kwa dakika 5
Anika ukauke
Mshumaa
Andaa maumbo  ya mshumaa
Weka utambi katikati ya chombo kwa kushikiza na ute wa mshumaa na funga utambi
Weka sufuria jikoni, changanya nta kilo 1, stearine vijiko 4, chemsha  
Changanya rangi, parfyumu, asidi na koroga hadi mchanganyiko uyeyuke
Epua, mimina mchanganyiko kwenye maumbo na weka kwenye kivuli hadi mchanganyiko unaganda
Ondoa mshumaa taratibu kutoka kwenye maumbo

*Vifungashio na lebo*

Fungasha mishumaa kwenye chombo kitakachomvutia mteja aweze kununua

Bandika lebo kwenye chombo kuhusu bidhaa: Aina, mchanganyiko wa malighafi, uzito au idadi, maelekezo ya matumizi na uhifadhi, jina na anwani ya mtengenezaji, namba ya simu na barua pepe

Onyesha nembo za ubora kamaTBS na GS1 (Barcode)
Fuata maelekezo na taratibu za TBS
Hati na vibali
Onana na mamlaka husika kupata vibali na vyeti: TBS and GS1
Pata hati ya TCCIA kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi
Fuata taratibu za uuzaji bidhaa nje ya nchi

MADE DEODORANT / JINSI YA KUTENGENEZA DEODORANT NYUMBANI

MADE DEODORANT / JINSI YA KUTENGENEZA DEODORANT NYUMBANI :

Mahitaji :

3/4 kikombe mafuta ya nazi safi

1/2 kikombe corn starch au corn flour

1/2 kikombe baking soda  (BICARBONATE OF SODA )

Maelezo :

Changanya mahitaji yote kwa pamoja katika  bakuli. Kisha mimina katika kikopo kisafi na kikavu na weka sehemu yenye ubaridi au katika fridge ili igande. Unatumia kama deodorant zingine.
Inaondoa weusi katika makwapa na kukata harufu mbaya ya kwapa na kupunguza kwa jasho kutoka kwa wingi.
Hata kama haijaganda ni sawa tu. Tumia hivyo hivyo.

Unatumia tu kama deodorant za madukani.

Saturday, 16 February 2019

VITU VIKUU VITATU VILIVYOBEBA TOFAUTI KATI YA WATU WALIOFANIKIWA NA FAILURES

VITU VIKUU VITATU VILIVYOBEBA TOFAUTI KATI YA WATU WALIOFANIKIWA NA FAILURES

Wote tunakuja duniani baada ya kuwa washindi katika mapambano makubwa yanayohusisha mabilioni ya washiriki.....Wote tunakaa mapumzikoni miezi tisa tukijaandaa na pambano lingine.....Wote tunakuja duniani tukiwa full packed na vitu muhimu vya kukusaidia kushinda mapambano mengine ya hapa duniani, ambapo Mungu humpa kila mtu vitu sahihi anavovihitaji kuendana na aina ya pambano lake.....Yaani tunapewa vitu kama vile Passion, talents, core abilities, potential, akili, nguvu, viungo kutokana na kuendana na aina ya mapambano unayoyaendea.......SWALI NI JE, NINI KINASABABISHA WENGINE WASHINDE MAPAMBANO YA HAPA DUNIANI NA WENGINE WASHINDWE ILI HALI WE ARE ALL WINNERS??.......Utofauti huanza kuonekana kutokana na;

1. Kutotumia nyenzo za Mapambano tulizopewa na Mungu.

Kila mtu amezawadia na Mungu vitu maalum vya kumsadia kwenye mapambano....Na kwa bahati nzuri ni kuwa yeyote anayeamua kuzitumia nyenzo hizi ni lazima awe mshindi kwenye hayo mapambano.

Na tofauti ya watu wanaofanikiwa na wasiofanikiwa huanza pale ambapo wengine wanaamua kuzitumia nyenzo hizi wengine wanapuuzia kuzitumia...... Am totally convinced kwamba "Kila mtu ana kipaji/ Uwezo fulani wa kipekee aliopewa na Mungu" ambao ndiyo nyenzo kuu kwake kwa mafanikio....... Kuna watu wamepewa kuchora, wengine kuimba, wengine kufundisha, wengine udaktari, wengine uhandisi, wengine uongozi, wengine Technology, wengine uvumbuzi wa vitu, wengine biashara na ujasiliamali, wengine kishauri, wengine utunzi, wengine habari, wengine ujeshi, wengine michezo etc......Vitu hivi vyote na vingine vingi Mungu ameweka ndani yetu kama Primary weapon ya kutusaidia kufanikiwa.... Tatizo ni kuwa kutokana na Malezi na kukua tukitamani maisha ya watu wengine waliotutangulia kutokana na kuangalia mahali panapoonekana panalipa kwa macho ya kibinadamu basi wengi wameiga na kijikuta wamekaa maeneo ambayo siyo ya kwao......Mtu alitakiwa kuwa daktari amekaa kwenye uhandisi, aliyetakiwa kuwa mwana michezo yupo kwenye udaktari, mwanajeshi yupo kufundisha watoto kama mwalimu, mchoraji yupo polisi, aliyeumbwa kuwa mwanasheria yupo hospitali kama daktari na aliyetakiwa kuwa mchungaji kanisani yupo kwenye siasa.....Yaani ni vururu vururu kila mtu amekaa mahali pasipo pake na hivyo kutotenda kwa viwango vikubwa vya hali ya juu na hivyo siyo rahisi kufanikiwa eneo ambalo siyo eneo lako sahihi. Kwani mtu aliyekaa kwenye eneo lake sahihi kuwa na uwezo wa tofauti na wengine kwenye eneo hilo na anaweza kuona zaidi ya wengine wanavyoona kwenye hilo eneo na pia huwa mbunifu na mvumbuzi wa mambo kwenye hilo eneo.....Sasa wachache waliofanikiwa kukaa kwenye maeneo yao sahihi ndilo kundi la watu waliofanikiwa sana na sisi tunawashangaa na kuwaona kuwa hawa watu wa maakili mengi lakini kumbe hata siyo akili bali ni kutambua eneo lao sahihi na kuamua kukaa hapo.

Watu waliokaa kwenye maeneo yao sahihi ni wabunifu, wavumbuzi wa vitu vipya, wanafanya kwa ubora kwani wao kwao ni kama hobby, wanajituma bila kuambiwa kwani wanaenjoy kufanya hata bila malipo wapo tayari kufanya.

Siyo rahisi kufanikiwa eneo ambalo siyo eneo lako sahihi...... Ukikaa eneo ambalo siyo eneo lako sahihi utaonekana kilaza tuu.....Nyani hakuumbwa akae majini hivyo kama akiwekwa majini utamcheka sana na kumuona hana uwezo.....Samaki hakuumbwa akae nchi kavu bali majini, ukimpleka samaki nchi kavu utamuona kilaza.....simba hakuumbwa kupanda miti, ukimshindanisha na nyani eneo hilo basi lazima simba ainekane mbumbumbu..... Hivyo ndivyo binadamu tumekosea kutokukaa maeneo yetu sahihi.... Leo ukimuona Diamond Platnums anafanikiwa ni kwa sababu yupo eneo lake sahihi, Mbwana Samatta anazidi kuchanja mbuga ni kwa sababu yupo eneo lake sahihi etc.....JITAFUTE, TAFUTA ENEO LAKO SAHIHI, THEN KAA HAPO KWANI NDIPO PENYE MAFANIKIO YAKO!!

2. Tabia zinazoongoza maisha yetu ya kila siku (HABITS).

Mafanikio ni muunganiko wa tabia mbalimbali zinazoleta mafanikio, na uzuri ni kuwa tabia ni kitu ambacho kila mtu anaweza kujifunza.....Ukimuona leo mtu ni Drug addict basi jua hakuzaliwa anatumia madawa ya kulevya bali ni tabia tu alianza kujifunza taratibu, na inawezekana alianza na pafu moja ya bangi na badae akazoea na kuona kuwa bangi hazina stimu za kutosha na kuamua kuanza na unga kidogo then finally addiction.....Tambua kuwa tofauti kubwa iliyopo kati ya watu waliofanikiwa na watu failures siyo akili wala mazingira bali ni tabia zao zinazoongoza maisha yao ya kila siku......Tofauti iliyopo kati ya masikini na tajiri siyo pesa bali ni tabia, kwani huyu ambaye anaonekana masikini leo kama akiamua kuishi kwa tabia za watu matajiri naye baada muda fulani atakuwa tajiri tu.

Kitu chochote ukikifanya maranyingi na kila siku huwa kinakuwa tabia.

Tabia za uvivu, uongo, kuto kujituma, ni miongoni mwa tabia zinazoleta umasikini na kufeli kwenye maisha....Lakini kujituma, ukweli, uaminifu, kumcha Mungu, ni tabia zinazoleta mafanikio.

Tabia ni kitu unaweza kujifunza, Anza leo kujijengea utaratibu wa kujijengea tabia zinazoleta mafanikio.... Kitu chochote ukikifanya kwa mfululizo kwa siku 21 huwa kinabadilika na kuwa tabia.....Na kikifika level ya kuwa tabia maana yake utakuwa unaifanya automatically bila kutumia nguvu.!!
AMUA KUUNGANA NA WASHINDI KWA KUJIJENGEA TABIA ZA MAFANIKIO!!

3. Maamuzi na Chaguzi Tunazozifanya Kila Siku (Decisions and Choices).

Maamuzi unayoyafanya  ndo kitu kinabeba Destiny yako......Unaamua uishi vipi, unaamua kuwa na tabia za aina gani, wewe ndo unaamua kuambatana na watu wa aina gani, wewe ndo unaamua ufuatilie habari za aina gani, wewe ndo unaamua ujaze vitu vya aina gani na taarifa za aina gani kichwani mwako kama ni udaku au skendo za wasanii au movies za kikorea au vitabu na maarifa chanya, Wewe ndo unaamua na kuchagua namna ya kuutumia muda wako na siku yako, wewe ndo unaamua utumiaje pesa unazozipata, wewe ndo unaamua uwe na mahusiano ya aina gani, wewe ndo unaamua uwe mvivu au uwe mtu wa kujituma, wewe ndo unaamua uwe mcha Mungu au mtu dhambi, wewe ndo unaamua kuwa mlevi au la, wewe ndo unaamua na kuchagua uwe kicheche au mwaminifu..... Chaguzi zako na maamuzi unayoyafanya kila siku kwenye vitu mbalimbali kuhusu maisha yako ndivyo vinaamua kama utafanikiwa ama la??!!

Kwenye huu ulimwengu Mungu ametuwekea Uhuru wa kuchagua tunachokitaka na kuamua tunavotaka.....Na bahati nzuri ni kuwa Mungu anatamani kila mtu afanikiwe kwa kiwango cha hali ya juu na ni hasara kubwa sana kwa Mungu kukuona wewe ukiwa failure kwenye maisha yako kwani amekuwekea vitu vingi kwa ajili ya kuwafaa wengine ambavyo ndivyo vingekupa mafanikio makubwa lakini kutokana na uhuru wa kuchagua na kuamua aliotupa wanadamu ndio maana anakuacha uamue wewe Na uchague wewe aina ya maisha unayotaka kuyaishi, Ukichagua kufanikiwa yupo pamoja nawe, ukiamua kufeli anaumia lakini hana namna ya kukulazimisha kufanikiwa.

Maamuzi yoyote na chaguzi ya aina yoyote ile huwa ina kuwa na matokea ndani yake, hivyo kila unapochagua au kuamua kufanya jambo linalokuangamiza na kukudidimiza jua kuwa matokeo yake yatakuwa saw a kabisa na vile ulivoamua au kuchagua..... Kumbuka Bible inavosema " ....Mungu hadhihakiwi, apandacho mtu hakika ndicho avunacho"......Unapofanya maamuzi ya kuvuta sigara jua kuwa matokeo yake ni Kansa ya mapafu, Unapochagua kuwa mzinzi jua kuwa matokeo yake ni HIV/ AIDS, Unapochagua kuwa Mvivu na kujionea huruma na kutoumiza kichwa jua kuwa matokeo yake ni umasikini wa kutupwa.....Lakini pia jua kuwa unapoaamua na kuchagua kujituma, bidii, kumcha Mungu, Uaminifu, maarifa na kutembea na washindi na watu positive jua kuwa matokeo yake ni Mafanikio makubwa.

Maamuzi haya na Chaguzi hizi zinapoendelea kwa muda mrefu huleta matokeo makubwa......Unavoamua na kuchagua leo, kesho na keshokutwa ndivyo vitakavyoleta matokea kuhusu future yako......Ukiamua kama watu waliofanikiwa wanavoamua na kuchagua basi nawe ni lazima utafanikiwa vinginevyo utajiunga na failures.

Dr. Myles Munroe huwa anasema "SUCCESS IS PREDICTABLE".....Unaweza kujua mtu kama atafanikiwa au hatafanikiwa kwa kuangalia kama je anajua anachokitafuta duniani, Tabia zinazoongoza maisha yake (Habits) na Chaguzi zake za Lea na Maamuzi anayoyafanya leo.
JIWEKE KWENYE KUNDI LA WATU AMBAO MAFANIKIO KWAO NI LAZIMA KWA KUTAMBUA ENEO LAKO SAHIHI, KUWA NA TABIA ZA WASHINDI NA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI!!

Live Your Dream!!

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO