Friday, 23 November 2018

FURSA ZA KIBIHASHARA

*FURSA ZA BIASHARA*

*1. Uuzaji wa nguo*

Biashara ya nguo za wakubwa na watoto inazidi kushamiri kila kukicha. Hii hutokana na watu kutaka kuenda na fashion ya mavazi.

Haina maana kuwa lazima uwe na duka kubwa la nguo ndio uweze kufanya biashara hii. Unaweza kuanza na mtaji mdogo hata laki tano ama pungufu.

Unachotakiwa kufanya ni kuyatumia maeneo ya mikusanyiko kujitengenezea wateja. Mikusanyiko iwe ya kidini, kisiasa, kijamii na kadhalika inaweza kukujengea idadi kubwa ya wateja.

Nguo za watoto pia unaweza kujijengea idadi kubwa ya wateja kuanzia kwa majirani mpaka kwenye mikusanyiko.

*2. Uuzaji wa vipodozi*

Hapa maana ya kufungua duka la vipodozi bali ni kuwa kama wakala wa bidhaa flani flani ambazo wewe umeona zina matokeo ya haraka sana katika kufanya kazi.

Unachotakiwa ni kuwa mtu wa watu – usiwe mtu mkimya sana – usiwe mtu mlweke sana – uwe mtu wa kujichanganya na watu – usiwe unajiona – uwe mtumiaji mzuri wa mitandao ya kijamii.

Unaweza anza na mtaji mdogo na kujikita na bidhaa chache na kila uwapo we stori zako iwe ni kuzisifia na uhakikishe hudanganyi na kila anaetumia apate matokeo mazuri na akikosa matokeo mazuri utafute cha kumshauri na kumsaidia.

Unahitaji mtaji mdogo tu kama laki tano ama pungufu kufanya biashara hii. Ila siri kubwa ni kujiweka smart na mwenye furaha muda wote. Picha zako kwenye mitandao ziendane na hiibiashara na ziwe zimejaa furaha na muonekano mzuri.

Watu huwa wanashindwa kuelewa kuwa hata wewe mwenyewe kwenda saluni kujiremba vizuri na kuweka picha mtandaoni ukiwa umeshikilia kipodozi flani ni njia kubwa sana ya kufikisha ujumbe na kutangaza biashara.

*3. Upambaji*

Upambaji unaweza kuwa wa kwenye tafrija mbalimbali ama kwenye mikusanyiko mbalimbali ama kwenye nyumba za watu wanapoamua kufanya birthday party zao ama za watoto wao nyumbani kwao.

Ili ufanikiwe katika biashara hii kwanza lazima uwe mbunifu sana. Pili lazima uwe mchangamfu na mtu wa watu. Tatu lazima uwe sio mtu wa kununa nuna mara kwa mara – cheka na kila mtu hata aliekuudhi. Uso wako usikunjwe hata kama ndani yako kuna huzuni.

Pia kuwa wa tofauti. Jaribu kutumia vitu simple ila kwa mpangilio mzuri ili vivutie watu. Tumia vyema mitandao ya kijamii kujionesha jinsi gani ulivyo mpambaji na mbunifu.

Unahitaji wastani wa laki tano kuiendea biashara hii kama utaweza kuanza polepole na kukua taratibu.

Angalizo

Mitandao ya kijamii sio sehemu ya kuweka mabango. Ni sehemu ya kuweka mada na picha za kijamii zinazovutia.

Utakuta mtu profile yake amejaza mabango ya bidhaa ama matangazo mpaka inaboa. Mwishowe anaambulia kupata like moja ama mbili ya kwake na ya mpenzi wake.

Andika mada nzuri kisha mwisho weka kijitangazo kidogo sana. Mada ikivutia watu watatembelea ukurasa wako. Ni rahisi kupata likes 300 kwenye picha ya harusi yako ila ukaambulia likes mbili kwenye tangazo la bidhaa yako.

Hivyo basi tangazo lako hakikisha unaliweka kwenye mada wanayoipenda watu.

Mfano umeweka picha za ulivyosherehekea birthday basi katika hizo picha unganisha na bidhaa yako japo katika picha moja

No comments:

Post a Comment

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO