Saturday, 18 March 2017

UZALISHAJI WA MALISHO KWA TEKNOLOGIA YA HYDROPONICS FOODER

UZALISHAJI WA MALISHO KWA TEKNOLOJIA YA HYDROPONIC

Hydroponic ni nini?
Ni mbinu ya kukuza mimea kwa kutumia mchanganyiko wa virutubisho vya madini katika maji bila kutumia udongo. Mchakato huu huchukua siku 6 hadi nane kukamilika.
Kilo moja ya mbegu huzalisha wastani wa kilo 6 hadi kumi za majani na mizizi.
Faida za Teknolojia hii
i. Malisho huzalishwa ndani ya muda mfupi katika eneo dogo.
ii. Chakula hiki hulika chote kwa mifugo. Wanakula najani yote pamoja na mizizi. Hakuna upotevu wa chakula.
iii. Mahitaji ya maji ni madogo na maji yanaweza kutumika tena na tena.
iv. Gharama za uendeshaji wake ni mdogo; hakuna kuandaa ardhi, palizi na gharama za uvunaji.
v. Uwezekano mdogo sana wa wadudu ama magonjwa kushambulia.
Faida katika ulishaji
i. Chakula hiki ni laini hivyo mmengényo wake katika mifugo ni mkubwa hivyo sehemu kubwa hutumika katika mwili wa mifugo na uzalishaji.
ii. Mazao ya mifugo uboreka zaidi na kuendana na mahtaji ya soko. Mfano:
 mayai ya kuku huwa na kiini cha njano zaidi wanapokula majani.
 Maziwa huwa na uwiano mzuri wa Omega 3 na Omega 6 amino acid ambazo hujenga afya imara ya mlaji.
iii. Hupunguza gharama za chakula na hivyo kuongeza faida.
iv. Virutubisho vingi hasa vitamin ambazo huchangia afya ya mifugo kuimalika.
v. Kinapolishwa kwa mchanganyiko na vyakula vingine kwa uwiano tutakaoutoa hapo mbele, uzalishaji na ukuaji wa mifugo huwa mzuri zaidi.

Vifaa mihimu katika kutengenezea Hydroponic ambavyo unaweza pata kutoka CHAKULACOM ni

 Sehemu/chumba cha kukuzia.
 Nguzo na fito za kutengeneza chanja kwa ajili ya kupanga trei.
 Trei za plastiki/aluminiamu.
 Dawa yenye Chlorine
 Virutubisho (nutrients): wengine hutumia buster za mazao (hakikisha haina madhara kwa mifugo).
 Pump (sprayer) kunyunyiza maji.
 Mbegu.
Mbegu zinazoweza kutumika
 Shayiri, mahindi, ngano, mtama na nafaka nyingine nyingi.

HYDROPONIC fodder
Mkombozi pekee wa wafugaji wa ng'ombe, kuku, nguruwe, mbuzi na kadhalika

HYDROPONIC ni sayansi/sanaa ya kuotesha mazao bora yenye tija kwa muda mfupi zaidi bila kutumia udongo kabisa, kwa kutumia maji na virutubisho (Hydroponic Nutrients).

Hydroponic fodder Ni nzuri zaidi kwa sasa maana Ni nafuu kulinganisha na vyakula vingine vya mifugo

Hydroponic fodder Ni uoteshaji wa mbegu pasipo kutumia udongo kwa muda wa siku 5- 7 tu kilo moja ya mbegu za ngano au mtama au shayiri au Mshindi zinaoteshwa na kumwagiliwa virutubisho maalum (HYDROPONIC NUTRIENTS) na kuongezeka kutoka kilo moja hadi kilo 10 za CHAKULA cha kuku.
Kwakuwa kuku mmoja hula gram kati ya 100-120gm hivyo kilo moja ya mbegu ikitoa kilo kumi za fodder zinatosha kulisha kuku wakubwa 100 kwa siku Hydroponic fodder Ni CHAKULA cha Mifugo wa aina zote chenye faida nyingi sana.

No comments:

Post a Comment

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO