JINSI YA KUANDAA MVINYO WA NDIZI (BANANA WINE)
Ndizi ni tunda lililozoeleka kutumika na watu wengi duniani, tunda hilo linaweza pia kutumika kuandaa mvinyo ambao unaweza kutumika kwa familia na pia unaweza kuuzwa na kujipatia kipato. Leo tumewaletea hatua kwa hatua namna ya kuandaa mvinyo wa ndizi (banana wine) kama ifuatavyo:
HATUA YA KWANZA :
* Chukua ndizi kg.3 zilizo menywa maganda na ambazo zimeiva vizuri, katakata vipande vidogo na weka katika chombo ambacho utatumia kuchachulia wine yako.
* Baada ya kupata hivyo vipande vidogo vidogo , vichanganye kwenye maji lita ( 5 ) na baada ya hapo chemsha kwa muda wa dakika 30.
* Acha mchanganyiko wako huo upoe.
HATUA YA PILI
* Changanya mchanganyiko wa ndizi na sukari kikombe kimoja cha chai, koroga kisha changanya na amira vijiko vinne ( 4 ) vya sukari, koroga tena.
* Acha kwa muda wa siku nne, siku ya nne utakapo kwenda kuitazama wine yako utakuta povu, hii ina maana kuwa wine yako itakuwa imeanza kuchachuka vizuri.
* Siku ya tano ( 5 ) chuja wine yako vizuri kwa kutumia kitambaa lakini bila kufinyanga, iache wine imwagike yenyewe.
HATUA YA TATU
* Iweke wine yako kwenye chombo cha kutolea hewa na kupunguza gas kwa siku 1 mpaka miezi 3.
* Baada ya siku 21 wine yako itakuwa tayari.
No comments:
Post a Comment