UTUNZAJI WA VITOTO VYA NGURUWE.
Ulishaji wa maziwa ya kwanza
Baada ya kuzaliwa na kusafishwa, hakikisha vitoto vinanyonyeshwa.Vitovu viwekewedawa (Iodine 5%) ili kuzuia magonjwa. Kama mama amefariki mara tu baada ya kuzaa na hakuna nguruwe mwingine anayeweza kunyonyesha; tumia maziwa ya ng'ombe. ongeza sukari na yai bichi koroga na uwanyonyeshe kwa kutumia chupa ya maziwa ya mtoto.
Joto
Vitoto vya nguruwe havizaliwi na manyoya na hawana mafuta mengi ya kutosha kuwaletea joto mwilini; hivyo ni rahisi kufa kwa baridi. Tumia taa ya stimu au chemli kuongeza joto.
Kuzuia upungufu wa damu
Maziwa ya nguruwe yana upungufu wa madini ya chuma yaongezayo damu. Hivyo baada ya majuma mawili au matatu watoto huanza udhoofu kwa kukosa madini hayo mwilini. Kuondoa tatizo hili inabidi vitoto vidungwe sindano ya madini kwenye misuli siku mbili au tatu tangu kuzaliwa. Kama sindano haipatikani njia nyingine za kuwapatia watoto madini hayo ni kwa kuwapa vidonge vya madini chuma, au kuwapa madini hayo kwenye dimi zao au chuchu za mama yao siku mbila hadi tatu baada ya kuzaliwa.
Ukataji meno
Siku chache kabla ya kuzaliwa, meno yaliochongoka • Meno hayo humuumiza mama wakati watoto wanapo nyonya mama hupiga mateke. Hii husababisha vifo vya watoto kutokana na kuumia inabidi meno hayo yakatwe na chombo kinachofanana kupunguza madhara hayo.
Kulisha chakula cha ziada
Chakula kigumu zaidi ya maziwa kianze kulishwa kidogo kidogo kuanzia siku ya kumi baada ya kuzaliwa, kwani wakati huu maziwa ya mama hayatoshelezi. Endelea kuwapa chakula hiki mpaka watakapo zoea kutokunywa maziwa ya mama yao tena. Chakula hiki kiwe na viini lishe vya kujenga mwili, kuleta nguvu na kuzui maradhi. Nguruwe wapewe chakula hiki kwa wingi na maji ya kutosha.
Kuachisha kunyonyesha
• Viachishe vitoto kunyonya wakifikia umri wa miezi miwili wanapokuwa na uzito wa kilo 10.
• Siku ya kuachisha kunyoyesha muondoe mama nguruwe kwa watoto wake na kumuweka chumba kingine
• Mpe mama chakula cha kutosha
7. Vyakula na ulishaji
Chakula bora kwa nguruwe ni moja ya mahitaji muhimu sana kwenye dhana nzima ya ufugaji wa nguruwe wenye tija na faida kwa mfugaji. Chakula cha nguruwe kinagharimu yapata asilimia hamsini sabini ya gharama zote za ufugaji wa nguruwe. Kati ya matatizo mengi yanayosababisha tija na ufanisi duni wa uzalishaji wa nguruwe yanatokana na lishe duni. Nguruwe wakipatiwa lishe bora, tija na ufanisi wa uzalishaji utakuwa mkubwa hivyo kuongeza faida kwa mfugaji.
Tukakushauri utumie *Hydroponic fodder* itakusaidia Sana wewe mfugaji kupunguza gharama za chakula pia ni lishe nzuri Sana itakayo wafanya Nguruwe wako waongezeke kilo kwa muda mfupi sana hasa wadogo.
Baadhi ya faida za lishe bora kwa nguruwe ni:
1. Lishe bora huharakisha ukuaji wa haraka wa nguruwe na hivyo kupata uzito unaohitajika kwa kipindi kifupi .
2. Lishe bora hupunguza gharama za ufugaji na hivyo kuongeza faida kwa mfugaji kwa sababu nguruwe atahitaji kiasi kidogo tu cha chakula na atachukua muda mfupi kupata uzito mkubwa
3. Lishe bora itapunguza maambukizi ya magonjwa.
4. Lishe bora huongeza kiasi cha mayai yatakayoivi shwa na mama nguruwe na hivyo kuongeza idadi ya watoto watakaozaliwa
5. Lishe bora huongeza kiasi cha maziwa yatakayotengenezwa na mama nguruwe kwa ajili ya watoto hivyo kuwafanya wawe na afya bora itakayo wawezesha wakue haraka na kupunguza idadi ya vifo kwa watoto.
6. Lishe bora inaongeza ufanisi wa madume ya nguruwe na hivyo kuongeza uwezo wa kupanda
Viini lishe muhimu kwenye lishe ya nguruwe
Nguruwe wana uwezo wa kula aina nyingi za vyakula lakini vyenye uwezo wa kumeng'enywa kwa urahisi. Chakula cha nguruwe kilichokamilika kinahitaji kuwa na mchanganyiko wa viini lishe vitano, navyo ni
1. Vyakula vyenye kutia nguvu mwilini (kama pumba za mahindi, ngano, mchele)
2. Vyakula vya kujenga mwili (kama mashudu ya alizeti, pamba, unga wa dagaa)
3. Vyakula vya asili ya madini (kama chumvi, chokaa, mifupa iliosagwa)
4. Vyakula vya asili ya vitamini (kama majani mabichi Hydroponic, mbogamboga na matunda)
5. Maji
No comments:
Post a Comment