Tuesday, 29 January 2019

KASHATA ZA NAZI

Kashata za nazi
Nazi  iliyokunwa mmoja kubwa
Jelly kiasi
Sukari robo
Maziwa ya unga 3tspoon
Hiliki chembe 5
Maji kiasi
Food colour

Chukua bakulia kavu weka nazi uliyoikuna tia hiliki na maziwa changanya uzuri mpk uwe kitu kimoja weka pembeni chukua sufuria tia maji weka jikoni subir yachemke weka sukari suburi mpk ifanye povu zito chota kwa mwiko halafu gusa na vidole ukiona inanata snaa km gundi weka nazi yako  n'a jelly changanya uzuri mpk mchanganyiko uwe kitu kimoja,mimina ktk kibao cha mkate ulichoweka mafuta ukimaliza sukuma na kifimbo ulichokipaka mafuta ukimaliza wacha ipoe halafu aaza kukata shepu uipendayo,andaa n'a kahawa Kula.

Wengi zinawapa tabu hizi kashata kwa sababu nazi inakuwa maji maji ukitaka uweze ikune mapema ukimaliza chukua sahani kubwa
zitandaze weka juani kidogo halafu ndoo upike n'a sio lazima kuweka jelly mm nimeweka km urembo tu.
  👩‍🍳 mapishi bora 👩‍🍳

JINSI YA KUTENGENEZA CHOCOLATE

JINSI YA KUTENGENEZA CHOCOLATE
Unaweza kutengeneza chocolate nyumbani kwa kutumia vifaa vya nyumbani na ingredients zinazo patikana madukani.

MAHITAJI KWA AJILI YA CHOCOLATE.
-Siagi kikombe kimoja
-Cocoa powder kikombe 1
-Icing sugar/Sukari iliyosagwa au asali kikombe 1/2
-Maji 1/2 kikombe
-Vanilla ya maji kijiko 1 ccha chai
-Chumvi tone

MAELEKEZO
1)Pima Sukari na Cocoa powder kwenye sufuria size ya kati.
2. Ongeza maji kwenye mchanganyiko wa sukari na cocoa poda.

3)Weka maji kwenye sufuria kubwa yajae 1/4 kisha weka kwenye moto mdogo.
4)Weka sufuria ya size ya kati iliyo na cocoa poda+sukari+maji juu ya sufuria kubwa(double boiler).

5)Wakati maji ya sufuria kubwa yanachemka, koroga mchanganyiko wako wa cocoa poda taratibu, kwa dk 15 mpaka iwe nyepesi kama uji.
6)Ondoa sufuria ya mchanganyiko wa chocolate kwenye moto, kisha ongeza  siagi iyeyukie, ongeza fleva kama vanila.

7)Blend mchanganyiko wako, tumia blender au hand mixer,lengo la kublend ni kufanya chocolate yake iwe smooth isiwe na mabuja.

8)Mimina chocolate mchanganyiko,kwenye ice cube tray,acha kidogo isawazike kwa dk2.
9)Weka ice cube tray iliyo na chocolate kwenye freezer, kwa masaa 1-2 au usiku kucha.
10)Waweza toa kwa lisaa limoja,kisha ukaweka juu ya chocolate karanga zilizosagwa,au peanut butter,au strawberry(Angalia pichani),kisha rudisha frijini kwa lisaa1.

-Chocolate tayari,toa tray, ondoa chocolate kwenye tray tayari kwa kuliwa.ENJOY
  👩‍🍳 mapishi bora 👩‍🍳

Monday, 14 January 2019

MALIGHAFI ZINAZO HITAJIKA WAKATI WA UTENGENEZAJI WA MISHUMAA

*Jinsi ya kutengeneza mishumaa*

*MALIGHAFI ZINAZO HITAJIKA WAKATI WA UTENGENEZAJI WA MISHUMAA*

1. Paraffin Wax
2. Utambi
3. Mould ( Umbo )
4. Stearine au mixture
5. Rangi
6. Jiko la mafuta ya taa au mkaa.
7. Sufuria.
8. Boric acid.

*VIDOKEZO MUHIMU*
1. Paraffin Wax :
Hii inatokana na nta na sega ya nyuki iliyo changanywa na mafuta ya taa. Ina rangi nyeupe na katika utengenezaji wa mishumaa ina ubora kuliko bee wax.

* Bee Wax : Inatokana na masega ya nyuki yaliyo changanywa na mafuta ya petroli na diesel na rangi yake ni ya njano.

2. STEARINE
Hii dawa maalumu inayo fanya mishumaa iungane ama ishikamane.

3. BORIC ACID :
Hii ni maalumu kwa ajili ya kuufanya utambi usiishe mapema na uwake bila kutoa moshi.

4. RANGI :
Rangi nzuri zinazo tumika katika utengenezaji mishumaa ni rangi za chakula na nyingi huwa ni za maji.

*JINSI YA KUTENGENEZA*

Andaa mould ( umbo lako ) utakalo litumia baada ya kuyeyusha ( paraffin wax ) na kuchanganya na michanganyo yote.

Kwa Mfano : ( Kipimo cha stearine )
1. Wax kilo moja - Stearine vijiko vinne vya chakula.
2. Wax nusu kilo - Stearine vijiko vinne vya chakula
3. Wax robo kilo - Stearine kijiko cha chakula.

Baada ya mould ( umbo ) kuwa tayari , chemsha wax mpaka iyeyuke na itoe kwenye vyombo ambavyo umetayarisha na usubiri ikauke ili uanze kutoa mishumaa

DAWA YA KUNG'ARISHA VIATU VYEUPE

Dawa ya kung'arisha Viatu vyeupe

Mahitaji

1*magadi soda

2*vinegar

3*maji

Utengenezaji..

Andaa bakuli lako linaloendana na wingi Wa mahitaji yako kisha weka magadi soda vijiko 5 vya chakula kisha weka vinegar vijiko 5 vya chakula kisha weka maji vijiko 5 vya chakula koroga

Hakika Viatu hata kama vilikua vimegandia uchafu sugu au kufubaa vitarudi katika hali yake ya zamani

Friday, 11 January 2019

UTENGENEZAJI WA SABUNI YA KUNAWIA MIKONO,KUSAFISHIA VIOO,

Utengenezaji Wa sabuni ya maji,_ shampoo, sabuni ya kunawia mikono   sabuni ya kusafishia vioo, dawa ya kusafishia choo   yote ndio hii

Tofauti unaweza kumbadirisha rangi tu na kumuwekea Vifungashio tofauti

Mahitaji

1* siles (ungaroli)

2*chumvi

3* rangi ya sabuni ya maji

4*manukato

Utengenezaji

Andaa ndoo Lita 20  kisha weka maji Lita 10 kisha weka siles (unga roli) Lita 2

Kisha koroga Kwa dakika 15  ila kila baada ya dakika 5 weka chumvi mikono (kiganja) kimoja kwahy hadi dakk 15  utakua umeweka chumvi viganja 3 

Baada ya kukoroga Kwa dakika 15 sasa weka manukato kiasi upendacho pamoja na rangi kiasi upendacho

Koroga tena kwa dakika 5  

Hapo utakua umekorga Mara   dakika 20 hadi kumalizika kwa sabuni

Na sabuni yako itakua tayar

Hakuna alie jaribu hii sabuni na sizani kama aliwai mtu kutengeneza ni nzito sana na malighafi chache

Tuesday, 8 January 2019

UTENGENEZAJI WA JAMU YA NANASI

*UTENGENEZAJI WA JAMU YA NANASI*

Jamu ya nanasi ni bidhaa inayotengenezwa kwa kutumia mchanganyiko wa mananasi yaliyosagwa (pulp) na kuchemshwa pamoja na sukari na acid. Ili kupata jamu yenye ubora mzuri ni sharti kuzingatia uwiano mzuri kati ya acid, sukari na pectin.


*Mahitaji/Viambaupishi*

Nanasi

Sukari

   
citric acid (Kutegemeana na aina ya matunda)

   *VIFAA*

SUFURIA

   KIJIKO CHA CHAI

  VISU

  KIPIMA JOTO (THERMOMETER)

   CHUJIO

   MWIKO

   NDOO

     SINIA
   REFRACTOMETER

  MZANI

MASHINE YA KUSAGA MATUNDA (BLENDER)AU ‘PULPER’


  UBAO WA KUKATIA MATUNDA

Hatua za uzalishaji

Osha matunda vizuri kwa maji safi na salama. Chagua matunda yalyoiva
Menya matunda na ondoa macho na moyo wa katikati, katakata vipande na uvizage.
Chemsha kupata pulp ya matunda

Weka

sukari
acid

Changanya vizuri, pika polepole ukikoroga hadi joto la kutosha litakapofikia.
Hakikisha jamu yako imeiva vizuri
Jaza kwenye chupa safi ikiwa bado ya moto.
Jamu tayari

JINSI YA KUTENGENEZA SHAMPOO

*JINSI YA KUTENGENEZA SHAMPOO*

shampoo zipo za aina nyingi inategemea virutubisho na kemikali zilizotengenezwa.kuna shampoo ambazo zina harufu nzuri .kwa mfano waweza tumia perform[harufu]kama havened lemon,jasmine,peach apples) na shampoo za virutubisho kama parachichi,karoti alovera,tango,mayai.

Mfano(i)
Kutengeneza shampoo (ambayo inatumia chemical)
zilizochanganywa harufu au perfume(vyote ni kuchanganya kwa pamoja
na kukoroga tu).

Mfano(ii)
malighafi za shampoo isiyo na virutubisho/shampoo hiyo
unaweza tengeneza kwa formula mbili
.    sulphonics Acid
.    soda ash
.    maji
.    sless
.    rangi
.    perfume
.    grycelin
.    chumvi.

*JINSI YA KUTENGENEZA*
*HATUA YA*

Kwanza tayarisha malighafi zote,ziwe juu ya meza utakayo fanyia kazi,vyombo vya kufanyia viwe visafi na kumbuka kusafisha kwa maji kila unachotumia.
Tayari vifaa vya  kufanyia kazi
Anza na sulphonic acid vijiko (4) vya chakula tumbukiza kwenye ndoo au mashine yako.

Fuatia na soda ash vijiko(2) vya chai lakini kumbuka kuchanganya na maji kidogo.
Koroga na mwiko au na mti baada ya mchanganyiko

Tia maji lita 4 nakuanzia hapo anza kukoroga kwa muda wa dakika kumi,kisha unafuatia malighafi zifuatazo
Strees-robo
Glycerine vijiko(3) vya chakula
Perfume-kijiko cha chai kimoja
Rangi-Kijiko cha chai kimoja.
Chumvi kijiko cha chai kimoja

   Usiweke kitu kingine na ukumbuke chumvi ni ya mwisho kama muda umefika ikiwa nzito kama uji/shampoo yako itakua tayari

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO