UFUGAJI WA NGURUWE (KISASA)
Upate wapi Nguruwe wa Kufuga
Nunua nguruwe wa kufuga kutoka kwenye mashamba au watu binafsi wanaoaminika ukizingatia yafuatayo.
• Usizalishe nguruwe wanaotokana na ukoo mmoja yaani ndugu kama kaka na dada. Nunua dume najike toka mahali tofauti.
• Tumia ushauri wa wataalamu kuchagua Nguruwe bora
Sifa za kuangalia kwa nguruwe bora wa mbegu:
• Nguruwe wa mbegu awe na sifa ya kukua haraka na asiwe na ulemavu wa aina yeyote, na hasa wa miguu kwa dume.
• Mama mzazi wa nguruwe awe na historia ya kuzaa watoto 10 hadi 12 kwa mzao mmoja
• Jike awe na chuchu zaidi ya 12.
• Dume awe na sehemu za kiume yaani korodani na uume unaoonekana sawa sawa. Pia awe na hamu ya kupanda majike.
Mbinu za uzalishaji
Matunzo ya dome la uzalishaji
• Chagua dume la mbegu bora, lisilokuwa na kilema au ugonjwa wowote. Tenganisha dume na majike iii kuepusha kupandwa kusiko na kumbukumbu. Dume la nguruwe halipaswi kunenepa, kwa hiyo usimlishe chakula kingi na mpatie mazoezi ya kutosha asije akawa mvivu
• Nguruwe dume anaanza kupanda majike akiwa na umri wa miezi 4 hadi miezi 9. Dume liruhusiwe kupanda mara moja tu kwa kila juma. Anapofika miezi 10 anaweza kupanda mara mbili hadi mara tatu kwa wiki. Akiwa na mwaka mmoja na zaidi anaweza kupanda kila siku kwa majuma mawili hadi matatu, kisha apumzike kwa majuma mawili. Ni vizuri nguruwe dume mmoja apande majike 15 hadi 20 kwa mwaka.
• Madume madogo yapande majike madogo, dume kubwa likimpanda jike dogo anaweza akamletea maradhi ya mgongo. Ni muhimu kupandisha dume kabla hajala chakula, na asitumiwe mara tu baada ya chakula ili asiwe mvivu.
Utunzaji nguruwe mwenye mimba
• Mimba ya nguruwe huchukuwa miezi mitatu (3) wiki tatu(3) na siku tatu(3) yaani siku 114
• Nguruwe mwenye mimba apewe chakula cha kutosha kiongezwe polepole tokea posho ya kawaida hadi kilo 3 - 3.5 kwa siku.
Matayarisho ya nyumba kabla ya kuzaa
• Osha banda la kuzalia kwa maji na kuliacha likauke
• Tandika nyasi kavu mara baada ya nyumba kukauka
• Ongeza taa ya chemli au umeme kama uko mikoa yenye baridi kwenye sehemu ya vitoto.
• Tengeneza sehemu ya kuzalia kwa mbao au mabomba
Kumuandaa nguruwe mama kabla ya kuzaa
• Mpe dawa ya minyoo siku 10 kabla ya kuzaa
• Mogeshe mama nguruwe kwa sabuni ya mkono na brashi
• Muhamishie katika churnba cha kuzalia siku 7 kabla hajazaa
• Mpunguzie lishe siku 2 kabla ya kuzaa
• Siku ya kuzaa mpe nguruwe maji ya kunywa na chakula kidogo ili kuepusha kula watoto
Matunzo ya vitoto vya nguruwe
Vitoto vya nguruwe vinyonye maziwa ya mama siku zote hadi wakifikisha siku 56.
No comments:
Post a Comment