Sunday, 20 March 2022

UFUGAJI WA NGURUWE (KISASA)

UFUGAJI WA NGURUWE (KISASA)

Upate wapi Nguruwe wa Kufuga
Nunua nguruwe wa kufuga kutoka kwenye mashamba au watu binafsi wanaoaminika ukizingatia yafuatayo.
• Usizalishe nguruwe wanaotokana na ukoo mmoja yaani ndugu kama kaka na dada. Nunua dume najike toka mahali   tofauti.
• Tumia ushauri wa wataalamu kuchagua Nguruwe bora

Sifa za kuangalia kwa nguruwe bora wa mbegu:
• Nguruwe wa mbegu awe na sifa ya kukua haraka na asiwe na ulemavu wa aina yeyote, na hasa wa miguu kwa dume.
• Mama mzazi wa nguruwe awe na historia ya kuzaa watoto 10 hadi 12 kwa mzao mmoja
• Jike awe na chuchu zaidi ya 12.
• Dume awe na sehemu za kiume yaani korodani na uume unaoonekana sawa sawa. Pia awe na hamu ya kupanda majike.

Mbinu za uzalishaji
Matunzo ya dome la uzalishaji
• Chagua dume la mbegu bora, lisilokuwa na kilema au ugonjwa wowote. Tenganisha dume na majike iii kuepusha kupandwa kusiko na kumbukumbu. Dume la nguruwe halipaswi kunenepa, kwa hiyo usimlishe chakula kingi na mpatie mazoezi ya kutosha asije akawa mvivu
• Nguruwe dume anaanza kupanda majike akiwa na umri wa miezi 4 hadi miezi 9. Dume liruhusiwe kupanda mara moja tu kwa kila juma. Anapofika miezi 10 anaweza kupanda mara mbili hadi mara tatu kwa wiki. Akiwa na mwaka mmoja na zaidi anaweza kupanda kila siku kwa majuma mawili hadi matatu, kisha apumzike kwa majuma mawili. Ni vizuri nguruwe dume mmoja apande majike 15 hadi 20 kwa mwaka.
• Madume madogo yapande majike madogo, dume kubwa likimpanda jike dogo anaweza akamletea maradhi ya mgongo. Ni muhimu kupandisha dume kabla hajala chakula, na asitumiwe mara tu baada ya chakula ili asiwe mvivu.

Utunzaji nguruwe mwenye mimba
• Mimba ya nguruwe huchukuwa miezi mitatu (3) wiki tatu(3) na siku tatu(3) yaani siku 114
• Nguruwe mwenye mimba apewe chakula cha kutosha kiongezwe polepole tokea posho ya kawaida hadi kilo 3 - 3.5 kwa siku.

Matayarisho ya nyumba kabla ya  kuzaa
• Osha banda la kuzalia kwa maji na kuliacha likauke
• Tandika nyasi kavu mara baada ya nyumba kukauka
• Ongeza taa ya chemli au umeme kama uko mikoa yenye baridi kwenye sehemu ya vitoto.
• Tengeneza sehemu ya kuzalia kwa mbao au mabomba

Kumuandaa nguruwe mama kabla ya  kuzaa
• Mpe  dawa ya minyoo siku 10 kabla ya kuzaa
• Mogeshe mama nguruwe kwa sabuni ya mkono na brashi
• Muhamishie katika churnba cha kuzalia siku 7 kabla hajazaa
• Mpunguzie lishe siku 2 kabla  ya kuzaa
• Siku ya kuzaa mpe nguruwe maji ya kunywa na chakula kidogo ili kuepusha kula watoto

Matunzo ya vitoto vya nguruwe
Vitoto vya nguruwe vinyonye maziwa ya mama siku zote hadi wakifikisha siku 56.

Tuesday, 19 March 2019

JUICE YA TANGO

🥒🥒JUICE YA TANGO🥒🥒

🥒Mahitaji:-
Matango 2
juice ya ndimu/limao 1/4 litre
sukari kadiria
Maji 1/2 litre

🥒🥒changanya vitu vyote then usage ukipenda unaweza kuchuja. au ukainywa hivyo hivyo.

🥒🥒juice hii inaondoa kitambi, mafuta mabaya.
inasafisha kibofu, pressure n.k
   enjoy

*AINA ZA NGOZI NA JINSI YA KUZITUNZA*

*1⃣ NGOZI YA KAWAIDA*

Kama ngozi yako si ya mafuta wala si kavu,iko nyororo,vitundu vyake viko kawaida,haina harara wala misukosuko yoyote,basi ngozi yako ni ya kawaida  yaani normal skin

➡Na kwa sababu hiyo bidhaa unazopaswa kutumia ni za kutunza tu ngozi kuipa unyevunyevu na kuzuia isiharibiwe na jua.

*2⃣ NGOZI YA MAFUTA*

Kama ngozi yako ina ng'aa kila wakati,unapata chunusi,madoa,matundu yake ni makubwa yanaonekana wewe ngozi yako ni ya Mafuta   yaani oily skin

Bidhaa unazopaswa kutumia ni zile za kubalance mafuta,kuzuia chunusi,kuondoa madoa lakini ni lazima bidhaa hizi ziwe hazikukaushi mafuta

Si kweli kwamba ukiwa na uso wa mafuta ni vibaya na kwamba mafuta hayatakiwa usoni mafuta ni muhimu lakini yana kiasi chake

*3⃣ NGOZI KAVU*

Huwezi toka bila kupaka mafuta,unapauka yaniuso unakuwa na mabaka mabaka,ngozi inafifia,haing'ai basi ukiona hivi ujue ngozi yako ni Kavu yaani Dry skin

Mtu wa ngozi kavu anahitaji bidhaa za kurudishia ngozi yake unyevunyevu

Lakini muhimu sana sana kuilinda isiharibiwe na jua kwa kutumia cream maalum za kuzuia ngozi isiungue.

*4 NGOZI NYETI*

Kama ukipaka kitu chochote usoni unapata irritation,au ngozi yako huwa inawasha,wakati mwingine unaona wekundu kama kuungua basi wewe ngozi yako ni sensitive

Mtu mwenye ngozi hii anapaswa kuwa makini sana na aina ya bidhaa anazotumia

Usipende kubadili badili bidhaa, epuka kutumia bidhaa zenye chemikali na ni vizuri ukapata ushauri kwa mtaalam wa maswala ya ngozi kwanza.

*5 NGOZI MCHANGANYIKO*

Kuna watu ambao baadhi tu ya sehemu usoni ndipo anakuwa na mafuta,sehemu zingine mkavu,anapata pia chunusi japo si nyingi na ni sehemu zile zenye mafuta.

Tunaweza sema sehemu zile zenye mafuta uso unakuwa na tabia za ngozi ya mafuta wakati seheme zenye ukavu zinakuwa na tabia za ngozi kavu

Mtu huyu ngozi yake ni mchanganyiko au Combination Skin

NJIA ASILI ZA KUONDOA WEUSI KWAPANI NA MAPAJANI

➿➿➿➿➿➿➿➿➿➿



*🍇Njia asili za kuondoa weusi kwapani na mapajani🍇*

🍇Msuguano kati ya sehemu mbili kwa muda mrefu, unene kupita kiasi, matumizi ya deodorant, spray, matumizi ya dawa za kunyolea, matumizi ya vipodozi vikali na ugonjwa wa kisukari ni baadhi ya visababishi kwa maeneo kadhaa ya mwili kupata weusi hasa katika mapaja na kwapa.

🍇hii ni kwa wanaume na wanawake kwasababu matumizi ya vitu hivyo huchangia seli kufa kwa kiasi kikubwa na kutengeneza weusi.

🍇Ifahamike kwamba weusi mapajani au makwapani sio ugonjwa bali ni mabadiliko tu ya ngozi ambayo huwapata wengi na kuwafanya wasiwe na raha pindi wawapo na waume zao

🍇Zifuatazo ni baadhi ya njia za asili ambazo mhanga wa tatizo hili anaweza kuzitumia kuondokana nalo ambalo limekuwa changamoto kwa watu wengi

🍇2.Njia nyingine ni matumizi ya mafuta ya nazi, mafuta haya ni tib anzuri sana kutokana na uwepo wa vitamini E yansaidia kusafisha na Kung’arisha ngozi.

🍇Unachotakiwa kufanya ni kupaa mafuta hayo sehemu ya mwili iliyoathirikana weusi kwa muda wa dakika 10 hadi 20 kisha osha eneo hili kwa maji ya vuguvugu, fanya hivyo kila siku mpaka utapoona mabadiliko.

🍇3.Matumizi ya Tango pia ni muhimu kwa kusaidia kuondoa weusi sehemu za mapajani na kwapani.

🍇Unachotakiwa kufanya, kata vipande kadhaa vya tango jipake kwapani na mapajani au lisage kisha paka ukishapaka kaa kwa muda wa dakika 10 hadi 20.

🍇4.Majani ya Aloevera, chukua utomvu wa jani la Aloevera, Paka kwenye sehemu yenye weusi na kisha acha ule utomvu kwa muda takribani nusu nasaa kisha osha na maji ya uvugu vugu,  Fanya hivi mara moja hadi mbili kwa siku ili kuweza kupata matokeo haraka.

🍇5.Viazi ulaya/mbatata

menya viazi kata vipande jipake makwapani yale maji yake yakiingia kwenye ngozi yanatoa rangi nyeusi au unaweza kuponda kikiwa kibichi na kujipaka kwa dk 10-20 utanawa utafanya hivyo mara 2 kwa siku mpaka weusi utakapoisha

🍇6.Sukari -chukua brown sugar changanya na olive oil paka  badaa ya mda osha

🍇7.Baking soda-inasaidia kutoa dead cells kwa urahisi .

changanya baking soda na maji iwe nzito nzito paka kwapani acha kwa dk 10 osha na jikaushe fanya hivyo mar 2-3 kwa wiki ,endelea na zoezi mpaka utakaopona umeridhika na mabadiliko

🍇Zoezi hili linaweza chukua mda mchache ukaona mabadiliko makubwa au ikachukua mda mrefu kuona  mabadiliko inategemea kila mtu na ngozi yake .

🍇Zingatia kutumia dodoki la kuogea usugulie sehemu hizo husika na hakikisha hukai na nywele ndefu.

🍇Tumia hand shaver isiwe kiwembe, na iwapo umetumia njia hizi kwa miezi 1-2 na hakuna mabadiliko mwone daktari.

🍇Kuna baadhi ya creams au deudorants nazo zinasaidia kutoa weusi.

*Tutaishia hapa, ni matumaini yangu mmenufaika*

➿➿➿➿➿➿➿➿➿➿

Monday, 18 March 2019

MBAAZI ZA NAZI

MBAAZI ZA NAZI

Mbaazi kavu nusu kg
Kitunguu maji 1 kikubwa
Tomato fresh 1 kubwa au 2 za kiasi
Pilipili boga/cupsicum kiasi
Bizari nyembamb/cumin powder 1 tablespoon
Pilipili manga /black pepper 1 teaspoon
Kitunguu saum/garlic 1 tablespoon
Tangawizi mbichi 1 teaspoon
Chumvi
Vegetable maggi /kidonge cha supu 1 (sio lazima)
Tui la maji vikombe 5 (3 tui jepesi na 2 tui zito )
Bizari ya mchuzi/tumeric kiasi
Chemsha mbaazi kwa maji mpaka ziwive, zikauke maji au zibaki na maji kidogo sana, kata kata kitungu, tomato, pilipili boga ndogo ndogo na uweke kwenye sufuria ya mbaazi, add na vitu vyote vilobaki isipokua tui/nazi,
tia nazi/tui jepesi na uwache zichemke, tui jepesi litaivisha vitu vyote, vikishawiva na tui limekaribia kukauka, tia tui zito, funika wacha zichemke mpaka iwe size unayotaka, angalia chumvi na spices kama ziko epua na ENJOY kwa mikate maandazi au wali, zangu mm mekula na 

Bamia robo kg
Kitunguu maji 1 kikubwa
Kitunguu saum kijiko 1 cha chakula
Tangawizi mbichi kijiko 1 cha chai
Chumvi kiasi
Bizari nyembamba /cumin powder 1 tsp
Mafuta ya kupikia 3 tbsp
Pilipili manga kiasi
Tui/Nazi ya maji kikombe 1

Kosha bamia zikate kate ndogo ndogo, kata kata Kitunguu maji, changanya na bamia zisage, kama unatumia blender tia na tui la maji  nusu kikombe, saga pamoja mpaka zinakua laini kiasi, zitoe

Weka sufuria kwenye moto, tia mafuta ya kupikia, tia kitunguu saum, tangawizi, bizari nyembamba na pilipili manga, wacha zipate moto kidogo, tia ile bamia uliyoisaga na kitunguu, ipike kwa dakika 5 malizia tui nusu kikombe tia chumvi , wacha lichemke mpaka iwive pamoja na kitunguu,

Kama uliposaga ulitia tui ni sawa, kama uliposaga hukutia tui , vile linachemka litie tui lote kikombe 1,  wacha lichemke mpaka liwe zito na kila kitu kiwe kimewiva, unaweza kuweka pilipili ya kuwasha ukipenda.

PILAU YA SAUCE YA SOYA NA MBOGA

PILAU YA SAUCE YA SOYA NA MBOGA

VIPIMO

Kuku (mkate mkate vipande) 1

Mchele wa Basmati (rowanisha) magi 3

Mdalasini  mchi 1                     

Vitunguu maji (vilivyokatwa vyembamba) 6

Mchanganyiko wa mboga za barafu (karoti, mahindi, njegere) - Magi 1

Kabichi (iliyokatwa katwa nyembamba) magi 1

Pilipili mbichi (iliyosagwa) 3

Pilipili boga iliyokatwa vipande vidogo vidogo 1

Pilipili manga kijiko cha chakula 1

Chumvi kijiko cha chakula 1

Sosi ya soya (soy sauce) vijiko vya chakula 5

Kotmiri iliyokatwa katwa magi 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa vijiko vya chakula 2

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1.  Tia mafuta ndani ya karai. Yakipata moto kiasi, mimina vitunguu maji na mdalasini 1 mzima kaanga. Itachukua muda kidogo. Kaanga mpaka viwe rangi ya hudhurungi (brown). Viepue na uweke kando.

2.  Ndani ya sufuria kubwa, mimina kuku, chumvi, thomu na tangawizi, sosi ya soya, pilipili manga, pilipili mbichi, chemsha mpaka kuku awive na maji yakauke.

3.  Changanya vitunguu  ulivyokaanga, kabichi, pilipili, mboga, kotmiri, mchanganyiko wa mboga za barafu na weka kwa muda wa dakika tano au kumi. Tia na mafuta kidogo uliyokaangia vitunguu .

4.  Chemsha mchele na chumvi uwive kama kawaida ya kupika wali wa kuchuja. Ukishauchuja umwagie katika masala ya kuku.

5.  Nyunyizia mafuta kidogo uliokaangia vitunguu.

6.  Weka moto mdogo mpaka wali ukishawiva.  Uchanganye ukiwa tayari kwa kuliwa.

KIDOKEZO:

Unaweza kuupika wali huo ndani ya jiko, yaani badala ya kutia masala kwenye sufuria ukayatia katika bakuli au treya ya jiko (oven), kisha ukamwagia wali uliouchuja humo na kuupika kaitka moto wa 400-450 Deg kwa muda wa dakika 15-20.

Enjoy!

COCONUT HALWA / HALUA YA NAZI

COCONUT HALWA / HALUA YA NAZI :

Mahitaji:

Tui zito –kikombe  1+1/4
Maziwa – 2/3 kikombe
Sukari – 2/3 kikombe
Nazi ilokunwa  – 1/4 kikombe
Siagi isokuwa na chumvi – vjk 2 vya kula
Lozi na Pistachios – kiganja kwajili ya kupambia

Maelekezo:

1. Bandika sufuria jikoni moto wa kiasi.
2. Tia tui zito na maziwa.
3. Acha ichemke.
4. Tia sukari na nazi ilokunwa.
5. Koroga hadi ishikane.
6. Tia siagi, koroga kisha epua.
7. Tandaza kwenye sahani ilopakwa mafuta ipate kupoa.
8. Mwagilia lozi na pistachios ukipenda.
9. Kabla haijapoa kabisa kata vipande.
10. Andaa.

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO