Tuesday, 19 March 2019

*AINA ZA NGOZI NA JINSI YA KUZITUNZA*

*1⃣ NGOZI YA KAWAIDA*

Kama ngozi yako si ya mafuta wala si kavu,iko nyororo,vitundu vyake viko kawaida,haina harara wala misukosuko yoyote,basi ngozi yako ni ya kawaida  yaani normal skin

➡Na kwa sababu hiyo bidhaa unazopaswa kutumia ni za kutunza tu ngozi kuipa unyevunyevu na kuzuia isiharibiwe na jua.

*2⃣ NGOZI YA MAFUTA*

Kama ngozi yako ina ng'aa kila wakati,unapata chunusi,madoa,matundu yake ni makubwa yanaonekana wewe ngozi yako ni ya Mafuta   yaani oily skin

Bidhaa unazopaswa kutumia ni zile za kubalance mafuta,kuzuia chunusi,kuondoa madoa lakini ni lazima bidhaa hizi ziwe hazikukaushi mafuta

Si kweli kwamba ukiwa na uso wa mafuta ni vibaya na kwamba mafuta hayatakiwa usoni mafuta ni muhimu lakini yana kiasi chake

*3⃣ NGOZI KAVU*

Huwezi toka bila kupaka mafuta,unapauka yaniuso unakuwa na mabaka mabaka,ngozi inafifia,haing'ai basi ukiona hivi ujue ngozi yako ni Kavu yaani Dry skin

Mtu wa ngozi kavu anahitaji bidhaa za kurudishia ngozi yake unyevunyevu

Lakini muhimu sana sana kuilinda isiharibiwe na jua kwa kutumia cream maalum za kuzuia ngozi isiungue.

*4 NGOZI NYETI*

Kama ukipaka kitu chochote usoni unapata irritation,au ngozi yako huwa inawasha,wakati mwingine unaona wekundu kama kuungua basi wewe ngozi yako ni sensitive

Mtu mwenye ngozi hii anapaswa kuwa makini sana na aina ya bidhaa anazotumia

Usipende kubadili badili bidhaa, epuka kutumia bidhaa zenye chemikali na ni vizuri ukapata ushauri kwa mtaalam wa maswala ya ngozi kwanza.

*5 NGOZI MCHANGANYIKO*

Kuna watu ambao baadhi tu ya sehemu usoni ndipo anakuwa na mafuta,sehemu zingine mkavu,anapata pia chunusi japo si nyingi na ni sehemu zile zenye mafuta.

Tunaweza sema sehemu zile zenye mafuta uso unakuwa na tabia za ngozi ya mafuta wakati seheme zenye ukavu zinakuwa na tabia za ngozi kavu

Mtu huyu ngozi yake ni mchanganyiko au Combination Skin

No comments:

Post a Comment

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO