*JINSI YA KUONDOA MIKUNJO (WRINKLES ) KWENYE USO*
*CARROT*
Tumia juisi ya carot kwa kupaka katika ngozi yako, hasa katika maeneo yaliyoathirika.
Caroti ina virutubisho muhimu kwa ngozi yako.
Pia ina uwezo mkubwa wa kuondoa sumu ndani ya ngozi.
Si hivyo tu, caroti inaweza kuondoa kabisa tatizo la mikunjo ya
ngozi hasa sehemu za pembeni ya macho, shingo na maeneo kama hayo
*Jinsi ya kufanya*
Chukua karoti, saga kwenye mashine kisha kamua ili kupata juisi yake.
Tumia pamba kupaka katika maeneo yaliyoathirika, fanya hivyo mara kwa mara, itakusaidia kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo hilo.
*MAZIWA*
Maziwa yana virutubisho vinavyochochea kunawiri kwa ngozi.
Pia yana chembechembe za 'Alfa-Hydroxide Acid' ambazo zina uwezo mkubwa kuondoa seli zilizokufa mwilini.
Yote haya husaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo la mikunjo katika ngozi.
Unachotakiwa kufanya
Kuchukua maziwa kiasi na chovya pamba ndani yake, kisha paka maeneo yaliyoathirika.
*ALOE VERA*
Jeli ya Alovera ndiyo hasa inayotakiwa katika zoezi hili.
Chukua jani lake na kisha likate ili kupata utomvu wake.
Chukua utomvu au jeli hiyo kama wengine wanavyoita na kisha pakaa sehemu iliyoathirika, itapunguza ama kuondoa kabisa tatizo hilo.
*PARACHICHI*
'Mask' ya Parachichi husaidia kuifanya ngozi iwe na mng'ao.
Siyo hivyo tu, bali huchangia kwa kiasi kikubwa pia kuifanya ngozi iwe laini na nyororo.
Unachotakiwa kufanya
Chukua parachichi liloiva vizuri, kisha saga hadi lilainike.
Baada ya hapo pakaa sehemu iliyoathirika na acha kwa muda wa dakika 10, kisha osha sehemu hiyo uikaushe.
*PAPAI*
Mask ya Papai pia husaidia kuondoa tatizo hili.
Unachotakiwa kufanya
Chukua kipande cha papai kilichoiva na kuchanganya na kijiko kimoja cha unga wa ngano.
Pakaa sehemu iliyoathirika na kaa nayo kwa muda usiopungua dakika kumi.
Mbali na kupaka pia unaweza ukatumia kula kwani lina vitamin E kwa wingi, ambavyo ni muhimu katika ukuaji wa ngozi.
*DANZI*
Juisi ya tunda hili husaidia katika uzalishaji wa sehemu ya juu ya ngozi 'collagen'.
Danzi lina kiwango kikubwa cha vitamini C.
Na kwa kawaida aina hii ya vitamin husaidia kuchochea ukuaji wa ‘collagen’, hivyo kuifanya ngozi yako kunawiri.
*MAJI*
Kunywa maji mengi kwani husaidia kuifanya ngozi yako iwe na unyevu muda wote.
Ikiwa utazingatia zoezi hili mikunjo kati ngozi yako itakuwa ni historia
No comments:
Post a Comment