*UTENGENEZAJI WA JAMU YA NANASI*
Jamu ya nanasi ni bidhaa inayotengenezwa kwa kutumia mchanganyiko wa mananasi yaliyosagwa (pulp) na kuchemshwa pamoja na sukari na acid. Ili kupata jamu yenye ubora mzuri ni sharti kuzingatia uwiano mzuri kati ya acid, sukari na pectin.
*Mahitaji/Viambaupishi*
Nanasi
Sukari
citric acid (Kutegemeana na aina ya matunda)
*VIFAA*
SUFURIA
KIJIKO CHA CHAI
VISU
KIPIMA JOTO (THERMOMETER)
CHUJIO
MWIKO
NDOO
SINIA
REFRACTOMETER
MZANI
MASHINE YA KUSAGA MATUNDA (BLENDER)AU ‘PULPER’
UBAO WA KUKATIA MATUNDA
Hatua za uzalishaji
Osha matunda vizuri kwa maji safi na salama. Chagua matunda yalyoiva
Menya matunda na ondoa macho na moyo wa katikati, katakata vipande na uvizage.
Chemsha kupata pulp ya matunda
Weka
sukari
acid
Changanya vizuri, pika polepole ukikoroga hadi joto la kutosha litakapofikia.
Hakikisha jamu yako imeiva vizuri
Jaza kwenye chupa safi ikiwa bado ya moto.
Jamu tayari
No comments:
Post a Comment