UTAMBUZI WA MAGONJWA YA KUKU KUPITIA RANGI YA KINYESI
1. Mharo mweupe(pullorum bacilary diarrhoea)
ugonjwa huu huathiri zaidi vifaranga kabla ya wiki nne
huharisha mharo mweupe,
TIBA kuu ni usafi pekee kwenye banda na kuepusha maji yasimwagike ovyo.
2.KIPINDUPINDU CHA KUKU(fowl cholera)
kinyesi cha kuku ni njano
tumia dawa za salfa, eg Esb3 au amprollium
3.COCCIDIOSIS
mwanzo kinyesi cha kijivu na baadae huharisha damu iliyochanganyika
Tumia dawa ya VITACOX au ANTICOX
4.MDONDO(Newcastle)
kuku hunya kinyesi cha kijani
sio kila kijani ni newcastle
HAKUNA TIBA
5.TYPHOID
Kinyesi cheupe
kinagandia sehemu za nyuma au hulowana sehemu za haja
dawa ni Eb3
6.GUMBORO
Huathiri zaidi vifaranga
kinyesi huwa ni majimaji
Dawa hakuna
tumia vitamini na antibiotic
MDONDO UGONJWA TISHIO KWA WAFUGAJI WA KUKU.
MDONDO
Ugonjwa unaosumbua sana wafugaji wa kuku ni Mdondo na wengine huuita Kideri (new castle disease). Chanzo cha ugonjwa huu ni virusi. Ni ugonjwa unaoathiri kuku wa rika zote na mara nyingi humaliza kuku wengi au wote vijijini.
DALILI ZA MDONDO NI:
• Kuku hukohoa
• Kuhema kwa shida
• Hushusha mbawa
• Kupoteza hamu ya kula, kuzubaa, kusinzia
• Manyoya kuvurugika
• Kuharisha kijani
• Kutokwa ute mdomoni na puani
• Kizunguzungu, shingo kujikunja, kurudi kinyumenyume, kupooza mabawa, kuanguka chali, kupoteza fahamu na hatimaye kufa.
• Kuku wengi kwenye kundi hufa katika kipindi kifupi kwa kufikia asilimia 90 hadi 100.
UENEZAJI WA UGONJWA HUU NI KWA NJIA ZIFUATAZO:
• Kinyesi cha kuku anayeumwa kikikanyagwa na miguu, magari, baiskeli na kuwafikia kuku nwengine.
• Kwa njia ya hewa (kuvuta hewa yenye virusi ) au upepo waweza kusafirisha virusi.
• Mabaki ya kuku anayeumwa kama utumbo, manyoya n.k. visipozikwa vitaeneza ugonjwa kwa kuku wazima kula mabaki hayo au wanyama watakaokula mabaki hayo huweza kuyasambaza na kueneza ugonjwa.
KUTHIBITI MDONDO
Kuchanja
(Kuku wapewe chanjo tangu vifaranga wa umri wa siku 3, baada ya wiki 3 – 4, na baadaye kila baada ya miezi 3)
Kwa kijijini
Kwanza kabisa ni chanjo ya Mdondo. Zipo aina tofauti za chanjo ya Mdondo. Lakini chanjo iliyo rahisi kutumiwa vijijini inaitwa I-2 Thermostable. Chanjo hii tofauti na chanjo nyingine nyingi inao uwezo wa kustahimili joto. Hutolewa kwa njia ya kuku kudondoshewa tone moja la dawa katika jicho moja tu. Hii ni dozi kamili kwa kuku wa umri wowote.
Dawa hii upatikana kwenye maduka ya madawa ya mifugo au ofisi za serikali za mifugo.
Utaratibu wa kuchanja kwa dawa ya I – 2 Thermostable
• Mdondo hauna tiba kwa hiyo unakingwa kwa chanjo Kuku wachanjwe mara baada ya kutotolewa bila kusubiri mzunguko au ratiba ya chanjo inayofuata katika eneo husika.
• Kuku wachanjwe kila baada ya miezi mitatu bila kukosa. Kama unayo kalenda weka alama kwenye tarehe za kuchanja ili uweze kufanya maandalizi mapema ya upatikanaji wa dawa.
• Kuku wachanjwe angalau mwezi mmoja kabla ya mlipuko wa ugonjwa . Kwa kawaida wafugaji wanafahamu miezi ya mlipuko wa ugonjwa huu katika maeneo yao•
• Angalia sana uchanje kuku ambao hawajaambukizwa. Kuku akiishaugua chanjo haitasaidia bali itaongeza kasi ya ugonjwa.
• Japo chanjo ya I-2 Thermostable, ni muhimu ihifadhiwe sehemu kavu na yenye ubaridi wa kawaida isipate joto, la sivyo itaharibika na haitafaa tena kwa chanjo. Pia unaposafirisha dawa hii tumia chombo amacho hakitaruhusu dawa kupata joto. Vile vile wakati wa kuchanja shughuli hii ifanyie kivulini dawa isipate mionzi ya jua.
NJIA NYINGINE ZA KUDHIBITI MDONDO
- Banda na vyombo vyote vinavyotumika ndani ya banda.viwe safi wakati wote.
- Tenga kuku wageni kwa muda wa wiki 2 na kuwachanja kabla ya kuwachanganya na kuku wenyeji.
- Choma mizoga inayoweza kuletwa kwenye eneo lako.
- Usiruhusu watu kuingia hovyo kwenye banda, ikibidi kuingia watumie viatu ulivyotenga kuingilia bandani kwako Kutoruhusu watu kuingia kwenye banda ovyo.
KUDHIBITI MDONDO USIENEE KUTOKA VIJIJI VINGINE NA NDANI YA KUNDI LAKO:
- Katika kipindi cha mlipuko wa ugonjwa huu epuka kununua kuku minadani na kutoka sehemu zenye ugonjwa huu.
- Kuku wako wakiugua Mdondo tenganisha wale waliougua ili wasiwaambukize walio wazima.
- Kumbuka kuku akiishaugua usimchanje bali mtenge na mpatie chakula na maji na sehemu nzuri ya kupumzikia.
- Kuku aliyekufa kwa Mdondo azikwe au achomwe
- Kuku aliyechinjwa baada ya kuugua sehemu zake ambazo hazikutumika kama mifupa, utumbo n.k . vizikwe vyote.
- Kuku wengi wakifa kwa ugonjwa huu usilete kuku wengine katika eneo au banda lako hadi angalau upite mwezi mmoja.
Tafadhali sana hakikisha unafuata taratibu na ratiba ya chanjo vizuri maana Ugonjwa huu ni habari sana.
No comments:
Post a Comment