Saturday, 22 September 2018

MVINYO WA ROSELA

1 MVINYO WA ROSELA

Mvinyo  ni kinywaji kinachotengenezwa kutokana na juisi za matunda kama vile ndizi mbivu ,machunga ,mapapai,mapera ,zabibu,malimao n.k., pia mvinyo unaweza kutengenezwa kwa kutumia juisi za matunda mchanganyiko kama ndizi na karoti,zabibu na karoti na machungwa nk.

Ili kupata mvinyo ,kuna njia za kikemikali zinazoendelea wakati sukari za hamira vinapochanganyika vikasaidiwa na viambaupishi vingine vinavyotumika .Kazi za viambaupishi vinavyotumika ni:

Juisi ya matunda  - Juisi ina sukari ambayo huchachuliwa kupata alkoholi na kemikali nyingine ambazo husababisha mvinyo uwe kama unavyotakiwa.Juisi ya machungwa na malimao – Hii hutumika kurekebisha kiwango cha tindikali katika juisi kinachotakiwa katika kuchachua .Kiwango cha tindikali kinachotakiwa katika  juisi wakati wa kuanza kuchachua ni 3.2 -3.5 .Kama juisi ina kiasi hicho cha tio na pia kuwezesha mvinyondikali hatuongezi limao wala chungwa .Pia citric acid yaweza kutumika badala ya malimao na machungwa.Sukari- Hii hutumika kuongeza kiwango cha sukari kinachotakiwa kuzalisha mvinyo na pia kuwezesha mvinyo kuwekwa katika makundi ya mvinyo mtamu au mkavu .Kipimo cha sukari hurekebishwa kwa kusoma  kiasi kilichomo kwa kutumia ballingmeter .Kabla ya kuanza kuchachua ,sukari katika juisi inatakiwa iwe kati ya 18– 250B. Baada ya mvinyo kuchachuaka sukari inatakiwa isomeke kati ya 0.5 – 50BChai – Hutoa kemikali inayoitwa ‘tannin’ ambayo husaidia katika kuimarisha mvinyo katika uchachukaji,ladha yake na rangi .Kemikali hii pia hupatikana katika matunda kama zabibu nk.Hamira – Hii   ndio hutumika kuchachua .Hamira ni chembechembe wanaobadilisha sukari iliyoyeyushwa kupata alkoholi.Viinilishe vya hamira – Viinilishe hivi viko mfumo wa noitrojeni katika kemikali inayoitwa ‘diammonium phosphate {DAP}’ na huuzwa  katika hali  ya vidonge .Kazi yake ni kuongezea nguvu hamira ambayo huzaliana na kuongezeka . Ongezeko  hili huimarisha nguvu ya uchachuaji .Kiasi  cha matumizi ni gramu 10 kwa lita 20 za juisi.Campden tablet – Hivi ni vidonge ambayo hutumika kusafishia vyombo na kuhifadhia mvinyo .Vidonge hivi ni kemikali hii hutumika katika kiasi cha gramu 2.5 kwa kilo 20 za matunda , wakati ya kusaga ni gram 0.6 kwa kila lita 10 za mvinyo baada ya kuchachuka . Kusafisha vyombo mfano chupa nk. Changanya  maji na metabisulphite 2%.Maji – Hutumika kuongeza  wingi wa mvinyo na kuyeyushia baadhi ya viambaupishi .Maji yatumikayo lazima yawe yenye usafi wa kunywewa.Dawa za kusafisha mvinyo  {fining agents} – Gelatine Yeyusha gramu 6 kwa maji moto kasha weka kwenye lita 100 za juisi kuondoa viini vinavyoelea vilivyosalia kwenye juisi .Hakikisha umechanganya  ‘geletine’ na juisi sawasawa.Tuliza mchanganyiko huo usiku kucha,kasha mimina juisi taratibu ukiacha masimbi chini .Baada ya hapo zoezi la kuchachua kama kawaida.

‘Pectolyclic enzyme’ –Hufanya kazi kama ‘Gelatine’ kiasi cha matumizi ni gramu 0.5 kwa lita 100 za juisi.

‘Bentonite’ Hutumika kusafisha mvinyo  baada ya kuchuja kwa mara ya kwanza {1 raking} ,kipimo ningramu 75 kwa lita 100 za mvinyo {Yeyusha gramu 75 kwenye maji ya moto 800C,kiasi cha mililita 750} Uyryushaji huu ufanyike masaa 12 kabla ya matumizi baada ya wiki 2  chuja tena {2nd raking}.

2 VIFAA VITUMIKAVYO KATIKA KUZALISHA MVINYO

Sufuria kubwa la kuchemshia juisiChujio la plastiki au chuma cha puaVyombo vya kuchachulia kama ndoo madumu nk.Mwiko wenye urefu wa kutoshaMirija ya kuchachuliaPima maji {hydrometer}Jagi la kuchukulia sampuliChupa au kikombe cha kupimia majimaji chenye ujazo wa mililita 250 -500KipimajotoKipimajotoKipimatindikaliMizani 2,moja ya uzito wa gram 0- 250,nyingine kg 0-25Mrija wa kunyonyea wenye urefu wa mita 1.5Kitambaa cheupe cha pamba cha chujio {filter with filterpads}

Matatizo yanayoweza kutokea wakati wa uzalishaji wa mvinyo kutokana na kutokufuata au kukosea taratibu

TATIZO

SABABU

MAREKEBISHO

Uchachukaji kukoma kabla ya wakati

Kusahau  kuongeza virutubisho vya hamira au tindikali

Juisi inayoanza kuchachuliwa inapokuwa ni ya baridi sana au joto

Hewa ya kabonidayoksaidi imekuwa nyingi

Ongeza tindikali virutubisho

Kuweka madumu ya kuchachulia mahali penye joto linalokubalika

Mwaga mvinyo katika chombo kisafi kwa nguvu iwezekanavyo {vigorously} ili hewa itoke ,pia ongeza virutubisho vya hamira.

Harufu isiyofurahisha kutokea

Vyombo vichafu vilitumika

Uchujaji haukufanyika vya kutosha na kwa wakati.

Usiache mvinyo ukakaa muda mrefu na masimbi au hamira waliokufa

Mvinyo kuwa na ladha ya siki

Vyombo vya kuchachulia havikusafishwa sawasaw au kuchemshwa.

Hewa iliachiwa ikaingia wakati wa uzalishaji.

Mvinyo haufai tena ,mwaga na kusafisha vyombo sawasawa.

3 MAMBO YA KUZINGATIA

Osha vyombo sawasawa mara tu ukimaliza kuvitumiaTumia hamira inayofaaWakati wote yeyusha sukari ndio utumie kutengenezea mvinyoUsizidishe sukari unapoanza kuchachuaChuja mvinyo katika vipindi na wakati muafaka ongeza campden tablets {saga na kuyeyusha katika maji kidogo} kila wakati unapochuja.Usifungashe mvinyo kwenye chupa mpaka uhakikishe umechachuka inavyotakiwa.

Bidhaa nyingine zinazotokana na utengenezaji wa mivinyo ni siki na champagne .

Matumizi ya mvinyo

Kinywaji  -kuongeza hamu ya kula na sacrament kanisaniDawa        - kuongeza vitamin {B Complex} na kusafisha kidondaKujipatia kipato

MVINYO WA ROSELA {Roselle Alcoholie Beverage}

Viambaupishi kwa lita 10 za juisi ya rosella

Mauwa ya rosella……………………..200kgSukari…………………………………3kgHamira……………………………….20gmChai………………………………….1 cup {250ml}

Hamira mama

Limao ……………………………………Chungwa…………………………………Hamira……………………………………Juisi ya rosella {1200ml katika nyuzi joto 300C

N.B. Majani ya chai 100gm huchemshwa na maji nusu lita  kupata kikombe kimoja cha chai iliyokolea {250ml}

4 HATUA ZA UTENGENEZAJI

Chambua mauwa ya rosella yaliyokauka kwa kuondoa uchafu na majani yaliyokauka kasha pima kujua uzito.Pima kiasi cha maji kinachotakiwa na weka kwenye sufuria na weka jikono ili yachemke.Weka mauwa ya rosella yaliyokwisha chambuliwa na kupimwa kwenye maji yaliyochemka na acha yachemke kwa muda wa dakika 5 huku ukikoroga vizuri ili kupata juisi.Ondoa jikoni na chuja ili kuondoa mauwa na kupata juisi ya rosella.Weka kiasi cha sukari kwenye juisi ya rosella kisha rudisha jikoni huku ukikoroga kuhakikisha sukari yote imeyeyukaChuja na weka juisi kwenye chombo cha kuchachulia na iache ipoe hadi kufikia nyuzi joto 300CWeka majani ya chai {250ml} na koroga vizuriWeka hamira {hamira mama} kiaha funika chombo cha kuchachulia vizuri na kuweka kifaa cha kutolea hewa ‘air lock’’9. Acha uchachukaji uendelee kwa siku ishirini na moja [21days|

N.B. Kwa siku saba koroga mara moja kila siku

 

10.  Chuja na rudisha tena kwenye chombo cha kuchachulia kilichosafishwa na acha uchachuaji uendelee mpaka mwisho kwa kiasi kinachohitajika.

11.  Chuja tena na mwisho fungasha kwenye chupa zilizosafishwa vizuri “sterilized bottle”

12.  Weka mfuniko na kuweka lebo tayari kwa kuuza.

N.B. Ikumbukwe mvinyo uliokaa muda mrefu zaidi ndiyo unakuwa bora na ladha nzuri zaidi

No comments:

Post a Comment

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO