*UTENGENEZAJI WA MISHUMAA YA KUUA MBU*
*MALIGHAFI*
1.PARAFFIN WAX
2.STERINE
3.BORIC ASID
4.MOULD(MAUMBO)
5.UZI (UTAMBI)
6.RANGI KAMA UKIPENDA
7.JIKO
8.SUFURIA
*MAANDALIZI*
andaa maumbo ya mshumaa kwa Jinsi unavopenda unaweza kutumia bati
andaa utambi kwa kuchukua boric asid vijiko vitano vya chakula changanya Na maji vijiko vinne vya chakula ,koroga kwa muda wa dakika tano, KISHA toa Na ANDIKA ili ukauke,sababu ya kufanya hivi ili utambi usiishe haraka wala kutoa moshi. Na hii ndio Kazi kubwa ya boric asid
*UANDAAJI WA MSHUMAA*
baadavya kuwa umeandaa maumbo Yako ya mshumaa chukua utambi wako Na uweke katikati ya mould Yako KISHA funga utambi wako juu ya chombo chako kwa kushikiza Na kijiti .kijiti kitakusaidia ili utambi usikae pembeni
Washa jiko Lako Na weka sufuria Yako jikoni chukua paraffin wax kilo moja ,sterine vijiko vinne,rangi kijiko kimoja cha chai, perfume kama ukipenda kijiko kimoja cha chai
wakati mchanganyiko wako unayeyuka koroga taratibu mpaka uchanganyike vizuri
Epua mchanganyiko wako Na anza kuweka kwenye maumbo Yako uliyoandaa kwa kuweka utambi ndani yake
weka sehemu ya kivuli ili mshumaa wako upate kuganda kwa urahisi ukisha ganda utoe taratibu kutoka katika hayo maumbo yake *BAADA YA HAPO MSHUMAA UTAKUWA TAYARI KWA MAUZO NA MATUMIZI YA NYUMBANI*
*NB:* SIMPRONELLA/CITRONELLA hii ni perfume Na pia ni dawa ya kuua mbu ko kama ukipenda mshumaa wa kuua mbu basi sehemu ya kuweka perfume weka aina hii
Asante kwa maelezo mazuri Je naweza kupata wapi simpronella au Citronella?
ReplyDeleteAsante, sijafamu ni wapi inapatikana utambi maana nimeenda Sido hawana, pia na kwenye maduka wanayouza marigafi za wajasiriamali hawana pia ni wapi zapatikana?
ReplyDeleteAhsante,lakini baadhi ya malighafi hazipatikani kama vile stearic acid na cintronela maeneo ya Mbeya je tunazipataje?
ReplyDeleteMbona hakuna vipimo vya malighafi hizo jaman
ReplyDelete