*JINSI YA KUTUNZA NYWELE ASILI ISIYO NA DAWA*
Shampoo
✅Unapoosha nywele zako hakikisha unatumia shampoo ambayo imetengenezwa kwa ajili ya natural hair
❌Usioshee shampoo zenye chemicals kama paraben na sulfate hizi hupelekea kukatika nywele Na kubaribika
✅Pia pendelea shampoo yenye conditioner yaani 2 in 1 Hii itasaidia nywele zako kuwa laini na kuzuia zisiwe kavu baada ya kuziosha itakusaidia pia kwenye kuzichana
Mafuta
✅Pendelea zaidi kuzipaka mafuta ya maji kama vile mafuta ya nazi olive oil, jojoba oil au castor oil kwasababu mafuta haya hulainisha ngozi ya kichwa, kufanya nywele zikue vizuri na kuzuia Kufanya mba
✅Mafuta ya mgando maranyingi hutengeneza mba kwenye nywele za asili kwa urahisi sana tofauti na nywele zenye dawa
Hot oil treatment/prepoo
✅Hii ni nzuri kwa nywele zako Hakikisha kabla hujaosha nywele zako unazifanyia prepoo kwa mafuta ya moto kama kwenye post zilizopita
Steaming
✅Hakikisha nywele zako unazifanyia steaming angalau Mara 2 kwa mwezi
✅Vizuri zaidi ukitumia mask za asili kama yai, parachichi Na nyengine tulizowahi kupost
Detangle Na kuzichana
✅Maranyingi nywele asilia hujisokota na huwa zinafungana, hivyo wakati wa kuchana inabidi uwe mwangalifu zisikatike
✅Hakikisha unatumia shanuo ambalo ni pana na hakikisha umepaka hair lotion (hair moisturizer) kwenye nywele na mafuta ndio uanze kuchana taratibu
✅Wakati unachana anzia chini kabisa kujia juu ili kuepusha kuzifunga zaidi Na kuzikata
✅Kudetangle ni muhimu sana hii ni kuzichambua nywele moja moja kwa kuzipaka moisturizer
Kusuka
✅Hakikisha unasuka misuko ambayo haivuti Na kukata nywele pendelea zaidi nywele za kilioni Hizi hazikati nywele zako
✅Kama utakua hunasuka Hakikisha Wakati wa kulala unaauka mabutu na kuvaa kofia ili nywele zisijifunge au kujisokota zaidi nywele ikiwa haina dawa inajisokota haraka
No comments:
Post a Comment