UKWELI KUHUSU UFUGAJI WA KUKU
Kumekuwa na upotoshaji kwa baadhi wa watu wanaojiita wataalamu wa ujasiriamali, hasa wanaofanya shughuli za ufugaji kwa maandiko ya whatsapp bila kuwa na hata kuku mmoja bandani. Nimesukumwa kuandika bandiko hili hapa kutokana na jumbe mbali mbali za uufugaji wa kimtandao unaoshawishi vijana kuwa watatajirika mapema kwa shughuli za ufugaji kwa kuanza na kuku wa kienyeji kumi na moja na kuweza kupata Zaidi ya kuku miatatu ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa uzalishaji. Hoja yao inaweza kuwa sahihi, ila ningependa kusisitiza mafanikio katika ufugaji hayapo katika idadi ya kuku unayomiki, bali ni namna ulivyoweza kumanage biashara ya ufugaji.
Hoja yangu leo hapa ni kwamba, Biashara ya kuku wa kienyeji hailipi na nikupoteza muda wako. Na nitatetea hoja yangu kwa mifano hai na uzoefu wangu katika ufugaji.
Biashara ya Mayai. (idadi isiyo na tija kibiashara)
Kwa asili ya kuku wa kienyeji,huwa wanatabia ya utagaji wa mayai 7-10 na mara nyingi ni siku kwa siku 10 mfululizo, utamiaji -siku 21, na uleaji wa vifaranga - siku 50-60. Hii inampelekea kwa kuku mmoja kuweza kutaga wastani wa mayai 35-50 kwa mwaka kwani anapoteza muda mwingi kwa shughuli za utamiaji na malezi ya vifaranga badala ya kutaga. Idadi hii ya mayai haina tija kibiashara kwani kuku mmoja anaweza kukuzalishia tray 1 mpka mbili kasoro pekee kwa mwaka ambayo kwa bei ya soko si Zaidi ya shilingi za kitanzania 20,000 tu kwa mwaka.
Changamoto kwenye soko la mayai ya kienyeji. (Uhifadhi wa mayai).
Mayai ya kienyeji ni kati ya bidhaa ngumu Zaidi kuhifadhika. Ikumbukwe kuwa tofauti na mayai ya kisasa, mayai ya kienyeji huwa yamerutubishwa na majogoo. Hivyo kuharibika ndani ya muda ya week moja au pungufu kama hayatatuzwa katika mazingira salama kwaajili ya utunzaji. Kipindi cha joto kali, mayai haya huanza kujitenenezea kifaranga au mishipa ya damu ambayo baada ya muda mfupi hugeuka viza na kutofaa kwa matumizi tena.
Kwa uzoefu wangu binafsi kunachangamoto kubwa sana ya kubadilisha mayai mara kwa mara kwani mteja akichukua yai viza ni kumpoteza kabisa. Hii ni changamoto ya kwanza ambayo mpaka sasa bado inasumbua wafugaji wengi.
Bei juu kwa mayai ya kienyeji
Gharama za mayai husika, bei ya mayai ya kienyeji iko juu ukilinganisha na gharama za mayai ya kuku wa kisasa. Soko kubwa la mayai ni pamoja na vibanda vya chips, migahawa na hoteli. hawa wanauhitaji mkubwa sana wa mayai na soko liko juu muda wote wa mwaka. Soko la mayai ya kienyeji lipo Zaidi kwenye households. (soko la familia) hasa kwa vigezo vya kuzingatia afya zaidi. Soko hili la familia sio kubwa, ni soko dogo na mara nyingi hutumia tray moja kwa kipindi cha wiki mbili au Zaidi. kwa mzalishaji mkubwa wa mayai ya kienyeji ni lazma awe na soko la familia pana Zaidi kuweza kupata faida ndogo, nasema faida ndogo maana ili kuzalisha mayai tray kumi (mayai 300) kwa siku, utahitaji Zaidi ya matetea 700 mpaka 1000 ya kienyeji pure. idadi ambayo ni kubwa kuliko idadi ya mayai yanayopatikana.
Biashara ya Nyama.
Na declare interest, mimi pia ni mtumiaji wa nyama ya kuku wa kienyeji, hivyo naongea kwa uzoefu, na niko tayari kukosolewa. Pamoja na kufugwa katika misingi ya kijani (organic rearing), iyo pekee haitoshi kumpa thamani inayostahili huyu kuku sokoni. Thamani ya kuku sokoni ni uzito alio nao, organic component ni jambo la ziada lililo muhimu pia. tunavyo jadili bei ya soko ya kuku huyu ni lazma tumliganishe na gharama za bidhaa pinzani zilizoko sokoni. Haitawezekana kumuuza kuku mwenye kilo moja au pungufu kwa bei ambayo tunashawishiana humu ya 15000-20000 wakati bidhaa pinzani (nyama nyeupe) kama samaki sato toka mwanza wanauzwakwa 7500 kwa kilo, au kitimoto, nyama ya ngombe ambazo nazo kilo ni 7500-8000. Hivyo basi. hoja yangu hapa ni uzito wa kuku husika. Ukiachana na jamii chache za kuku wa kienyeji (kuchi etc) wenye uzito mzuri, majority ya kuku pure wa asili/kienyeji kwa majogoo huwa na pungufu ya kilo moja na nusu. Kumbuka uzito wa kuku hawa sio kwasababu ya malisho duni, laah
No comments:
Post a Comment