Tuesday, 29 January 2019

JINSI YA KUTENGENEZA CHOCOLATE

JINSI YA KUTENGENEZA CHOCOLATE
Unaweza kutengeneza chocolate nyumbani kwa kutumia vifaa vya nyumbani na ingredients zinazo patikana madukani.

MAHITAJI KWA AJILI YA CHOCOLATE.
-Siagi kikombe kimoja
-Cocoa powder kikombe 1
-Icing sugar/Sukari iliyosagwa au asali kikombe 1/2
-Maji 1/2 kikombe
-Vanilla ya maji kijiko 1 ccha chai
-Chumvi tone

MAELEKEZO
1)Pima Sukari na Cocoa powder kwenye sufuria size ya kati.
2. Ongeza maji kwenye mchanganyiko wa sukari na cocoa poda.

3)Weka maji kwenye sufuria kubwa yajae 1/4 kisha weka kwenye moto mdogo.
4)Weka sufuria ya size ya kati iliyo na cocoa poda+sukari+maji juu ya sufuria kubwa(double boiler).

5)Wakati maji ya sufuria kubwa yanachemka, koroga mchanganyiko wako wa cocoa poda taratibu, kwa dk 15 mpaka iwe nyepesi kama uji.
6)Ondoa sufuria ya mchanganyiko wa chocolate kwenye moto, kisha ongeza  siagi iyeyukie, ongeza fleva kama vanila.

7)Blend mchanganyiko wako, tumia blender au hand mixer,lengo la kublend ni kufanya chocolate yake iwe smooth isiwe na mabuja.

8)Mimina chocolate mchanganyiko,kwenye ice cube tray,acha kidogo isawazike kwa dk2.
9)Weka ice cube tray iliyo na chocolate kwenye freezer, kwa masaa 1-2 au usiku kucha.
10)Waweza toa kwa lisaa limoja,kisha ukaweka juu ya chocolate karanga zilizosagwa,au peanut butter,au strawberry(Angalia pichani),kisha rudisha frijini kwa lisaa1.

-Chocolate tayari,toa tray, ondoa chocolate kwenye tray tayari kwa kuliwa.ENJOY
  👩‍🍳 mapishi bora 👩‍🍳

No comments:

Post a Comment

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO