Thursday, 29 November 2018

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA UNGA

#DONDOO.!! ZA FAIDA..!!!
.....
@JIFUNZE JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA UNGA...!!!
.....
...Jinsi ya kutengeneza sabuni ya unga.
MAHITAJI.
.Optical bright
.Sodium carbonate
.Sulphonic acid
.Soda ash
.Nasa
.Perfume
Mwiko, Beseni, Gloves
JINSI YA KUTENGENEZA.
Andaa beseni lako linaloendana na wingi wa sabuni unayotaka kutengeneza na anza kutengeneza kwa kufuata hatua zifuatazo.
.Weka Sulphonic Acid lita 1 kwenye beseni lako
.Weka sodium carbonate Lita 3
.Koroga kwa muda wa dakika kumi.
.Baada ya hapo weka Optical bright vijiko 6 vya chakula.
.Weka Nasa vijiko 16 vya chakula.
.Soda ash kilo 5
Malizia kwa kuweka perfume kiasi
Changanya mchanganyiko wako vizuri
.Baada ya mchanganyiko huo kuwa tayari anika kwenye kuvuli kwa kuwa juani inaweza kuyeyuka. Sabuni yako itakauka kwa kujiachia.Kusanya weka kwenye mifuko tayari kwa kuuza.
ONYO:Baadhi ya malighafi ni acid kwahiyo umakini unatakiwa wakati wa kutengeneza, hakikisha mikono yako imelindwa kwa gloves na usishike acids au kula wakati unafanya kazi.
...
....MATUNAINI YANGU UTAKUA UMEFULAIA

Tuesday, 27 November 2018

UTENGENEZAJI WA SODA

Utengenezaji Wa soda

Mahitaji

1* maji

2*sukari

3*rangi

4*phosphoric acid

5*ladha

🙏🙏🙏

JINSI YA KUANDAA BOGA/TANGO

Boga/ tango

Boga
Sukari utakisia
Hiliki kiasi
Tui utakisia
Custard powder utakisia mm nimetumia vijiko vidogo viwili.

Nimekata vipande vya kiasi boga langu na  kulimenya na kuondoa zile  mbegu za kati. Chukuwa sufuria  weka boga lako na maji kiduchu ili lipate kuiva kidogo kwa mvuke kabla hujaweka tui lako. Ukiona linaanza kuiva bado lina ubichi ubichi weka sukari hiliki na tuli lako hivyo vyote utakisia. Wacha lichemkie mpaka kuiva na kubakia tui kiasi ndio uchukuwe ile custard kidogo changanya na maji mimina kwenye mchanganyiko wako. Wacha tena lichemkie kidogo epua itakuwa tayar.  Subiri lipoe pakuwa tayar kwa kuliwa. Ukipenda utakunywa kwa uji au kutoelea na wali

MKATE WA MAYAI

*Mkate Wa Mayai*

Mkate Wa Mayai

Vipimo
·         Mayai 4
·         Sukari ¼  Kikombe
·         Unga wa Ngano Vijiko 5 ½ vya chakula
·         Hiliki ya kusaga ½  kijiko cha chai
·         Baking powder  ½  Kijiko cha chai
·         Zabibu kavu  ¼  kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Chukua bakuli la kiasi, weka sukari, hiliki na vunja juu yake mayai  yote manne.

Changanya sukari,  hiliki na mayai   kwa kutumia mashine ya kukorogea keki (cake mixer), mpaka sukari ivurugike yote na kuumuka.

Washa jiko lako (oven) 350F lianze kupata moto.
Weka baking powder kwenye unga na uanze kuuchanganya kidogo kidogo kwenye mchanganyiko  wa mayai na sukari. Hakikisha kila ukiweka unga kidogo unauchanganya vyema usiwe na madonge.
Mimina unga  ndani ya sufuria ya kuchomea keki ya kiasi.

Tupia zabibu  juu ya mchanganyiko wako.
Ingiza sufuria   ndani ya jiko (oven) kwa dakika 20 kisha utoe.

Uhakikishe mkate wako kama umeiva kwa kijiti cha kuchomea mshikaki au toothpick.

Ingiza kijiti  katikati ya mkate kisha kitoe na ukiguse uangalie kama kikavu mkate umeiva kama bado kuna ubichi basi rudisha mkate kwa dakika 5 nyingine kisha ukague.
Wacha mkate upoe kisha utoe ndani ya sufuria na uweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

KAMAITI YA SUKARI YA NJE

Kaimati za sukari ya nje

Maitaji

◾Sukari robo
◾Unga wa ngano nusu
◾Amira kijiko cha chai
◾Iliki kijiko cha chai nusu
◾Samli au mafuta yakukandia
◾Tui la nazi na maji yake ya Nazi

Matayarisho

chukua unga weka kwa bakuli  lako

chukua iliki yakusaga weka chukua samli weka au

mafuta chukua Amira iweke kwenye tui lako la nazi

liache kiasi anza kuchanganya unga hadi

uchanganyike tia tui kiasi changanya weka tena ikiwa

Lipo changanya tena ukiona umelainika vizuri weka

yale maji ya nazi chukua mwiko wakupikia sima anza

kuvurugia hadi uwe sawa usiwe mzito sana zikawa

na donge ndani wala usiwe mwembamba zikawa

nyepesi  uwe katikati utafutie maali uweke.

Chukua sufuria tia sukari tia maji kiasi bandika jikoni

iache ichemke hadi iive ambapo ukiishika kwa vidole

yanata ukiona ipo hivyo iepue angalia unga wako

umeumuka au ikiwa upo tayari bandika karai lako tia

mafuta mengi ili zichomeke vizuri yaache yapate

moto anza kuchoma hadi umalize.

ukimaliza zitiie kwenye sufuria bandika jikoni moto kiasi

chukua sukari zimwagilie anza kuzipepeta kiasi,

regesha jikoni hadi zishike sukari vizuri

Aandaa tayari kwa kuliwa

Monday, 26 November 2018

JINSI YA KUTENGENEZA KASHATA

-----KASHATA
Sukari kg 1
Nazi1
Njugu nusu na robo
Maziwa ya unga robo
Hiliki
Maji kikombe kimoja
Unaweka maji na sukari mpaka ichemke ikishachemka unatianazi uloikunana kuisaga ikisha unakoroga mpaka inakuwa nzito unatia njugu unakoroga mpaka ukeshaona karibu inakauka unatia maziwa pamoja na hiliki ikisha unaweka kwenye kibao chako ulotia mafuta unasukuma ikisha unakata tayari kwakuliwa na kahwa

Friday, 23 November 2018

JINSI YA KUTENGENEZA MAFUTAYA KUKUNZIA NYWELE NA KUONDOA MBA NA KUZIFANYA NYWELE KUWA LAINI

Mahitaji

1" mafuta ya mnyonyo

2*unga wa mbegu za parachichi

3*yai

4*unga wa muhogo

5*Unt bakteria.

  Utengenezaji

Andaa blenda kisha weka unga wa mbegu za mlonge

Kisha weka mayai 3 ya kuku wa kienyeji

Kisha saga na kupata mchanganyiko laini

Baada ya kuchanganya weka sefuria jikon na weka maji nusu Lita na weka unga wa muhogo vijiko 3 vya chakula kisha acha ichemke kwa muda kisha ipua

Baada ya hapo weka ule mchanganyiko ulikua kwenye blenda kwa kuchota vijiko 5 vya chakula

Baada ya hapo  mafuta ya mnyonyo ml.100

Koroga na utaweza kupata dawa laini na nzito

Paki katika Vifungashio na anza soko

Hukuza nywele na kuondoa mba na kufanya nywele kua laini

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO