Thursday, 14 March 2019

UTENGENEZAJI WA MISHUMAA YA KUUA MBU

*UTENGENEZAJI WA MISHUMAA YA KUUA MBU*

*MALIGHAFI*
1.PARAFFIN WAX
2.STERINE
3.BORIC ASID
4.MOULD(MAUMBO)
5.UZI (UTAMBI)
6.RANGI KAMA UKIPENDA
7.JIKO
8.SUFURIA

*MAANDALIZI*
andaa maumbo ya mshumaa kwa Jinsi unavopenda unaweza kutumia bati

andaa utambi kwa kuchukua boric asid vijiko vitano vya chakula changanya Na maji vijiko vinne vya chakula ,koroga kwa muda wa dakika tano, KISHA toa Na ANDIKA ili ukauke,sababu ya kufanya hivi ili utambi usiishe haraka wala kutoa moshi. Na hii ndio Kazi kubwa ya boric asid

*UANDAAJI WA MSHUMAA*

baadavya kuwa umeandaa maumbo Yako ya mshumaa chukua utambi wako Na uweke katikati ya mould Yako KISHA funga utambi wako juu ya chombo chako kwa kushikiza Na kijiti .kijiti kitakusaidia ili utambi usikae pembeni

Washa jiko Lako Na weka sufuria Yako jikoni chukua paraffin wax kilo moja ,sterine vijiko vinne,rangi kijiko kimoja cha chai, perfume kama ukipenda kijiko kimoja cha chai

wakati mchanganyiko wako unayeyuka koroga taratibu mpaka uchanganyike vizuri

Epua mchanganyiko wako Na anza kuweka kwenye maumbo Yako uliyoandaa kwa kuweka utambi ndani yake

weka sehemu ya kivuli ili mshumaa wako upate kuganda kwa urahisi ukisha ganda utoe taratibu kutoka katika hayo maumbo yake *BAADA YA HAPO MSHUMAA UTAKUWA TAYARI KWA MAUZO NA MATUMIZI YA NYUMBANI*

*NB:* SIMPRONELLA/CITRONELLA hii ni perfume Na pia ni dawa ya kuua mbu ko kama ukipenda mshumaa wa kuua mbu basi sehemu ya kuweka perfume weka aina hii

6 comments:

  1. Asante kwa maelezo mazuri Je naweza kupata wapi simpronella au Citronella?

    ReplyDelete
  2. Asante, sijafamu ni wapi inapatikana utambi maana nimeenda Sido hawana, pia na kwenye maduka wanayouza marigafi za wajasiriamali hawana pia ni wapi zapatikana?

    ReplyDelete
  3. Ahsante,lakini baadhi ya malighafi hazipatikani kama vile stearic acid na cintronela maeneo ya Mbeya je tunazipataje?

    ReplyDelete
  4. Mbona hakuna vipimo vya malighafi hizo jaman

    ReplyDelete
  5. Asante.
    Naweza kupata wapi maligafi, km: modu, utambi nk

    ReplyDelete
  6. Nataka kutoa ushuhuda kuhusu jinsi nilivyopona kutokana na Virusi vya Herpes. Miezi michache iliyopita nilikuwa na dalili kadhaa. Nilienda kumuona daktari na vipimo vingi vya damu vilifanywa kwangu, baadaye niliambiwa nilikuwa na Herpes. Daktari wangu aliniambia kwamba hakuna tiba ya Herpes. Nilijisikia vibaya, niliingia mtandaoni nikitafuta tiba inayowezekana ya Virusi vya Herpes, niliona chapisho la Dkt. Dawn, daktari wa mitishamba anayewasaidia watu kupona kutokana na Herpes. Saratani. VVU na mengineyo. Niliwasiliana naye na kumwambia jinsi ninavyohisi. Alisema dawa yake ya mitishamba inaweza kuniponya. Alinitumia dawa kupitia huduma ya utoaji wa UPS na nilipokea dawa siku 6 baada ya kuituma, nilichukua dawa kama alivyoniagiza. Kabla sijakamilisha dawa dalili zilisimama. Nilienda kwa daktari na kufanya kipimo kingine cha damu, cha kushangaza nilikuwa hasi. Sijapata dalili tena. Dkt. Dawn ni mzuri na unaweza
    kuwasiliana kwenye WhatsApp: +2349046229159
    Gmail ( dawnacuna314@gmail.com )

    Ikiwa unahitaji dawa za mitishamba kutibu magonjwa yoyote sugu au ya zinaa kama.
    HERPES.
    SARATANI.
    VVU/UKIMWI na zaidi

    ReplyDelete

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO