Tuesday, 19 March 2019

JUICE YA TANGO

🥒🥒JUICE YA TANGO🥒🥒

🥒Mahitaji:-
Matango 2
juice ya ndimu/limao 1/4 litre
sukari kadiria
Maji 1/2 litre

🥒🥒changanya vitu vyote then usage ukipenda unaweza kuchuja. au ukainywa hivyo hivyo.

🥒🥒juice hii inaondoa kitambi, mafuta mabaya.
inasafisha kibofu, pressure n.k
   enjoy

*AINA ZA NGOZI NA JINSI YA KUZITUNZA*

*1⃣ NGOZI YA KAWAIDA*

Kama ngozi yako si ya mafuta wala si kavu,iko nyororo,vitundu vyake viko kawaida,haina harara wala misukosuko yoyote,basi ngozi yako ni ya kawaida  yaani normal skin

➡Na kwa sababu hiyo bidhaa unazopaswa kutumia ni za kutunza tu ngozi kuipa unyevunyevu na kuzuia isiharibiwe na jua.

*2⃣ NGOZI YA MAFUTA*

Kama ngozi yako ina ng'aa kila wakati,unapata chunusi,madoa,matundu yake ni makubwa yanaonekana wewe ngozi yako ni ya Mafuta   yaani oily skin

Bidhaa unazopaswa kutumia ni zile za kubalance mafuta,kuzuia chunusi,kuondoa madoa lakini ni lazima bidhaa hizi ziwe hazikukaushi mafuta

Si kweli kwamba ukiwa na uso wa mafuta ni vibaya na kwamba mafuta hayatakiwa usoni mafuta ni muhimu lakini yana kiasi chake

*3⃣ NGOZI KAVU*

Huwezi toka bila kupaka mafuta,unapauka yaniuso unakuwa na mabaka mabaka,ngozi inafifia,haing'ai basi ukiona hivi ujue ngozi yako ni Kavu yaani Dry skin

Mtu wa ngozi kavu anahitaji bidhaa za kurudishia ngozi yake unyevunyevu

Lakini muhimu sana sana kuilinda isiharibiwe na jua kwa kutumia cream maalum za kuzuia ngozi isiungue.

*4 NGOZI NYETI*

Kama ukipaka kitu chochote usoni unapata irritation,au ngozi yako huwa inawasha,wakati mwingine unaona wekundu kama kuungua basi wewe ngozi yako ni sensitive

Mtu mwenye ngozi hii anapaswa kuwa makini sana na aina ya bidhaa anazotumia

Usipende kubadili badili bidhaa, epuka kutumia bidhaa zenye chemikali na ni vizuri ukapata ushauri kwa mtaalam wa maswala ya ngozi kwanza.

*5 NGOZI MCHANGANYIKO*

Kuna watu ambao baadhi tu ya sehemu usoni ndipo anakuwa na mafuta,sehemu zingine mkavu,anapata pia chunusi japo si nyingi na ni sehemu zile zenye mafuta.

Tunaweza sema sehemu zile zenye mafuta uso unakuwa na tabia za ngozi ya mafuta wakati seheme zenye ukavu zinakuwa na tabia za ngozi kavu

Mtu huyu ngozi yake ni mchanganyiko au Combination Skin

NJIA ASILI ZA KUONDOA WEUSI KWAPANI NA MAPAJANI

➿➿➿➿➿➿➿➿➿➿



*🍇Njia asili za kuondoa weusi kwapani na mapajani🍇*

🍇Msuguano kati ya sehemu mbili kwa muda mrefu, unene kupita kiasi, matumizi ya deodorant, spray, matumizi ya dawa za kunyolea, matumizi ya vipodozi vikali na ugonjwa wa kisukari ni baadhi ya visababishi kwa maeneo kadhaa ya mwili kupata weusi hasa katika mapaja na kwapa.

🍇hii ni kwa wanaume na wanawake kwasababu matumizi ya vitu hivyo huchangia seli kufa kwa kiasi kikubwa na kutengeneza weusi.

🍇Ifahamike kwamba weusi mapajani au makwapani sio ugonjwa bali ni mabadiliko tu ya ngozi ambayo huwapata wengi na kuwafanya wasiwe na raha pindi wawapo na waume zao

🍇Zifuatazo ni baadhi ya njia za asili ambazo mhanga wa tatizo hili anaweza kuzitumia kuondokana nalo ambalo limekuwa changamoto kwa watu wengi

🍇2.Njia nyingine ni matumizi ya mafuta ya nazi, mafuta haya ni tib anzuri sana kutokana na uwepo wa vitamini E yansaidia kusafisha na Kung’arisha ngozi.

🍇Unachotakiwa kufanya ni kupaa mafuta hayo sehemu ya mwili iliyoathirikana weusi kwa muda wa dakika 10 hadi 20 kisha osha eneo hili kwa maji ya vuguvugu, fanya hivyo kila siku mpaka utapoona mabadiliko.

🍇3.Matumizi ya Tango pia ni muhimu kwa kusaidia kuondoa weusi sehemu za mapajani na kwapani.

🍇Unachotakiwa kufanya, kata vipande kadhaa vya tango jipake kwapani na mapajani au lisage kisha paka ukishapaka kaa kwa muda wa dakika 10 hadi 20.

🍇4.Majani ya Aloevera, chukua utomvu wa jani la Aloevera, Paka kwenye sehemu yenye weusi na kisha acha ule utomvu kwa muda takribani nusu nasaa kisha osha na maji ya uvugu vugu,  Fanya hivi mara moja hadi mbili kwa siku ili kuweza kupata matokeo haraka.

🍇5.Viazi ulaya/mbatata

menya viazi kata vipande jipake makwapani yale maji yake yakiingia kwenye ngozi yanatoa rangi nyeusi au unaweza kuponda kikiwa kibichi na kujipaka kwa dk 10-20 utanawa utafanya hivyo mara 2 kwa siku mpaka weusi utakapoisha

🍇6.Sukari -chukua brown sugar changanya na olive oil paka  badaa ya mda osha

🍇7.Baking soda-inasaidia kutoa dead cells kwa urahisi .

changanya baking soda na maji iwe nzito nzito paka kwapani acha kwa dk 10 osha na jikaushe fanya hivyo mar 2-3 kwa wiki ,endelea na zoezi mpaka utakaopona umeridhika na mabadiliko

🍇Zoezi hili linaweza chukua mda mchache ukaona mabadiliko makubwa au ikachukua mda mrefu kuona  mabadiliko inategemea kila mtu na ngozi yake .

🍇Zingatia kutumia dodoki la kuogea usugulie sehemu hizo husika na hakikisha hukai na nywele ndefu.

🍇Tumia hand shaver isiwe kiwembe, na iwapo umetumia njia hizi kwa miezi 1-2 na hakuna mabadiliko mwone daktari.

🍇Kuna baadhi ya creams au deudorants nazo zinasaidia kutoa weusi.

*Tutaishia hapa, ni matumaini yangu mmenufaika*

➿➿➿➿➿➿➿➿➿➿

Monday, 18 March 2019

MBAAZI ZA NAZI

MBAAZI ZA NAZI

Mbaazi kavu nusu kg
Kitunguu maji 1 kikubwa
Tomato fresh 1 kubwa au 2 za kiasi
Pilipili boga/cupsicum kiasi
Bizari nyembamb/cumin powder 1 tablespoon
Pilipili manga /black pepper 1 teaspoon
Kitunguu saum/garlic 1 tablespoon
Tangawizi mbichi 1 teaspoon
Chumvi
Vegetable maggi /kidonge cha supu 1 (sio lazima)
Tui la maji vikombe 5 (3 tui jepesi na 2 tui zito )
Bizari ya mchuzi/tumeric kiasi
Chemsha mbaazi kwa maji mpaka ziwive, zikauke maji au zibaki na maji kidogo sana, kata kata kitungu, tomato, pilipili boga ndogo ndogo na uweke kwenye sufuria ya mbaazi, add na vitu vyote vilobaki isipokua tui/nazi,
tia nazi/tui jepesi na uwache zichemke, tui jepesi litaivisha vitu vyote, vikishawiva na tui limekaribia kukauka, tia tui zito, funika wacha zichemke mpaka iwe size unayotaka, angalia chumvi na spices kama ziko epua na ENJOY kwa mikate maandazi au wali, zangu mm mekula na 

Bamia robo kg
Kitunguu maji 1 kikubwa
Kitunguu saum kijiko 1 cha chakula
Tangawizi mbichi kijiko 1 cha chai
Chumvi kiasi
Bizari nyembamba /cumin powder 1 tsp
Mafuta ya kupikia 3 tbsp
Pilipili manga kiasi
Tui/Nazi ya maji kikombe 1

Kosha bamia zikate kate ndogo ndogo, kata kata Kitunguu maji, changanya na bamia zisage, kama unatumia blender tia na tui la maji  nusu kikombe, saga pamoja mpaka zinakua laini kiasi, zitoe

Weka sufuria kwenye moto, tia mafuta ya kupikia, tia kitunguu saum, tangawizi, bizari nyembamba na pilipili manga, wacha zipate moto kidogo, tia ile bamia uliyoisaga na kitunguu, ipike kwa dakika 5 malizia tui nusu kikombe tia chumvi , wacha lichemke mpaka iwive pamoja na kitunguu,

Kama uliposaga ulitia tui ni sawa, kama uliposaga hukutia tui , vile linachemka litie tui lote kikombe 1,  wacha lichemke mpaka liwe zito na kila kitu kiwe kimewiva, unaweza kuweka pilipili ya kuwasha ukipenda.

PILAU YA SAUCE YA SOYA NA MBOGA

PILAU YA SAUCE YA SOYA NA MBOGA

VIPIMO

Kuku (mkate mkate vipande) 1

Mchele wa Basmati (rowanisha) magi 3

Mdalasini  mchi 1                     

Vitunguu maji (vilivyokatwa vyembamba) 6

Mchanganyiko wa mboga za barafu (karoti, mahindi, njegere) - Magi 1

Kabichi (iliyokatwa katwa nyembamba) magi 1

Pilipili mbichi (iliyosagwa) 3

Pilipili boga iliyokatwa vipande vidogo vidogo 1

Pilipili manga kijiko cha chakula 1

Chumvi kijiko cha chakula 1

Sosi ya soya (soy sauce) vijiko vya chakula 5

Kotmiri iliyokatwa katwa magi 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa vijiko vya chakula 2

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1.  Tia mafuta ndani ya karai. Yakipata moto kiasi, mimina vitunguu maji na mdalasini 1 mzima kaanga. Itachukua muda kidogo. Kaanga mpaka viwe rangi ya hudhurungi (brown). Viepue na uweke kando.

2.  Ndani ya sufuria kubwa, mimina kuku, chumvi, thomu na tangawizi, sosi ya soya, pilipili manga, pilipili mbichi, chemsha mpaka kuku awive na maji yakauke.

3.  Changanya vitunguu  ulivyokaanga, kabichi, pilipili, mboga, kotmiri, mchanganyiko wa mboga za barafu na weka kwa muda wa dakika tano au kumi. Tia na mafuta kidogo uliyokaangia vitunguu .

4.  Chemsha mchele na chumvi uwive kama kawaida ya kupika wali wa kuchuja. Ukishauchuja umwagie katika masala ya kuku.

5.  Nyunyizia mafuta kidogo uliokaangia vitunguu.

6.  Weka moto mdogo mpaka wali ukishawiva.  Uchanganye ukiwa tayari kwa kuliwa.

KIDOKEZO:

Unaweza kuupika wali huo ndani ya jiko, yaani badala ya kutia masala kwenye sufuria ukayatia katika bakuli au treya ya jiko (oven), kisha ukamwagia wali uliouchuja humo na kuupika kaitka moto wa 400-450 Deg kwa muda wa dakika 15-20.

Enjoy!

COCONUT HALWA / HALUA YA NAZI

COCONUT HALWA / HALUA YA NAZI :

Mahitaji:

Tui zito –kikombe  1+1/4
Maziwa – 2/3 kikombe
Sukari – 2/3 kikombe
Nazi ilokunwa  – 1/4 kikombe
Siagi isokuwa na chumvi – vjk 2 vya kula
Lozi na Pistachios – kiganja kwajili ya kupambia

Maelekezo:

1. Bandika sufuria jikoni moto wa kiasi.
2. Tia tui zito na maziwa.
3. Acha ichemke.
4. Tia sukari na nazi ilokunwa.
5. Koroga hadi ishikane.
6. Tia siagi, koroga kisha epua.
7. Tandaza kwenye sahani ilopakwa mafuta ipate kupoa.
8. Mwagilia lozi na pistachios ukipenda.
9. Kabla haijapoa kabisa kata vipande.
10. Andaa.

Thursday, 14 March 2019

UTENGENEZAJI WA MISHUMAA YA KUUA MBU

*UTENGENEZAJI WA MISHUMAA YA KUUA MBU*

*MALIGHAFI*
1.PARAFFIN WAX
2.STERINE
3.BORIC ASID
4.MOULD(MAUMBO)
5.UZI (UTAMBI)
6.RANGI KAMA UKIPENDA
7.JIKO
8.SUFURIA

*MAANDALIZI*
andaa maumbo ya mshumaa kwa Jinsi unavopenda unaweza kutumia bati

andaa utambi kwa kuchukua boric asid vijiko vitano vya chakula changanya Na maji vijiko vinne vya chakula ,koroga kwa muda wa dakika tano, KISHA toa Na ANDIKA ili ukauke,sababu ya kufanya hivi ili utambi usiishe haraka wala kutoa moshi. Na hii ndio Kazi kubwa ya boric asid

*UANDAAJI WA MSHUMAA*

baadavya kuwa umeandaa maumbo Yako ya mshumaa chukua utambi wako Na uweke katikati ya mould Yako KISHA funga utambi wako juu ya chombo chako kwa kushikiza Na kijiti .kijiti kitakusaidia ili utambi usikae pembeni

Washa jiko Lako Na weka sufuria Yako jikoni chukua paraffin wax kilo moja ,sterine vijiko vinne,rangi kijiko kimoja cha chai, perfume kama ukipenda kijiko kimoja cha chai

wakati mchanganyiko wako unayeyuka koroga taratibu mpaka uchanganyike vizuri

Epua mchanganyiko wako Na anza kuweka kwenye maumbo Yako uliyoandaa kwa kuweka utambi ndani yake

weka sehemu ya kivuli ili mshumaa wako upate kuganda kwa urahisi ukisha ganda utoe taratibu kutoka katika hayo maumbo yake *BAADA YA HAPO MSHUMAA UTAKUWA TAYARI KWA MAUZO NA MATUMIZI YA NYUMBANI*

*NB:* SIMPRONELLA/CITRONELLA hii ni perfume Na pia ni dawa ya kuua mbu ko kama ukipenda mshumaa wa kuua mbu basi sehemu ya kuweka perfume weka aina hii

Saturday, 9 March 2019

UJASIRIAMALI* YATAKAYOKUWEZESHA KUJIAJIRI MWENYEWE NA KUTIMIZA NDOTO ZAKO.                                              *Masomo 80

*UJASIRIAMALI* YATAKAYOKUWEZESHA KUJIAJIRI MWENYEWE NA KUTIMIZA NDOTO ZAKO.
                                             *Masomo 80
1:SABUNI YA MAJI NZITO(AINA NNE)
2:SABUNI YA MKAA- CHUNUSI.
3:SABUNI YA MCHELE - USOFT
4:SABUNI YA NYANYA.
5:SABUNI YA MAZIWA & ASALI.
6:SABUNI YA KIAZI- MAKOVU.
7: *JIKI.*
8:SHAMPOO.
9:LEMON SOAP.
10:MANJANO SOAP.
11:MISHUMAA/CANDLES.
12: *CHAKI/CHALKS.*
13:SABUNI YA MCHE/LAUNDRY BAR SOAP.
14: *SABUNI YA MAGADI.*
15:SABUNI YA MLONGE.
16:SABUNI YA TANGO.
17:SABUNI YA ALOVERA.
18:SABUNI YA MAJIVU.
19:SABUNI YA UKWAJU
20:SABUNI YA PAPAI.
21:SABUNI YA SULFUR/ NGOZI YA MAFUTA NA CHUNUSI.
22:TILES) SINK CLEANER.
23:SABUNI YA MWAROBAINI.
24:SABUNI YA KUNAWIA MIKONO.
25:MAZULIA/CARPETS.
26:SHAMPOO YA ALOVERA.
27:SHAMPOO YA TANGO.
28:SABUNI YA TANGAWIZI.
29:SABUNI YA  MAWESE NA ASALI.
30:SABUNI YA  CHUNGWA.
31:MITO/PILLOWS.
32:BATIKI TIE & DIE  TONE LA MAJI.
33:BATIKI YA MUHURI.
34:MASHUKA/BEDSHEETS.
35:BATIKI TIE & DIE  CRANCKE. PARTERN.
36:BATIKI YA CHAPA{printing}
37:BATIKI YA KUCHUBUA{Bleach.}
38: *VIATU*
39:BATIKI PUBBLE PRISM.
40:BATIKI TIE & DIE NYOTA.
41:BATIKI TIE & DIE UPINDE  WA MVUA.
42:BATIKI TIE & DIE  DOUBLE SPYRAL.
43:BATIKI ZA MSHUMAA.
44: *MIKOBA/HANDBAGS*
45:MAZIWA YA SOYA.
46:SOYA MASALA.
47:SIAGI YA KARANGA.
48:MAZULIA/CARPETS.
49:CRIPS ZA VIAZI.
50:JUISI YA DUKANI.
51:KARANGA ZA MAYAI.
52:TOMATO SAUCE.
53:CHILI SAUCE.
54:UBUYU WA VIMTO.
55:UFUTA
56:KASHATA ZA KARANGA.
57:ICE CREAM ZA UBUYU.
58:MKAA.
59:UNGA WA LISHE.
60:VIBANIO VYA MAPAZIA.                                                                                                                                                 61: *KEKI NA UPAMBAJI WAKE.*
62:MAFUTA YA KAROTI.
62:AIR FRESHENER.
63:DAWA YA KUUA WADUDU.
64:ICE CREAM YA MAZIWA.
65:LEMON ICE CREAM.
66:BISKUTI.
67:FUDGE AINA ZOTE.
68: *UPAMBAJI WAKUMBI ZA SHEREHE.*
69: MAFUTA YA MNYONYO{Castor oil}
70: *ANTI AGING LOTION*
71:HAND WASHING GEL.
72:MAFUTA YA NAZI.
MAFUTA YA MGANDO.
73:MAFUTA YA NGOZI{MAKUNYANZI}
74:JUISI ZA MATUNDA.
75:SABUNI YA
78: *LEMON OIL.*
79:ALOE VERA GEL.
80:SABUNI YA UNGA

Tuesday, 5 March 2019

JINSI YA KUTENGENEZA MASK KWA AJILI YA NGOZI ZA AINA ZOTE

*JINSI YA KUTENGENEZA MASK KWA AJILI YA NGOZI ZA AINA ZOTE*

*NGOZI YENYE CHUNUSI*

*Mahitaji*

🍇Kungumanga🌰
🍇Asali🍯
🍇Maziwa 🥛

*Jinsi ya kufanya*

Changanya mahitaji yote kwenye bakuli safi mpaka uhakikishe umepata mchanganyiko mzuri

Safisha uso kisha paka na ukae nayo kwa muda wa nusu saa kisha osha vizuri na maji ya uvugu kisha malizia na maji baridi

Futa na taulo laini uso wako kisha jipe unyevu kama kawaida

*NGOZI YA MAFUTA*

*Mahitaji*

🍇Unga wa ngano🍚
🍇Mtindi 🥛
🍇Manjano

*Jinsi ya kufanya*

Changanya mahitaji yote mpaka uhakikishe imechanganyika vizuri

Safisha uso kisha paka paste yako na uiache kwa muda wa nusu saa kisha osha kwa maji ya uvugu ukifuatisha na maji baridi

Futa uso kwa taulo safi kisha paka moisturizer kama kawaida

*NGOZI YENYE MIKUNJO*

*Mahitaji*

🍇Aloe vera gel🌿
🍇Asali 🍯
🍇Mafuta ya nazi

*JINSI YA KUFANYA*

Changanya mahitaji yote mpaka uhakikishe imechanganyika vizuri

Safisha uso kisha paka paste yako na uiache kwa muda wa nusu saa kisha osha kwa maji ya uvugu ukifuatisha na maji baridi

Futa uso kwa taulo safi kisha paka moisturizer kama kawaida

*NGOZI KAVU*

*Mahitaji*

🍇Ndizi mbivu🍌
🍇Asali🍯

*JINSI YA KUFANYA*

Changanya mahitaji yote mpaka uhakikishe imechanganyika vizuri

Safisha uso kisha paka paste yako na uiache kwa muda wa nusu saa kisha osha kwa maji ya uvugu ukifuatisha na maji baridi

Futa uso kwa taulo safi kisha paka moisturizer kama kawaida

JINSI YA KUTENGENEZA COFFEE SCRUB

*JINSI YA KUTENGENEZA COFFEE SCRUB*

*Mahitaji*

🍇¼ kikombe ya kahawa iliyosagwa

🍇½ kikombe ya mafuta ya nazi/olive oil extra virgin

🍇2 Tbs ya mdalasini wa unga au manjano

*JINSI YA KUFANYA*

Changanya mahitaji yote kwenye bakuli safi.

Osha mwili wako kwanza ili kuondoa uchafu kwenye ngozi kisha jikaushe na taulo

Sugua ukitumia scrub yako kwa kufuata mduara

Iache kwa dakika 15 kisha osha vizuri

Kama una sensitive skin hakikisha unasugua taratibu sana

Coffe ni kama exfoliator ambayo inasaidia kuondoa dead cells na itaiacha ngozi yako ikiwa laini ya kupendeza...

Mafuta ya nazi /olive yataipa unyevu ngozi yako na kuiacha ikiwa na afya na yenye mng'ao

Manjano na mdalasini vitaondoa bacteria wanaosababisha chunusi na kuiacha ngozi yako na ikipendeza zaid

JINSI YA KUTENGENEZA LOTION ASILIA KWA NGOZI NYORORO YENYE MNG'AO (NATURAL)

*JINSI YA KUTENGENEZA LOTION ASILIA KWA NGOZI NYORORO YENYE MNG'AO  (NATURAL)*

*Chagua moja kati ya lotion zifuatazo*

*Mahitaji*

🍇Vitamin c powder/unga1 Tbs

🍇Vitamin e Capsule/oil matone 5

🍇Rose water 1Tbs🌹

🍇Glycerin 1 Tsp

🍇Shea butter au Vaseline lotion/Lotion yoyote uipendayo 100ml

*Jinsi ya kufanya*

Tia rose water kwenye bakuli safi kisha tia kijiko kimoja cha unga wa vitamin C

Changanya vizuri na ukoroge kwa muda wa dakika 5 mpk vitamin c iyeyuke kabisa kisha ongezea glycerin na vitamin e na uchanganye vizuri

Tia lotion yako ya vaseline ujazo wa ml 100 ama shea butter ama cream yoyote uipendayo mwenyewe kisha changanya vizuri hadi ichanganyike

Weka kwenye chupa safi tayari kwa matumizi

Hii itafanya ngozi yako kua laini na kuondoa ukavu wa ngozi pamoja na kuiacha ikipendeza zaidi na zaidi

Unaweza kupaka kwenye mwili hata usoni na ni salama kabisa haina sumu

Lotion ya pili

*Mahitaji*

🍇Mafuta ya nazi
🍇Aloe Vera gel
🍇Rose water
🍇Glycerin
🍇Vitamin e Capsule/oil

*Jinsi ya kufanya*

Weka kwenye bakuli safi kijiko kimoja cha chakula cha aloe vera gel (ya dukani iwe 100% natural)

Ongeza kijiko kimoja cha chakula cha mafuta ya nazi pamoja na glycerin na rose water kisha ongezea na vitamin e kama ngozi yako ya mafuta tumia capsule kama kavu unaweza kutumia vitamin e oil

Changanya vizuri mpaka ichanganyike na uone imekua na rangi ya kupendeza na ipo laini kisha hifadhi kwenye kichupa safi tayari kwa matumizi

DAWA YA KUKUZA NA KUNYOOSHA NYWELE,KUONDOA WEUSI MAKAPANI,VIDOLENI,MAGOTI

Utengenezaji  dawa ya kukuza nywele/kuondoa michirizi kwapani,vidole,magoti,kunyoosha nywele

      Mahitaji

1*mafuta ya mzaituni

2*mdalasini ya unga

3*asali

Uandaaji

Andaa sefuria jikon na acha ipate moto

Baada ya kupata moto weka mafuta ya mzaituni nusu Lita acha yachemke (kupata moto )

Baada ya kupata moto weka mdalasini kijae kikombe kimoja cha chupa ya chai acha jikon ukiwa unakoroga

Koroga hadi kuona inaacha kuchemka yani kupata moto sana maana haichemki kama mboga😁

Acha usikoroge na kusubiri hadi ibadirike rangi na kua kahawia nyeusi ipua na subiri kupoa

Baada ya kupoa weka asali vijiko 10 vya chakula kisha koroga tena

Baada ya kuweka asali na kukoroga mafuta yapo tayar kwa matumizi

Matumizi

Paka kichwa kuanzia kwenye ngoz ya kichwa (utosi) hadi juu ya nywele

Nb isikae kichwani zaidi ya robo Saa (dakika 15 )

🍉🍅na kuondoa weusi makwapani,vidoleni na magotini🍒
changanya mchuzi wa limao au ndimu ,na asali au sukari alafu jisugue sehemu husika kila siku kabla ya kuoga.baada ya kujisugua kaa dkk 10 then nawa au oga kama kawaida

♥DAWA YA MICHILIZI
🌷🌷@umbo_la_asili
Mahitaji⤵
🔹limao 1
🔹olive oil vijiko 5
🔹kahawa vijiko 4
🔹sukari vijiko 2

♥♥NJIA♥♥♥
Weka kahawa ktk bakuri ongeza mafuta ya olive oil  vijiko 5 pamoja na sukari vijiko 2
Koroga ongeza na limao ktk mchanganyiko
Paka sehemu za michirizi km unasugua.fanya hiv kwa mda km dkk mbili.acha kusugua kaa kidogo km dkk 20
Baada ya hapo kaoge kisha paka mafuta ya nazi hasa mafuta ya naz ya minara.🌷🌷🌷🌷🌷♥♥♥♥♥♥♥
@umbo_la_asili

KUNYONYOKA KWA  NYWELE
wale walio na tatizo la kunyonyoka kwa nywele,wanaweza kupaka kichwani uji wenye mchanganyiko wa mafuta ya mzeituni yaani olive oil,asali kijiko kimoja cha chakula,mdalsini kijiko kimoja cha chai kabla ya kuoga na kuuacha kichwani kwa muda wa dk 15 na kisha kuosha kichwa.hii husaidia kurudisha nywele

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO