KASHATA ZA MAYAI
Mahitaji:
1. Sukari nusu kg,
2. Samli (aseel ) nusu kg,
3. Mayai 15 mpaka 16,
4. Maziwa mazito ya sona,
5. Iliki kijiko kimoja cha chai,
6. Arki ya vanilla Na rose kijiko kimoja chai.
Namna ya kupika:
Yeyusha samli yako iwe liquid, iache ipoe kdg isiwe moto sana. Then kwenye bakuli safi weka samli yako, sukari Na mayai yako. Piga au changanya kwa mchapo mpaka vichanganyike vizuri. Then minina mchanganyiko wako kwenye sufuria ya kiasi ambayo haitokupa tabu kukoroga then weka kwenye jiko lako kwa ajili ya kuanza mapishi. Moto usiwe mkali sana wala mdogo sana.
Anza kukoroga kwa mwiko usiachie mkono ili isigande kwenye sufuria au kuungua kabla kuwiva.
Endelea kukoroga itaanza kuwa nzito kama crumble eggs, Endelea kukoroga itaanza kubadilika rangi taratibu from white to brown light. Ikianza kuwa brown light weka iliki Na arki zako huku bado unaendelea kukoroga.
Ikianza kukoza brown minina maziwa ya sona kiasi nusu kikopo. Then koroga koroga kdg tu kiasi maziwa yachanganyike then epua.
NB: maziwa ya sona unaweka karibia kuepua)
Vile vile usiache kuwa brown dark itakuwa haina test nzuri.
Tunaendelea: ukisha epua sufuria mimina mchanganyiko wako kwenye sinia ya kiasi yenye nafasi nzuri. Unapomimina, mimina upande mmoja kwa sababu samli huwa inabaki nyingi so utapata kuinua sinia yako upande Na kuitoa samli yote. Ukiacha sinia ikalala Kashata zako zitakua Na samli nyingi Na zitakuwa Si nzuri. Kata kata kashata zako vi square wakati bado haijapoa.
Iegemeze sinia yako sehemu ili samli itiririke upande mmoja Upate uitoe kwa kijiko.
Ukisha hakikisha samli haiteremki tena laza sinia yako usubiri kashata zigande. Inachukua masaa kadhaa kuganda so make sure huzibandui kashata mpaka zigande vizuri.
Zikisha kuganda vizuri bandua uweke kwenye bakuli zipate kuhifadhika vizuri. Kashata zako tayari, Ni nzuri kula kwa gahwa.
No comments:
Post a Comment