Sunday, 10 February 2019

TIBA YA MATATIZO YA MACHO ;KONJACTIVA (CONJUCTIVITS)

*MATATIZO YA MACHO: KONJACTIVA (CONJUCTIVITS):*

Ni maradhi ya macho sehemu ya utando au ute sehemu ya conjuctiva, ambayo inaunganisha sehemu ya ndani ya jicho na kope.

*SABABU:*

Yanaweza kusababishwa na vumbi, moshi, upepo ulio na ubaridi, kuweza kutumia macho kwa muda mrefu kutizama kwa mfano kusoma, kukaa katika mwanga mkali wa jua, upepo wenye ukavu na ujoto wenye hali ya umoto, mvuke, gesi, moto, kemikali, n.k.

*DALILI:*

Kujikuna, kuvimba macho, macho kuwa mekundu, macho kutoa maji au machozi, kuhisi kuna mchanga ndani ya macho, kuogopa mwanga mkali, n.k.

*TIBA:*

Weka macho yawe safi na uyakoshe kwa maji ya baridi. Epusha macho kutokana na joto, baridi, moshi, vumbi, macho yasitumie nguvu sana kama vile kusoma sana.

Tumia dawa za kulainisha choo ikiwa hupati choo vizuri kwa sababu pia huchangia katika maumivu ya kichwa na macho

No comments:

Post a Comment

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO