HOMEMADE FONDANT ICING / NAMNA YA KUANDAA FONDANT KWA AJILI YA KEKI NYUMBANI :
MAHITAJI
🔸Icing sugar, ilochekechwa vikombe 7 na 1/2
🔸Maji ya baridi 1/4 kikombe
🔸Unflavored gelatin kijiko 1 chakula (kwa waislam hakikisha ni halali gelatin) maana zingine zatengenezwa kwa mafuta ya nguruwe
🔸Glucose 1/2 kikombe
🔸Glycerine kijiko 1 1/2 chakula
🔸Vanilla kijiko 1
*NOTE*
GLYCERINE YA CAKE NA GLUCOSE YA CAKE. SIO VYA KUPAKIA MWILINI. NI VIFAA KWAJILI YA CAKE🎂
NAMNA YA KUTAYARISHA:-
1. Tia icing uliochekecha katika bakuli kubwa kisha weka kishimo kati
2. Katika kisufuria kidogo tia maji kisha nyunyiza gelatin juu acha ilainike kwa muda wa dk 5.
3. Ipashe moto gelatin ukiwa wakoroga hadi iyeyuke yote , usiache *ikachemka.* Zima jiko kisha tia glucose na glycerine na koroga vizuri hadi vichanganyike.
4. Tia radha, kisha mimina katika kishimo ulichoweka karika icing yako na changanya hadi icing yote ichanganyike vizuri.
5. Kanda foundant yako katika sehemu ya kukandia au sinia hadi iwe smooth na soft, ukiona inanata ongeza icing kidogo.
6. Fanya duara kisha zungusha vizuri na plastic na tia katika container lenye mfuniko.
NOTE
Usiweke katika fridge tumia kwa muda wa wiki 2
Ni vyema uiache ikae kwa muda wa masaa 8 kabla ya matumizi
Mahitaji yanapatikana maduka ya vifaa vya keki,na supermarket.
No comments:
Post a Comment