Friday, 27 July 2018

NAMNA YA KULAINISHA NGOZI

Namna ya kulainiasha ngozi yako👇

Utengenezaji

Andaa blenda kisha weka viazi mbatambata vikiwa vimemenywa kisha katakata vipande vidogo vidogo kisha saga katika blenda

Baada ya hapo weka katika bakuli kisha weka baking soda vijiko viwili vya chai koroga

Kisha acha kwa muda wa dakika kumi kisha jipake👇

Kama una ngozi yenye makovu,kavu,michirizi au ilio jikunja tumia dawa hii

DAWA YA KUREKEBISHA USO

Dawa ya ajabu katika uso

Utengenezaji wa dawa ya kuondoa chunusi na kukupa muonekano mzuri wa kisura

Chukua mualovera kisha kamua maji yake tu upate robo Lita

Chukua binzari au manjano ya Unga

Baada ya hapo weka binzari vijiko viwili vya chakula kisha weka mualovera robo Lita anza kukoroga kupata mchanganyiko safi na mzuri acha kwa dakika 5

Baada ya hapo paka usoni kisha acha kwa masaa 3 kisha unawe Fanya kwa siku 7

Wednesday, 25 July 2018

UTENGENEZAJI WA ROSENI

Utengenezaji wa rosheni👇

Maligahafi
1*microwax
2*griselini
3*manukato ya mafuta
4*rangi ya mafuta
5.olive oil au asali

Utengenezaji

Andaa sefuria kisha weka jikoni hakikisha una moto wa wastani

Baada ya kuweka sefuria jikoni acha ipate moto kisha weka microwax nusu kilo acha iyeyuke

Baada ya hapo weka gliselini Lita moja acha iyeyuke

Baada ya hapo weka mafuta ya oliva oil au asali vijiko vinne vya chakula acha ipate moto

Ukiona inakua ya moto ipua na uweke manukato na rangi kiasi upendacho na koroga kwa dakika moja kupata mchanganyiko sawa

Baada ya hapo usisubiri kupoa weka katika vifungashio vyako acha ipoe ikiwa katika vifungashio

Baada ya kupoa tayari kwa matumizi

Friday, 13 July 2018

RATIBA NA CHANJO KWA VIFARANGA WA ASILI YA KIENYEJI

Fahamu ratiba na chanjo kwa vifaranga wa Asili ya kienyeji kama ifatavyo.

siku 1-5 --dawa ya kufunga vitovu-
siku 7 --NEWCASTLE
siku 8, 9,10,11--VITAMIN
siku 14--Gomboro
Siku ya 15-20-VITAMIN
siku 21--gomboro Baada ya hapo endelea na vitamin hadi siku ya 27
Siku ya 28-NEWCASTLE Kisha endelea na vitamin
wiki ya 5 chanjo ya ndui
wiki ya 6--Ampronium + ctc (siku tano)
wiki ya 7--Vitamin
wiki ya 8--dawa ya minyoo

FOMULA YA UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI

Fomula Ya Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Kienyeji.
Watu wengi wamekuwa wakijaribu ufugaji wa kuku na kushindwa mara kwa mara. Hii inatokana na kuto kuzingatia na kufuata fomula sahihi ya ufugaji wa kuku hawa. Hapa naelezea kwa ufupi, njia nzuri ya kufuata katika ufugaji wa kuku, ili uweze kufanikiwa katika biashara hii.
Kuku wa kienyeji ni wazuri kwa ufugaji kwa sababu: Wanavumilia sana magonjwa, Ni rahisi kuwahudumia, Chakula chao ni cha bei ya chini, Wavumilivu wa hali tofauti za hewa, Hawahitaji uangalizi wa karibu, na soko lake ni kubwa sana na bei nzuri (Mayai trei moja SHs 10,000 mpaka 15,000, kuku wakubwa wanaanzia SHs 15,000 mpaka 30,000). Hii haimaanishi kwamba, uwaache kuku bila uangalizi, kwani nao hupata magonjwa kama wasipo patiwa chanjo sahihi, hupungua uzito na uzalishaji mayai hushuka kama wasipo patiwa chakula chenye virutubisho vyote. Hapa naelezea vitu muhimu katika hii formula ya ufugaji kuku wa kienyeji kwa mafanikio:
1. Aina ya kuku: Chagua aina ya kuku wenye uwezo wa kutaga mayai mengi na wakati huohuo, kuzalisha nyama nyingi. Hii itakupa faida kote, kwenye upande wa nyama na upande wa mayai. Kuku hawa wanajulikana kama Chotara, wanatabia sawa na kuku wa kienyeji wenye asili ya Tanzania wanaopatikana maeneo mengi nchini; kutokana na uvumilivu wao wa magonjwa na hali tofauti za mazingira. Pia wanauwezo wa kutaga mayai mengi (Wastani wa mayai matano kwa wiki) karibu sawa na kuku wa kizungu. Aina ya kuku hawa ni kama vile, Chotara wekundu (Rhode Island Red), Black Australorp (Weusi/Malawi), Barred Plymouth Rocks (Madoa), New Hamshire Red, Kuroila wanapatikana sana Uganda, na Kari kutoka Kenya. Hizi ni aina ya kuku zinazo patikana Tanzania.
2. Chanjo: Kama nilivyosema mwanzo, kuku wa kienyeji ni wavumilivu wa magonjwa lakini si kwamba hawayapati, kuna magonjwa ambayo ni hatari pia kwa kuku wa kienyeji. Chanjo ni muhimu kuwaepusha na hatari ya kuyapata magonjwa haya. Chanjo muhimu kwa kuku wa kienyeji ni; New Castle, Gumboro, Marek’s na Ndui ya kuku. Fuata utaratibu wa chanjo kutokana na ushauri wa daktari. Nitawaletea pia makala ya magonjwa na chanjo hivi karibuni.
3. Chakula: Kuku wa kienyeji pia wanahitaji mchanganyiko sahihi wa chakula, ili waweze kukupatia mazao mengi na bora, na kuwaepusha na magonjwa. Zipo fomula mbalimbali za chakula kutokana na umri wa kuku, na aina ya kuku. Kuku wote wanahitaji chakula chenye mchanganyiko sahihi wa Madini, Vitamini, Protini, Fats, Wanga, Vyakula vya kulinda mwili ili usipatwe na maradhi, na Maji safi. Muhimu kuwapatia kuku majani kama ziada ya chakula, hii hupunguza gharama za chakula na kuwafanya kuku waonekane wenye afya bora. Ni vizuri kuwapatia vifaranga chakula spesheli cha dukani kama huna ujuzi wa kutengeneza mwenyewe. Kwani vifaranga wengi hufa kutokana na kutokupata chakula chenye mchanganyiko sahihi kwao. Kuku wa mayai pia wanahitaji mchanganyiko sahihi ili waweze kutaga mayai kwa wingi.
4. Banda: Kuku wa kienyeji pia, wanahitaji banda au nyumba ya kuku imara ili kuweza kuwakinga na baridi kali, wanyama hatari, na wizi. Banda pia liwe na semu nzuri za kutagia na sehemu za kulala ziwe juu , kwani kuku hupendelea kulala juu. Ni muhimu banda liwe katika hali ya usafi muda wote. Kwa hivyo ni vizuri linyanyuliwe juu kidogo ili kuruhusu uchafu kuanguka chini na lijengwe ka kutumia mbao, mabanzi, milunda, nyavu, na mabati. Vifaranga wanahitaji kutenganishwa na kuku wakubwa. Banda si lazima liwe la gharama kubwa, kwani mafanikio ya ufugaji wa kuku ni vile unavyo waangalia na si banda. Mada inayohusu mabanda bora ya kuku itakuja hivi karibuni.
5. Majogoo kwa majike: Ili mayai mengi yaweze kutotolewa, ni vizuri jogoo mmoja aweze kuwahudumia majike wasio zidi 7. Kwani kuku wanaweza kutaga bila ya jogoo, lakini mayai hayatoweza kuleta kifaranga. Ili mayai yalete vifaranga ni lazima yawe yamerutubishwa (Fertilized eggs) na jogoo. Kwa hivyo ni vizuri kuweka Jogoo 1 kwa majike 7, hivyohivyo Jogoo 2 majike 14, Jogoo 3 majike 21, n.k. Pia hakikisha kuku wanao tumika kuendeleza kizazi ni wale wenye afya bora.
6. Vyombo vya chakula: Hakikisha vyombo vya chakula ni visafi na vinawatosheleza kuku wote. Vyombo hivi ni vizuri vifanyiwe usafi wa mara kwa mara, ili kuwaepusha kuku na magonjwa. Maji machafu huwa ni chanzo kikuu cha magonjwa hasa ya kuhara. Hakikisha kuku wako wanabadilishiwa maji angalau mara mbili kwa siku.

FAIDA ZA KUROILER

OFA ] ONGEZA KIPATO FUGA  KUROILER!!!!

Sifa na Ubora wa KUROILER.

1. Wanakua kwa haraka.
2. Wana Uzito Mkubwa 3.5-5kg
3. Wanataga sana
4. Mayai yao yanauwezo wa Kutotoleka kwani yana mbegu 95%
5. Wana uwezo mkubwa wa Kuvumilia Magonjwa.
6. Unaweza kuwafuga katika eneo lolote, lenye Baridi au Joto.
7. Hukua Zaidi ukilinganisha na breed nyingine.
8. Hufugwa kwa Nyama na Mayai.

KUROILER

1. Wanataga sana
2. Wanakua kwa haraka sana
3. Soko lake ni la uhakika kwa mayai na nyama
4. Nyama yake ni laini na tamu
5.Wanastahimili magonjwa
6. Wanafugwa kienyeji

UTAMBUZI WA MAGONJWA YA KUKU KUPITIA RANGI YA KINYESI

UTAMBUZI WA MAGONJWA YA KUKU KUPITIA RANGI YA KINYESI

1. MHARO MWEUPE (pullorum bacilary diarrhoea)
ugonjwa huu huathiri zaidi vifaranga  kabla ya wiki nne
huharisha mharo mweupe,
TIBA kuu ni usafi pekee kwenye banda na kuepusha maji yasimwagike ovyo.

2.KIPINDUPINDU CHA KUKU(fowl cholera)
kinyesi cha kuku ni njano
tumia dawa za salfa, eg Esb3 au amprollium

3.COCCIDIOSIS
mwanzo kinyesi cha kijivu na baadae huharisha damu iliyochanganyika
Tumia dawa ya VITACOX au ANTICOX

4.MDONDO(Newcastle)
kuku hunya kinyesi cha kijani
sio kila kijani ni newcastle
HAKUNA TIBA

5.TYPHOID
Kinyesi cheupe
kinagandia sehemu za nyuma au hulowana sehemu za haja
dawa ni Eb3

6.GUMBORO
Huathiri zaidi vifaranga
kinyesi huwa ni majimaji
Dawa hakuna
tumia vitamini na antibiotic kupunguza magonjwa mengine nyemelezi.

MABANDA BORA YA KUKU

MABANDA BORA YA KUKU (PART 3)
.
.
PAA LA BANDA:
Paa la banda liwe madhubuti ili kuzuia maji ya mvua kuingia hasa wakati wa masika. Sakafu ya banda iwe juu zaidi ya usawa wa nje. Paa linaweza kuezekwa kwa mabaki ya vipande vya bati , madebe na kama ikishindikana tumia nyasi zinazofaa kwa ajili ya kuezeka nyumba katika eneo hilo.
.
.
MATANDIKO
Nilazima kuweka matandio katika sakafu ya banda la kuku. Sehemu ambayo kukuwakubwa wanaweza kutagia. Ni vizuri kutumia maranda, na si Pumba zinazo tokana na mbao
Kuku wanaweza kula pumba za mbao. Kwa kuku wanaohatamia, vipande vidogo na vilaini vya miti na makapi kama vile pumba za mpunga zinaweza kutumika
.
.
NAFASI YA KUFANYA KAZI:
Banda la kuku lisiwe na nguzo au mbao nyingi sana ndani kiasi cha kumfanya mhudumiaji wa kuku ashindwe kufanya kazi zake. Hali hiyo itamfanya apoteze muda mwingi katika kuzizunguka nguzo hizo, hasa wakati wa kuokota mayai au kufanya usafi.

MCHANGANUO WA TSH 300,000/=(LAKI TATU) KWA KUANZISHA MTAJI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI

MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MTADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.
Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka.

Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.

Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula.

Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.
Mchanganuo Wa 69500 ni:-

Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.

- paraza kilo 25 = 700x25 =17500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.

-mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500
- layer's consetraite
Kilo 25 kifuko. = 21500.

Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.
Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.

Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku

Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300.
Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.

TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.
Mchanganuo wake
Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000.
Jogoo 1 = 20000
Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
Itakuwa imebaki shs. 60500

-Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga

Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.
Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4.

Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.

Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000.
Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200.

Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe.

Nikiwa na maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua C1hakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.

Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.

JINSI YA KUPATA FAIDA KWA KUZALISHA MAYAI KUKU WA KIENYEJI

JINSI YA KUPATA FAIDA KUBWA KWA KUZALISHA MAYAI  KUKU WA KIENYEJI

Utangulizi
Kupata Mayai ya Kienyeji fresh ni moja ya faida kubwa ya kufuga kuku wa Kienyeji. Pia Mayai haya ni Biashara nzuri, ambayo kama itafanywa kiusahihi, inaweza kurudisha mtaji wako haraka na kukupa faida nzuri.

Kama unapanga kuanza au umeshaanza Ufugaji wa kuku wa Kienyeji kwa lengo la kufanya biashara ya mayai, unatakiwa kuelewa kwamba, kama zilivyo biashara nyingine, vitu utakavyovitumia kwenye biashara (mfano, chakula, maji na nguvukazi) ni gharama zako, na mayai ni mapato yako.

Ili kupata mapato mazuri (mayai mengi), unatakiwa kujua uwezo wa utagaji wa kuku wako, na pia ujue vitu vingine vinavyochangia kuathiri uzalishaji wa mayai.

Kuku anaweza kutaga yai moja tu kwa siku, na kuna siku ambazo hatataga kabisa. Inachukua muda wa saa 26 kwa mwili wa kuku kutengeneza yai.

Kuku 1000 wanaweza kutaga mayai 700 - 800 kwa siku, wakifikia kiwango cha juu cha utagaji (mature egg laying cycle).

Vitu vinavyoweza kupunguza utagaji wa kuku wako ni pamoja na chakula, maji safi, hali ya hewa, ukosefu wa mwanga wa jua na umri wa kuku wako. Kuku wengi hutaga kiwango cha juu kwa mwaka mmoja, kisha wanaanza kupunguza utagaji taratibu.

Kuku wa Kienyeji wanaanza kutaga wakiwa na miezi 5. Unaweza kununua kuku wanaokaribia kutaga kama kuna sehemu ya kuaminika wanapofuga vizuri, na utaanza kupata mayai mapema. Au nunua vifaranga na uvikuze wewe mwenyewe (njia hii ni nzuri zaidi).

Idadi ya mayai unayoweza kupata na idadi ya miaka kuku wako watataga mayai, inategemeana na:
1. Aina ya kuku
2. Utunzaji wa vifaranga na mitemba (kabla hawajaanza kutaga)
3. Utayarishaji wa banda la kutagia
4. Usafi wa banda
5. Joto na unyevunyevu
6. Mwanga
7. Chakula na maji

Katika siku zijazo tutachambua kitu kimoja kimoja kinachoathiri utagaji wa kuku.

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO