VITU VIKUU VITATU VILIVYOBEBA TOFAUTI KATI YA WATU WALIOFANIKIWA NA FAILURES
Wote tunakuja duniani baada ya kuwa washindi katika mapambano makubwa yanayohusisha mabilioni ya washiriki.....Wote tunakaa mapumzikoni miezi tisa tukijaandaa na pambano lingine.....Wote tunakuja duniani tukiwa full packed na vitu muhimu vya kukusaidia kushinda mapambano mengine ya hapa duniani, ambapo Mungu humpa kila mtu vitu sahihi anavovihitaji kuendana na aina ya pambano lake.....Yaani tunapewa vitu kama vile Passion, talents, core abilities, potential, akili, nguvu, viungo kutokana na kuendana na aina ya mapambano unayoyaendea.......SWALI NI JE, NINI KINASABABISHA WENGINE WASHINDE MAPAMBANO YA HAPA DUNIANI NA WENGINE WASHINDWE ILI HALI WE ARE ALL WINNERS??.......Utofauti huanza kuonekana kutokana na;
1. Kutotumia nyenzo za Mapambano tulizopewa na Mungu.
Kila mtu amezawadia na Mungu vitu maalum vya kumsadia kwenye mapambano....Na kwa bahati nzuri ni kuwa yeyote anayeamua kuzitumia nyenzo hizi ni lazima awe mshindi kwenye hayo mapambano.
Na tofauti ya watu wanaofanikiwa na wasiofanikiwa huanza pale ambapo wengine wanaamua kuzitumia nyenzo hizi wengine wanapuuzia kuzitumia...... Am totally convinced kwamba "Kila mtu ana kipaji/ Uwezo fulani wa kipekee aliopewa na Mungu" ambao ndiyo nyenzo kuu kwake kwa mafanikio....... Kuna watu wamepewa kuchora, wengine kuimba, wengine kufundisha, wengine udaktari, wengine uhandisi, wengine uongozi, wengine Technology, wengine uvumbuzi wa vitu, wengine biashara na ujasiliamali, wengine kishauri, wengine utunzi, wengine habari, wengine ujeshi, wengine michezo etc......Vitu hivi vyote na vingine vingi Mungu ameweka ndani yetu kama Primary weapon ya kutusaidia kufanikiwa.... Tatizo ni kuwa kutokana na Malezi na kukua tukitamani maisha ya watu wengine waliotutangulia kutokana na kuangalia mahali panapoonekana panalipa kwa macho ya kibinadamu basi wengi wameiga na kijikuta wamekaa maeneo ambayo siyo ya kwao......Mtu alitakiwa kuwa daktari amekaa kwenye uhandisi, aliyetakiwa kuwa mwana michezo yupo kwenye udaktari, mwanajeshi yupo kufundisha watoto kama mwalimu, mchoraji yupo polisi, aliyeumbwa kuwa mwanasheria yupo hospitali kama daktari na aliyetakiwa kuwa mchungaji kanisani yupo kwenye siasa.....Yaani ni vururu vururu kila mtu amekaa mahali pasipo pake na hivyo kutotenda kwa viwango vikubwa vya hali ya juu na hivyo siyo rahisi kufanikiwa eneo ambalo siyo eneo lako sahihi. Kwani mtu aliyekaa kwenye eneo lake sahihi kuwa na uwezo wa tofauti na wengine kwenye eneo hilo na anaweza kuona zaidi ya wengine wanavyoona kwenye hilo eneo na pia huwa mbunifu na mvumbuzi wa mambo kwenye hilo eneo.....Sasa wachache waliofanikiwa kukaa kwenye maeneo yao sahihi ndilo kundi la watu waliofanikiwa sana na sisi tunawashangaa na kuwaona kuwa hawa watu wa maakili mengi lakini kumbe hata siyo akili bali ni kutambua eneo lao sahihi na kuamua kukaa hapo.
Watu waliokaa kwenye maeneo yao sahihi ni wabunifu, wavumbuzi wa vitu vipya, wanafanya kwa ubora kwani wao kwao ni kama hobby, wanajituma bila kuambiwa kwani wanaenjoy kufanya hata bila malipo wapo tayari kufanya.
Siyo rahisi kufanikiwa eneo ambalo siyo eneo lako sahihi...... Ukikaa eneo ambalo siyo eneo lako sahihi utaonekana kilaza tuu.....Nyani hakuumbwa akae majini hivyo kama akiwekwa majini utamcheka sana na kumuona hana uwezo.....Samaki hakuumbwa akae nchi kavu bali majini, ukimpleka samaki nchi kavu utamuona kilaza.....simba hakuumbwa kupanda miti, ukimshindanisha na nyani eneo hilo basi lazima simba ainekane mbumbumbu..... Hivyo ndivyo binadamu tumekosea kutokukaa maeneo yetu sahihi.... Leo ukimuona Diamond Platnums anafanikiwa ni kwa sababu yupo eneo lake sahihi, Mbwana Samatta anazidi kuchanja mbuga ni kwa sababu yupo eneo lake sahihi etc.....JITAFUTE, TAFUTA ENEO LAKO SAHIHI, THEN KAA HAPO KWANI NDIPO PENYE MAFANIKIO YAKO!!
2. Tabia zinazoongoza maisha yetu ya kila siku (HABITS).
Mafanikio ni muunganiko wa tabia mbalimbali zinazoleta mafanikio, na uzuri ni kuwa tabia ni kitu ambacho kila mtu anaweza kujifunza.....Ukimuona leo mtu ni Drug addict basi jua hakuzaliwa anatumia madawa ya kulevya bali ni tabia tu alianza kujifunza taratibu, na inawezekana alianza na pafu moja ya bangi na badae akazoea na kuona kuwa bangi hazina stimu za kutosha na kuamua kuanza na unga kidogo then finally addiction.....Tambua kuwa tofauti kubwa iliyopo kati ya watu waliofanikiwa na watu failures siyo akili wala mazingira bali ni tabia zao zinazoongoza maisha yao ya kila siku......Tofauti iliyopo kati ya masikini na tajiri siyo pesa bali ni tabia, kwani huyu ambaye anaonekana masikini leo kama akiamua kuishi kwa tabia za watu matajiri naye baada muda fulani atakuwa tajiri tu.
Kitu chochote ukikifanya maranyingi na kila siku huwa kinakuwa tabia.
Tabia za uvivu, uongo, kuto kujituma, ni miongoni mwa tabia zinazoleta umasikini na kufeli kwenye maisha....Lakini kujituma, ukweli, uaminifu, kumcha Mungu, ni tabia zinazoleta mafanikio.
Tabia ni kitu unaweza kujifunza, Anza leo kujijengea utaratibu wa kujijengea tabia zinazoleta mafanikio.... Kitu chochote ukikifanya kwa mfululizo kwa siku 21 huwa kinabadilika na kuwa tabia.....Na kikifika level ya kuwa tabia maana yake utakuwa unaifanya automatically bila kutumia nguvu.!!
AMUA KUUNGANA NA WASHINDI KWA KUJIJENGEA TABIA ZA MAFANIKIO!!
3. Maamuzi na Chaguzi Tunazozifanya Kila Siku (Decisions and Choices).
Maamuzi unayoyafanya ndo kitu kinabeba Destiny yako......Unaamua uishi vipi, unaamua kuwa na tabia za aina gani, wewe ndo unaamua kuambatana na watu wa aina gani, wewe ndo unaamua ufuatilie habari za aina gani, wewe ndo unaamua ujaze vitu vya aina gani na taarifa za aina gani kichwani mwako kama ni udaku au skendo za wasanii au movies za kikorea au vitabu na maarifa chanya, Wewe ndo unaamua na kuchagua namna ya kuutumia muda wako na siku yako, wewe ndo unaamua utumiaje pesa unazozipata, wewe ndo unaamua uwe na mahusiano ya aina gani, wewe ndo unaamua uwe mvivu au uwe mtu wa kujituma, wewe ndo unaamua uwe mcha Mungu au mtu dhambi, wewe ndo unaamua kuwa mlevi au la, wewe ndo unaamua na kuchagua uwe kicheche au mwaminifu..... Chaguzi zako na maamuzi unayoyafanya kila siku kwenye vitu mbalimbali kuhusu maisha yako ndivyo vinaamua kama utafanikiwa ama la??!!
Kwenye huu ulimwengu Mungu ametuwekea Uhuru wa kuchagua tunachokitaka na kuamua tunavotaka.....Na bahati nzuri ni kuwa Mungu anatamani kila mtu afanikiwe kwa kiwango cha hali ya juu na ni hasara kubwa sana kwa Mungu kukuona wewe ukiwa failure kwenye maisha yako kwani amekuwekea vitu vingi kwa ajili ya kuwafaa wengine ambavyo ndivyo vingekupa mafanikio makubwa lakini kutokana na uhuru wa kuchagua na kuamua aliotupa wanadamu ndio maana anakuacha uamue wewe Na uchague wewe aina ya maisha unayotaka kuyaishi, Ukichagua kufanikiwa yupo pamoja nawe, ukiamua kufeli anaumia lakini hana namna ya kukulazimisha kufanikiwa.
Maamuzi yoyote na chaguzi ya aina yoyote ile huwa ina kuwa na matokea ndani yake, hivyo kila unapochagua au kuamua kufanya jambo linalokuangamiza na kukudidimiza jua kuwa matokeo yake yatakuwa saw a kabisa na vile ulivoamua au kuchagua..... Kumbuka Bible inavosema " ....Mungu hadhihakiwi, apandacho mtu hakika ndicho avunacho"......Unapofanya maamuzi ya kuvuta sigara jua kuwa matokeo yake ni Kansa ya mapafu, Unapochagua kuwa mzinzi jua kuwa matokeo yake ni HIV/ AIDS, Unapochagua kuwa Mvivu na kujionea huruma na kutoumiza kichwa jua kuwa matokeo yake ni umasikini wa kutupwa.....Lakini pia jua kuwa unapoaamua na kuchagua kujituma, bidii, kumcha Mungu, Uaminifu, maarifa na kutembea na washindi na watu positive jua kuwa matokeo yake ni Mafanikio makubwa.
Maamuzi haya na Chaguzi hizi zinapoendelea kwa muda mrefu huleta matokeo makubwa......Unavoamua na kuchagua leo, kesho na keshokutwa ndivyo vitakavyoleta matokea kuhusu future yako......Ukiamua kama watu waliofanikiwa wanavoamua na kuchagua basi nawe ni lazima utafanikiwa vinginevyo utajiunga na failures.
Dr. Myles Munroe huwa anasema "SUCCESS IS PREDICTABLE".....Unaweza kujua mtu kama atafanikiwa au hatafanikiwa kwa kuangalia kama je anajua anachokitafuta duniani, Tabia zinazoongoza maisha yake (Habits) na Chaguzi zake za Lea na Maamuzi anayoyafanya leo.
JIWEKE KWENYE KUNDI LA WATU AMBAO MAFANIKIO KWAO NI LAZIMA KWA KUTAMBUA ENEO LAKO SAHIHI, KUWA NA TABIA ZA WASHINDI NA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI!!
Live Your Dream!!