JINSI YA KUPATA FAIDA KUBWA KWA KUZALISHA MAYAI KUKU WA KIENYEJI
Utangulizi
Kupata Mayai ya Kienyeji fresh ni moja ya faida kubwa ya kufuga kuku wa Kienyeji. Pia Mayai haya ni Biashara nzuri, ambayo kama itafanywa kiusahihi, inaweza kurudisha mtaji wako haraka na kukupa faida nzuri.
Kama unapanga kuanza au umeshaanza Ufugaji wa kuku wa Kienyeji kwa lengo la kufanya biashara ya mayai, unatakiwa kuelewa kwamba, kama zilivyo biashara nyingine, vitu utakavyovitumia kwenye biashara (mfano, chakula, maji na nguvukazi) ni gharama zako, na mayai ni mapato yako.
Ili kupata mapato mazuri (mayai mengi), unatakiwa kujua uwezo wa utagaji wa kuku wako, na pia ujue vitu vingine vinavyochangia kuathiri uzalishaji wa mayai.
Kuku anaweza kutaga yai moja tu kwa siku, na kuna siku ambazo hatataga kabisa. Inachukua muda wa saa 26 kwa mwili wa kuku kutengeneza yai.
Kuku 1000 wanaweza kutaga mayai 700 - 800 kwa siku, wakifikia kiwango cha juu cha utagaji (mature egg laying cycle).
Vitu vinavyoweza kupunguza utagaji wa kuku wako ni pamoja na chakula, maji safi, hali ya hewa, ukosefu wa mwanga wa jua na umri wa kuku wako. Kuku wengi hutaga kiwango cha juu kwa mwaka mmoja, kisha wanaanza kupunguza utagaji taratibu.
Kuku wa Kienyeji wanaanza kutaga wakiwa na miezi 5. Unaweza kununua kuku wanaokaribia kutaga kama kuna sehemu ya kuaminika wanapofuga vizuri, na utaanza kupata mayai mapema. Au nunua vifaranga na uvikuze wewe mwenyewe (njia hii ni nzuri zaidi).
Idadi ya mayai unayoweza kupata na idadi ya miaka kuku wako watataga mayai, inategemeana na:
1. Aina ya kuku
2. Utunzaji wa vifaranga na mitemba (kabla hawajaanza kutaga)
3. Utayarishaji wa banda la kutagia
4. Usafi wa banda
5. Joto na unyevunyevu
6. Mwanga
7. Chakula na maji
Katika siku zijazo tutachambua kitu kimoja kimoja kinachoathiri utagaji wa kuku.
No comments:
Post a Comment