Utengenezaji Wa sabuni ya magadi/mawingu
Mahitaji
1*kaustiki soda (kama chumvi)
2*maji
3*mafuta ya mise au Nazi
4*magadi soda
5*chumvi
6*sodium silket au cde kimoja wapo (kama mafuta)
Vifaa vya usalama
Grops za mikono
Mask kuziba pua wakat Wa kukoroga kaustiki
Ndoo
Mti Wa kukoroga
Boksi za kawaida kwaajiri ya kufanya maumbo
Utengenezaji
Hatua ya kuanza
Andaa ndoo Lita 10 weka maji Lita 5
Baada ya kuweka maji weka magadi soda vijiko 3 vya chakula ..
Baada ya hapo mimina kaustiki soda kilo 1
Anza kukoroga Kwa dakik 5
Baada ya hapo acha kwa siku 3 uwe umefunika au umeacha wazi ni sawa
Maelezo
Wakati Wa kuweka kaustiki maji yatakua ya moto ndio hali yake ila utakiwi kuchezea kwa mikono
Hatua ya kumalizia
Baada ya siku 3 kaustiki itakua imepoa kwahy tumeleweka kwenye maji ili isichubue mikono sabuni yetu
Sasa chukua ndoo yenye maji ya kaustiki anza kumimina malighafi zifuatazo
Sidiuom silket au c.d.e vijiko 3 vya chakula
Kama unayo soda ash unaweza kuweka vijiko 3 vya chakula kama hauna acha tu
Baada ya hapo chemsha mafuta yako yawe ya vugu vugu sababu yana asili ya kuganda kwahy lazima uyachemshe hata kama hayajaganda
Baada ya kuchemsha sasa utaangalia ukubwa Wa umbo lako
Mimi Nina boksi Dogo nimeomba dukani kwahy nitachota Yale maji ya kaustiki soda Lita 1 alafu nitaweka kwenye ndoo isiokua na kitu chochote alafu nitachanganya na mafuta Lita 2 nitakoroga kidogo Sana kama sekunde 20 alafu namimina kwenye boksi langu ili ikauke kisha nikate vipande
Ila wakat Wa kuandaa boksi kwa ndani nitaweka maironi ili sabuni ikikauka isinasie kwenye boksi
Pia ile naironi nitaitoboa vitobo kidogo ili kuna maji maji niyape nafasi ya kupita
No comments:
Post a Comment