Boga/ tango
Boga
Sukari utakisia
Hiliki kiasi
Tui utakisia
Custard powder utakisia mm nimetumia vijiko vidogo viwili.
Nimekata vipande vya kiasi boga langu na kulimenya na kuondoa zile mbegu za kati. Chukuwa sufuria weka boga lako na maji kiduchu ili lipate kuiva kidogo kwa mvuke kabla hujaweka tui lako. Ukiona linaanza kuiva bado lina ubichi ubichi weka sukari hiliki na tuli lako hivyo vyote utakisia. Wacha lichemkie mpaka kuiva na kubakia tui kiasi ndio uchukuwe ile custard kidogo changanya na maji mimina kwenye mchanganyiko wako. Wacha tena lichemkie kidogo epua itakuwa tayar. Subiri lipoe pakuwa tayar kwa kuliwa. Ukipenda utakunywa kwa uji au kutoelea na wali
No comments:
Post a Comment