KILIMO CHA DENGU ,FAIDA NA SOKO LAKE
Utangulizi
Dengu ni nafaka kama zilivyo nafaka zingine, ni zao la jamii ya mikunde pia ni zao la biashara, ni miogoni Mwa zao muhimu sana la biashara ukanda wa ziwa kwa sababu ya thamani yake Kuwa juu sana, zao hili hutumika pia kama zao la chakula kama mbonga , mchaganyo wa wali mseto , makande , kutegeneza Bagia , chiichiri namengineyo mengi. Kanda ya ziwa hili ndiyo Zao llinalotegenewa zaidi likiogozwa na zao la choroko kwa kuwa na thamani kubwa, hivyo zao hili nizao muhimu kwa uchumi wa wanakanda ya ziwa.
HATUA MUHIMU KATIKA KILIMO CHAKE
Kilimo cha ndegu ni kilimo rahisi sana hakina usubufu sana kama yalivyo mazao mengine hasa ukifata utaratibu wa hatua za mwanzo
Mambo ya kuzingatia
1. Kuwa makini na hali ya hewa ya mwaka husika kwa kuangalia ukame katika mbuga utaaisha lini pia hali ya mvua ikoje kwa maana kuwa msimu wa kulima huwa mwezi wa tatu mwishoni kwenye maeneo ambayo mbuga huwahi kukauka mapema yaani muda huo ndiyo watu huanza kuandaa shamba kwa kulilima mara ya kwanza kama hatua ya kukiandaa shamba pia hatua hii hufanyika mwenzi nne lakini iwe kwenye kumbukumbu sahihi kuwa ndegu kwa hali ya uzuri kabisa hulimwa mwezi nne na mwanzoni kabisa mwa mwezi wa tano kabla mbuga hazichakauka .
2 Uchaguzi wa Mbengu, mbengu bora za dengu ni muhimu kuzifahamu na kuzitumia katika kilimo hiki
Ziko mbengu ambazo hazihimili magonjwa lakini zipo zinazohimili magonjwa na zinakuwa na uzito hii husaidia katika swala la uuzaji kwa maana ya kuwa mara nyungi dengu kwa sasa huuzwa kwa kilo ili mkulima apate faida zaidi
3 Baada ya kulima mara ya kwanza kama kuliandaa shamba unapaswa kulima mara ya pili na kupanda mbengu kwa kufata misitari au kufata tumba au vitalu au misingi itakayokuwa imeadaliwa
4 Hakikisha dengu unapanda katika mbunga isiyo na maji yaliyotuama , unyevunyevu wa udogo wa shambani ndiyo hitaji muhimu la uoteshaji dengu hairuhusiwi kabisa kupanda dengu kwenye shamba lenye maji
5 Ardhi inayofaa kwenye kilimo cha dengu ni shamba nyeusi au udongo mweusi ambao hutumika pia katika kilimo cha mpunga, mahidi, choroko na mengineyo .
6 Baada ya dengu kuota hakijisha hakuna maji yaliyotwama katika shamba lako
7 katika ulimaji wa dengu palizi haina ulazima mara nyingi dengu haina palizi kabisa ukizigatia hatua za mwanzo za uandaaji wa shamba
8. Dengu hutumia miezi mitatu mpaka kuvuna hivyo inajulazimu kusubiri ikauke mpaka hali ujano itokee kwenye mmea, mavuno ya dengu mara zato hufanyika kwa kung'oa mmea wote na kukusanya sample dogodogo ili kumaliza mapema mavuno yake baada ya hatua hiyo unaleta mkokoteni shambani unajusanya kwa mkokoteni nakupeleka sehemu kavu iliyosafi kwa ajili ya kutoa maganda ya zao la dengu,hatua ya kutoa maganda ya dengu inaweza fanyika kwa kienyeji kwa kupiga na miti au ikatumika kwa kitaalamu kwa kupiga na Tractor yaan tractor inapita kwa mzuguko kwenye navuno ya dengu yaliyosambazwa mpaka kuputua maganda ya juu ya dengu na kubaki dengu yenyewe tayari kwa biashara au kukoborewa tena kwa chakula
9 Uhifadhi wa zao la dengu
Hauna chagamoto sana japo hushambuliwa na wadudu baada ya miezi mitatu bila kuweka dawa unapaswa kuhifadhi kwenye eneo la wazi yaan kama ni chumba kiwe na uwazi wa hewa ya kutosha lakini pia kunagunia special nitazieleza kwenye utatuzi wa chagamoto.
CHAGAMOTO KATIKA KILIMO CHA DENGU
zipo chagamoto kadhaa katika kilimo cha dengu kama ifatavyo
1. Wakati wa kupanda huwa kunachagamoto ya mvua ambazo hujitokeza na kuharibu zao la dengu kwa kisukuma tunaita SHIBOJA yaani mvua za kuozesha dengu chagamoto hiyo ikijitokeza subiri maji yakauke katia mbengu upya kama zao limeathiriwa kidogo kama limeathiriwa sana unarudia shamba lote
2 Chagamoto ya Funza baada ya mmea kutoa maua . mmea ukitoa maua funza hushambulia kwa kasi kama eneo hilo liko na funza tiba ya funza hao nikupulizia dawa unaenda duka la kilimo watakupatia
3 chagamoto ya wadudu wakati wakati mmea unatoa zao lenyewe
Wakati huu pia unapulizizia dawa kama wakijitokeza
Jambo la funza na wadudu hujitokeza mara chache sana hivyo ni vyema kuwa na.tahadhali hiyo.
4 chagamoto ya panya
Panya hujitokeza kwenye shamba wakati zao
Linaanza kukomaa wao hutafuna dengu kamili hivyo unaweza jikuta unapata hasara wakati dengu zilisitawi vyema
Utatuzi wa chagamoto hiyo ni kuwatega panya kwa sumu kwa ukanda wa mkoa wa shinyanga serikali hutoa dawa nasi huchaganya na mahidi nakusambaza pembezoni mwa shamba maana panya hutokea kwenye nyasi hivyo watakutana na mahidi nakuyala .
Chagamoto nyingine ni za masika unaweza lima mwishoni sana kwenye mavuno ukakutana na mvua
5 chagamoto ya uhifadhi
Hapo kunachagamoto ya kushambuliwa na wadudu ndani ya miezi mitatu ya mwanzo unashauriwa kuhifadhi kwenye magunia nasiyo mifuko ya plastic
Unashauriwa kutia dawa inaitwa AKTERIA mapema kabisa unapohifadhi kama unahifadhi kwa muda mrefu baada ya miezi mitatu unatia tena
Au unaweza hifadhi kwaifuko maalumu ambayo imetiwa dawa kabisa na dani inajuwa kama mfuko wa sukari na upaswa kuifuga kitaalamu kama maeelekezo yalivyo .
Chagamoto nyingine ni ya soko naieleza hapa chini na utatuzi wake
MAVUNO NA SOKO LA DENGU
Mavuno ya dengu kwa heka yanaweza kuwa gunia 6,5,4
Inategemeana na eneo ulilolima linarutuba kiasi ngani na umefata taratibu zote.
Soko la dengu ni la uhakika sana kwa maana ya uhitaji wa dengu katika soko la ndani na nje
Dengu ndiyo zao ambalo mkulima wa mkoa wa shinyanga na niko jirani hulitegemea kwa kipato cha juu
Mfano halisi
Dengu gunia moja huuuzwa mpaka sh 250,000 /= , 200,000/=
180,000/= 150,000/=
Hizo ndiyo mbei za gunia la dengu
Lakini bei hizo hutegemea msimu au mnunuzi na muuzaji .
Pia gunia linakuwa na debe sita
Ukitaka kuuza kwa kilo
Misimu hutofautina wastani wa bei ni 1000 mpaka 1800 kwa kg 1 ya dengu
Gunia moja huwa lina chukua kg 120 au zaidi inategeena na upimaji namakubaliano ya muuzaji na mnunuaji
Msimu wa kulima ni baada ya mvua za masika dengu haihitaji maji walamvua only humidity.
Asante Sana ndgu kwa maelezo na ufafanuzi mzuri juu ya hiki kilimo Cha dengu binafsi nimevutiwa Sana tafadhali Kama hutojali nipigie kwa 0767212612 ili niweze pata mwongozo zaidi kuhusu zao.
ReplyDeleteufafanuzi wako upo vizur na nimependa hasa juu ya kutufungua fikra zetu juu ya swala zima la kilimo hiki cha dengu
ReplyDelete