Tuesday, 8 January 2019

YOUTH OPPORTUNITY

Please share these opportunities within your students and friends and networks👇

1. Australia Award  Scholarship (http://australiaawardsindo.or.id)
2. LPDP Scholarsh hip (http://www.beasiswalpdp.org/index.html)
3. DIKTI Scholarship a. Dalam Negeri (http://www.beasiswa.dikti.go.id/dn/)b. Luar Negeri (http://beasiswa.dikti.go.id/ln/)
4. Turkey Government Scholarship (http://www.turkiyeburslari.gov.tr/index.php/en)
5. General Cultural Scholarship India (http://www.iccrindia.net/gereralscheme.html)
6. USA Government Scholarship a. (http://www.aminef.or.id/index.php)b. (http://www.iief.or.id)
7. Netherland Government Scholarship (http://www.nesoindonesia.or.id/beasiswa)
8. Korean Government Scholarship (http://www.niied.go.kr/eng/contents.do…)
9. Belgium Government Scholarship (http://www.vliruos.be/4273.aspx)
10. Israel ... ... xxx
11. Sciences Po France (http://formation.sciences-po.fr/…/the-emile-boutmy-scholars…)
12. Utrecht University Netherland (http://www.uu.nl/…/grantsandscholarships/Pages/utrechtexcel…)
13. Prasetya Mulya Business School Indonesia (http://www.pmbs.ac.id/s2/scholarship.php?lang=ENG)
14. Brunei Darussalam Government Scholarship (http://www.mofat.gov.bn/index.php/announcement)
15. Monbugakusho Scholarship Japan (http://www.id.emb-japan.go.jp/sch.html)
16. Paramadin ba University Master Fellowship Indonesia (https://gradschool.paramadina.ac.id/…/paramadina-medco-fell…)
17. PPM School of Management Indonesia (http://ppm-manajemen.ac.id/beasiswa-penuh-s2-mm-reguler/)
18. University of Twente Netherland (http://www.utwente.nl/internationa…/scholarshipsandgrants/…/)
19. Sweden Government Scholarship (http://www.studyinsweden.se/Scholarships/)
20. Chinese Government Scholarship (http://www.csc.edu.cn/laihua/scholarshipdetailen.aspx…)
21. Taiwan Government Scholarship (http://www.studyintaiwan.org/taiwan_scholarships.html)
22. United Kingdom Government SCholarship (http://www.chevening.org/indonesia/)
23. Panasonic Scholarship Japan (http://panasonic.net/citizensh…/scholarships/…/requirements/)
24. Ancora Foundation Scholarship (http://ancorafoundation.com)
25. Asian Public Intellectuals Fellowship Japan (http://www.api-fellowships.org/body/)
26. AUN/SEED-Net Scholarship (http://www.seed-net.org/index.php)
27. Art Asia Major Scholarship Korea National University of Arts (http://eng.karts.ac.kr:81/karts/board/list.jsp…)
28. Ritsumeikan Asia Pacific University Japan (http://www.apu.ac.jp/home/life/index.php?content_i
d=30)
29. Seoul National University Korea (http://en.snu.ac.kr/…/gradu…/scholarships/before-application)
30. DIKTIS Overseas Scholarship (http://www.pendis.kemenag.go.id/beasiswaln/)
31. Honjo International Scholarship Foundation Japan (http://hisf.or.jp/english/sch-f/)
32. IDB Merit Scholarship Programme for High Technology (http://www.isdb.org/irj/portal/anonymous…)
33. International HIV & Drug Use Fellowship USA (http://www.iasociety.org/fellowship.aspx)
34. Nitori International Scholarship Foundation Japan (http://www.nitori-shougakuzaidan.com/en/)
35. School of Government and Public Policy Indonesia (http://sgpp.ac.id/pages/financial-conditions)
36. Inpex Scholarship Foundation Japan
37. Asia University Taiwan (http://ciae.asia.edu.tw/AdmissionsScholarship.html)
38. Macquaire University Australia (http://www.mq.edu.au/…/macquarie_university_international_…/ .

Please share for the benefit of our youth. You will be surprised with  the difference you can make.

Monday, 7 January 2019

HOMEMADE FONDANT ICING / NAMNA YA KUANDAA FONDANT KWA AJILI YA KEKI NYUMBANI

HOMEMADE FONDANT ICING / NAMNA YA KUANDAA FONDANT KWA AJILI YA KEKI NYUMBANI :

MAHITAJI

🔸Icing sugar, ilochekechwa vikombe 7 na  1/2
🔸Maji ya baridi 1/4 kikombe
🔸Unflavored gelatin kijiko 1 chakula (kwa waislam hakikisha ni halali gelatin) maana zingine zatengenezwa kwa mafuta ya nguruwe
🔸Glucose 1/2 kikombe
🔸Glycerine kijiko 1 1/2 chakula
🔸Vanilla kijiko 1
*NOTE*
GLYCERINE YA CAKE NA GLUCOSE YA CAKE. SIO VYA KUPAKIA MWILINI. NI VIFAA KWAJILI YA CAKE🎂

NAMNA YA KUTAYARISHA:-

1. Tia icing uliochekecha katika bakuli kubwa kisha weka kishimo kati

2. Katika kisufuria kidogo tia maji kisha nyunyiza gelatin juu acha ilainike kwa muda wa dk 5.

3. Ipashe moto gelatin ukiwa wakoroga hadi  iyeyuke yote , usiache *ikachemka.* Zima jiko kisha tia glucose na glycerine na koroga vizuri hadi vichanganyike.

4. Tia radha, kisha mimina katika kishimo ulichoweka karika icing yako na changanya hadi icing yote ichanganyike vizuri.

5. Kanda foundant yako katika sehemu ya kukandia au sinia hadi iwe smooth na soft, ukiona inanata ongeza icing kidogo.

6. Fanya duara kisha zungusha vizuri na plastic na tia katika container lenye mfuniko.

NOTE
Usiweke katika fridge tumia kwa muda wa wiki 2

Ni vyema uiache ikae kwa muda wa masaa 8 kabla ya matumizi

Mahitaji yanapatikana maduka ya vifaa vya keki,na supermarket.

Sunday, 6 January 2019

JINSI YA KUTENGENEZA MAFUTA YA MGANDO

*JINSI YA KUTENGENEZA MAFUTA YA MGANDO*.

*tujifunze namna Kutengeneza mafuta ya mgando(meupe)*

*Mahitaji*

Micro wax kilo moja
White oil Lita mbili
Perfume vijiko viwili
Kutengeneza
Chukua sufuria kavu bandika jikoni weka micro wax kilo moja
Kisha white oil Lita mbili iache mpaka ichemke kwa muda mfupi utaweka perfume vijiko viwili mimina humo
Baada ya hapo utaiacha ichemke kidogo kisha isikae sana ichemke mana italipuka kwahyo wakati unaipika moto uwe wa wastani kisha acha ipoe ibakie ya uvuguvugu
Mpaka hapo itakua imekamilika mgando wako weka lebo

SABUNI YA MAWESE NA ASALI

SABUNI YA MAWESE NA ASALI

MAHITAJI

ASALI PURE VIJIKO 10,

MAFUTA YA MAWESE MILS 200

OLIVE OIL VIJIKO 2

BASE SOAP GM 700

RANGI( UKIPENDA ) NJANO ROBO KIJIKO.

HATUA YA 01:

YEYUSHA BASE SOAP NDANI YA SUFURIA LA MAJI YA MVUKE( DOUBLES  BOILER)

IKISHAYEYUKA ONGEZA MAFUTA YA MAWESE , ONGEZA  OLIVE OIL, RANGI, KISHA KOROGA KUPATA UJI AMBAO UTAMIMINA KTK MOLD ULIYOANDAA.

SABUNI HII IPO TAYARI KWA MATUMIZI MARA TUU IKISHAPOA NA KUGANDA.

Saturday, 5 January 2019

PSYCHOLOGY: SAIKOLOJIA DALILI 7 KUWA MKEO ANAHITAJI UMSIKILIZE

PSYCHOLOGY: SAIKOLOJIA DALILI 7 KUWA MKEO ANAHITAJI UMSIKILIZE


PSYCHOLOGY: SAIKOLOJIA DALILI  7 KUWA MKEO ANAHITAJI UMSIKILIZE
Wakati fulani kitu pekee ambacho mwanamke anakihitaji ni mtu wa kumsikiliza. Njia maridhawa ya kumsaidia mkeo katika
matatizo yake, kwanza ni kumsikiliza na kumakinika kwa anachosema kisha utoe maoni yako juu ya suluhisho la tatizo husika iwapo ataomba ufanye hivyo.
Iwapo hutambui ujumbe ambao mkeo anajaribu kuutuma, basi Famasia ya Ndoa Maridhawa inakuletea ishara saba za wazi zinazoonesha kuwa mkeo anahitaji sana umsikilize:

1. ANAPOONESHA TABASAMU AMBALO SIO HALISI:
Mwanamke anayeweza kutabasamu hali ya kuwa hajisikii vizuri, basi huyo ni mwanamke madhubuti, lakini bado anahitaji faraja yako. Mkumbatie na umuombe afunguke.
2. IWAPO SIKU NZIMA ALIKUWA PEKE YAKE NA WATOTO
Anahitaji kupata mazungumzo ya mtu mzima. Kama ni mama wa nyumbani, bila shaka atakachokuwa akikisikia kwa siku nzima ni makelele ya watoto, vilio vyao na sauti za vipindi vya katuni. Unaporudi nyumbani muulize kuhusu siku yake ilivyokuwa ili kumpa mazungumzo ya kiutu-uzima ambayo alikuwa na shauku nayo kwa kutwa nzima.
3. ANAPOKUWA KIMYA KULIKO KAWAIDA
Anapokuwa na ukimya usiokuwa wa kawaida, anaweza kuwa na hasira au msongo. Mkumbatie na umuulize kinachoendelea akilini mwake.

4. ANAPOSEMA KWA HASIRA "SAWA"
Iwapo uko kwenye ndoa kwa muda mrefu au unazifahamu silika za wanawake, anaposema "sawa" yaweza kumaanisha "sio sawa". Yumkini tatizo lisionekane, lakini huhitaji kuchimbua kutafuta mzizi wa tatizo. Muulize tu mambo gani hayako sawa na namna unavyoweza kusaidia kuyaweka sawa. Atapenda sana kuona kuwa unajali sana hisia zake.

5. ANAPOKUWA KATIKA MOOD NZURI
Anataka umsikilize anapokuwa na furaha kwa kiwango kilekile anachotaka umsikilize anapokuwa na huzuni. Muulize kuhusu siku yake ilivyokuwa. Yumkini anatamani kukupa habari njema.

6. ANAPOCHOSHWA NA MAJUKUMU YA KUTWA NZIMA
Tengeneza utayari wa kumsikiliza pindi anapokuwa na siku iliyojaa majukumu kayaya. Mkumbushe namna unavyothamini yote anayoyafanya kwa ajili yako na familia yenu pia. Hatua hii maridhawa itamthibitishia kuwa yote anayoyafanya yanaonekana na kumpa hamasa ya kuendelea kufanya mambo mazuri na kujituma zaidi.

7. ANAPOJIANDAA KULALA
Tengenezeni mazingira na utaratibu wa kuzungumza kabla ya kulala. Mweleze namna siku yako ilivyokuwa na usikilize upande wake pia. Muda huu wa ukuruba huwaleta pamoja kihisia, na atafurahia kutumia dakika hizo za mwisho kuzungumza nawe.
Kaka yangu, zichunguze ishara zinazoonesha kuwa mke anahitaji umsikilize. Anahitaji uwe pembeni yake anapokuwa na msongo au anapokuwa na furaha. Aidha, kwa upande wako pia, kama unataka mkeo akusikilize, mwambie. Ndoa yenye afya huimarika zaidi pindi wanandoa wanapokuwa na uwazi, ukweli na wakawa tayari kusikiliza.

Friday, 4 January 2019

TENGENEZA ELA NYINGI KWA KUFUNGUA KIWANDA KWA MTAJI MDOGO

Tengeneza ela nyingi kwa kufungua kiwanda kwa mtaji mdogo na chini

1* sabuni ya maji Lita 10 kwa 12000

2*sabuni ya kipande miche 10 kwa 10000

3*sabuni ya unga kilo 3 kwa 9000

4*sabuni za urembo vipande 40 kwa 6000 unauza 500 au hata 1000 kila kipande

5*kiwanda cha rosheni kwa 12000

6*kiwanda cha chaki kwa 5000

7*kiwanda cha juice kwa 4000

8* kiwanda cha pili pili tomato au chills kwa 8000

9" kiwanda cha mikate kwa 40000

10*kiwanda cha mafuta ya mnyonyo. Buree

11*Kiwanda cha mafuta ya alizet kwa 30000

12*kiwanda cha unga Wa lishe kwa watoto na wanao nyonyesha Kwa 50000 ila kila mfuko 1 unauza 5000 una unapata mifuko si chini ya 30 inabust maziwa

13*Kiwanda cha batiki kwa 28000

14 .kiwanda cha maji 300,000

15*kiwanda cha Viatu Kwa 20,000

16*kiwanda cha viungo vya chakula Kwa  10,000

17*kiwanda cha kusafishia masink kwa 20000

18*kiwanda cha chakula cha kuku kwa 100,000

19,kiwanda cha pafyum kwa 12,000

20*kiwanda cha kusindika samaki kwa 200,000

Hivyo ni baadhi tu za viwanda unavyoweza mm na wewe hadi mwezi Wa 12 tukawa kivingne kila jengo limeanza na tofari 1 na kila safari imeanza na hatua 1

Ukianza juu utashuka chini

Ukianza chini utapanda juu

Wewe ni champion

Tuesday, 1 January 2019

UTENGENEZAJI WA SABUNI YA MAGADI/MAWINGU

Utengenezaji Wa sabuni ya magadi/mawingu

Mahitaji

1*kaustiki soda (kama chumvi)

2*maji

3*mafuta ya mise au Nazi

4*magadi soda

5*chumvi

6*sodium silket au cde kimoja wapo (kama mafuta)

Vifaa vya usalama

Grops za mikono

Mask kuziba pua  wakat Wa kukoroga kaustiki

Ndoo

Mti Wa kukoroga

Boksi za kawaida kwaajiri ya kufanya maumbo

Utengenezaji

Hatua ya kuanza

Andaa ndoo Lita 10 weka maji Lita 5

Baada ya kuweka maji weka magadi soda vijiko 3 vya chakula ..

Baada ya hapo mimina kaustiki soda kilo 1

Anza kukoroga Kwa dakik 5
Baada ya hapo acha kwa siku 3 uwe umefunika au umeacha wazi ni sawa

Maelezo

Wakati Wa kuweka kaustiki maji yatakua ya moto ndio hali yake ila utakiwi kuchezea kwa mikono

Hatua ya kumalizia

Baada ya siku 3 kaustiki itakua imepoa  kwahy tumeleweka kwenye maji ili isichubue mikono sabuni yetu

Sasa chukua ndoo yenye maji ya kaustiki anza kumimina malighafi zifuatazo

Sidiuom silket au c.d.e vijiko 3 vya chakula

Kama unayo soda ash unaweza kuweka vijiko 3 vya chakula kama hauna acha tu

Baada ya hapo chemsha mafuta yako yawe ya vugu vugu sababu yana asili ya kuganda kwahy lazima uyachemshe hata kama hayajaganda

Baada ya kuchemsha sasa utaangalia ukubwa Wa umbo lako

Mimi Nina boksi Dogo nimeomba dukani kwahy nitachota Yale maji ya kaustiki soda Lita 1  alafu nitaweka kwenye ndoo isiokua na kitu chochote alafu nitachanganya na mafuta Lita 2 nitakoroga kidogo Sana kama sekunde 20 alafu namimina kwenye boksi langu ili ikauke kisha nikate vipande

Ila wakat Wa kuandaa boksi kwa ndani nitaweka maironi ili sabuni ikikauka isinasie kwenye boksi

Pia ile naironi nitaitoboa vitobo kidogo ili kuna maji maji niyape nafasi ya kupita

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO