MKATE WA SEMBE mkate wa dona WA KINGAZIJA
Unga wa sembe vikombe 3
Sukari ya brown vikombe 2
Nazi (tui) kikopo 1
Asali kijiko 1cha kulia
Samli kijiko1cha kulia
Hiliki robo kijiko cha chai
Mdalasini kijiko 1 cha kulia
Uzile kijiko 1 cha chai
Bizari tamu kijiko 1 cha chai
Pilipili manga kijiko 1cha chai kama Unataka spicey ongeza na nusu
Maziwa (optional)
Kungumanga robo kijiko cha chai
NAMNA YA KUFANYA
Unguza sukari kikombe kimoja kama ya pudding ikiwa tayari tia tui lako la nazi wacha ichemke pamoja mpaka ishikane nazi na sukari tia spices zako zote, tia asali na samli, tia na sukari kikombe kimoja iliyobaki wacha ichemke zichanganyike, ondoa kwenye jiko mwisho malizia na Unga wako huku unakoroga ikiwa utakuwa mzito unaweza kutia maziwa au maji iwe kama uji mwepesi sasa hapo rejesha tena kwenye jiko usonge kama Ugali sio Lazima uwe kama Ugali hasa ukisha kama uji mzito uweke . uuchome kwenye OVEN kwa muda wa saa moja mpaka saa moja na robo kwa moto 350°F au 180°C, inategemea na Unga wako kama hauna machenga sana basi haukawii kuwiva. Tayari kwa kuliwa
No comments:
Post a Comment