HAKIKISHA MAPAMBANO YAKO YANAENDANA NA NDOTO YAKO.
Kuna msemo mmoja unasema "The big the dream, the higher the grinding"...... Yaani "Ndoto inapokuwa kubwa basi lazima mapambano yawe makubwa".
Ili malengo yaitwe malengo na ndoto iitwe ndoto ni lazima sifa ya kwanza kabisa malengo au ndoto iwe ni kubwa kuliko level uliyopo sasa na kiwe ni kitu ambacho kita ku-challenge.....Sasa kitu unachotakiwa kukijua ni kuwa kadri unavokuwa na ndoto kubwa au malengo makubwa ndivyo ambavyo mapambano yako ni lazima yawe makubwa zaidi.....Kwa mfano: Mwamafunzi kwenye malengo ya kupata Division One, hawezi kupiga msuli sawa na mwanafunzi mwenye malengo ya kupata Division Three, Mwenye Malengo ya Division One lazima akubali kuumia zaidi ya mwenye malengo ya Division Three....AU, Mtu mwenye ndoto za kuwa Rais ni lazima akubali kuumia sana na zaidi kuliko kijana mwenye malengo ya kuwa Diwani.
Sasa Miongoni mwa swali unalotakiwa kujiuliza mara kwa mara ni hili "JE, MAPAMBANO YANGU YANAENDANA NA NDOTO AU MALENGO YANGU??"........Kama Jibu ni YES basi keep grinding, yaani endelea na Mapambano kwa style hiyohiyo bila kupunguza.....Lakini kama jibu ni NO basi unatakiwa kuongeza Mapambano.
Sasa ili kijiweka kwenye level ya Mapambano kuendana na ndoto au malengo yako basi ni lazima uzingatie na uhakikishe unajifanyia self assessment kwenye maeneo yafuatayo:
Je, Unautumia muda wako sawa na ukubwa wa ndoto yako??
Je, Discipline yako na Commitment na Bidii yako inaendana na ukubwa wa ndoto yako??
Je, Tabia zako za kila zinaendana na ukubwa wa ndoto yako??
Je, Marafiki Unaoambatana wanaendana na ukubwa wa ndoto yako??
Je, kiwango cha Maarifa Uliyonayo sasa yanaendana na ukubwa na ndoto yako na Je, speed yako ya kutafuta Maarifa yakukupeleka kwenye ndoto yako inaendana na ukubwa wa ndoto yako??
Je, Maamuzi unayoyafanya kila siku kwenye maisha yako yanakupeleka kwenye ndoto yako kubwa??
Kimsingi ni kuwa kama una ndoto kubwa lazima na standards zako ziwe kubwa kwenye kila eneo......Eneo muhimu kabisa kupima kiwango cha mapambano yako ni kujiangalia kiwango cha discipline, commitments, hard working yako,marafiki unaoambatana nao, kiwango cha Maarifa Uliyonayo na mambo mengine mengi, kwenye maeneo haya ni lazima uhakikishe standards zako zinakuwa kubwa kama ndoto yako ni kubwa.....Lakini pia ni muhimu ukajua kuwa haya mambo yote kama vile Discipline, Hard working, kiwango cha Maarifa, Marafiki vimejikita kwenye namna unavotumia muda wako...... Kama unatumia muda mwingi Kufanya mambo ambayo hayahusiani na ndoto yako basi jua kuwa mapambano yako hayaendani na ndoto yako, hapa kama kweli upo serious na ndoto yako basi ni lazima ubadili style...... Kumbuka kuwa you are not alone mwenye ndoto kama yako, kuna wengine wana ndoto ya kuwa Rais kama wewe, kuna wengine wana ndoto ya kuwa best singer in Tanzania kama wewe, kuna wengine wana ndoto ya kuwa wanasiasa mashuhuri kama wewe...... Sasa input ndogo unayoiweka usidhanie hata siku moja kama utashindana na mtu ambaye 24/7 anapambana dhidi ya ndoto yake na ameweka standards za hali ya juu kwenye ndoto yake, ambaye muda wote anajifua ili kuwa bora zaidi na kujiweka sehemu nzuri zaidi ya kutimiza ndoto yake......Yaani haijalishi umejaaliwa uwezo au kipaji kikubwa kiasi gani kama wenzako wenye ndoto kama yako wanafanya zaidi ya wewe unavofanya na wanapambana zaidi yako basi jua kuwa utashika mkia na utaishia level za wakaida sana!!
KUMBUKA YOU ARE IN THE RACE....YOU ARE IN THE COMPETITION!! HAUPO PEKEYAKO UNAYEKITAKA HICHO KITU!! RAISE YOUR STANDARDS!!
Live Your Dream!!
No comments:
Post a Comment