WHAT IS YOUR REASONS TO LIVE??.
"Your reasons to live, gives you the reasons to die".......Katika uumbaji wa Mungu kila kitu na kila mtu alimuumba kwa sababu maalum.....Ile sababu ambayo ilimfanya Mungu akuumbe ndiyo inatakiwa iwe sababu yako ya kukufanya uishi na iwe ndo sababu ya kukufanya uwe tayari kufa kwa ajili ya hiyo.
Miongoni mwa kitu kitakachkokufanya ufanikiwe kirahisi kwenye maisha yako ni kuitafuta sababu ya wewe kuishi na ambayo utakuwa tayari kufa kwa ajili ya hiyo pia.
Kila mtu aliyefanikiwa kuipata sababu muhimu ya kumfanya aendelee kuishi na ambayo alikuwa tayari kufa kwa ajili ya hiyo basi alifanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu sana na watu wa aina hii waliacha alama kubwa duniani ambazo zimefanya ulimwengu usiwasahau!!
Martin Luther King Jr aliwahi kusema “If you haven’t found something worth dying for, you aren’t fit to be living.”.....Alimaanisha kuwa "Kama hujapata sababu ambayo uko tayari kufa kwa ajili ya hiyo basi hustahili kuendelea kuishi".
Martin Luther King Jr alishafariki miaka mingi iliyopita lakini bado anaishi kutokana na mambo aliyoyafanya enzi za uhai wake, kutokana na uthamani wa maisha aliyoishi, kutokana na sababu iliyokuwa inamfanya awe tayari kufa. JE SABABU YAKO YA KUISHI NI NINI?? NA JE UPO TAYARI KUFA KWA AJILI YA HIYO??
Inatakiwa ifike hatua uishi ukiwa na STRONG REASON ya kuishi kiasi kwamba hata kama Mungu akiamua kupunguza watu wanaoishi maisha ya ilimradi akiisikia Sababu yako awe na kila sababu za kukuacha uendelee kuishi!! JE, MUNGU AKIAMUA KUWAONDOA WATU WASIO NA SABABU MUHIMU ZA KUISHI, WEWE UTAKUWA KUNDI GANI??
Fid Q kwenye moja kati ya nyimbo zake aliwahi kusema "JE, UNAISHI ILI ULE AU UNAKULA ILI UISHI??".
Kama Unaishi Ili ule, uwe na Magari au na Majumba au tajiri BASI NAKUPA POLE SANA NA NAKUONEA HURUMA SANA KWANI HUJAJUA NI KWA KIASI GANI UNAMHUZUNISHA ALIYEKUUMBA!!
Na kama UNAKULA ILI UISHI, Basi kuna Sentensi mbele unatakiwa kuimalizia " UISHI ILI UFANYE NINI??".....Kama jibu lako linaishia kwenye "KULA ILI UISHI TU" basi hauna utofauti na yule mtu wa kwanza ambaye ANAISHI ILI ALE!!
Ungana na kundi la watu ambao wamejitoa kuifanya dunia kuwa sehemu nzuri kuishi, Ishi kufanya kile Mungu alikuumba kufanya, Ishi kuweka thamani kwenye maisha ya wengine.
Dr. Myles Munroe alikuwa anapenda kusema "DON'T JUST MAKE A LIVING, BUT LIVE TO MAKE A DIFFERENCE"
Ukifika hatua ukapata kitu ambacho utakuwa tayari kufa kwa ajili ya hicho basi jua kuwa itakuwa ndo mwanzo wako wa kufanya mambo ya ajabu duniani na utafanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu and you will be UNSTOPPABLE!!
JE UPO TAYARI KUFA KWA AJILI YA NDOTO YAKO?? Kama Jibu ni HAPANA basi jua kuwa HAUNA PASSION NA NDOTO YAKO NA JUA KUWA HILO ENEO SIYO ENEO LAKO SAHIHI.
"Ndoto ya kweli ni ile ambayo upo tayari kufa kwa ajili ya hiyo".......Maranyingi huwaga nasema " Ili ufanikiwe ni lazima ukubali kuingia kwenye mapambano ya kufa na kupona" Sasa huwezi kufanya mapambano ya kufa na kupona kwenye ndoto yako kama haupo TAYARI KUFA KWA AJILI YA NDOTO YAKO!!
"FIND YOUR REASON TO DIE THAT WILL GIVE YOU THE REASON TO LIVE"
Martin Luther King Jr alipata sababu ya kupinga ubaguzi wa rangi ambayo alikuwa tayari kufa kwa ajili ya hiyo,.... Mwalimu Julius Nyerere alipinga ukoloni na alikuwa tayari kufa kwa ajili ya kupambana dhidi ya ukoloni.....Nelson Mandela alipingana na ukoloni na ubaguzi kiasi kwamba ilimpelekea kukaa jera miaka 27 alikataa kila ofa ya cheo, pesa, magari na kila kitu cha kumfanya ayafurahie maisha, alikubali kuendelea kuteseka kwenye chumba ambacho kilikuwa kifupi kuliko yeye ili tu asimamie Kusudi lake na sababu yake ya kuishi......Mahatma Gandhi aliwaambia Wakoloni wakizungu kuwa hatakula chakula wala kunywa maji mpaka afe kama hawatawaachia wananchi wake, WHAT A SPIRIT??
Unaikumbuka Sababu iliyompleta YESU duniani?? Na Je, Unakumbuka Sababu iliyomfanya auawe??
TAFUTA SABABU YAKO YA KUISHI!!
Live Your Dream!!
No comments:
Post a Comment