*FAIDA ITOKANAYO NA MAZAO YANAYOPANDWA KATIKA KITALU SHAMBA (GREENHOUSE/NET HOUSE).*
*KILIMO BIASHARA*
Greenhouse Ni Nini? Katika Kilimo Cha Kisasa Greenhouse Inaweza Kuwa Na Maana Nyingi , Hii Inatokana Na Ugeni Wa Teknolojia Hii Mpya , Nchini Tanzania .
Kwa Mujibu Wa Kitabu Cha *“RURAL STRUCTURE IN THE TROPICS”* Ambacho Kinaelezea *DESIGN AND DEVELOPMENT* Katika Masuala Mbalimbali Ya Usanifu Na Ujenzi Wa Mabanda Ya Kisasa Ya Kuku,Ng’ombe, Nguruwe ,Ujenzi Mzuri Wa Greenhouse (Kitalu Shamba) N.K Kilichoandikwa Na Wanazuoni Nguli Katika Fani Ya Uhandisi Kilimo , Ambao Ni ;
-Prof Geoffrey C. Mrema; Aliyewahi Kuhudumu Kama Mkuu Wa Idara Ya Uhandisi Kilimo Na Mipango Ardhi ,Chuo Kikuu Cha Kilimo Sokoine(SUA) Kuanzia Mwaka (1979-1987), Vile Vile Kama Mshauri Wa Kitivo Cha Kilimo Chuo Kikuu Cha Botswana(1987-1995), Katibu Mkuu Mtendaji Wa Kwanza Wa Association For Strengthening Agricultural Research In Eastern And Central Africa (ASARECA- (1995-2001) Na Kuhudumu Pia Kama Mkurugenzi Wa Wa Agricultural Support System Division FAO, Makao Makuu, Rome-Italia (2001-2011 )Alipostaafu Na Kurudi Nchini Tanzania Kufundisha Chuo Kikuu Cha Sokoine Idara Ya Uhandisi Kilimo Na Mipango Ardhi.
-Mtunzi Mwingine Mshiriki Katika Kitabu Hiki Chenye Jumla Ya Kurasa 481, Ni Prof Lawrence O. Gumbe Toka Chuo Kikuu Cha Nairobi Nchini Kenya , Ambaye Alitoka Idara Ya Mazingira Na Uhandisi .
-Mtunzi Mwingine Ni Dr. Hakgamalang J. Chepete , Ambaye Ni Mhadhiri Mwandamizi Katika Idara Ya Uhandisi Kilimo Na Mipango Ardhi Katika Chuo Kikuu Cha Botswana Nchini Botswana .
Mtunzi Wa Mwisho Ni Mhandisi Januarius O. Agullo , Toka Chuo Kikuu Cha Nairobi Nchini Kenya Katika Idara Ya Mazingira Na Uhandisi .
Nimejaribu Kuweka Wasifu Wa Watunzi Wa Kitabu Hiki Muhimu , Ambacho Nilipewa Kama Zawadi Na Prof Geoffrey Mrema, Wakati Nilipokwenda Kumtembelea Ofisini Kwake Na Kuamua Kunipa Kitabu Hiki Ili Kinipanue Kimaono Na Kitaaluma Katika Ufanyaji Wa Kazi Zangu Za Greenhouse Na Kupanua Wigo Mpana Wa Kiuhandisi , Kupitia Kilimo Cha Kisasa Ali Maarufu Greenhouse, Kitabu Hiki Kiliandikwa Chini Ya Udhamini Wa FAO ( Food Agricultural Organisation)
Kitabu Hiki Kinaelezea Zaidi , Greenhouse Ambazo Ni Sahihi Kujengwa Katika Nchi Za Kusini Mwa Jangwa La Sahara Hasa Katika Nchi Zenye Hali Ya Kitropiki ( Tropical Climate) , Ambapo Sisi Kama RIWADE Ndio Hutumia Katika Wateja Wetu.
*Maana Ya Greenhouse Ni Nini?*
Hii Ni Nyumba Maalum , Iliyosanifiwa Na Ambayo Hutumia Mwanga Wa Asili Ndani Yake Na Kutengeneza Mazingira Mahususi, Kama Joto Maalum Kwa Mazao Ya Mbogamboga Na Matunda ( Nyanya, Hoho, Tango , Tikiti Maji N.K) Vile Vile Hutumika Kwa Ajili Ya Utafiti Na Kuepusha Mimea Iliyomo Ndani Kushambuliwa Na Wagonjwa Pamoja Na Wadudu.
*Tofauti Ya Greenhouse Na Net House*
Kiusanifu Na Kiujenzi Hakuna Tofauti Ya Greenhouse Na Net House , Bali Tofauti Pekee Ni Matilio Yanayotumika Kufunika Nyumba Iliyosanifiwa,
-Huitwa Greenhouse Sababu Imefunikwa Na Matilio Yajulikanayo Kama Greenhouse Cover/ Plastic Film /Glass N.K
-Huitwa Net House Sababu Hufunikwa Na Matilio Yajulikanayo Kama Net Maalum( Agricultural Net) Ambayo Ni Maalum Kwa Kilimo Kama Nilivyoeleza Huko Juu.
- Faida Za Zinazopatikana Kwenye Greenhouse Na Net House Ni Sawa
- Utofauti Mwingine Wa Greenhouse Na Net House Ni Kuwa Mvua Ikinyesha Kiasi Cha Maji Katika Net House Kitaingia Ndani Lakini Kwenye Greenhouse Maji Hayaingii Ndani
-Vilevile Kuna Greenhouse Mseto Hii , Hutengenezwa Kwa Kuchanganya Matilio Ya Poly Cover /Greenhouse Cover Na Net Na Hii Ndio Maarufu Sana Nchini Tanzania Hasa Kwa Wajasiliamali Wadogowadogo Na Wa Kati.
- Maelezo Ni Mengi Hasa Katika Uchambuzi Wa Greenhouse , Aina Zake N.K Lakini Naomba Kwa Hayo Machache Nijielekeze Kwenye Faida Za Greenhouse Kama Kichwa Cha Habari Kinavyojieleza.
*FAIDA ZA KIUCHUMI KWA MAZAO MBALIMBALI*
Kilimo Cha Greenhouse , Huzalisha Faida Kubwa Katika Eneo Dogo Sana Kulinganisha Na Eneo La Wazi
*1.Zao La Nyanya*
Katika Zao La Nyanya Kuna Aina Mbalimbali Za Nyanya Zinazopandwa Katika Greenhouse , Mimi Nitaelezea Nyanya Iitwayo Kwa Kitaalam “ Montezoul” Inayozalishwa Na Kampuni Ya Kiholanzi Iitwayo “ Afrisem” Ambayo Ni Tawi La Kampuni Mama Iitwayo “ Rijkzwaan”
Mbegu Ya Montezoul , Hutoa Kilo 25 Kwa Mche Mmoja Ambao Toka Upandwe Hadi Kung’olewa Shambani Huchukua Miezi 6, Yaani Siku 21 Za Kuotesha Miche , Miezi Miwili Na Nusu Matunda Kukomaa Na Miezi Mitatu Mfululizo Ni Ya Kuvuna Tu.
*Mfano : 1,*
Kwa Greenhouse Ya Ukubwa 120m2( Yaani Upana Mita 8 Na Urefu Mita 15), Greenhouse Hii Ina Kuwa Na Jumla Ya Matuta 6, Yenye Urefu Wa Mita 14 Kila Tuta.
-Katika Tuta 1, Zitafungwa Mipira 2 Ya Umwagiliaji ( Double Line)
- Ikiwa Upandaji Wa Kutoka Mche Kwenda Mche Itakuwa Ni Sentimita 50 Kwa Mujibu Wa Maelekezo Ya Mbegu
- Katika Tuta Moja Tutapata Miche 56 Ya Nyanya
- Kwa Matuta 6 Tutakuwa Na Miche 336 Ya Nyanya
- Miche 336 Ya Nyanya Ni Sawa Na Kilo 8400 Za Nyanya Zitakazo Patikana Katika Greenhouse Ya Ukubwa Wa 120m2.
- Kwa Bei Ya Kawaida Sokoni Kilo Moja Huuzwa Tsh 1000- 1500/=
- Chukua Kilo 8400 Kwa Tsh 1000 Utapata Milioni 8,400,000/= Kwa Muda Wa Miezi 3
-Ukipata Soko Zuri Bei Itakuwa Mara Mbili Ama Tatu Ya Bei Ya Kawaida , Na Kwa Kipindi Hiki Ambapo Nyanya Ni Adimu Ukipiga Kwa Kilo Moja Ni Tsh 4000, Hivyo Kwa Anayeuza Sasa Hivi Anatarajiwa Kuingiza 33,600,000/=( Sio Ndoto Bali Ni Ukweli , Naamini Hapa Wasomaji Wataduwaa)
*Mfano 2,*
Greenhouse Ya Ukubwa Wa 480m2(Yaani Upana Mita 16 Na Urefu Mita 30)
Hii Inakuwa Na Jumla Ya Matuta 12 Yenye Urefu Wa Mita 29 Kila Tuta
-Katika Kila Tuta Itafungwa Mipira 2 Ya Umwagiliaji Yaani (Double Line)
-Kwa Upandaji Wa Hatua 50sentimita Kutoka Mche 1 Kwenda Mche Mwingine
-Kila Tuta Moja Itaingia Miche 116 Ya Nyanya
-Kwa Matuta 12 Tutakuwa Na Miche 1392
-Miche 1392 Ni Sawa Na Kilo 34,800 Za Nyanya
-Kwa Bei Ya Kawaida Sokoni Kilo Moja Huuzwa Tsh 1000-1500
-Chukua Kilo 34800 Kwa Tsh 1000/= Utapata Tsh 34,800,000/= Kwa Muda Wa Miezi 3 Ya Kuvuna Na Kuuza Tu.
-Ukipata Soko Zuri Bei Itakuwa Mara 2 Ama 3 Ya Bei Ya Kawaida Katika Soko La Kawaida Katika Halmashauri Zetu, Lakini Kwa Sababu Sasa Nyanya Ni Adimu Bei Imefika Hadi 4000 Kwa Kilo 1, Sasa Chukua Kilo 34,800 Kwa Tsh 4000 Utapata Tsh 139,200,000/= ( Kilimo Cha Kisasa Kinalipa Sana, Utajiri Tumeulalia)
*2. Zao La Tango*
Katika Zao La Tango Kuna Aina Mbalimbali Za Tango Zinazopandwa Katika Greenhouse , Mimi Nitaelezea Tango Liitwalo Kwa Kitaalam “ Midas” Inayozalishwa Na Kampuni Ya Kiholanzi Iitwayo “ Afrisem” Ambayo Ni Tawi La Kampuni Mama Iitwayo “ Rijkzwaan”
Mbegu Ya Midas , Hutoa Kilo 30 -55 Kwa Mche Mmoja Ambao Toka Upandwe Hadi Kung’olewa Shambani Huchukua Miezi Takribani 6, Yaani Mbegu Ikishapandwa Baada Ya Siku 45 Unaanza Kuvuna , Na Miezi Mitatu Mfululizo Ni Ya Kuvuna Tu.
*Mfano : 1*,
Kwa Greenhouse Ya Ukubwa 120m2 ( Yaani Upana Mita 8 Na Urefu Mita 15), Greenhouse Hii Ina Kuwa Na Jumla Ya Matuta 6, Yenye Urefu Wa Mita 14 Kila Tuta.
-Katika Tuta 1, Zitafungwa Mipira 2 Ya Umwagiliaji ( Double Line)
- Ikiwa Upandaji Wa Kutoka Mche Kwenda Mche Itakuwa Ni Sentimita 50 Kwa Mujibu Wa Maelekezo Ya Mbegu
- Katika Tuta Moja Tutapata Miche 56 Ya Tango
- Kwa Matuta 6 Tutakuwa Na Miche 336 Ya Tango
- Miche 336 Ya Tango Ni Sawa Na Kilo 13440( Nimetumia Kilo 40 Kila Mche) Za Tango Zitakazo Patikana Katika Greenhouse Ya Ukubwa Wa 120m2.
- Kwa Bei Ya Kawaida Sokoni Tango Moja Huuzwa Tsh 500
- Chukua Kilo 13440 Kwa Tsh 500 Utapata Milioni 6,720,000/= Kwa Muda Wa Miezi 3
-Ukipata Soko Zuri Bei Itakuwa Mara Mbili Ama Tatu Ya Bei Ya Kawaida.
*Mfano 2,*
Greenhouse Ya Ukubwa Wa 480m2(Yaani Upana Mita 16 Na Urefu Mita 30)
Hii Inakuwa Na Jumla Ya Matuta 12 Yenye Urefu Wa Mita 29 Kila Tuta
-Katika Kila Tuta Itafungwa Mipira 2 Ya Umwagiliaji Yaani (Double Line)
-Kwa Upandaji Wa Hatua 50 Sentimita Kutoka Mche 1 Kwenda Mche Mwingine.
-Kila Tuta Moja Itaingia Miche 116 Ya Tango
-Kwa Matuta 12 Tutakuwa Na Miche 1392
-Miche 1392 Ni Sawa Na Kilo 55,680 Za Tango
-Kwa Bei Ya Kawaida Sokoni Kilo Moja Huuzwa Tsh 500
-Chukua Kilo 55680 Kwa Tsh 500/= Utapata Tsh 27,840,000/= Kwa Muda Wa Miezi 3ya Kuvuna Na Kuuza Tu.
-Ukipata Soko Zuri Bei Itakuwa Mara 2 Ama 3 Ya Bei Ya Kawaida Katika Soko La Kawaida.
*3. Zao La Hoho*
Katika Zao La Hoho Kuna Aina Mbalimbali Za Hoho Zinazopandwa Katika Greenhouse , Mimi Nitaelezea Zote Aina Tatu Kwa Ujumla Wake, Hoho Za Kijani Ziitwazo “Redjet” , Hoho Nyekundu Ziitwazo “Perisela” Na Hoho Za Njano Ziitwazo ”Ilanga” Zinazozalishwa Na Kampuni Ya Kiholanzi Iitwayo “ Afrisem” Ambayo Ni Tawi La Kampuni Mama Iitwayo “ Rijkzwaan”
Mbegu Ya Hizi , Hutoa Kilo 11 Kwa Mche Mmoja Ambao Toka Upandwe Hadi Kung’olewa Shambani Huchukua Miezi 6, Yaani Siku 24 Za Kuotesha Miche , Miezi Miwili Na Nusu Matunda Kukomaa Na Miezi Mitatu Mfululizo Ni Ya Kuvuna Tu.
*Mfano : 1*,
Kwa Greenhouse Ya Ukubwa 120m2 ( Yaani Upana Mita 8 Na Urefu Mita 15), Greenhouse Hii Ina Kuwa Na Jumla Ya Matuta 6, Yenye Urefu Wa Mita 14 Kila Tuta.
-Katika Tuta 1, Zitafungwa Mipira 2 Ya Umwagiliaji ( Double Line)
- Ikiwa Upandaji Wa Kutoka Mche Kwenda Mche Itakuwa Ni Sentimita 40 Kwa Mujibu Wa Maelekezo Ya Mbegu
- Katika Tuta Moja Tutapata Miche 70 Ya Hoho
- Kwa Matuta 6 Tutakuwa Na Miche 420 Ya Hoho
- Miche 420 Ya Hoho Ni Sawa Na Kilo 4620 ( Nimetumia Kilo 11 Kila Mche) Za Hoho Zitakazo Patikana Katika Greenhouse Ya Ukubwa Wa 120m2.
- Kwa Bei Ya Kawaida Sokoni Hoho , Kilo Moja Huuzwa Tsh 3000
- Chukua Kilo 4620 Kwa Tsh 3000 Utapata Milioni 13,860,000/= Kwa Muda Wa Miezi 3.
-Ukipata Soko Zuri Bei Itakuwa Mara Mbili Ama Tatu Ya Bei Ya Kawaida , Na Kwa Kipindi Hiki , Kwa Jiji La Dar Es Salaam Hasa Hoho Za Rangi Kilo Inafika Hadi 9000, Hivyo Ukichukua Kilo 4620 Kwa Tsh 9000 Utapata Tsh 41,580,000/=
*Mfano 2,*
Greenhouse Ya Ukubwa Wa 480m2(Yaani Upana Mita 16 Na Urefu Mita 30).
Hii Inakuwa Na Jumla Ya Matuta 12 Yenye Urefu Wa Mita 29 Kila Tuta
-Katika Kila Tuta Itafungwa Mipira 2 Ya Umwagiliaji Yaani (Double Line)
-Kwa Upandaji Wa Hatua 40sentimita Kutoka Mche 1 Kwenda Mche Mwingine.
-Kila Tuta Moja Itaingia Miche 145 Ya Hoho
-Kwa Matuta 12 Tutakuwa Na Miche 1740
-Miche 1740 Ni Sawa Na Kilo 19140 Za Hoho
-Kwa Bei Ya Kawaida Sokoni Kilo Moja Huuzwa Tsh 3000
-Chukua Kilo 19140 Kwa Tsh 3000/= Utapata Tsh 57,420,000/= Kwa Muda Wa Miezi 3 Ya Kuvuna Na Kuuza Tu.
- Na Kwa Kipindi Hiki , Kwa Jiji La Dar Es Salaam Hasa Hoho Za Rangi Kilo Inafika Hadi 9000, Hivyo Ukichukua Kilo 19140 Kwa Tsh 9000 Utapata Tsh 172,260000/=
No comments:
Post a Comment