Monday, 14 January 2019

MALIGHAFI ZINAZO HITAJIKA WAKATI WA UTENGENEZAJI WA MISHUMAA

*Jinsi ya kutengeneza mishumaa*

*MALIGHAFI ZINAZO HITAJIKA WAKATI WA UTENGENEZAJI WA MISHUMAA*

1. Paraffin Wax
2. Utambi
3. Mould ( Umbo )
4. Stearine au mixture
5. Rangi
6. Jiko la mafuta ya taa au mkaa.
7. Sufuria.
8. Boric acid.

*VIDOKEZO MUHIMU*
1. Paraffin Wax :
Hii inatokana na nta na sega ya nyuki iliyo changanywa na mafuta ya taa. Ina rangi nyeupe na katika utengenezaji wa mishumaa ina ubora kuliko bee wax.

* Bee Wax : Inatokana na masega ya nyuki yaliyo changanywa na mafuta ya petroli na diesel na rangi yake ni ya njano.

2. STEARINE
Hii dawa maalumu inayo fanya mishumaa iungane ama ishikamane.

3. BORIC ACID :
Hii ni maalumu kwa ajili ya kuufanya utambi usiishe mapema na uwake bila kutoa moshi.

4. RANGI :
Rangi nzuri zinazo tumika katika utengenezaji mishumaa ni rangi za chakula na nyingi huwa ni za maji.

*JINSI YA KUTENGENEZA*

Andaa mould ( umbo lako ) utakalo litumia baada ya kuyeyusha ( paraffin wax ) na kuchanganya na michanganyo yote.

Kwa Mfano : ( Kipimo cha stearine )
1. Wax kilo moja - Stearine vijiko vinne vya chakula.
2. Wax nusu kilo - Stearine vijiko vinne vya chakula
3. Wax robo kilo - Stearine kijiko cha chakula.

Baada ya mould ( umbo ) kuwa tayari , chemsha wax mpaka iyeyuke na itoe kwenye vyombo ambavyo umetayarisha na usubiri ikauke ili uanze kutoa mishumaa

No comments:

Post a Comment

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO