Thursday, 29 November 2018

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA UNGA

#DONDOO.!! ZA FAIDA..!!!
.....
@JIFUNZE JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA UNGA...!!!
.....
...Jinsi ya kutengeneza sabuni ya unga.
MAHITAJI.
.Optical bright
.Sodium carbonate
.Sulphonic acid
.Soda ash
.Nasa
.Perfume
Mwiko, Beseni, Gloves
JINSI YA KUTENGENEZA.
Andaa beseni lako linaloendana na wingi wa sabuni unayotaka kutengeneza na anza kutengeneza kwa kufuata hatua zifuatazo.
.Weka Sulphonic Acid lita 1 kwenye beseni lako
.Weka sodium carbonate Lita 3
.Koroga kwa muda wa dakika kumi.
.Baada ya hapo weka Optical bright vijiko 6 vya chakula.
.Weka Nasa vijiko 16 vya chakula.
.Soda ash kilo 5
Malizia kwa kuweka perfume kiasi
Changanya mchanganyiko wako vizuri
.Baada ya mchanganyiko huo kuwa tayari anika kwenye kuvuli kwa kuwa juani inaweza kuyeyuka. Sabuni yako itakauka kwa kujiachia.Kusanya weka kwenye mifuko tayari kwa kuuza.
ONYO:Baadhi ya malighafi ni acid kwahiyo umakini unatakiwa wakati wa kutengeneza, hakikisha mikono yako imelindwa kwa gloves na usishike acids au kula wakati unafanya kazi.
...
....MATUNAINI YANGU UTAKUA UMEFULAIA

Tuesday, 27 November 2018

UTENGENEZAJI WA SODA

Utengenezaji Wa soda

Mahitaji

1* maji

2*sukari

3*rangi

4*phosphoric acid

5*ladha

🙏🙏🙏

JINSI YA KUANDAA BOGA/TANGO

Boga/ tango

Boga
Sukari utakisia
Hiliki kiasi
Tui utakisia
Custard powder utakisia mm nimetumia vijiko vidogo viwili.

Nimekata vipande vya kiasi boga langu na  kulimenya na kuondoa zile  mbegu za kati. Chukuwa sufuria  weka boga lako na maji kiduchu ili lipate kuiva kidogo kwa mvuke kabla hujaweka tui lako. Ukiona linaanza kuiva bado lina ubichi ubichi weka sukari hiliki na tuli lako hivyo vyote utakisia. Wacha lichemkie mpaka kuiva na kubakia tui kiasi ndio uchukuwe ile custard kidogo changanya na maji mimina kwenye mchanganyiko wako. Wacha tena lichemkie kidogo epua itakuwa tayar.  Subiri lipoe pakuwa tayar kwa kuliwa. Ukipenda utakunywa kwa uji au kutoelea na wali

MKATE WA MAYAI

*Mkate Wa Mayai*

Mkate Wa Mayai

Vipimo
·         Mayai 4
·         Sukari ¼  Kikombe
·         Unga wa Ngano Vijiko 5 ½ vya chakula
·         Hiliki ya kusaga ½  kijiko cha chai
·         Baking powder  ½  Kijiko cha chai
·         Zabibu kavu  ¼  kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Chukua bakuli la kiasi, weka sukari, hiliki na vunja juu yake mayai  yote manne.

Changanya sukari,  hiliki na mayai   kwa kutumia mashine ya kukorogea keki (cake mixer), mpaka sukari ivurugike yote na kuumuka.

Washa jiko lako (oven) 350F lianze kupata moto.
Weka baking powder kwenye unga na uanze kuuchanganya kidogo kidogo kwenye mchanganyiko  wa mayai na sukari. Hakikisha kila ukiweka unga kidogo unauchanganya vyema usiwe na madonge.
Mimina unga  ndani ya sufuria ya kuchomea keki ya kiasi.

Tupia zabibu  juu ya mchanganyiko wako.
Ingiza sufuria   ndani ya jiko (oven) kwa dakika 20 kisha utoe.

Uhakikishe mkate wako kama umeiva kwa kijiti cha kuchomea mshikaki au toothpick.

Ingiza kijiti  katikati ya mkate kisha kitoe na ukiguse uangalie kama kikavu mkate umeiva kama bado kuna ubichi basi rudisha mkate kwa dakika 5 nyingine kisha ukague.
Wacha mkate upoe kisha utoe ndani ya sufuria na uweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

KAMAITI YA SUKARI YA NJE

Kaimati za sukari ya nje

Maitaji

◾Sukari robo
◾Unga wa ngano nusu
◾Amira kijiko cha chai
◾Iliki kijiko cha chai nusu
◾Samli au mafuta yakukandia
◾Tui la nazi na maji yake ya Nazi

Matayarisho

chukua unga weka kwa bakuli  lako

chukua iliki yakusaga weka chukua samli weka au

mafuta chukua Amira iweke kwenye tui lako la nazi

liache kiasi anza kuchanganya unga hadi

uchanganyike tia tui kiasi changanya weka tena ikiwa

Lipo changanya tena ukiona umelainika vizuri weka

yale maji ya nazi chukua mwiko wakupikia sima anza

kuvurugia hadi uwe sawa usiwe mzito sana zikawa

na donge ndani wala usiwe mwembamba zikawa

nyepesi  uwe katikati utafutie maali uweke.

Chukua sufuria tia sukari tia maji kiasi bandika jikoni

iache ichemke hadi iive ambapo ukiishika kwa vidole

yanata ukiona ipo hivyo iepue angalia unga wako

umeumuka au ikiwa upo tayari bandika karai lako tia

mafuta mengi ili zichomeke vizuri yaache yapate

moto anza kuchoma hadi umalize.

ukimaliza zitiie kwenye sufuria bandika jikoni moto kiasi

chukua sukari zimwagilie anza kuzipepeta kiasi,

regesha jikoni hadi zishike sukari vizuri

Aandaa tayari kwa kuliwa

Monday, 26 November 2018

JINSI YA KUTENGENEZA KASHATA

-----KASHATA
Sukari kg 1
Nazi1
Njugu nusu na robo
Maziwa ya unga robo
Hiliki
Maji kikombe kimoja
Unaweka maji na sukari mpaka ichemke ikishachemka unatianazi uloikunana kuisaga ikisha unakoroga mpaka inakuwa nzito unatia njugu unakoroga mpaka ukeshaona karibu inakauka unatia maziwa pamoja na hiliki ikisha unaweka kwenye kibao chako ulotia mafuta unasukuma ikisha unakata tayari kwakuliwa na kahwa

Friday, 23 November 2018

JINSI YA KUTENGENEZA MAFUTAYA KUKUNZIA NYWELE NA KUONDOA MBA NA KUZIFANYA NYWELE KUWA LAINI

Mahitaji

1" mafuta ya mnyonyo

2*unga wa mbegu za parachichi

3*yai

4*unga wa muhogo

5*Unt bakteria.

  Utengenezaji

Andaa blenda kisha weka unga wa mbegu za mlonge

Kisha weka mayai 3 ya kuku wa kienyeji

Kisha saga na kupata mchanganyiko laini

Baada ya kuchanganya weka sefuria jikon na weka maji nusu Lita na weka unga wa muhogo vijiko 3 vya chakula kisha acha ichemke kwa muda kisha ipua

Baada ya hapo weka ule mchanganyiko ulikua kwenye blenda kwa kuchota vijiko 5 vya chakula

Baada ya hapo  mafuta ya mnyonyo ml.100

Koroga na utaweza kupata dawa laini na nzito

Paki katika Vifungashio na anza soko

Hukuza nywele na kuondoa mba na kufanya nywele kua laini

TIBA YA UGONJWA WA KISUKARI

Tiba ya ugonjwa wa kisukari

Mahitaji

1*mbegu za mlonge

2*mbegu za parachichi

3*kitunguu maji

Utengenezaji

Andaa blenda na utengenezaji juisi nzito ya vitunguu

Kisha andaa tunda za mlonge na uzisage

Kisha tengeneza unga wa mbegu za parachichi

Kisha weka jikoni mchanganyiko wote huo na kuongeza kikombe 1 cha chai acha ichemke

.baada ya kuchemka utapata uji mzito hapo dawa itakua tayari

Matumizi

Changanya dawa ikiwa na vijiko 5 vya chakula weka katika uji au chai isiokua na sukar wala chumvi

Tumia kwa siku 14 mfurulizo kisha kapime

FAIDA ZITOKANAZO NA MATUMIZI YA PAPAI

FAIDA ZITOKANAZO NA MATUMIZI YA PAPAI

ASILI ya mpapai ni Amerika ya Kati, ambapo kuanzia matunda, majani na utomvu wa mmea huu hutumiwa kama dawa maeneo mbalimbali duniani. Vile vile, matunda na utomvu wake yamekuwa yakitumika kutengeneza pombe na mvinyo katika baadhi ya nchi, huku wengine wakitumia mpapai kama dawa kwa mifugo na binadamu.

Inaelezwa kuwapo na tafiti zilizowahi kufanyika na kuchapishwa katika jarida lijulikanalo kwa jina la ‘Archieve’ la nchini India mnamo Oktoba 27 mwaka 2010, ambapo jarida hilo lilieleza kwamba juisi ya majani ya mpapai iliweza kusaidia wagonjwa watano waliowahi kupata homa ya dengue.

Mbali na utafiti huo, pia kuna tafiti zilizowahi kufanywa na madaktari wa nchini Marekani na Japani na kubaini kuwa, juisi ya majani ya mpapai ina uwezo wa kutibu malaria na saratani, japokuwa tafiti hizo hazikukubawaliwa kisayansi.
Faida za kiafya za tunda la papai

Aidha, wataalam wa lishe nao wanaeleza kwamba, watu wenye matatizo ya kupatwa na majipu, uvimbe na vidonda mara kwa mara huwa na upungufu wa virutubisho muhimu, ambavyo huweza kupatikana ndani ya papai, hivyo imegundulika watu wenye matatizo hayo wakitumia papai hupata nafuu na kupona haraka.

Pia papai husaidia kuleta nuru ya macho, kama inavyoaminika kwa karoti, hali kadhalika papai pia husaidia kupunguza madhara yatokanayo na moshi wa sigara.

Hivyo wavutaji wa sigara ni vyema wakatumia tunda hili mara kwa mara ili kujipunguzia madhara ya moshi wa sigara, ingawaje ni vyema wakakumbuka matumizi ya sigara si mazuri kwa afya hivyo ikibidi ni vizuri kuacha kabisa.

Ni wazi kuwa papai ni tunda lililosheheni kila aina ya utajiri wa vitamin kuliko matunda mengine, kwani lina vitamin A, B, C, D na E.

Wataalam wa tiba za asilia pia wanaeleza kwamba tunda hili linauwezo wa kutibu tatizo la usagaji wa chakula tumboni pia hutibu kisukari na pumu na mara nyingine hata kifua kikuu.

Tunda la papai lina faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kuwa na uwezo wa:

Kutibu tatizo la Shida ya kusaga chakula tumboni
Kutibu Udhaifu wa tumbo
Kutibu Kisukari na asthma au pumu.
Kutibu Kikohozi kitokacho mapafuni
Kutibu Kifua kikuu
Tunda hili huleta afya nzuri ukitumia kila siku
Maziwa yanayotoka katika jani lake huponya vidonda
Vilevile yanasaidia kutibu sehemu palipoungua moto
Kama hiyo haitoshi, maziwa yanayotoka katika jani la mpapai yanatibu kiungulia na Ugonjwa wa colon (njia ya haja kubwa ndani)

Pia yanasaidia kutofunga choo
Maganda ya tunda la papai yanasaidia kutibu tatizo la kuungua, vipele na saratani ya ngozi.
Mbegu zake zinatibu ini zikitafunwa 10 – 12 kwa siku 5.
Majani yake yakaushie ndani, yanatibu pumu. Inapoanza kubana yachome majani yaliyokaushwa kisha jifukize, kule kubanwa kutakisha.
Majani yake yanasaidia katika kutibu shinikizo la damu.
Papai likimenywa na kupondwa linafaa Sana katika masuala ya urembo kwani linaweza kutumika Kama vile unavyotumia lotion kulainisha uso.
Mbegu za papai zina uwezo wa kutibu homa. Meza mbegu za papai kiasi cha kijiko cha chakula mara 3 kwa ajili ya kutibu homa.
Mbegu za papai zilizokaushwa ndani kisha zikasagwa kuwa unga zinatibu malaria, tumia kijiko 1 cha chai changanya na uji, kunywa mara 3 kwa siku 5 Mgonjwa wa kifua kikuu akila matunda haya kwa muda mrefu atapona bila dawa nyingine.
Mizizi yake ikipondwa na kulowekwa katika maji yaliyochemshwa, lita 2 na nusu kwa dakika 15, yanatibu figo, bladder, yanazuia kutapika. Nusu kikombe cha chai kutwa mara 3 kwa siku....

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA KUONDOA MICHIRIZI, MABAKA MABAKA , MAKUNYANZI USONI

Mahitaji

1*alovera

2*kitunguu swaum

3*sulphonic

4*chumvi

5*griselin

6*manukato

   Utengenezaji

Saga alovera na kupata maji Lita 5

Saga kitunguu vikubwa 3

Kisha changanya alovera na kitunguu

Ongeza maji kidogo Lita 2

Jumla utapata Lita 7 anza kukoroga kuelekea upande 1

Baada ya hapo weka sulphonic acid Lita 1 endelea kukoroga

Baada ya hapo weka griselin Lita 1

Baada ya hapo weka chumvi vijiko 4 vya chakula

Endelea kukoroga

Kisha weka rangi

Endelea kukoroga

Kisha wek manukato

Endelea kukoroga kwa dakika 5

Acha kwa masaa 2

Sasa sabuni yako ipo tayar

Tiba hii sabuni

Kuondoa mabaka na chunusi usoni.

Mba na makunyazi ya ngozi

Michirizi nk

MJASIRIA MALI NA HARAKATI ZAKE ZA UJASIRIA MALI

____________________
MJASIRIA MALI NA  HARAKATI ZAKE ZA UJASIRIA MALI..
____________________

____________________

  (1) MJASIRIA MALI NI NANI..?

     ==>Mjasiria Mali ni mtu anae tazama fursa kwa jicho la mbali yani mtu anae  fikiria kutatua changa moto kabla yakuwa tatizo na sikufikiria  kuhusu changa moto.. Mjasiria Mali ni mtu anae ona fursa nakuanza kuifanyia kazi kabla fursa hiyo haijawa kikwazo kwa watu kikwazo kwa maana kwamba tuna amini fursa nyingi hutokana na changa moto zinazo wakabili watu  katika eneo flani.. Kuwa Mjasiria Mali hau hitaji usome sana Bali una hitaji uwe ni mtu mwenye maarifa yatakayo kusaidia wewe kukuwa vema katika sekta hii ya ujasiria Mali ..Mjasiria Mali lazima uwe ni mtu wakujali thamani kabla ya fedha tanguliza thamani na pesa ita kufwata maana pesa ni matokeo ya thamani unayo iweka kwenye kila jambo ....tazama ujasiria Mali KWA jicho la mbali chukuwa maamuzi kwa wakati na amuwa maamuzi sahihi..

  (2)CHANGA MOTO

      ==>Changa moto katika ujasiria Mali zipo nyingi sana tena nyingine za kukatisha tamaa lakini wewe kama Mjasiria Mali makini na unae juwa nini una Fanya na nn una taka lazima ukabiliane  nazo kiuthubutu bila kuvunjika moyo maana changa moto ni sehemu ya kipimo cha Mjasiria Mali makini na mwenye nia ya kuwa Mjasiria Mali Mkubwa lazima uwe mtu mwenye hekima na busara pale unapo kabiliana na changa moto unazo kumbana nazo usi litazame tatizo kama kikwazo cha kudumu litazame tatizo kama sehemu ya kujifunza.... Wapo watakao kuja kukwambia ww huwezi ww hufai lakini usi Kate tamaa ... Jiamini na amini katika unacho kifanya iambie nafsi yako kuwa wewe una weza kabla hajaja mtu yeyote kukwambia una weza... Changa moto nyingine zifanye kama fursa zitumie hizo kuvuka milima na mabonde zitumie kama daraja ... Waoneshe wengine kuwa wewe ni zaidi ya maumivu ya donda ndugu una weza vumilia kila maumivu zidisha vitendo kuliko maneno... Neno moja liamba Tane na matendo kumi ...

  (3) MTAJI WA MJASIRIA MALI

   ==>Mtaji wa Mjasiria Mali sio pesa mtaji wa Mjasiria Mali ni ubunifu na viwango vya ubunifu wake .. Maana una weza kuwa na pesa lakini isi kusaidie chochote pesa ni matokeo ya ubunifu na thamani ya ubunifu wa Mjasiria Mali kuwa na pesa na ujui chakufanya ni sawa na bure  ongeza jitihada ongeza maarifa kukuza kile ulicho nacho kwanza jenga uaminifu kwawatu maana watu ndio watakao kuvusha wewe watu ndio watakao kupromot wewe watu Hao Hao ndio watakao kukwamisha wewe... Pia lazima uwe na skills ya kutoa kupokea na kuzalisha pesa lasivyo uta jikuta una tafuta vitu ambavyo ni ndoto kuvipata...

  (4)MASOKO

   ==> Wewe kama Mjasiria Mali makini na unae jali kile unacho kifanya lazima jali sana hii sehemu ya masoko ambapo masoko huambatana na mauzo ... Ukipata soko lazima uuze uwezi kuuza bila kupata soko.. Na masoko sio vibanda from nk: masoko ni sisi masoko ni watu watu ndio masoko yako watu ndio walengwa wa biashara au bidhaa zako bila watu WEWE na ujasiria Mali wako sikitu bila watu WEWE na biashara yako sikitu ... Jifunze kuongea na watu jifunze kutenge neza watu. Jifunze kujali watu ... Watu wengi hudhani biashara zao zina endeshwa kwa mitaji ya fedha walizo nazo wana sahau kuwa mitaji ya fedha bila mitaji ya watu sikitu jali watu... Fikiria watu utakao wauzia au kuwa fanyia Huduma yako kabla ya kufikiria kuhusu pesa...

  (6)MREJESHO KWA MTEJA

    ==> Hi ni sehemu iliyo sahaulika sana katika kipingele cha mauzo usi sahau ku chukuwa na kipengele hichi cha MREJESHO hichi ni kipengele muhimu sana katika kukuza soko na kukuza ujasiria Mali wako.... Watu wengi huwa wana uza bidhaa au kutoa Huduma kama wana enda haja huwa hawa pendi kufwatilia wala hawapendi kuweka njia ya kupokea maoni kutoka kwa Wateja wao hii ina wafanya wajasiria Mali wengi kukwama kwa kukosa masoko kwasababu tu hawajui wanapo kosea hawajui Mteja wake napokea vipi Huduma yake hawa jui kama ame ipenda ama lah hii ina wafanya wengi wao kupoteza Wateja na kujikuta kila siku ana tumia nguvu kuzalisha Wateja wapya na huku wale wa. Awali kuto rudi tena ... Hii sawa na kuminya Uhuru wa Mteja wako bidhaa yako ikisha enda mikononi mwamteja nivema kuifwatili kama kweli imempendeza au ana maoni gani ndio pale tuna jifanya wakongwe kumbe wakongwe wa MUDA na sihuduma bora jali sana watu unao wahudumia jifunze kupokea feedback kwa Wateja wako .. Hii itakufanya ata kupata maoni ya uboreshaji au pongezi au ushauri wowote kuhusu Huduma yako  badilika sasa kila mtu ana takiwa kuwa huru katika eneo lake Mteja ana takiwa kuwa huru katika maoni maana katoa hela halali punguzeni Ku chakachuwa hasa pale munapo sifiwa sana huwa muna lewa sifa na kusahau Huduma bora....

...................................
        

FURSA ZA KIBIHASHARA

*FURSA ZA BIASHARA*

*1. Uuzaji wa nguo*

Biashara ya nguo za wakubwa na watoto inazidi kushamiri kila kukicha. Hii hutokana na watu kutaka kuenda na fashion ya mavazi.

Haina maana kuwa lazima uwe na duka kubwa la nguo ndio uweze kufanya biashara hii. Unaweza kuanza na mtaji mdogo hata laki tano ama pungufu.

Unachotakiwa kufanya ni kuyatumia maeneo ya mikusanyiko kujitengenezea wateja. Mikusanyiko iwe ya kidini, kisiasa, kijamii na kadhalika inaweza kukujengea idadi kubwa ya wateja.

Nguo za watoto pia unaweza kujijengea idadi kubwa ya wateja kuanzia kwa majirani mpaka kwenye mikusanyiko.

*2. Uuzaji wa vipodozi*

Hapa maana ya kufungua duka la vipodozi bali ni kuwa kama wakala wa bidhaa flani flani ambazo wewe umeona zina matokeo ya haraka sana katika kufanya kazi.

Unachotakiwa ni kuwa mtu wa watu – usiwe mtu mkimya sana – usiwe mtu mlweke sana – uwe mtu wa kujichanganya na watu – usiwe unajiona – uwe mtumiaji mzuri wa mitandao ya kijamii.

Unaweza anza na mtaji mdogo na kujikita na bidhaa chache na kila uwapo we stori zako iwe ni kuzisifia na uhakikishe hudanganyi na kila anaetumia apate matokeo mazuri na akikosa matokeo mazuri utafute cha kumshauri na kumsaidia.

Unahitaji mtaji mdogo tu kama laki tano ama pungufu kufanya biashara hii. Ila siri kubwa ni kujiweka smart na mwenye furaha muda wote. Picha zako kwenye mitandao ziendane na hiibiashara na ziwe zimejaa furaha na muonekano mzuri.

Watu huwa wanashindwa kuelewa kuwa hata wewe mwenyewe kwenda saluni kujiremba vizuri na kuweka picha mtandaoni ukiwa umeshikilia kipodozi flani ni njia kubwa sana ya kufikisha ujumbe na kutangaza biashara.

*3. Upambaji*

Upambaji unaweza kuwa wa kwenye tafrija mbalimbali ama kwenye mikusanyiko mbalimbali ama kwenye nyumba za watu wanapoamua kufanya birthday party zao ama za watoto wao nyumbani kwao.

Ili ufanikiwe katika biashara hii kwanza lazima uwe mbunifu sana. Pili lazima uwe mchangamfu na mtu wa watu. Tatu lazima uwe sio mtu wa kununa nuna mara kwa mara – cheka na kila mtu hata aliekuudhi. Uso wako usikunjwe hata kama ndani yako kuna huzuni.

Pia kuwa wa tofauti. Jaribu kutumia vitu simple ila kwa mpangilio mzuri ili vivutie watu. Tumia vyema mitandao ya kijamii kujionesha jinsi gani ulivyo mpambaji na mbunifu.

Unahitaji wastani wa laki tano kuiendea biashara hii kama utaweza kuanza polepole na kukua taratibu.

Angalizo

Mitandao ya kijamii sio sehemu ya kuweka mabango. Ni sehemu ya kuweka mada na picha za kijamii zinazovutia.

Utakuta mtu profile yake amejaza mabango ya bidhaa ama matangazo mpaka inaboa. Mwishowe anaambulia kupata like moja ama mbili ya kwake na ya mpenzi wake.

Andika mada nzuri kisha mwisho weka kijitangazo kidogo sana. Mada ikivutia watu watatembelea ukurasa wako. Ni rahisi kupata likes 300 kwenye picha ya harusi yako ila ukaambulia likes mbili kwenye tangazo la bidhaa yako.

Hivyo basi tangazo lako hakikisha unaliweka kwenye mada wanayoipenda watu.

Mfano umeweka picha za ulivyosherehekea birthday basi katika hizo picha unganisha na bidhaa yako japo katika picha moja

JINSI YA KUPIKA UFUTA

UFUTA

MAHITAJI

UFUTA kg 1 ½
Sukari ¼
Maji kiasi
Kinu na mti
Meza
Sufuria
Mwiko
Jiko
Chombo cha kuhifadhi

JINSI YA KUTENGENEZA

Chambuwa UFUTA na utoe taka taka zote kwa kupepeta

OSHA na pembuwa kutoa mchanga wote na anika

Ukikauka weka kwenye kinu na twanga kutoa kama kuna pumba zime baki kisha pepeta

Weka kwenye sufuria na bandika jikoni kisha kaanga paka uive uwe wa brown au kahawia angalia usiunguze

Epuwa na weka kwenye chombo kisafi

Bandika sufuria nyingine jikoni na weka sukari koroga paka iyeyuke yote

Mimi nia UFUTA na koroga paka uchanga nyike vizuri na sukar

Epuwa na mimina kwenye meza nawa mikono na hakikisha iko safi kisha anza kutenge neza madonge kwa ukubwa unao taka

Weka kwenye chombo safi tayari kwa kula na biashara pia

JINSI YA KUTENGENEZA MAFUTA YA WATOTO YA NAZI YA MGANDO

Mafuta ya Watoto ya Nazi ya mgando

White oil 1 Lita

Micro wax 1 lita

Pure Coconut oil 1/4 lita

Jinsi ya kutengeneza

Weka vyote jikoni kwenye sufuria na moto mdogo

Kisha ipua

Vikipoa weka kwenye  package yagande tayari kwa kutumia

JINSI YA KUTENGENEZA MAFUTA YA KUREFUSHA NYWELE

Mafuta ya kurefusha nywele

White oil 1 Lita
Micro wax 1lita
Olive oil vijiko 6

Castro oil

Majani ya mvuje vijani 10

Majani ya rosemary kichane 1

Vitunguu saum punje 6

Vitunguu maji 3

Jinsi ya kutengeneza

Yeyusha white oil na microwax ikiyeyuka
kwa moto mdogo weka  castro oil

kisha ipua weka pembeni

Chemsha olive oil vitunguu saum na vitunguu maji kisha chuja changanya vyote na vile vya kwanza koroga

Chukua tena olive oil vijiko 5 chemsha na mvuje na rosemary chuja
Changanya vyote koroga
Weka rangi ya mafuta kijani au njano
Weka perfume

Vikipoa weka kwenye  package yagande tayari kwa kutumia au kuuza

Wednesday, 14 November 2018

jinsi ya kutengeneza sabuni ya unga

*jinsi ya kutengeneza sabuni ya  unga*

*MAHITAJI*

.Optical bytina.

.sodium carbonate.

.sulphonic acid.

.Sodium sulphate.

.Hoda ash.

.Hydrogen peroxide.

.Rangi.

.Perfume.

*JINSI YA KUTENGENEZA*

Andaa chombo chochote kinachoendana na wingi wa sabuni unayotaka kutengeneza na anza kutengeneza kwa kufuata hatua zifuatazo.

.weka sodium carbonate kwenye chombo ulichoandaa kg2 na nusu.

.Baada ya hapo weka optical bytina vijiko kumi(10)vya chakula.

.halafu weka sodium sulphate vijiko vitano vya chakula.

.weka soda ash kg7 na ukoroge kwa muda wa dakika kumi.

*HATUA YA PILI*

.Sulphonic acid kilo 2 na nusu.

.nausa vijiko 15 vya chakula.

.Hydrogen peroxide kama ni ya unga weka kilo mbili kama ya maji weka lita mbili.

.rangi vijiko vitano vya chakula.

. changanya na perfume vijiko sita vya chakula.

.baada ya mchanganyiko huo anika kwenye kuvuli kwa kuwa juani inaweza kuyeyuka.sabuni yako itakauka kwa kujiachia.

Kusanya weka kwenye mifuko tayari kwa kuuza.

*ONYO: Baadhi ya malighafi ni acid kwahiyo umakini unatakiwa wakati wa kutengeneza,hakikisha mikono yako imelindwa kwa gloves na usishike acids au kula wakati unafanya kazi.Tafadhari watu wazima ndio wafanye kazi hii*

Jinsi ya kutengeneza ant -aging na whitening night cream

Jinsi ya kutengeneza ant -aging na whitening night cream.

Mahitaji

Almond
Maziwa fresh mabichi
Limao

Jinsi ya kuandaa.
Loweka almonds usiku mpaka asubuhi,
Asubuhi menya maganda yake
Anika kwenye jua
Saga almonds kwenye blender ya vitu vigumu mpaka uoate unga
Changanya unga wa almond robo kijiko na maziwa mabichi kijiko
Acha kwa masaa 2, weka drop 2 za maji ya limao.
Paka kwenye ngozi iliyooshwa.
Lala nayo
Asubuhi nawa paka mafuta kawaida na utaona matokeo baada ya week.

Fungua sehemu yako ya kuwafanyia watu facial uwe unafanya ivo na watu wataitana.

Asante.

JINSI YA KUONDOA MIKUNJO (WRINKLES ) KWENYE USO

*JINSI YA KUONDOA MIKUNJO (WRINKLES ) KWENYE USO*

*CARROT*

Tumia juisi ya carot kwa kupaka katika ngozi yako, hasa katika maeneo yaliyoathirika.

Caroti ina virutubisho muhimu kwa ngozi yako.

Pia ina uwezo mkubwa wa kuondoa sumu ndani ya ngozi.
Si hivyo tu, caroti inaweza kuondoa kabisa tatizo la mikunjo ya
ngozi hasa sehemu za pembeni ya macho, shingo na maeneo kama hayo

*Jinsi ya kufanya*

Chukua karoti, saga kwenye mashine kisha kamua ili kupata juisi yake.

Tumia pamba kupaka katika maeneo yaliyoathirika, fanya hivyo mara kwa mara, itakusaidia kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo hilo.

*MAZIWA*

Maziwa yana virutubisho vinavyochochea kunawiri kwa ngozi. 

Pia yana chembechembe za 'Alfa-Hydroxide Acid' ambazo zina uwezo mkubwa kuondoa seli zilizokufa mwilini.

Yote haya husaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo la mikunjo katika ngozi.

Unachotakiwa kufanya
Kuchukua maziwa kiasi na chovya pamba ndani yake, kisha paka maeneo yaliyoathirika.

*ALOE VERA*

Jeli ya Alovera ndiyo hasa inayotakiwa katika zoezi hili.

Chukua jani lake na kisha likate ili kupata utomvu wake.

Chukua utomvu au jeli hiyo kama wengine wanavyoita na kisha pakaa sehemu iliyoathirika, itapunguza ama kuondoa kabisa tatizo hilo.

*PARACHICHI*

'Mask' ya Parachichi husaidia kuifanya ngozi iwe na mng'ao.

Siyo hivyo tu, bali huchangia kwa kiasi kikubwa pia kuifanya ngozi iwe laini na nyororo.

Unachotakiwa kufanya
Chukua parachichi liloiva vizuri, kisha saga hadi lilainike.

Baada ya hapo pakaa sehemu iliyoathirika na acha kwa muda wa dakika 10, kisha osha sehemu hiyo uikaushe.

*PAPAI*

Mask ya Papai pia husaidia kuondoa tatizo hili.

Unachotakiwa kufanya
Chukua kipande cha papai kilichoiva na kuchanganya na kijiko kimoja cha unga wa ngano.

Pakaa sehemu iliyoathirika na kaa nayo kwa muda usiopungua dakika kumi.

Mbali na kupaka pia unaweza ukatumia kula kwani lina vitamin E kwa wingi, ambavyo ni muhimu katika ukuaji wa ngozi.

*DANZI*

Juisi ya tunda hili husaidia katika uzalishaji wa sehemu ya juu ya ngozi 'collagen'.

Danzi lina kiwango kikubwa cha vitamini C. 

Na kwa kawaida aina hii ya vitamin husaidia kuchochea ukuaji wa ‘collagen’, hivyo kuifanya ngozi yako kunawiri.

*MAJI*

Kunywa maji mengi kwani husaidia kuifanya ngozi yako iwe na unyevu muda wote.

Ikiwa utazingatia zoezi hili mikunjo kati ngozi yako itakuwa ni historia

Tuesday, 6 November 2018

jinsi ya kutengeneza sabuni ya unga

*jinsi ya kutengeneza sabuni ya  unga*

*MAHITAJI*

.Optical bytina.

.sodium carbonate.

.sulphonic acid.

.Sodium sulphate.

.Hoda ash.

.Hydrogen peroxide.

.Rangi.

.Perfume.

*JINSI YA KUTENGENEZA*

Andaa chombo chochote kinachoendana na wingi wa sabuni unayotaka kutengeneza na anza kutengeneza kwa kufuata hatua zifuatazo.

.weka sodium carbonate kwenye chombo ulichoandaa kg2 na nusu.

.Baada ya hapo weka optical bytina vijiko kumi(10)vya chakula.

.halafu weka sodium sulphate vijiko vitano vya chakula.

.weka soda ash kg7 na ukoroge kwa muda wa dakika kumi.

*HATUA YA PILI*

.Sulphonic acid kilo 2 na nusu.

.nausa vijiko 15 vya chakula.

.Hydrogen peroxide kama ni ya unga weka kilo mbili kama ya maji weka lita mbili.

.rangi vijiko vitano vya chakula.

. changanya na perfume vijiko sita vya chakula.

.baada ya mchanganyiko huo anika kwenye kuvuli kwa kuwa juani inaweza kuyeyuka.sabuni yako itakauka kwa kujiachia.

Kusanya weka kwenye mifuko tayari kwa kuuza.

*ONYO: Baadhi ya malighafi ni acid kwahiyo umakini unatakiwa wakati wa kutengeneza,hakikisha mikono yako imelindwa kwa gloves na usishike acids au kula wakati unafanya kazi.Tafadhari watu wazima ndio wafanye kazi hii*

Monday, 5 November 2018

LOSHENI (LOTION)

*LOSHENI (LOTION)*

*Hii inatengenezwa kama inavyokuwa kwa mafuta ya mgando, ila tofauti ni kama ifuatavyo*

Malighafi

White oil lita 4

Micro wax kilo 1

Pafyum (harufu) vijiko viwili (2) vya chakula
Ladha (flavour),

hapa ndipo tofauti huanza kuonekana kati ya aina moja ya loshen na aina nyingine.

Unaweza kuweka vijiko 5 kila kimoja kati ya;

= karoti
= parachichi
= choklet
=aloe vera
= limao

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO