Friday, 21 September 2018

GREENHOUSE NA FAIDA ZAKE

GREENHOUSE

*Maana Ya Greenhouse Ni Nini?*
Hii Ni Nyumba Maalum , Iliyosanifiwa Na Ambayo Hutumia Mwanga  Wa Asili Ndani Yake Na Kutengeneza Mazingira Mahususi, Kama Joto  Maalum Kwa Mazao Ya Mbogamboga Na Matunda ( Nyanya, Hoho, Tango , Tikiti Maji N.K) Vile Vile Hutumika Kwa Ajili Ya Utafiti Na Kuepusha Mimea Iliyomo Ndani Kushambuliwa Na Wagonjwa Pamoja Na Wadudu.

*Tofauti Ya Greenhouse Na Net House*

Kiusanifu Na Kiujenzi Hakuna Tofauti Ya Greenhouse Na Net House , Bali Tofauti Pekee Ni Matilio Yanayotumika Kufunika Nyumba Iliyosanifiwa,
-Huitwa Greenhouse Sababu Imefunikwa Na Matilio Yajulikanayo Kama Greenhouse Cover/ Plastic Film /Glass N.K
-Huitwa Net House Sababu Hufunikwa Na Matilio Yajulikanayo Kama Net Maalum( Agricultural Net) Ambayo Ni Maalum Kwa Kilimo Kama Nilivyoeleza Huko Juu.
- Faida Za Zinazopatikana Kwenye Greenhouse Na Net House Ni Sawa
- Utofauti Mwingine Wa Greenhouse Na Net House Ni Kuwa Mvua Ikinyesha Kiasi Cha Maji Katika Net House Kitaingia Ndani Lakini Kwenye Greenhouse Maji  Hayaingii Ndani
-Vilevile Kuna Greenhouse Mseto Hii , Hutengenezwa Kwa Kuchanganya Matilio Ya Poly Cover /Greenhouse Cover Na Net Na Hii Ndio Maarufu Sana  Nchini Tanzania Hasa Kwa Wajasiliamali Wadogowadogo Na Wa Kati.
*Lakini kwa majibu mafupi tu ni kwamba tofauti ya Greenhouse na Nethouse ni kwamba Greenhouse ni kwa ajili ya sehemu zenye baridi na Nethouse ni kwaajili ya sehemu zenye joto* .

Kwanza tuanze kwa kupata tafsiri ya neno lenyewe, Greenhouse imekua ikipatiwa majina tofauti tofauti, wapo watu wanaiita Nyumba ya Kijani, wengine wanaiita Banda Kitalu n.k Vyovyote utakavyopenda kuiita teknolojia hii, cha muhimu ni kuelewa nini hasa maana yake.
Greenhouse(Banda Kitalu):  ni teknolojia ya kuipatia mimea mazingira mazuri ambayo yataisaidia mimea/mazao kumea vizuri na kua na uzao mkubwa, mimea hii inapandwa kwenye banda, au nyumba maalumu. Teknolojia hii inatumika hasa kuikinga mimea usiathiriwe na mazingira haribifu ya hali ya hewa. Mazingira haribifu ni kama upepo mkali, baridi kali, mvua kubwa, au mvua za mawe, mionzi mikali ya jua, joto kali , wadudu pamoja na magonjwa. Hayo ndio mazingira ambayo teknolojia hii inaleta suluhisho, kuhakikisha mimea inastawi vizuri bila ya kuathiriwa na moja ya matatizo hayo yaliyotajwa.

Teknolojia hii ilivumbuliwa huko kwenye nchi baridi, zaidi ya karne moja na nusu (miaka 150) iliyopita. Nchi zilizopo ukanda wa baridi, mazao ya kitropiki (mazao yanayo pendelea joto) ilikua haiwezekani kabisa kulimwa maeneo hayo ya ukanda wa baridi. Ndipo hapo wazo la kuvumbua Greenhouse lilipoibuka. Nchi hizi walianza kutumia teknolojia hii maana nyumba hii ya kijani ilikua ina uwezo wa kutunza joto, na hivyo wakaanza kulima mazao ya ukanda wa joto kama mbogamboga (nyanya, hoho) na matunda. Pamoja na teknolojia hii kuanza kitambo kidogo katika nchi zilizoendelea, lakini kwa upande wa nchi zinazoendelea bado teknolojia hii ni mpya kwa watu wengi.  Teknolojia hii pia inatumika katika nchi za joto, japo kuna utofauti  kati yake na  zile za nchi za ukanda wa baridi.
Faida za Greenhouse
1.     Mavuno yanakua mara 10 hadi 12 zaidi ya kilimo cha eneo la wazi, ikitegemea aina ya mazao yanayolimwa humo, aina greenhouse pamoja na vifaa vya kudhibiti mazingira ya ndani ya greenhouse.
2.     Uhakika wa kuvuna mazao unaongezeka. Maana Greenhouse inaweza kuzuia visababishi vya  uharibifu wa mazao.
3.     Uzalishaji wa mazao katika kipindi chote cha  mwaka, maana huhitaji kusubiri mpaka msimu wa zao ufike ndio ulime.
4.     Uwezo wa kuzalisha kipindi ambacho sio cha msimu (off- season) kwa vile kipindi hiki watu wengi hawazalishi kutokana na mazingira kutoruhusu,  ukiwa na greenhouse una uwezo wa kuzalisha kipindi hicho na ukapata bei ya juu na
5.     Ufanisi katika utumaji wa dawa, viwatilifu katika kudhibiti.
6.     Matumizi ya maji ni madogo sana na udhibiti  wake  ni rahisi. Miundombinu ya umwagiliaji inayotumika hapa ni umwagiliaji wa matone (drip irrigation) ambapo maji yanakwenda pale penye mmea pekee.
7.     Uwezo wa kutunza mimea inayozalishwa maabara kutokana na teknolojia ya tishu (tissue culture technology) mimea inapotoka maabara kabla haijapelekwa shambani inatunzwa kwanza kwenye greenhouse maalumu kwa ajili  ya kuzoea mazingira ya nje kwanza.
8.     Uwezo wa kupanda mimea bila kutumia udongo (soilless culture).  Kutokana na changamoto ya magonjwa na vijidudu vya kwenye udongo kama Nematodes, ndipo uvumbuzi  wa teknolojia ya kupanda mimea kwa kutokutumia udongo ulipotokea


Baadhi ya Nchi zinazofanya vizuri kilimo cha  Greenhouse.
·        Kuna nchi zaidi ya 50 katika dunia ambapo kilimo kinalimwa kwenye greenhouse. Tutaangalia baadhi ya nchi ambazo zimekua zikifanya vizuri kupitia teknolojia hii. Tuanze na Marekani, Marekani  ina eneo takribani 4000 hekta ambazo zina greenhouse kwa ajili ya kilimo cha maua, Marekani kupitia kilimo hicho wanapata pato la zaidi ya Dola bilioni 2.8 (zaidi ya trilioni 5 hela za Tz) kwa mwaka. Nchini Hispania inakadiriwa zaidi 25,000hekta na Italia ni hekta 18,500, zimefungwa  greenhouse kwa kilimo cha pilipili hoho, strawberry, matango, maharagwe machanga,  pamoja na nyanya. Canada greenhouse ni kwa kilimo cha maua na mboga mboga wakati ambapo  hazilimwi kwingine. Mazao maarufu  yanayolimwa kwenye Greenhouse za Canada kama nyanya, matango na hoho.
·        Uholanzi ni zaidi ya hecta 89,600 zipo nchini ya greenhouse. Uholanzi sekta ya greenhouse ndio iliyo bora zaidi duniani. Uholanzi ndio nchi inayoongoza kwa  teknolojia hii na wamepiga hatua mbali sana. Yapo makampuni makubwa ya Kiholanzi yanayotumia teknolojia hii baadhi yao yapo hapa Tanzania katika kilimo cha maua, matunda, mbogamboga, pamoja na mbegu. Mfano : CHAKULACOM, Kili Hortex, Multi flower, Mount Meru Flower, Enza Zaden, RJK ZWAAN (Q-SEM na AFRISEM)
·        Israel: 15000 hekta. Israel ndiyo nchi inayoongoza kwa kuuza maua (cut flowers) nje ya nchi. Japokuwa  nchi ya Israel eneo lake ni kubwa ni jangwa. Pia Nchi ya Israel imekua moja ya nchi zilizopo mstari wa mbele katika teknolojia ya umwagiliaji na Greenhouse. 

·        Uturuki: hekta 10,000 zinalimwa maua na mbogamboga kwa kutumia teknolojia hii ya Green house. Saudi Arabia: 90% ya mazao yanya na tango yanalimwa kwenye green house. Misri  10,000 hekta nyanya, matango na pilipili hoho. Teknolojia ya Greenhouse nchini China inakua kwa kasi sana kuliko nchi yeyote  duniani. Japokuwa teknolojia hii haijaanza muda mrefu kivile huko China lakini mpaka sasa zaidi ya hekta 48,000 tayari zimefungwa Greenhouse.  Nchi nyingine zinzofanya vizuri barani Asia ni kama  Japan (40,000hekta) na Korea kusini (21,000 hekta).

Aina za Greenhouse.
Greenhouse zinagawanyika makundi mbalimbali kutegemeana na vigezo vifuatavyo:
1.     Aina za Greenhouse kwa  kigezo cha sura/umbile (shape)
Zipo aina aina 8 za greenhouse, hapa nitataja chache tu kwa majina yake ya kitaalamu
·        Quonset Greenhouse
·        Saw tooth type
·        Even span type greenhouse
·        Uneven span type greenhouse

2.     Aina za Greenhouse kwa kigezo cha Matumizi
·        Green house zinazoongeza joto (Hizi ni kwa maeneo ya baridi)
·        Greenhouse zinazopunguza joto (hizi ni kwa maeneo ya joto)

3.     Aina za greenhouse kwa kigezo cha matengenezo yake (construction)
·        Greenhouse za miti (Wooden framed structure)
·        Pipe framed structure (Greenhouse zinazotumia mabomba)
·        Truss/Aluminium framed structure ( Geenhouse zinazojengwa kwa vyuma

4.     Aina za Greenhouse kwa kigezo  aina ya zana za ufunikaji (covering types)
·        Greenhouse zinazofunikwa kwa  zana za Vioo (glass)- hizi zinatumika sana maeneo ya baridi kali, ili kutunza joto kwa muda mrefu ndani   greenhouse
·        Greenhouse zinazofunikwa kwa mifuko ya plaski (plastic film)

5.     Aina ya Greenhouse kwa kigezo cha uwekezaji unaofanywa
·        Greenhouse za gharama kubwa (High cost greenhouse) ( Zaidi ya milioni 50)
·        Greenhouse za gharama za kati (medium cost greenhouse) (milioni 20 hadi 50)
·        Greenhouse za gharama ndogo (Low cost greenhouse) (chini ya milioni 20)

Kwa hapa Tanzania Chakulacom tunajenga  Greenhouse na  Nethouse za gharama nafuu tukiwa tumepunguza 20% ya gharama za ujenzi wa kawaida hii inatokana punguzo la kodi na dhamira ya dhati ya serikali katika kuinua uchumi wa mkulima wa Tanzania hivyo karibuni wakulima mchangamikie fursa hi kupitia Chakulacom.

Endelea kufwatilia somo la Greenhouse/Nethouse litaendelea tukielezea faida za kiuchumi kwa baadhi ya mazao......


Kilimo Cha Greenhouse , Huzalisha Faida Kubwa Katika Eneo Dogo Sana Kulinganisha Na Eneo La Wazi

*1.Zao La Nyanya* 
Katika Zao La Nyanya Kuna Aina Mbalimbali Za Nyanya Zinazopandwa Katika Greenhouse , Mimi Nitaelezea Nyanya Iitwayo Kwa Kitaalam “ Montezoul” Inayozalishwa Na Kampuni Ya Kiholanzi Iitwayo “ Afrisem”

Mbegu Ya Montezoul , Hutoa Kilo 25 Kwa Mche Mmoja Ambao Toka Upandwe Hadi Kung’olewa Shambani Huchukua Miezi 6, Yaani Siku 21 Za Kuotesha Miche , Miezi Miwili Na Nusu Matunda Kukomaa Na Miezi Mitatu Mfululizo Ni Ya Kuvuna Tu.

*Mfano : 1,*
Kwa Greenhouse Ya Ukubwa  120m2( Yaani Upana Mita 8 Na Urefu Mita 15), Greenhouse Hii Ina Kuwa Na Jumla Ya Matuta 6, Yenye Urefu Wa Mita 14 Kila Tuta.
-Katika Tuta 1, Zitafungwa Mipira 2 Ya Umwagiliaji ( Double Line)
- Ikiwa Upandaji Wa Kutoka Mche Kwenda Mche Itakuwa Ni Sentimita 50 Kwa Mujibu Wa Maelekezo Ya Mbegu
- Katika Tuta Moja Tutapata Miche 56 Ya Nyanya
- Kwa Matuta 6 Tutakuwa Na Miche 336 Ya Nyanya
- Miche 336 Ya Nyanya Ni Sawa Na Kilo 8400 Za Nyanya Zitakazo Patikana Katika Greenhouse Ya Ukubwa Wa 120m2.
- Kwa Bei Ya Kawaida Sokoni Kilo Moja Huuzwa Tsh 1000- 1500/=
- Chukua Kilo 8400 Kwa Tsh 1000 Utapata Milioni 8,400,000/= Kwa Muda Wa Miezi 3
-Ukipata Soko Zuri Bei Itakuwa Mara Mbili Ama Tatu Ya Bei Ya Kawaida , Na Kwa Kipindi Nyanya Ni Adimu Ukipiga Kwa Kilo Moja Ni Tsh 4000, Hivyo Anatarajiwa Kuingiza  33,600,000/=

*Mfano 2,*
Greenhouse Ya Ukubwa Wa 480m2(Yaani Upana Mita 16 Na Urefu Mita 30)
Hii Inakuwa Na Jumla Ya Matuta 12 Yenye Urefu Wa Mita 29 Kila Tuta
-Katika Kila Tuta Itafungwa Mipira 2 Ya Umwagiliaji Yaani (Double Line)
-Kwa Upandaji Wa Hatua 50sentimita Kutoka Mche 1 Kwenda Mche Mwingine
-Kila Tuta Moja Itaingia Miche 116 Ya Nyanya
-Kwa Matuta 12 Tutakuwa Na Miche 1392
-Miche 1392 Ni Sawa Na Kilo 34,800 Za Nyanya
-Kwa Bei Ya Kawaida Sokoni Kilo Moja Huuzwa Tsh 1000-1500
-Chukua Kilo 34800 Kwa Tsh 1000/= Utapata Tsh 34,800,000/= Kwa Muda Wa Miezi 3 Ya Kuvuna Na Kuuza Tu.
-Ukipata Soko Zuri Bei Itakuwa Mara 2 Ama 3 Ya Bei Ya Kawaida Katika Soko La Kawaida Katika Halmashauri Zetu, Ukivuna kipindi ambacho Nyanya Ni Adimu Bei Imefika Hadi 4000 Kwa Kilo 1, Sasa Chukua Kilo 34,800 Kwa Tsh 4000 Utapata Tsh 139,200,000/= ( Kilimo Cha Kisasa Kinalipa Sana, Utajiri Tumeulalia)

*2. Zao La Tango*

Katika Zao La Tango  Kuna Aina Mbalimbali Za Tango Zinazopandwa Katika Greenhouse , Mimi Nitaelezea Tango  Liitwalo Kwa Kitaalam “ Midas” Inayozalishwa Na Kampuni Ya Kiholanzi Iitwayo “ Afrisem”

Mbegu Ya Midas , Hutoa Kilo 30 -55 Kwa Mche Mmoja Ambao Toka Upandwe Hadi Kung’olewa Shambani Huchukua Miezi Takribani 6, Yaani Mbegu Ikishapandwa Baada Ya Siku 45 Unaanza Kuvuna ,  Na Miezi Mitatu Mfululizo Ni Ya Kuvuna Tu.

*Mfano : 1*,
Kwa Greenhouse Ya Ukubwa  120m2 ( Yaani Upana Mita 8 Na Urefu Mita 15), Greenhouse Hii Ina Kuwa Na Jumla Ya Matuta 6, Yenye Urefu Wa Mita 14 Kila Tuta.
-Katika Tuta 1, Zitafungwa Mipira 2 Ya Umwagiliaji ( Double Line)
- Ikiwa Upandaji Wa Kutoka Mche Kwenda Mche Itakuwa Ni Sentimita 50 Kwa Mujibu Wa Maelekezo Ya Mbegu
- Katika Tuta Moja Tutapata Miche 56 Ya Tango
- Kwa Matuta 6 Tutakuwa Na Miche 336 Ya Tango
- Miche 336 Ya Tango  Ni Sawa Na Kilo 13440( Nimetumia Kilo 40 Kila Mche) Za Tango Zitakazo Patikana Katika Greenhouse Ya Ukubwa Wa 120m2.
- Kwa Bei Ya Kawaida Sokoni  Tango Moja Huuzwa Tsh 500
- Chukua Kilo  13440 Kwa Tsh 500 Utapata Milioni 6,720,000/= Kwa Muda Wa Miezi 3
-Ukipata Soko Zuri Bei Itakuwa Mara Mbili Ama Tatu Ya Bei Ya Kawaida.

*Mfano 2,*
Greenhouse Ya Ukubwa Wa 480m2(Yaani Upana Mita 16 Na Urefu Mita 30)
Hii Inakuwa Na Jumla Ya Matuta 12 Yenye Urefu Wa Mita 29 Kila Tuta
-Katika Kila Tuta Itafungwa Mipira 2 Ya Umwagiliaji Yaani (Double Line)
-Kwa Upandaji Wa Hatua 50 Sentimita Kutoka Mche 1 Kwenda Mche Mwingine.
-Kila Tuta Moja Itaingia Miche 116 Ya Tango
-Kwa Matuta 12 Tutakuwa Na Miche 1392
-Miche 1392 Ni Sawa Na Kilo 55,680 Za Tango
-Kwa Bei Ya Kawaida Sokoni Kilo Moja Huuzwa Tsh 500
-Chukua Kilo 55680 Kwa Tsh 500/= Utapata Tsh 27,840,000/= Kwa Muda Wa Miezi 3ya Kuvuna Na Kuuza Tu.
-Ukipata Soko Zuri Bei Itakuwa Mara 2 Ama 3 Ya Bei Ya Kawaida Katika Soko La Kawaida.

*3. Zao La Hoho*
Katika Zao La Hoho Kuna Aina Mbalimbali Za Hoho Zinazopandwa Katika Greenhouse , Mimi Nitaelezea Zote Aina Tatu Kwa Ujumla Wake, Hoho Za Kijani Ziitwazo “Redjet” , Hoho Nyekundu Ziitwazo “Perisela” Na Hoho Za Njano Ziitwazo ”Ilanga” Zinazozalishwa Na Kampuni Ya Kiholanzi Iitwayo “ Afrisem”

Mbegu Ya Hizi , Hutoa Kilo 11 Kwa Mche Mmoja Ambao Toka Upandwe Hadi Kung’olewa Shambani Huchukua Miezi 6, Yaani Siku 24 Za Kuotesha Miche , Miezi Miwili Na Nusu Matunda Kukomaa Na Miezi Mitatu Mfululizo Ni Ya Kuvuna Tu.

*Mfano : 1*,
Kwa Greenhouse Ya Ukubwa  120m2 ( Yaani Upana Mita 8 Na Urefu Mita 15), Greenhouse Hii Ina Kuwa Na Jumla Ya Matuta 6, Yenye Urefu Wa Mita 14 Kila Tuta.
-Katika Tuta 1, Zitafungwa Mipira 2 Ya Umwagiliaji ( Double Line)
- Ikiwa Upandaji Wa Kutoka Mche Kwenda Mche Itakuwa Ni Sentimita 40 Kwa Mujibu Wa Maelekezo Ya Mbegu
- Katika Tuta Moja Tutapata Miche 70 Ya Hoho
- Kwa Matuta 6 Tutakuwa Na Miche 420 Ya Hoho
- Miche 420 Ya Hoho  Ni Sawa Na Kilo 4620 ( Nimetumia Kilo 11 Kila Mche) Za Hoho Zitakazo Patikana Katika Greenhouse Ya Ukubwa Wa 120m2.
- Kwa Bei Ya Kawaida Sokoni  Hoho , Kilo Moja Huuzwa Tsh 3000
- Chukua Kilo 4620 Kwa Tsh 3000 Utapata Milioni 13,860,000/= Kwa Muda Wa Miezi 3.
-Ukipata Soko Zuri Bei Itakuwa Mara Mbili Ama Tatu Ya Bei Ya Kawaida , Na Kwa Kipindi Hiki , Kwa Jiji La Dar Es Salaam Hasa Hoho Za Rangi Kilo Inafika Hadi 9000, Hivyo Ukichukua  Kilo 4620 Kwa Tsh 5000 Utapata Tsh 23,100,000/=

*Mfano 2,*
Greenhouse Ya Ukubwa Wa 480m2(Yaani Upana Mita 16 Na Urefu Mita 30).
Hii Inakuwa Na Jumla Ya Matuta 12 Yenye Urefu Wa Mita 29 Kila Tuta
-Katika Kila Tuta Itafungwa Mipira 2 Ya Umwagiliaji Yaani (Double Line)
-Kwa Upandaji Wa Hatua 40sentimita Kutoka Mche 1 Kwenda Mche Mwingine.
-Kila Tuta Moja Itaingia Miche 145 Ya Hoho
-Kwa Matuta 12 Tutakuwa Na Miche 1740
-Miche 1740 Ni Sawa Na Kilo 19140 Za Hoho
-Kwa Bei Ya Kawaida Sokoni Kilo Moja Huuzwa Tsh 3000
-Chukua Kilo 19140 Kwa Tsh 3000/= Utapata Tsh 57,420,000/= Kwa Muda Wa Miezi 3 Ya Kuvuna Na Kuuza Tu.
- Na Kwa Kipindi Hiki , Kwa Jiji La Dar Es Salaam Hasa Hoho Za Rangi Kilo Inafika Hadi 9000, Hivyo Ukichukua  Kilo 19140 Kwa Tsh 5000 Utapata Tsh 95,700,000/=

Pamoja na offer ya 20% Chakulacom tutakuunganisha na soko la uhakika ambalo sisi tuna mkataba nalo hivyo jukumu la wapi utauza bidhaa yako ni lakwetu.

Pia tuta ukatia Bima mradi wako ili kuepuka hasara zisizo zuilika Kama Moto,Mafuriko n.k

No comments:

Post a Comment

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO