ZEBRA CAKE / CAKE YA MISTARI YA PUNDAMILIA :
Mahitaji:
Unga wa ngano Vikombe 2
Mafuta ya kupikia kikombe 1
Sukari kikombe 1
Mayai 4
Maziwa fresh kikombe 1
1/2 kijiko cha chai vanilla essence
Vijiko 2 Vikubwa vya unga wa Cocoa
Kijiko 1 cha chakula Baking powder
Maelezo :
Changanya pamoja sukari na mayai..hadi mchanganyiko uwe laini na kufanya povu...
Kisha mimina maziwa na mafuta na endelea kuchanganya hadi vichanganyike vizuri...
Sasa kwenye bakuli lingine kavu, changanya baking powder, Vanilla essence na unga pamoja...Ukishafanya hivyo, sasa umimine huo mchanganyiko wa unga kwenye mchanganyiko wa mayai na sukari...endelea kuchanganya...
Ukiona vyote vimekuwa kitu kimoja…gawanya huo mchanganyiko mara 2 kwenye bakuli 2 tofauti zilizo sawa kwa size...
Nusu moja weka kando mchanganyiko wa cake na nusu ya pili imwagilie unga wa cocoa na ichanganye vizuri...
Sasa kwa makini kwenye chombo cha kuokea…hapa kitapendeza mduara, ambacho utakuwa umekipaka siagi kwa wembamba na kukinyunyizia unga ili keki yetu isigande…
Chota kila mchanganyiko kijiko kimoja kimoja huku ukipangilia mchanganyiko juu kwa juu kama hapo kwenye picha. Usisubiri mchanganyiko usambae wala usitingishe chombo.
Oka keki hii kwa joto la 180 degrees C…
-Ikishaiva….itoe kwenye oven na iwache ipoe kwa dakika 10 kisha uitoe kwenye chombo na iwache ipoe zaidi ndio uikate. KAMA UNAOKEA KWA MKAA BASI MOTO WAKO UWE WA WASTANI KAMA WA KUPALILA WALI JUU NA CHINI.
No comments:
Post a Comment