Thursday, 30 August 2018

UTENGENEZAJI WA SUBUNI YA KUONDOA HARUFU MBAYA NA MUASHO SEHEMU ZA SIRI

Utengenezaji wa sabuni ya kuondoa harufu mbaya na muasho sehemu za Siri

Maligahafi
1*kaustiki soda
2*maji
3*griselini
4*vinegar cider
5*mafuta ya mise
6*manukato

Hatua ya kuanza

Weka kaustiki soda nusu Lita maji Lita 4 kisha weka vinegar cider nusu Lita hadi Lita 1 upendacho hapo

Kisha anza kukoroga kwenye chombo chochote cha plastiki tu koroga kwa muda wa dakika 5 na kisha acha kwa siku 3 hayo maji

Hatua inayofuata

Baada ya siku 3 chukua maji yako Yale na anza kukoroga tena na uweke griselini robo Lita ukiwa unakoroga kama dakika ,5 tena kisha acha yatulie

Baada ya kuacha maji yako sasa chemsha mafuta ya mise Lita 10 yawe katika hali ya uvuguvugu

Baada ya kupasha moto weka manukato katika mafuta na koroga kidogo kupata mchanganyiko sawa

Baada ya hapo chukua mafuta yote na uweke katika Yale maji  na anza kukoroga kwa haraka na kwa muda mfupi

Baada ya hapo weka katika maumbo na subiri kuganda kwa muda wa Massa 6 hadi 8

Nb sabuni inaganda sana ikiwa sehemu yenye upepo au baridi

Wednesday, 29 August 2018

UTENGENEZAJI WA MACHO YA NGAMIA

Karibuni macho ya ngamia

Siagi 500g
Sukari 450g
Mayai 5
Custard powder 300g
Vanilla essence 2tbsp
Unga ngano 850g
Baking powder 1½ tspn
Nutella kopo 1

Saga sukari,vanilla na siagi,halafu tia mayai na usage kwa mda wa dakika 3 hivi,kisha tia baking powder na custard powder na uchanganye kwa kijiko.halafu tia unga na uchanganye kwa mkono hadi upate donge laini

Kata vidonge vidogo vidogo size ya vishimo vya machine.

Ukimaliza washa machine  ipate moto,halafu vipange vidonge kwenye vishimo vyote,na ufinike machine viive.

Baada ya dakika tano au utakapopata signal ya kuonesha cookies zipo tayari,fungua machine na vitoe .

kwangua za pembeni zilizozidi ili upate shape nzuri.jaza nutella kwenye kila kipande na ugandishe vipande viwili.

Nb si lazima utumie nutella,waweza kutia tende au peanut butter au chochote utakachopenda

Enjoy

UTENGENEZAJI WA KASHATA ZA NAZI

*Mapishi ya kashata za nazi*
Nazi-2 cups
Sukari-1 cup
Maziwa nido-1 cup
Maji-1/2 cup
Fanya shira maji na sukari
Mpaka upate shira nzito
Kisha changanya nazi na maziwa geuza hadi iwe tayari
weka katika sinia iliyopakazwa mafuta tandaza na acha igande kisha kata mraba
Hio itakuwa rangi nyeupe
Ukipenda rangi 2 hivi👇🏼

UTENGENEZAJI WA MAFUTA YA KULAINISHA NGOZI

Utengenezaji Wa mafuta ya kulainisha ngozi

       Jamani ya mti wa ukwaju yana maajabu katika ngozi na kukufanya uwe mlaini na kukung'arisha

   Alovera
Ni aina safi ya mti wa ajabu baada ya mlonge huu alovera hutibu magonjwa yalio ndani ya mwili na kwenye ngozi

    Viazi mbatata
Huondoa makunyanzi katika ngozi na kukuweka weupe

   Asali tiba kuu ya ngozi

  Binzari au manjano

Hukufanya uwe mweupe na kung'aa

Hizo ni aina za maligahafi kuu katika mafuta yetu
👇
[

Utayarishaji

Andaa blenda na weka maji robo Lita kisha weka viazi mbatata vikubwa 2 kwa vipande vidogo vidogo vikiwa vibichi

Kisha weka asali vijiko 8 vya chakula kisha weka manjano ya unga au mbegu kama majani vijiko 5 kama mbegu ipo kama tangawizi weka moja ikiwa vipande vidogo

Baada ya hapo weka maji ya alovera kwa kukata kwa juu na  kukwangua 
Hakikisha unapata maji robo Lita
Kisha saga upate mchanganyiko laini

Baada ya hapo toa na uweke katika bakuli safi kisha chukua unga wa majani ya ukwaju weka vijiko 10 vya chakula kisha koroga paka kila siku muda wowote ikae kwa lisaa 1 au paka kama mafuta na uache yote sawa  utakua mzuri na utapendeza kama mpenz Wang🙏

Friday, 24 August 2018

NAMNA YA KUTENGENEZA SABUNI YA KUFUA AINA YA G1 YA MAJI

G1 ni aina ya sabuni inayotumika kufulia nguo bila kufikicha japo ipo ya unga ila sisi tutajifunza ya unga maji na vidonge

Utengenezaji wa sabuni ya kuloweka bila kufua ya maji

      Maligahafi
1*sulphonic
2*siles nusu
3*soda ash
4*chumvi ya jikoni
5*kaustiki soda
6*formalin
7*sodium silket

Utengenezaji

Andaa ndoo ya Lita 10 weka maji Lita 5 kisha weka kaustik soda kilo moja koroga kuelekea upande 1 kwa muda wa dakika 5

Baada ya hapo funika acha kwa siku 2

Tuesday, 21 August 2018

NAMNA YA KUTENGENEZA WINE YA NANASI

Namna ya kutengeneza wine,shampeni au mvinyuu wa nanasi

Mahitaji

Nanasi

Maji

Amila

Sukari

          Uandaaji

Menya nanasi kisha utaamua kutumia maganda au nyama za nanasi chagua kimoja ila kama unatumia nyama za nanasi usikate ule moyo wa ndani

Utengenezaji

Andaa sefuria kisha weka jikoni wenye moto wa wastani kisha weka maji Lita 5

Baada weka weka maganda au nyama za nanasi kilo 3

Acha ichemke kwa muda mrefu

Baada ya kuchemka ipua na uweke sukari vijiko 6 vya chakula koroga kwa dakika 1

Baada ya hapo weka amira vijiko 4 vya chakula kisha koroga tena kwa muda







Baada ya hapo acha ipoe

Baada ya kupoa chuja maji kwa chujio au kitambaa safi  weka katika dumu

Baada ya kuweka katika dumu funika na kila baada ya siku 5 unafunua hadi kufika siku 21 utakua mvinyu Upo tayari

Monday, 20 August 2018

ZEBRA CAKE

ZEBRA CAKE / CAKE YA MISTARI YA PUNDAMILIA :

Mahitaji:

Unga wa ngano Vikombe 2
Mafuta ya kupikia kikombe 1
Sukari kikombe 1
Mayai 4
Maziwa fresh kikombe 1
1/2 kijiko cha chai vanilla essence
Vijiko 2 Vikubwa vya unga wa Cocoa
Kijiko 1 cha chakula Baking powder

Maelezo :

Changanya pamoja sukari na mayai..hadi mchanganyiko uwe laini na kufanya povu...
Kisha mimina maziwa na mafuta na endelea kuchanganya hadi vichanganyike vizuri...

Sasa kwenye bakuli lingine kavu, changanya baking powder, Vanilla essence na unga pamoja...Ukishafanya hivyo, sasa umimine huo mchanganyiko wa unga kwenye mchanganyiko wa mayai na sukari...endelea kuchanganya...

Ukiona vyote vimekuwa kitu kimoja…gawanya huo mchanganyiko mara 2  kwenye bakuli 2 tofauti zilizo sawa kwa size...

Nusu moja weka kando mchanganyiko wa cake na nusu ya pili imwagilie unga wa cocoa na ichanganye vizuri...
Sasa kwa makini kwenye chombo cha kuokea…hapa kitapendeza mduara, ambacho utakuwa umekipaka siagi kwa wembamba na kukinyunyizia unga ili keki yetu isigande…

Chota kila mchanganyiko kijiko kimoja kimoja huku ukipangilia mchanganyiko juu kwa juu kama hapo kwenye picha. Usisubiri mchanganyiko usambae wala usitingishe chombo.

Oka keki hii kwa joto la 180 degrees C…
-Ikishaiva….itoe kwenye oven na iwache ipoe kwa dakika 10 kisha uitoe kwenye chombo na iwache ipoe zaidi ndio uikate. KAMA  UNAOKEA KWA MKAA BASI MOTO WAKO UWE WA WASTANI KAMA WA KUPALILA WALI JUU NA CHINI.

CAKE

Cake🍰 

Mahitaji

Siagi 500g
Sukari 400g
Mayai makubwa 6
Arki ya vanilla ile ya powder robo kijiko,, arki ya rose 1 tsp na arki ya hiliki 1 tsp.
Baking powder 1 tbsp
Unga utapimia kikopo kilichotoka siagi. Utapima kikopo kimoja mfuto na nusu.
Na rangi upendayo.

Weka siagi, sukari na baking powder pamoja. Anza kusaga mpaka ichanganyike vizuri. Ikisha vunja mayai yako weka, saga tena mpaka ichanganyike. Anza kuweka unga wako saga tena mpaka mchanganyiko wako uwe tayari ndio utaweka hizo arki zako na kusaga tena kidogo ili zichanganyike.

Chukuwa tray yako ipake siagi au mafuta. Chukuwa ute mchanganyiko wako punguza kidogo kwenye kibakuli then weka rangi uipendayo  changanya vizuri. Now kwenye tray weka mchanganyiko wako mweupe kwanza ikisha weka wa rangi then mweupe tena.

Kabla ya yote nimesahau oven uli washe kabla ya kuanza matayarisho kwa moto mdogo ili oven lipate ujoto. Ukisha kupaliza kuweka kwenye tray choma kwa oven at 150c. Mie huwa naweka kwa muda wa saa nzima. cooker silifungui maana ukifungua kutizama keki yako inaweza ika collapse. Kwa hio usifungue oven mpaka hilo saa moja lifike.
Ikisha kuiva toa cake yako wacha ipoe. Enjoy with coffe or tea. 😋

TIPS KUMI ZA KEKI

📎TIPS KUMI ZA KEKI:-

1. Kuoka ni sayansi hivyo ni muhimu Sana kuzingatia vipimo,hakikisha unapima kwa usahihi kila hitaji lako usiongeze wala kupunguza hitaji muhimu hasa unapojaribu kwa Mara ya kwanza

2. Hakikisha umepima kila kitu mezani kabla ya kuanza upishi wa keki,zoezi la keki ni la haraka ili kuepusha keki kuanza kuumuka kabla ya kuingia katika oven na hatimaye kupata matokeo mabaya. Pia hakikisha oven umewasha  tayari inapata moto.

3. Pendelea zaidi kuchekecha unga wako ili upate keki nyepesi na ya kuchambuka vizuri.

3.  Paka chombo chako mafuta kisha nyunyiza unga ili kurahisisha keki kutoka kwa urahisi bila kushika kwa pan au zungusha kwa karatasi ya kuokea

3. Pendelea zaidi kutumia mwiko au spatula wakati wa kutia unga ili kuepusha kupiga Sana na kuua nguvu ya baking powder, NA kama utatumia machine basi changanya kwa speed ndogo kabisa.

4. Usifungue oven yako kabla ya nusu saa ya uokaji ,ikiingia hewa wakati keki bado mbichi itanywea na kutoiva vizuri. Angalia maendeleo ya keki yako kupitia kioo cha oven yako. Kufungua fungua oven kunathiri pia moto na kuharibu keki yako

5. Acha keki ipoe katika chombo chake kwa muda wa dk 10 kisha itoe iache ipoe kabisa kabla ya kukata au kupamba. Usiache keki ipoe katika pan moja kwa moja itatengeneza unyevu na hatimaye kusumbua kutoka wakati wa kutoa..keki unazoweza kuacha zipo katika chombo chake ni zile sticky au keki za kunata zenye matunda,asali nk pia coffee cakes ambazo zinakatwa zikiwa katika chombo chake.

6. Itie keki katika freezer kwa muda wa dk 15 ikiwa wataka kuipamba itakurahisisha kupamba kwa urahisi bila kupata crumbs nyingi.

7. Zingatia moto usiwe mkali wala mdogo, moto ukiwa mkali keki itaiva kwa haraka na kupasuka pia itakuwa kavu haiwezi kuchambuka na moto ukiwa mdogo itanywea na kuiva kwa kunata ndani hivyo zingatia Sana moto. Usitegemee Sana motmaswali
ndikwa katika recipe oven zinatofautiana pima kujua moto upi sahihi kwako

8. Tumia chombo kinachoendana na kipimo cha keki yako usitumie chombo kikubwa Sana keki itaiva kwa kusambaa na kutopanda vizuri pia usitumie chombo kidogo itaiva kwa kujibana na matokeo yake kupasuka na kutochambuka vizuri.

9. Ili kujua keki yako imeaiva wakati wa kuitoa chukua kiniti safi choma Kati kikitoka safi basi keki imeiva au ibinye kwa vidole ukiona yarudi usawa basi keki imeiva pia ukiona imeachia kidogo pembezoni ni moja ya ishara ya keki kuiva.

10. Keki ikiwa imepata rangi Sana juu na bado haijaiva usipate wasi chukua kipande cha alminium foil kinachotoshea chombo chako ,paka mafuta au siagi ule upande utakaofunika kisha funika keki yako acha iendelee kuiva bila kuungua juu

Saturday, 18 August 2018

JINSI YA KUTENGENEZA MAFUTA YA KUREFUSHA NYWELE NDANI YA WEEK MOJ TU


JINSI YA KUREFUSHA NYWELE.

Malighafi;
1.Mafuta ya mnyonyo 1/4lt
2.Mafuta ya nazi 1/4lt
3.Mafuta ya mzeituni 1/4lt.

Jinsi ya kutengeneza.
Changanya malighafi zako vizur mpaka upate mchanganyiko wako bora kwenye chombo kimoja.

Matumizi.
Safisha nywele zako vizur kwa maji safi na salama.
Kisha kausha kichwa chako vizuri .
Kisha anza kupata mchanganyiko wa dawa zako vizuri na ukisha ona dawa imesha kolea vizuri unaweza suka mabutu vizur ya kulalia.
Kisha utajifunga railoni kichwani utalala nazo mpaka asubuhi.
Kisha asubuhi una fumua mabutu na kuosha nywele zako vizuri.Nakupaka mafuta yako ya kawaida ya nywele kisha unazichana.
Utafanya hivyo ndani ya wiki moja kisha utapata majibu yako vizuri kabisa bila wasi wasi yoyote.

🙏🙏🙏

Thursday, 16 August 2018

DAWA YA KUONDOA WEUSI WA KWAPA AU MADOA USONI

Dawa ya kuondoa weusi wa kwapa au madoa usoni

Maligahafi

1*maji ya limao
2*magadi soda
3* chumvi

Uandaaji

Andaa bakuli safi linaloendana na wingi wa maligahafi zako kisha weka maji ya limao vijiko 5 vya chakula kisha weka magadi soda na sio (paking powder) vijiko 2 vya chakula kisha weka chumvi kijiko 1 cha chai

Baada ya kuchanganya koroga kupata mchanganyiko sawa

         Matumizi
Osha kwa maji safi uso wako kisha chovya kitambaa chako kwenye dawa yako kisha paka kwa kusugua taratibu

Paka kila siku kabla ya kulala Mara 1 kwa siku 12 utapona

Wednesday, 15 August 2018

UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA ASILI

Utengenezaji Wa sabuni ya asili

Maligahafi
1*mafuta ya Nazi au mise
2*majivu yanayotokana na vitu asili

Angalia tumia chungu na usitumie chombo cha bati kupikia au kuhifadhia sabuni yeyote

Utengenezaji

Andaa migomba au karatasi nyeupe isio na doa ya herufi au mimea tu kisha katakata vipande na uchome moto kupata majivu

Baada ya kupata majivu mfano kilo 5

Basi itakupaswa uwe na mafuta Lita 5

Chukua majivu na uweke katika ndoo  na weka maji Lita 5 na hifadhi kwa Saa 24

Baada ya masaa 24(siku 1)  chukua kitambaa au chujio lolote na chuja maji tu ya Yale majivu

Baada ya hapo weka jikoni na acha ichemke kwa dakika 20 yani maji yawe Lita 3

Baada ya hapo weka mafuta yako na acha ichemke

Utaona povu linatoka acha tu ukiona tu kwa muda

Kisha ipua na weka katika katika maumbo yako na acha ikauke

UTENGENEZAJI WA DAWA YA NYWELE

Utengenezaji Wa dawa ya nywele

Maligahafi
1*unga Wa muhogo
2*juice ya limao
3*mafuta ya Mnyonyo

Utengenezaji

Weka sefuria jikoni ikiwa na maji nusu Lita kisha weka unga Wa muhogo vijiko 5 vya chakula acha ichemkr kwa muda ukiwa unakoroga mpaka upate uji mzito

Baada ya hapo ipua weka weka juice ya limao robo Lita koroga kisha weka mafuta ya Mnyonyo gram 200 koroga kupata mchanganyiko weka rangi na manukato kiubunifu kisha acha ipoe na upaki katika vifungashio peleka sokoni

    matumizi
Tikisa kabla ya matumizi kisha paka kuanzia kwenye ngozi ya nywele hadi juu ya nywele kisha acha kwa dakika 10 kisha osha

Hii dawa ya maajabu hukuza nywele na kuifanya kua nyeusi na kuondoa m'ba

Sunday, 12 August 2018

DAWA YA KUPUNGUZA UNENE

Dawa ya kupunguza unene

Mahitaji
1*Abdalasini
2*limao
3*tangawizi
4*majani ya mlonge

Uandaaji

Saga tangawizi au katakata vipande vidogo kisha weka katika sefuria

Baada ya hapo weka majani ya Mlonge kama kikombe 1 cha chai
Kisha weka abdalasini vijiti 8 au vifuko 2

Baada ya hapo weka maji katika sefuria Lita 2 kisha weka jiko acha ichemke mpaka kufika Lita 1

Baada ya hapo ipua na uchuje kutoa mabaki

Baada ya kuchuja katakata vipande vidogo limao bila kutoa kitu chochote hata tunda usitoe kisha weka katika maji yako uliochuja

Kisha acha kwa muda wa Massa 6 hadi 8

Baada ya huo muda chuja tena kutoa mabaki ya limao

Sasa unaweza kunywa kutengeneza umodo tena mwenye shepu ya muarubaini na sio mnazi wala mgomba😁

Usikopi masomo yangu kuwafundisha wengine nikikupata kesi

UPIKAJI WA KEKI NA VIPIMO VYAKE

Jaribu vipimo hivi:- sukari robo kg, sukari robo kg punguza kidogo, unga ngano robo kg, mayai 4 kama madogo sana weka 5, vanilla kijiko 1 cha chai,  baking powder kijiko 1 cha chakula kama unatumia kijiko cha kawaida usikijaze sana. Kisha changanya sukari na siagi  kama hauna mashine tumia mwiko ichanganye vizuri mpaka iwe laini kisha weka mayai na vanilla changanya kisha tia unga uchanganye na baking powder, changanya kisha pakaza siagi chombo chako cha kuokea mimina mchanganyiko wa cake, oka kwa dakika 40 mpaka lisaa 1, moto usiwe mkali sana

VIPIMO VYA KEKI

*Vipimo vya keki*

*Keki*
Mayai 12
Sukari 1/2
Siagi 1/2
Unga 1/2 na viganja 2

*Keki*
Mayai 10
Sukari 1/2
Siagi 1/2
Unga 1/2 na kiganja 1

*Keki*
Mayai 8
Sukari 1/2 punguza kidogo
Siagi 1/2
Unga 1/2

*Keki*
Mayai 6
Sukari 1/4
Siagi 1/4
Unga 1/4
😍😘
*Vipimo vya mkate wa mayai*

*Mkate*
Mayai 12
Sukari 1/4
Unga 1/4
Baking powder 1tbsp
Hiliki na vanilla extract

*Mkate*
Mayai 10
Sukari 1/4
Unga 1/4
Baking powder, hiliki na vanilla extract

*Mkate*
Mayai 8
Sukari 1/4
Unga 1/4
Baking powder, hiliki na vanilla extract

*Mkate*
Mayai 6
Sukari 1/4 punguza kidogo
Unga 1/4
Baking powder, hiliki na vanilla extract

*KIDOKEZO*
Ktk mkate wa mayai ikiwa mayai ni 12 utatia unga vijiko vya kulia 12, km mayai 10 utatia unga vijiko 10, km mayai 8 utatia unga vijiko 8 na km mayai 6 utatia unga vijiko 6. For a good result follow this instructions😘😘

VIPIMO VYA KEKI KWA MAHITAJI TOFAUTI

*KEKI*

*VIPIMO VYA KEKI KWA MAHITAJI TOFAUTI*

1)siagi 1cup
    Sukari 1cup
Unga 2cups
Maziwa 1/2cup
Mayai 4
Baking powder 1kjk
Ark kdg

2)unga 1 1/2cup
Siagi 10vjk vdg
Sukari 1/2cup
B/p 1 3/4
Mayai 2
Vanilla 1/2kjk

3)unga 850gm
Siagi 450gm
Sukari 425gm
Mayai 10
B/p 1kjk
Vanilla 1kjk

4)keki ya mayai 6 nakupa vipimo tofauti

1)siagi 200gm
Unga 2vkmb
Sukari 1kikombe
Vanillah 1/2kjk
Mayai 6
B/p 2kjk

2)unga wa ngano 2cups
Siagi 1cup
Mayai 6
Sukari 1cup
B/p 1kjk

Sikuzote degree ya Ku bake cake huwa
300°_400Cdegree

Ndondoo za upikaji keki
Sukari nyeupe ndio nzuri sana kwa keki

Maziwa mazuri ya unga

Tumia sufuria zito au treya nzito kdg ambyo haina mikwaruzo

Pendele kuchekecha unga

Wednesday, 8 August 2018

UTEGENEZAJI WA DAWA KWA AJILI YA HEDHI

Maligahafi
1*tunda la parachichi
2*mbegu za mlonge
3*uji

Hatua ya kuanza

Chukua mbegu ya parachichi saga katika blenda ya mkono kupata unga

Tafuta mbegu za mlonge zilizo kauka na twanga kupata unga laini

Pika uji wowote kisha weka katika bakuli safi

Weka unga wa parachichi vijiko 2 vya chakula

Kisha weka unga wa mlonge kijiko 1 cha chakula

Tumia Mara 2 kwa siku 14

Mwenye kukosa hedhi kwa wakati

Mwenye kukosa hamu ya kula

Mwenye hedhi iliyo pitiliza

Tumia dawa hii

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO