Monday, 20 March 2017

UZALISHAJI WA TIKITI MAJI KWA KIWANGO KIBWA KIBIHASHARA

UZALISHAJI WA TIKITIMAJI

Tikitimaji ni zao la kitropiki linalo tumia miezi mitatu kutoka kupandwa hadi kuvunwa.

ENEO
Chagua eneo ambalo halina historia ya kuwa na magonjwa ama wadudu wanaoshambulia tikiti maji.Eneo ambalo maji yanapatikana kwa urahisi kwa ajili ya umwagiliaji wa tikiti maji litafaa,pia eneo lisilo na udongo wenye chumvi chumvi ama maji yenye chumvi chumvi.

KUANDA SHAMBA.

Lima shamba lako vizuri kwa kuvunja vunja udongo na pia andaa matuta yenye upana wa mita 2 na urefu kwenda juu sentimita 30 ili kusaidia mizizi ya tikiti kukua vizuri na kuzuia maji kutwaama hasa katika kipindi cha mvua.

MAHITAJI YA TIKITIMAJI

Tikiti linakua vizuri ktk udongo unaoshika maji vizuri lakini yasio tamwa na kuruhusu mzunguko mzuri wa hewa na maji.Udongo wenye pH 5.8-6.6.
Tikiti halistawi vyema ktk baridi na linahitaji joto la udongo kiasi cha 18-29 0c.

Joto chini ya 18 0c na juu 29 0c litaathiri kuota kwa mbegu na ukuwaji wa mmea.Katika kipindi cha ukuwaji tikitimaji linahitaji unyenyevu wa udongo wakati wote lakini maji yakizidi ktk udongo wakati wowote wa ukuwaji na uwekaji wa matunda hupelekea upasukaji wa matunda na kupunguza mavuno na ubora wa matunda.

UPANDAJI

Mbegu/mche wa tikiti maji utapandwa mita 1-2 kati ya mmea na mmea na uwekwa sentimita 2.5 kwenda chini, na kati ya mstari na mstari iwe mita 2,kwa umbali huu panda mbegu 2 kila shimo.Au weka umbali wa sentimita 50 kwa mita 2 lakini hapa panda mbegu moja moja.
Mbegu ya tikitimaji utokeza baada ya siku 5-7.
UTUNZAJI WA MMEA.
a) Mbolea.
Mbolea ya samadi kwa kiasi cha 4-6 tani kwa ekari,ichanganye na udongo wiki kadha kabla ya kupanda,pia mbolea hii unaweza iweka katika kila shimo siku kadhaa kabla ya kupanda kisha mwagilia ili kupunguza kiasi kikubwa kitakacho hitajika kuweka ktk ekari moja.Kama huna samadi tumia Yaramila winner au DAP weka gram 5 kwa kwa kila shimo ,hakikisha mbolea na mbegu havigusani.

Wiki mbili baada ya miche yako kutokeza weka mbolea ya kiwandani -N-P-K (Yaramila winner) gram 5 tena kwa kila shimo,hakikisha unaichimbia chini na isigusane na mmea.

Weka mbolea yenye Calcium kana Yaramila nitrabo gram 10 kwa kila shina unapoona matunda yameanza ili kusaidia kupata matunda makubwa na mazuri.

UMWAGILIAJI
Maji kwa sentimita 1-5 katika udongo yanatakiwa kwa mvua ama umwagiliaji ili kupata tikitimaji zuri,kipindi cha muhimu sana kwa mahitaji ya maji kwa tikitimaji ni :kabla ya mche kutokeza ,mwanzo wa kutoa maua na siku 10 za mwisho kabla ya kuvuna.Maji machache kipindi cha kupanda husababisha kutoota kwa mbegu,kipindi  cha kuweka maua husababisha matunda machache kutokeza na matunda kukosa maumbo yake.Siku 10 za kuelekea kuvuna husababisha matunda kuwa madogo kama maji ya kutosha yasipopatikana.Matunda yakielekea kuiva punguza umwagiliaji maana kiasi kikubwa cha maji kitasababisha kiasi kidogo cha sukari kutengenezwa na kupasuka kwa matunda.

Angalizo:
Usimwagilie jion sana hii itasababisha kukua kwa magonjwa kwa sababu ya kuacha majani ya mmea yakiwa na unyevunyevu .Pia angalia wakati mzuri wa uchavushaji /wakati ambao  nyuki wanakuwepo shambani mwako hivyo jitahidi kumwagilia mda ambao hautawasumbua nyuki.

Matandazo.
Ni muhimu kutumia matandazo ktk shamba lako ili kusaidia kutunza unyevunyevu ktk udongo na matandazo haya baadaye yakioza uongeza rutuba ktk udongo na pia kusaidia kuzuia kumea kwa magugu na husaidia tunda kutogusana na udongo kitu ambacho kinaweza sababisha tunda kuathiliwa na joto la udongo ama magonjwa kirahisi.Weka matandazo pale mche wako utakapo fikia urefu wa sentimita 10.

Punguza urefu wa mmea
Ili kupata matunda mazuri na yenye afya ni vema kuupunguza mmea kwa mbele ,pale unapoona mmea umefika urefu wa kutosha ili kusaidia kutengeneza matawi ya pembeni ambayo mara nyingi ndio ubeba maua ya kike.

Kuondoa magugu

Ni muhimu sana kuondoa magugu ktk shamba lako hasa wiki za mwanzo ili kuzuia ushindani  wa mahitaji kati ya magugu na mmea ambapo hupelekea kupungua kwa mavuno na muda mwingine magugu haya yanaweza kuwa ndio chanzo cha baadhi ya magonjwa ktk mmea wako

Uchavushaji
Ili kupata kiasi kikubwa cha matunda ni vyema kuwa na mzinga wa nyuki karibu na shamba lako ili kusaidia uchavushaji wa maua ya tikitimaji.Waweza pia pands alizeti jilani na shamba lako ili kuvuta nyuki.Pia zuia kupulizia dawa za wadudu kipindi cha maua maana unaweza wakimbiza ama waua nyuki

Punguza idadi ya matunda 
Kwa kawaida tikitimaji uweka zaidi ya matunda manne ,ili kupata matunda makubwa na yenye afya ni vyema kupunguza matunda kwa kuondoa baadhi ya matunda ambayo yanaonekana hayana afya nzuri na yaliopoteza umbo zuri na kuhakikisha kila mche unabaki na matunda 2-3 tu.

Uvunaji
Tikitimaji uvunwa baada ya miezi mitatu kutoka siku ya kupanda,lakin yapo ambayo hukomaa kwa siku 60-75 kutokana na aina ya mbegu.
Mangonjwa 
1) Ubwiru chini (Downy mildew)
Huu ungonjwa husababishwa na fangasi (Pseudoperonosporacubensis).Ni kati ya mangonjwa yanayoshambulia majani na hupendelea sana wakati wa baridi,
Dalili zake:
Majani yaliyoshambuliwa hugeuka rangi na kuwa kama ya njano huku baadhi ya majani yakiwa kama yanakauka  na madoadoa meus kwa mbali..

Tiba yake.
Tafuta dawa yenye viambato...Metalaxyl na mancozeb ....kama vile Ridomil gold.

2) Ubwiru juu (Powdery mildew )  
Dalili za huu ungonjwa...utaona majani yanakuwa kama yamemwagiwa unga ua majivu

Tiba yake
Tafuta dawa yenye kiambato...Difenoconazole ..kama vile Score.

3) Kata kiuno.(Damping off)

Huu ugonjwa husumbua sana miche midogo,huanzia aridhini ,husababisha miche midogo kuanguka chini baada ya kula sehemu ya shina.

Tiba yake.
Tafuta Ridomil gold na anza kupulizia mara tu baada ya mimea yako kuota.
Wadudu..
1) Wadudu mafuta (Aphid)
Hawa hushambulia majani na kufyonza juis ya mmea na baada ya kushambulia majani hujikunja na baadaye kupelekea mangonjwa ya virusi.

Dawa yao.
Tafuta Actara na pulizia majani pamoja na udongo.

Wadudu wengine ni;Nzi weupe (whitefly )-Actara itawamaliza.

,Utitiri mwekundu (Redspidermites)-Dynamec itawamaliza,Thrips-Actara na Dynamec itawamaliza kabisa.
Mbegu bora za tikitimaji.
Kuna mbegu chotara na opv(Sio chotara)
But mbegu bora ni chotara na baadhi ya hizo mbegu ni...
1) Arashani F1-kutoka syngenta
2) Sukari F1-Kutoka East Africa seeds.
3) Sugar king F1-kutoka africasia
4) Juliana F1-kutoka Kiboseed
5) zebra F1-Kutoka Balton.
6) Pato F1-Kutoka Agrichem

NB:F1 ni mbegu chotara za utafiti zote bora ,chagua upendayo

Tikiti dogo kabisa ni kilo 8 na kubwa kabisa ni kilo 18 but wastani ni kilo 14.
SOKO LA TIKITI 
Napenda kuwashauri wakulima wetu kuwa njia nzuri ya kulima tikitimaji ni ile ya umwagiliaji, ukiwa mkulima wa tikitimaji lazima uwe mjanja kupanda zao lako ili uje uvune wakati soko liliwa vizuri, mzunguko mzuri wa kupanda tikiti ni huu, panda zao lako katikati ya msimu wa mvua wakati walimaji wa matikiti kwa kutegemea mvua (ambao ni wengi) mazao yao yametoa maua ili wakati wao wanavuna tikiti zao, mazao yako yawe ndio yanaanza kutoa maua kwa hiyo wakati unavuna wakulima wa kutemea mvua watakuwa washamaliza soko lao.Pia kwa wale wanaotegemea mvua ni vizuri uchunguze soko lako vizuri ili uwe na uhakika wa kuuza matunda yako wakati yakiwa tayari yamekomaa.

No comments:

Post a Comment

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO