📎TIPS KUMI ZA KEKI:-
1. Kuoka ni sayansi hivyo ni muhimu Sana kuzingatia vipimo,hakikisha unapima kwa usahihi kila hitaji lako usiongeze wala kupunguza hitaji muhimu hasa unapojaribu kwa Mara ya kwanza
2. Hakikisha umepima kila kitu mezani kabla ya kuanza upishi wa keki,zoezi la keki ni la haraka ili kuepusha keki kuanza kuumuka kabla ya kuingia katika oven na hatimaye kupata matokeo mabaya. Pia hakikisha oven umewasha tayari inapata moto.
3. Pendelea zaidi kuchekecha unga wako ili upate keki nyepesi na ya kuchambuka vizuri.
3. Paka chombo chako mafuta kisha nyunyiza unga ili kurahisisha keki kutoka kwa urahisi bila kushika kwa pan au zungusha kwa karatasi ya kuokea
3. Pendelea zaidi kutumia mwiko au spatula wakati wa kutia unga ili kuepusha kupiga Sana na kuua nguvu ya baking powder, NA kama utatumia machine basi changanya kwa speed ndogo kabisa.
4. Usifungue oven yako kabla ya nusu saa ya uokaji ,ikiingia hewa wakati keki bado mbichi itanywea na kutoiva vizuri. Angalia maendeleo ya keki yako kupitia kioo cha oven yako. Kufungua fungua oven kunathiri pia moto na kuharibu keki yako
5. Acha keki ipoe katika chombo chake kwa muda wa dk 10 kisha itoe iache ipoe kabisa kabla ya kukata au kupamba. Usiache keki ipoe katika pan moja kwa moja itatengeneza unyevu na hatimaye kusumbua kutoka wakati wa kutoa..keki unazoweza kuacha zipo katika chombo chake ni zile sticky au keki za kunata zenye matunda,asali nk pia coffee cakes ambazo zinakatwa zikiwa katika chombo chake.
6. Itie keki katika freezer kwa muda wa dk 15 ikiwa wataka kuipamba itakurahisisha kupamba kwa urahisi bila kupata crumbs nyingi.
7. Zingatia moto usiwe mkali wala mdogo, moto ukiwa mkali keki itaiva kwa haraka na kupasuka pia itakuwa kavu haiwezi kuchambuka na moto ukiwa mdogo itanywea na kuiva kwa kunata ndani hivyo zingatia Sana moto. Usitegemee Sana motmaswali
ndikwa katika recipe oven zinatofautiana pima kujua moto upi sahihi kwako
8. Tumia chombo kinachoendana na kipimo cha keki yako usitumie chombo kikubwa Sana keki itaiva kwa kusambaa na kutopanda vizuri pia usitumie chombo kidogo itaiva kwa kujibana na matokeo yake kupasuka na kutochambuka vizuri.
9. Ili kujua keki yako imeaiva wakati wa kuitoa chukua kiniti safi choma Kati kikitoka safi basi keki imeiva au ibinye kwa vidole ukiona yarudi usawa basi keki imeiva pia ukiona imeachia kidogo pembezoni ni moja ya ishara ya keki kuiva.
10. Keki ikiwa imepata rangi Sana juu na bado haijaiva usipate wasi chukua kipande cha alminium foil kinachotoshea chombo chako ,paka mafuta au siagi ule upande utakaofunika kisha funika keki yako acha iendelee kuiva bila kuungua juu
No comments:
Post a Comment