Monday, 31 December 2018

LAMBA LAMBA ZA CUSTURD NA MAZIWA

LAMBA LAMBA ZA CUSTURD NA MAZIWA🥛🥛🥛👌🏼😋

                  * MAHITAJI*
1; MAZIWA LITA 1

2; CUSTURD VIKOMBE 2

3; SUKAR KIAS CHAKO

4; MAJI LITA MOJA

              *MAANDALIZ*
1;  CHANGANYA VITU VYOTE KWA PAMOJA NA UCHEMSHE

2; IKICHEMKA VIZUR EPUA JAZA KWENYE VIFUNGASHIO NA UGANDISHE😋👌🏼

BISCUT YA NAZI NA SUKARI

*BISKUT YA NAZI NA SUKARI*@BY COOKING THEORY&PRACTICAL Kiko Sukari Ya Kusaga    Nusu. kikombe Siagi Mafuta Kikombe 1. Changanya Usage Vizuri Mpaka Iwenzito Km Cream Kish Weka Mayai 2 Na Vanilla Kisha Each Ichanganyike Vizuri Weka Unga Vikombe 3 Unusu Ukita Unga Was Ata Au was  Ngano Na Kikombe 1 Nazi Kavu Changanya Vizuri Kisha Weka Kwenye Friji Muda Was Masaa 4 Kish Usukume Duara Na Kibati Stlye Upendayo Kisha Toboa Na Umma Mwagia Sukari juu  Choma  Kwenye Oven Muda Wa Dk 12

Saturday, 29 December 2018

JINSI YA KUTUNZA NYWELE ZENYE DAWA

*JINSI YA KUTUNZA NYWELE ZENYE DAWA*

💐Muhimu kuzingatia dawa  ya nywele kutokana na nywele zako

💐Kama una  nywele   nywepesi  hakikisha unatafta dawa kwaajili ya nywele nyepesi bila ya hivyo unajibebea dawa ambayo sio sahihi kwa nywele zako na matokeo yake zitakatika Na kunyonyoka kupita kiasi

💐Hakikisha unapangilia  muda wa kuweka nywele dawa nywele zako

💐Hakikisha unaweka dawa kila  baada ya miezi minne kuweka dawa chini ya miezi 4 hupelekea kukatika nywele zako

💐Hakikisha unaosha nywele zako Mara ili kuondoa mrundikano wa uchafu kwenye maoteo ya nywele zako

💐Hakikisha unaosha nywele zako kila wiki mara 1

💐Tumia mafuta ambayo yataenda sambamba na nywele zako

💐Hakikisha unatumia Mafuta yenye uwezo wa kutunza unywevu na kuzuia nywele kukatika

💐Si vibaya ukichanganya baadhi ya mafuta ambayo yanasifika kama castor, Jojoba, Argan Na Shea butter oil

💐Epuka matumizi ya moto kwenye nywele kama kutumia pasi ya nywele kwaajili kuzinyoosha nywele kwani hupelekea nywele kutokuwa na nguvu Na hatimae kukatika


💐Hakikisha unapolala unajifunika Na kofia (satin) hii itasaidia ukuaji mzuri Wa nywele zako...

💐Hakikisha kila wiki unaposha nywele unafanya Na conditioner Na mwezi Hakikisha unazifanyia deep treatment ili kuzipa protein

JINSI YA KUTUNZA NYWELE ASILI ISIYO NA DAWA

*JINSI YA KUTUNZA NYWELE ASILI ISIYO NA DAWA*

Shampoo

✅Unapoosha nywele zako hakikisha unatumia shampoo ambayo imetengenezwa kwa ajili ya natural hair

❌Usioshee shampoo zenye chemicals kama paraben na sulfate hizi hupelekea kukatika nywele Na kubaribika

✅Pia pendelea shampoo yenye conditioner yaani 2 in 1 Hii itasaidia nywele zako kuwa laini na kuzuia zisiwe kavu baada ya kuziosha itakusaidia pia kwenye kuzichana

Mafuta

✅Pendelea zaidi kuzipaka mafuta ya maji kama vile mafuta ya nazi olive oil, jojoba oil au castor oil kwasababu mafuta haya hulainisha ngozi ya kichwa, kufanya nywele zikue vizuri na kuzuia Kufanya mba

✅Mafuta ya mgando maranyingi hutengeneza mba kwenye nywele za asili kwa urahisi sana tofauti na nywele zenye dawa

Hot oil treatment/prepoo

✅Hii ni nzuri kwa nywele zako Hakikisha kabla hujaosha nywele zako unazifanyia prepoo kwa mafuta ya moto kama kwenye post zilizopita

Steaming

✅Hakikisha nywele zako unazifanyia steaming angalau Mara 2 kwa mwezi

✅Vizuri zaidi ukitumia mask za asili kama yai, parachichi Na nyengine tulizowahi kupost

Detangle Na kuzichana

✅Maranyingi nywele asilia  hujisokota na huwa zinafungana, hivyo wakati wa kuchana inabidi uwe mwangalifu zisikatike

✅Hakikisha unatumia shanuo ambalo ni pana na hakikisha umepaka hair lotion (hair moisturizer) kwenye nywele na mafuta ndio uanze kuchana taratibu

✅Wakati unachana anzia chini kabisa kujia juu ili kuepusha kuzifunga zaidi Na kuzikata

✅Kudetangle ni muhimu sana hii ni kuzichambua nywele moja moja kwa kuzipaka moisturizer

Kusuka

✅Hakikisha unasuka misuko ambayo haivuti Na kukata nywele pendelea zaidi nywele za kilioni Hizi hazikati nywele zako

✅Kama utakua hunasuka Hakikisha  Wakati wa kulala unaauka mabutu na kuvaa kofia ili nywele zisijifunge au kujisokota zaidi nywele ikiwa haina dawa inajisokota haraka

JINSI YA KUONDOA NA KUZUIA MBA KICHWANI

*JINSI YA KUONDOA NA KUZUIA MBA KICHWANI*

🌹🌹🌹

_Chagua moja kati ya njia hizi ili uweze kuondoa tatizo la mba kichwani_

                       🌹🌹🌹

_✅ Maganda ya limao 🍋_

✅Chukua maganda ya malimao manne hadi matano......

✅Ongeza maji vikombe vinne kisha chemsha kwa moto wa kiasi kwa dakika 10 hadi 15

✅Ikipoa oshea nywele zako na uhakikishe imegusa kwenye ngozi ya kichwa

                              🌹🌹🌹
_✅ Fenugreek 🌾 uwatu_

Vijiko 2 vya uwatu loweka kwenye maji kiasi usiku mzima...

✅Asubuhi yake saga kwenye blender upate mchanganyiko

✅Paka kwenye ngozi ya kichwa na uoshe baada ya dakika 30

🌹🌹🌹

_✅ Limao juice🍋_

✅Paka kwenye ngozi ya kichwa kisha osha baada ya dakika 15 hadi 20

                           🌹🌹🌹

_✅Vinegar na maji_

Kisia kwa ujazo sawa wa vinegar na maji paka kwenye kichwa usiku na ulale nayo asubuhi osha nywele zako

                               🌹🌹🌹
_✅ Mayai 🥚🥚_

✅Mayai 2 yachanganye vizuri kisha paka kichwani na uoshe nywele baada ya lisaa 1...

✅Hii itasaidia kuondoa mba na kuzuia nywele zako kukatika

🌹🌹🌹

_✅Aloe Vera gel 🌱_

Paka kwenye ngozi ya kichwa aloe Vera gel na umassage taratibu nywele zako kisha osha baada ya dakika 30

                         🌹 🌹🌹
_✅Lemon Juice na extra virgin coconut oil_

✅ Kijiko kimoja cha limao changanya na vijiko vitano vya mafuta ya nazi...

✅Paka kwenye kichwa na umassage taratibu kisha osha baada ya dakika 20 hadi 30

                              🌹🌹🌹

_✅ Chungwa na Apple 🍊🍏_

✅Saga Apple na chungwa kisha paka na uoshe baada ya dakika 20 hadi 30

🌹🌹🌹

_✅Kitunguu Thom na limao_

✅Changanya kitunguu thom na limao paka kichwani kisha osha baada ya dakika 30 hadi 40
                             🌹🌹🌹

_✅Kitunguumaji🌰_

✅Saga kitunguu juice yake paka kichwani kuondoa harufu ya kitunguu unaweza kuongezea limao kidogo....

✅Osha baada ya saa 1

💝Asante💝

💝UREMBO ASILIA💝

MKATE WA SEMBE NA DONA WA KINGAZIJA

MKATE WA SEMBE  mkate wa dona WA KINGAZIJA

Unga wa sembe vikombe 3

Sukari ya brown vikombe 2

Nazi (tui) kikopo 1

Asali kijiko 1cha kulia

Samli kijiko1cha kulia

Hiliki robo kijiko cha chai

Mdalasini kijiko 1 cha kulia

Uzile kijiko 1 cha chai

Bizari tamu kijiko 1 cha chai

Pilipili manga kijiko 1cha chai kama Unataka spicey ongeza na nusu

Maziwa (optional)

Kungumanga robo kijiko cha chai

NAMNA YA KUFANYA

Unguza sukari kikombe kimoja kama ya pudding ikiwa tayari tia tui lako la nazi wacha ichemke pamoja mpaka ishikane nazi na sukari tia spices zako zote, tia asali na samli,  tia na sukari kikombe kimoja iliyobaki wacha ichemke zichanganyike, ondoa kwenye jiko mwisho malizia na Unga wako huku unakoroga ikiwa utakuwa mzito unaweza kutia maziwa au maji iwe kama uji mwepesi sasa hapo rejesha  tena kwenye jiko usonge kama Ugali sio Lazima uwe kama Ugali hasa ukisha kama uji mzito uweke . uuchome kwenye OVEN kwa muda wa saa moja mpaka saa moja na robo kwa moto 350°F au 180°C, inategemea na Unga wako kama hauna machenga sana basi haukawii kuwiva. Tayari kwa kuliwa

Thursday, 27 December 2018

FAIDA ZA NDIMU

Faida za ndimu.

Umesikia mara nyingi kuwa kunywa maji kwa wingi hasa asubuhi kuna faida kubwa sana za kiafya mwilini,lakini kunywa maji yenye ndimu na vuguvugu kuna faida maradufu na ni rahisi kufanya kila siku. Vitamin C nyingi iliyomo katika limao na ndimu ni siri ya faida za tunda hili,ukiachia vitamini C ndimu ina vitamini B-complex,  madini ya Kalsiamu, chuma, magnesiamu na potasiumu, na fiba (Ndimu ina potasiumu kwa wingi kuliko tofaa(apple) au  Zabibu).

Kunywa maji peke yake (yasiyo na kitu) wakati wa asubuhi huwapa tabu baadhi ya watu,wengine hupata kichefuchefu . Lakini maji yaliyotiwa ndimu kidogo huwa na radha nzuri zaidi na watu wote wanaweza kunywa bila shida.

Kuna faida nyingi ambazo utazipata kwa kunywa maji yenye ndimu au limao na katika makala hii tunazitaja faida 11 muhimu.

Faida 11 za Kunywa Maji Yenye Ndimu

Faida #1: Huchochea Mmeng’enyo wa Chakula Tumboni
Maji yenye ndimu husaidia chakula kusagika vizuri na haraka katika mfumo wa chakula. Japo limao lina asidi(acid) lakini likiwa tumboni huwa alkali (alkaline) na kufanya mazingira mazuri kwa usagaji wa chakula.

Pia maji ya uvuguvugu husaidia kusawazisha utumbo uliojikunja na kutoa mawimbi tumboni na kufanya chakula kusukumwa vizuri.

Faida #2: Huboresha Kinga za Mwili
Vitamini C na potasiumu iliyomo kwa wingi katika limao inasaidia katika utengenezaji wa seli za kinga katika mwili.

 Faida #3: Husaidia Unyonywaji wa Madini Mwilini
Vitamini C iliyomo katika limao husaidia kunyonywa kwa madini mwilini hasa madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa utengenezaji wa damu. Hata kama maji ya ndimu yakiwa baridi.

Faida #4: Husaidia Kinga Dhidi ya Saratani
Vitamini C ni antioksidant (antioxidant) ambayo inasaidia kuondoa free radicals mwilini ambazo zimetambulika kusababisha saratani (cancer).

 Faida #5: Husaidia Kupunguza Hatari ya Kiharusi
Kutokana na matokeo ya kitafiti ulaji wa matunda jamii ya limao(citrus fruits) inasaidia kupunguza hatari ya kupatwa na shambulio la kiharusi aina ya ischemic (ischemic stroke) hasa kwa wanawake.

Faida #6: Usafishaji wa Mwili na Damu
Limao husaidia kusafisha damu kwa kuondoa uchafu. Limao pia husafisha figo ,ini na mfumo wa chakula.

 Faida #7: Kurekebisha Sukari katika Mwili
Limao husaidia kuweka kiasi cha sukari tumboni na katika mwili kuwa katika kiasi stahili.

Hii inawasaidia sana wagonjwa wa kisukari katika ulaji wao.

Faida #8: Dawa ya Kikohozi na Mafua
Limao ikitiwa katika maji ya uvuguvugu na asali husaidia sana katika kutibu mafua na kikohozi kwa njia ya asili.

Faida #9: Inasaidia Urekebishaji wa Ngozi na Kupona Makovu
Limao inasaidia kufanya ngozi isizeeke. Kama unataka kubaki kijana basi limao litakusaidia.

Tabia za vitamin C za kusafisha uchafu zinasababisha kufanya ngozi kuwa na afya na kutozeeka haraka.

 Faida #10: Husaidia Kupungua Uzito
Limao hupunguza hamu ya kula. Na inajulikana kuwa sababu kubwa ya watu kuwa na uzito mkubwa ni kula chakula kingi au kula mara kwa mara. Limao litakufanya ujisikie kushiba muda mrefu hivyo kusaidia wale amabao wanataka kupungua uzito.

 Faida #11: Kuondoa Harufu ya Mdomo
Limao husaidia kuua bakteria wabaya mdomoni ambao husababisha harufu mbaya.

 Anza Siku Kwa Kunywa Maji yenye Ndimu Kila Siku
Ni zoezi rahisi na haraka kabisa, weka maji yenye joto kidogo (vuguvugu) katika glasi au kikombe , kata limao au ndimu vipande viwili na kamua kipande kimoja tu ndani ya glasi yenye maji.

Kunywa na uanze siku mpya. Ni vizuri ukafanya hivi dakika 30 kabla ya kula chochote kingine kwa faida zaidi.

Anza leo kwa kunywa maji yenye ndimu kila siku asubuhi na uone mabadiliko ndani ya mwili wako. Mshirikishe mwenzio ili naye afaidike

MFUMO WA MAHISHA KWA AFYA BORA

Mfumo Bora Wa Maisha
Kwa Afya Bora.

Mfumo wa maisha wa mwanadamu unatakiwa kuwa bora ili awe na afya bora,afya nzuri hailetwi kwa lishe tu ,inachangia na  lifestyle yako. Lazima uwe na mpangilio ulio mzuri kuanzia unapoinza siku asubauhi yako mpaka unaporudi kulala usiku.

Afya nzuri inajengwa na lishe na mazoezi ,binadamu unatakiwa uwe makini kwenye vitu vifutavyo iwapo utafatilia utaishi kwa afya nzuri.

Kunywa maji ya kutosha-

binadamu unatakiwa kunywa maji glasi 8 kwa siku ,hilo unatakiwa ulizingatie na wanao ishi maeneo ya joto sana wanaweza kunywa zaid ya hayo,maji yatakusafisha mwili na kutoa sumu,maji hayo hayo yatakufanya kuwa na ngozi laini ,kulainisha choo ,maji yana faida nyingi sana kwa mwili wa mwanadamu hivyo ni muhimu kuzingatia hilo.

Jipe muda wa kulala-

binadamu anatakiwa kulala masaa 8 kwa siku hivyo nivizuri kupumzisha mwili na akili itakusaidia kuwa na kumbukumbu ya kutosha,kukuepusha na kiharusi,kukusaidia kunenepa,

Kula matunda na mboga za majani za kutosha-

zinakupa virutubisho vya kutosha,kukukinga na maradhi,kusaidia kupata choo kwa urahisi kwa wale wenye tatizo la constipation,kusaidia kuwa na ngozi laini ,kuweza kuona vizuri (kuimarisha macho) na faida nyinginezo nyingi.

Mazoezi-

binadamu tunatakiwa kufanya mazoezi ya miili yetu ili kuikinga na maradhi,kupunguza uzito,kutoa mafuta na sumu tunayoila kupitia vyakula,mazoezi muhimu kwa mama mjamzito,watu wenye pressure, uzito mkubwa, na maradhi mengine sugu ,mazoezi yapo ya aina nyingi unaweza kwenda gym,au ukafanya nyumbani ya kukimbi,kuruka kamba,kuogelea,kutembe mwendo mrefu,kuendesha baiskeli,kucheza mpira na mengineo mengi irimradi mwili wako uwe na movements nyingi.

Epuka kula vyakula visivyo na virutubisho-proccessed foods kawaida zinakuwa sio fresh vinakuwa na chemicals na sukari kwa wingi,acha kula vyakula vya kukaangwa vinatumia mafuta mengi na yana calories nyingi itakayo kuletea unene au matatizo ya moyo.

Epuka sukari nyingi -

kula vitu vya sukari sio vizuri kwa afya yako utaongezeka uzito kwa haraka,utaoza meno n.k. Kama ulaji ya ice cream,chocolate ,pipi  n.k sio mzuri kwa afya yako.

Positive mental health-

kaa na watu wenye mawazo chanya sio hasi ,watu wenye mawazo chanya wanafaida kwako na afya yako hawata kupa stress ila watu wenye mawazo hasi watakufanya uwe na msongo wa mawazo wao wanawaza kumsema mtu vibaya au kufanya matendo mbaya.
 
Jiamini-

unatakiwa kujiamini kwa kila ufanyalo kwani usipo jiamini utapata msongo wa mawazo na hapo utahadhiri afya yako kwa namna moja au nyingine.
 
Zingatia size ya mwili wako-

hutakiwi kuwa mnene wala mwembamba kuwa size ya kawaida kulingana na urefu wako ,uzito mkubwa au uzito mdogo sana ni madhara kwa afya yako.

Epuka pombe na sigara-

vinahadhiri afya yako kwa kiwango kukibwa kuadhiri maini,mapafu au figo n.k  ,na ni gharama kubwa unatumia kununua na kwa wakati huo huo unaboamoa afya kwa pesa yako.

Epuka kula bila kuhisi njaa-

ni makosa kula wakati tumbo limejaa hapo unajaza tumbo .

Kula mapema-

zingatia ratiba ya mlo kama asubuhi ni sa 2-3,chakula cha mchana ni  saa 6-7,usiku ni 12 jioni mpaka saa 2 usiku binadamu anatakiwa kula chakula cha usiku masaa 3 kabla ajalala kiafya chakula kinatakiwa kusagwa ukiwa ujalala,pili kula usiku sana kunasababisha kunenepa.

Usafi wa mwili wako-

ujali mwili wako uwe safi kwa kuoga,kupiga mswaki,kunyoa nywele zisizo hitajika sehemu za mwili wako.

Usafi wa mazingira unayoishi -yanatakiwa kuwa masafi unapolala,kupika,kuoga n.k itakuepusha na maradhi haswa ya mlipuko.

Kutana na marafiki kubadilishana mawazo-

unahitaji kutoka nje baada ya kazi au week end nenda kutana na marafiki mbadilishane mawazo kama mnavikundi vya maendeleo au umoja wa kikundi cha kidini ,upate habari mpya muhimu kwako ,nenda kacheze tennis,bowling,mpira au nenda shopping,fanya kitu ambayo hufanyi mara kwa mara kurelax maind yako.

LIST YA VITU ASIVYOTAKIWA KULA MTOTO CHINI YA MWAKA 1

List Ya Vitu Asivyotakiwa Kula Mtoto Chini Ya Mwaka 1

Watoto wachanga  wana miili isiyo komaa bado wanakuwa wanahitaji kulelewa kwa umakini na kwa kuzingatia lishe .Mwili wa mtoto alie chini ya mwaka hauna kinga ya kutosha kupigana na bacteria au virus wanao tokana na vyakula .Hivyo mzazi inakubidi kuwa makini kwa kupika kwa kuzingatia usafi na kuosha matunda na mikono yake kabla ajala.
 
Hii ni list ya vitu asivyotakiwa lishwa mtoto mpaka atakapo fikisha mwaka 1.

Asali -kaiwa inatabia ya kubeba bacteria ambao wanakuja kumwadhiri mtoto japo hao bacteria kwa mtoto wa mwaka 1 mwili wake unakinga ya kupigana nao,ila kwa alie chini ya mwaka 1(miezi 12) si rahisi hivyo ni vizuri asipewe.

Mafuta ya kupikia -mtoto haitaji mafuta kwenye chakula chake kwani vyakula anavyopikiwa vinamafuta ya asilia kama nyama,kuku,samaki iwapo ukatumia mafuta tumia butter isiyo na chumvi  au Olive oil ni mazuri hayana calories kama mafuta mengine na  na yatamsaidia kwenye ukuaji wa ubongo wake.

Soya-inatengeneza allergy ,inapoteza vitamins,minerals ,amino acid na fatty acid kwenye mwili wa mtoto hivyo ni vizuri wapewe wakiwa na umri zaidi ya mwaka 1.

Chumvi -wazazi wengi wanadhani chakula kisipo na chumvi mtoto hawezi kula hapana yeye ndio anaanza jifunza kula hajui ladha yoyote kuwe na chumvi au lah ,chumvi ina madini ya sodium ambayo yanaweza kwenda kuadhiri figo au  ikaenda hadhiri moyo na kupata matatizo ya  (high blood pressure) hivyo haitajiki chakula kiwe na chumvi hata kama ikatumia ni kiwango kidogo pima kwa vidole kidogo sana.

Sukari -kiwango kikubwa cha sukari sio kizuri kwa watoto inamwaribu  meno ya mtoto ,ufisi upo kwenye process za kuoteshwa meno iwapo mtoto akapewa sukari hapo anaharibu ukuwaji wa meno , au mtoto kupata matatizo ya kisukari baadae. Kwenye uji unaweza kutumia ndizi mbivu inasukari ya kutosha kwa kutumia kwa chakula cha mtoto,saga ndizi mbivu then changanyia kwenye uji  ulioiva utapata sukari asilia na ladha nzuri ,ukishindwa tumia kiwango kidogo sana cha sukari.

Maziwa ya ngo’mbe-haya yana madhara zaidi japo jamii yetu ya Tanzania iashazoea vizazi na vizazi wanapewa maziwa ya ngo’mbe ila kiukweli ni makosa yana protein nyingi sana ambayo mtoto hawezi kuimudu kuisaga na inakuja kusababisha madhara kwenye Ini baada ya mda mrefu,pili yana leta allergies kwa watoto unaweza mpa mtoto maziwa ukaona anatapika au kuhara hapo usimpe mwache ,ukiendelea kumpa itatengeneza allegry na baadae atashindwa kutumia dairy product yoyote ,Tatu ng’ombe akipewa madawa akiwa mgonjwa au chanjo yanakimbilia kwenye maziwa na ndio hayo mtoto anapewa itakuja kuwa sumu mwilini mwake na kumwadhiri.

Vyakula vibichi -vinaweza mpa bacteria kama mayai mabichi,nyama au samaki (sushi)

Saturated fat-vyakula vyenye mafuta kwaa wingi chips,crips,burger au cakes mtoto asipewe,hata chocolate ,mabisi au ice cream asipiwe umri wake bado.

Samaki wenye madini ya zebaki(mercury)nyingi  kama papa ,chuchunge,dagaa wakubwa n.k wataadhiri nervous system,badala yake mpe sangara ,sato au salmon hawa hawana mercury nyingi hawa wana mafuta ya kutosha na omega 3 zitakazo msaidia kukuza ubongo na kumfanya kuwa na akili.

Nuts-karanga au korosho mtoto asipewe kutafuna itamkwama kooni kama ni karanga basi iwe ni yakusagwa  na wapewe watoto kuanzia miezi 6 ila fahamu karanga zinaleta allergy kwa baadhi ya watoto.

Wednesday, 26 December 2018

JINSI YA KUUFANYA USO WAKO UWE WA KITOTO ZAIDI


1) JINSI YA KUUFANYA USO WAKO UWE WA KITOTO ZAIDI.
🌷Ni rahisi sana kama unatumia cream yoyote usoni acha kutumia kwani zinazeesha haraka uso wako.
🌷siyo kusema kwamba hutazeeka, lahasha ! Kuzeeka kupo lakini unaweza kuufanya  uso  wako uchelewe kuzeeka .
MAHITAJI
a) unga wa mchele  2 tsp
b) juice ya nyanya 2 tsp
c) limao 2 tsp
d)asali 1 tsp
e) vitamin E vidonge 2
JINSI YA KUTUMIA
🌷chukua mahitaji yako yote changanya pamoja kwa kukoroga.
🌷koroga vizuri ili upate mchanganyiko uliochanganyika vizuri.
🌷kisha paka usoni mwako taratibu kwa kumassage kwa dk 2
🌷kisha kaa saa  1 nawa usoni.

KUMBUKA
🌷njia hii hung'arisha  sana USO wako pale unapoitumia kila siku.
🌷uso  wako kuwa Wa kitoto  zaidi kadri unavyotumia.
🌷pia kuondoa madoa  ,mikunjo, makunyanzi usoni.
🌷kama hauna  chunusi USIWEKE LIMAO.
🌷UNAWEZA KUTENGENEZA MCHANGANYIKO MWINGI NA KUUTUNZA KWENYE FRIJI UNADUMU WIKI NZIMA.

JINSI YA KUNGA'RISHA MENO NA KUTIBU HARUFU MDOMONI

Jinsi ya kunga'risha meno na kutibu harufu ya mdomo!
Mahitaji
🌳limao moja
🌳bakingsoda kijiko kimoja
🌳asali kijiko cha chai
🌳mdalasin kijiko cha chai
🌳maji moto kikombe
.
.
Jinsi ya kufanya
🍃Chukua mdalasin na maji ya ndimu changanya ktk jagi dogo.
🍃chukua asali koroga sana kisha ongeza yale maji moto na bakingsoda ,changanya kdgo kisha acha maji yawe vuguvugu.
🍃chukua mchanganyiko kdgo wake mdomoni sukutua kisha acha kwa dk 2 kisha tema !! Fanya ivo kila upatapo nafasi meno yatakuwa meupe na harufu mbaya hotousikia tena
NB. Baada y kupiga mswaki na dawa piga na mchanganyiko huu meno yatakuwa meupe pee👏🏻👏🏻
.

Tuesday, 25 December 2018

VISHETI VYA MAZIWA

VISHETI VYA MAZIWA :

Mahitaji :

Unga nusu na robo
Siagi robo
Maziwa vikombe 3 vya kahawa (ya unga)
Baking Powder kijiko 1 cha chai
Yai 1
Sukari kiasi chako
Vanilla kijiko 1/2 cha chai
Iliki ya unga 1/2 cha chai

Maelezo :

Changanya pamoja unga na siagi kisha weka baking powder maziwa na yai, chanyanya tena. Yeyusha maziwa ya unga kwa maji kisha kandia mchanganyiko wa visheti.
Ukimaliza kuuchanganya kisha tengeneza shape uipendayo. Baada ya hapo kaanga visheti kwenye mafuta ya kutosha.

Shira ya visheti :

Sukari kikombe 1 cha chai
Maji 1/2 kikombe cha chai
Hiliki kiasi
Vanilla essence 1/2 kjk cha chai

Mimina kwenye sufuria sukari,maji na hiliki na vanilla essence jwa moto kwa kiasi huku unakorogoa kidogo.
Wacha sukari ichemke kidogo na ukiona imetoa povu na ukishika inanata vasi epua na zima jiko na mimina visheti vichanganye na shira na peta kisha mimina kaika sahani na acha vipoe. Baada ya hapo tayari kuliwa.

UTENGENEZAJI WA SHAMPOO

Jinsi ya kutengeneza shampoo
Malighafi
-sulphonic acid
-ciles
-rangi
-perfume
-chumvi
-CDE
-gycerine
-sodash

Jinsi ya kutengeneza
-andaa vyombo kuwa na mwiko wa kukorogea,ndoo,beseni na maji
-anza na sulphonic acid vijiko vi 3
-fuata na ciles changanya vijiko 41/2
-koroga kwa dakika 3

NB:TUNAKOROGA UPANDE MMOJA ILI SHAMPOO YAKO
ISIKATIKE

-Chukua sodash ichanganye na maji kidogo then ukoroge kwa dakika kadhaa hadi mchanganyiko ukae sawa.
-chukua mchanganyiko wako huo wa sodash mimina kwenye mchanganyiko wa kwanza koroga mpaka ilainike.
-mimina glycerine vijiko 2 then koroga
-mimina rangi kiasi
-mimina perfume
-weka CDE kichupa kizima mimina
-Unaweka maji yako lita kumi then koroga
-unamalizia na chumvi kilo 1 unakoroga mpaka ilainike
NOTE: Tunatumia chumvi ya mawe,na chumvi ni hatua ya mwisho kabisa katika utengenezaji wako.

UTENGENEZAJI WA SABUNI YA UNGA

*jinsi ya kutengeneza sabuni ya  unga*

*MAHITAJI*

.Optical bytina.

.sodium carbonate.

.sulphonic acid.

.Sodium sulphate.

.Hoda ash.

.Hydrogen peroxide.

.Rangi.

.Perfume.

*JINSI YA KUTENGENEZA*

Andaa chombo chochote kinachoendana na wingi wa sabuni unayotaka kutengeneza na anza kutengeneza kwa kufuata hatua zifuatazo.

.weka sodium carbonate kwenye chombo ulichoandaa kg2 na nusu.

.Baada ya hapo weka optical bytina vijiko kumi(10)vya chakula.

.halafu weka sodium sulphate vijiko vitano vya chakula.

.weka soda ash kg7 na ukoroge kwa muda wa dakika kumi.

*HATUA YA PILI*

.Sulphonic acid kilo 2 na nusu.

.nausa vijiko 15 vya chakula.

.Hydrogen peroxide kama ni ya unga weka kilo mbili kama ya maji weka lita mbili.

.rangi vijiko vitano vya chakula.

. changanya na perfume vijiko sita vya chakula.

.baada ya mchanganyiko huo anika kwenye kuvuli kwa kuwa juani inaweza kuyeyuka.sabuni yako itakauka kwa kujiachia.

Kusanya weka kwenye mifuko tayari kwa kuuza.

*ONYO: Baadhi ya malighafi ni acid kwahiyo umakini unatakiwa wakati wa kutengeneza,hakikisha mikono yako imelindwa kwa gloves na usishike acids au kula wakati unafanya kazi.Tafadhari watu wazima ndio wafanye kazi hii*

UTENGENEZAJI WA WA DAWA YA KUONDOA MADOA KWENYE NGUO ( JIK)

Utengenezaji Wa dawa ya kuondoa madoa kwenye nguo (jik)

Mahitaji

1*Chloride acid ( krolaid asidi)

2*Soda ash

3*maji

  Utengenezaji

Andaa ndoo ya Lita 20 kisha weka maji Lita 10 anza kukoroga maji  kuelekea upande mmoja ukitumia mti au mwiko

Baada ya kuanza kukoroga maji mimina na chloride acid kilo 1 uku ukiendelea kukoroga

Kisha muda huo huo mimina soda ash vijiko 3 vya chakula endelea kukoroga kwa dakika 10

Baada ya dakika 10 jik yako ipo tayar kwa matumizi

Nb kwa wakaz wa dar maduka yapo k.koo mtaa wa Swahili na nyamwez

Soda ash upo kama unga wa ngano

Chloride ipo ya chenga chenga

Sunday, 23 December 2018

UTENGENEZAJI WA SABUNI YA UNGA

UTENGENEZAJI WA SABUNI YA UNGA
➖➖➖➖➖➖
*Malighafi*
1:maji----nusu Lita
2:sodaash---kilo 6
3:sodiam metasiliketi----kilo 1(kg1)
4:optical praitina---vijiko 10 vya chakula
5:manukato(perfume)---vijiko 2 vya chakula
6:Nansa----vijiko 15 vya chakula
7:rangi--vijko viwili vya chakula jpo sio lazima
8:Sulphuric acid ( asidi ya salfa) au salphonic acid--- Lita 1
*JINSI YA KUANDAA*
☑Andaa beseni yenye ujazo wa Lita 20-25,liwe kavu au tupu,kisha tia salphuric acid ikifuatiwa na maji na uanze kukoroga kuelekea upande mmoja hadi vichngnyikane vizri ndan ya dk3 au 5
↗Tia iptical praitina,nansa na manukato halafu koroga kuelekea upande mmoja ndani ya dak 3-4
🔼Wakati ukiendelea kukoroga katika mchangnyiko wa pili ,tia sodaash nusu ya kilogram 1,kutoka katika zile kg 6,endelea kukoroga ,wakati ukiendlea kukoroga tia sodiamu metasiliketi 1kg yote,kisha endelea kukoroga uhakikishe hyo sodiam metasiliketi inachanganyikan vzr ,baadae malizia ile sodaash iliyo baki kutoka kwenye ile kilo 6 ambayo ni kg 5 na nusu kisha koroga kuelekea ule upande mmoja na uhakikishe imechanganikan vizur ndan ya dak5
◀Mwisho tia rangi kama utapenda sabuni yko iwe na rangi na kam hupendi acha na kam pia utapenda sabun yko iwe na rangi tofauti unaweza kuchanganyachangnya rangi hizo mbalimbali upendavyo ,baada ya hapo tumia nailon kubwa au mfuko wowte kuianika sabuni yko katika kivuli kwa mda wa masaa 3 au 4 ,hapo itakuwa iko tayari kwa matumizi
🖤kumbuka rangi sio lazim san katika aina hii ya sabuni aksanteni san nawasilisha

Saturday, 22 December 2018

DAWA YA KUONDOA MAUMKVU WAKATI WA TENDO

Hii ndio dawa ya kuondoa maumivu wakati wa tendo

Mahitaji
1*mafuta ya mzaituni

2*majani ya mbahazi

Utengenezaji

Saga/twanga majani ya mbahazi mabichi

Baada ya kusaga changanya na mafuta ya mzaituni hakikisha ni yamekua lain

Baada ya hapo unaweza kuchukua ped na kuweka dawa yako kwa mbele na kuivaa na acha kwa masaa 4 pia Fanya Mara 1 kwa siku 4 mfurulizo utapata hamu ya tendo

Utaondoa maumivu wakati wa tendo

Utaongeza utamu wakati wa tendo

Utaondoa harufu mbaya wakati wa tendo kwa kutumia dawa hii hii matumizi haya haya

Nb utapata joto sehemu za Siri wakat wa dawa inafanya kazi

Nb hakikisha anakuandaa ukiona unaumia ndio utumie hii dawa

Thursday, 20 December 2018

JINSI YA KUONDOA MATEGE KWA MAFUTA MAALUM YA KUMASSAGE

👉🏻5) JINSI YA KUONDOA MATEGE KWA MAFUTA MAALUM YA KUMASSAGE.
🥒hii ni njia ambayo itaondoa matege  miguuni  kadri utakavyotumia ,hadi matege  yatisha  kabisa.
MAHITAJI
a) mafuta ya kitunguu swaum
JINSI YA KUTUMIA
🥒chukua mafuta ya kitunguu swaum paka kwenye miguu yako ,anza kuimasage kwa kuinyoosha taratibu kwa dk 5
🥒tumia mafuta haya Mara 2 kwa siku.
🥒MAFUTA YA KITUNGUU SWAUM UTAYAPATA MADUKA YA ASILI.
🥒MATOKEO YA NJIA HII YANACHELEWA KUONEKANA ,HIVYO BASI USIKATE TAMAA PAKA HADI UPATE KILE UNACHOKITAKA.

JINSI YA KUKUZA MAKALIO ,NJIA YA ASILI

Mchanganyiko wa dawa

Mahitaji

1*amira

2*bamia

3*magadi soda

4*,,mafuta ya mzaituni

Utengenezaji

Andaa bamia zisizo komaa 3

Andaa magadi soda vijiko 3

Andaa mafuta robo Lita

Andaa amira vijiko 2 vya chakula

Kisha kwa wingi wa mahitaji hayo utatumia kwa siku 1

Kwa wingi wa mahitaji hayo weka katika blenda na usage kupata uji lain wenye kuteleza

Baada ya kupata mchanganyiko ondoa kwenye blenda na uweke katika bakuli na acha sehemu ya barido kwa dakika 30

Baada ya dakika 30 ingia kwenye matumizi

Ma tu mi zi

Chukua mchanganyiko huo paka sehemu ya makalio na Fanya kama unabinya na kupiga piga pia kumbuka usisahau kwenye mahipsi usipo Fanya ivyo utakua kituko

Paka wakat mzuri wa usiku ukiwa hauna vazi lolote ili usichafue ngue na hii dawa inaendana na ubaridi ivyo ukivaa nguo haitasaidia haraka

Fanya Kwa siku 21 mfurulizo na dawa haitakiwi kulala kwa siku 3

Tuesday, 18 December 2018

UTENGENEZAJI WA TAMBI

Utengenezaji Wa tambi kwa kiwanda kidogo
Mahitaji

1*Unga wa ngano

2*mchele

3*binzali

4* mchele

5*maji

6*chumvi

Utengenezaji

Chemsha mafuta kiasi cha vijiko 3 vya chakula kisha weka na binzali nyembamba kijiko 1 cha chakula kisha weka na chumvi vijiko 2 vya chakula pamoja na maji robo Lita kisha saga katika blenda kupata mchanganyiko laini

Kisha chukua unga wa ngano nusu changanya na unga wa mchele robo kisha chukua chujio la chai chuja ule mchanganyiko uliopo kwenye blenda ukiwa unachuja hali ya kua unamwagia kwenye mchanganyiko wa unga

Baada ya kuchanganya weka tena mafuta ya moto kiasi kwenye unga na ukande uwe laini
Kisha baada ya kupata unga laini
Utaweka donge la unga  ukiwa unazungusha basi unatoa tambi nyembamba

Wakati unatoa tambi haki kisha mashne umeitegesha kwenye kalai la mafuta kusudi tambi ziangukie jikoni

Ila haki kisha mafuta yawe makali na tambi zisikae sana jikoni
Tambi zako zipo tayar kwa matumizi

Monday, 17 December 2018

VITUMBUA VYA NAZI

VITUMBUA Vya Nazi 😋😋😋

Mahitaji:

Unga wa mchele kikombe 1
Unga wa ngano vjk 4 vya kula
Nazi ya unga pakiti 1
Ute wa yai 1
Maji ya vugu vugu 1/2 kikombe
Hamira kjk 1 cha chai
Sukari 1/4 kikombe
Hiliki ilipondwa kjk 1 cha chai
Mafuta

Maelekezo:

Changanya unga wa mchele, ngano, ute wa yai, sukari, hamira, hiliki na nazi kisha ongeza maji kidogo kidogo huku unakoroga mpaka uwe uji mzito
Funika na acha iumuke kwa dakika 45-60 hadi ifanye mapovu kwa juu na umejaa mara mbili yake
Wapishi wengine hupenda kuacha unga uumuke usiku kucha
Koroga unga wa vitumbua
Weka chuma jikoni na utie mafuta kidogo na unga wa vitumbua hakikisha iwe 3/4 isijae mpaka juu
Pika kwa dakika 2-3 mpaka kiwe cha kahawia geuza upande wa pili nao uwive. Kikiiva ipua weka kwenye sinia vipate hewa. Andaa enjoy sweet

UTENGENEZAJI WA JAMU YA NANASI

*UTENGENEZAJI WA JAMU YA NANASI*

Jamu ya nanasi ni bidhaa inayotengenezwa kwa kutumia mchanganyiko wa mananasi yaliyosagwa (pulp) na kuchemshwa pamoja na sukari na acid. Ili kupata jamu yenye ubora mzuri ni sharti kuzingatia uwiano mzuri kati ya acid, sukari na pectin.


*Mahitaji/Viambaupishi*

Nanasi

Sukari

   
citric acid (Kutegemeana na aina ya matunda)

   *VIFAA*

SUFURIA

   KIJIKO CHA CHAI

  VISU

  KIPIMA JOTO (THERMOMETER)

   CHUJIO

   MWIKO

   NDOO

     SINIA
   REFRACTOMETER

  MZANI

MASHINE YA KUSAGA MATUNDA (BLENDER)AU ‘PULPER’


  UBAO WA KUKATIA MATUNDA

Hatua za uzalishaji

Osha matunda vizuri kwa maji safi na salama. Chagua matunda yalyoiva
Menya matunda na ondoa macho na moyo wa katikati, katakata vipande na uvizage.
Chemsha kupata pulp ya matunda

Weka

sukari
acid

Changanya vizuri, pika polepole ukikoroga hadi joto la kutosha litakapofikia.
Hakikisha jamu yako imeiva vizuri
Jaza kwenye chupa safi ikiwa bado ya moto.
Jamu tayari

Saturday, 15 December 2018

TIBA YA KUONDOA HARUFU MBAYA UKENI

Tiba ya dawa ya kuondoa harufu mbaya ukeni

Mahitaji

1*kitunguu swaumu

2*maziwa mtindi

3*magadi soda

Utengenezaji

Andaa blenda na uweke maji vijiko 10 yani mililita 100

Kisha weka kitunguu swaumu 1 kikubwa

Kisha weka maziwa robo Lita yawe mtindi au fresh ila yawe ya ng'ombe

Kisha weka na magadi soda kijiko 1

Kisha saga iwe laini kabisa alafu huo mchanganyiko utumia kunawa kwa kuchovya kwenye kitambaa

Fanya Mara 1 kwa siku kwa siku 7 mfurulizo

Ila kama tatzo la muda mrefu tumia kwa siku 21

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO