Tuesday, 19 March 2019

JUICE YA TANGO

🥒🥒JUICE YA TANGO🥒🥒

🥒Mahitaji:-
Matango 2
juice ya ndimu/limao 1/4 litre
sukari kadiria
Maji 1/2 litre

🥒🥒changanya vitu vyote then usage ukipenda unaweza kuchuja. au ukainywa hivyo hivyo.

🥒🥒juice hii inaondoa kitambi, mafuta mabaya.
inasafisha kibofu, pressure n.k
   enjoy

*AINA ZA NGOZI NA JINSI YA KUZITUNZA*

*1⃣ NGOZI YA KAWAIDA*

Kama ngozi yako si ya mafuta wala si kavu,iko nyororo,vitundu vyake viko kawaida,haina harara wala misukosuko yoyote,basi ngozi yako ni ya kawaida  yaani normal skin

➡Na kwa sababu hiyo bidhaa unazopaswa kutumia ni za kutunza tu ngozi kuipa unyevunyevu na kuzuia isiharibiwe na jua.

*2⃣ NGOZI YA MAFUTA*

Kama ngozi yako ina ng'aa kila wakati,unapata chunusi,madoa,matundu yake ni makubwa yanaonekana wewe ngozi yako ni ya Mafuta   yaani oily skin

Bidhaa unazopaswa kutumia ni zile za kubalance mafuta,kuzuia chunusi,kuondoa madoa lakini ni lazima bidhaa hizi ziwe hazikukaushi mafuta

Si kweli kwamba ukiwa na uso wa mafuta ni vibaya na kwamba mafuta hayatakiwa usoni mafuta ni muhimu lakini yana kiasi chake

*3⃣ NGOZI KAVU*

Huwezi toka bila kupaka mafuta,unapauka yaniuso unakuwa na mabaka mabaka,ngozi inafifia,haing'ai basi ukiona hivi ujue ngozi yako ni Kavu yaani Dry skin

Mtu wa ngozi kavu anahitaji bidhaa za kurudishia ngozi yake unyevunyevu

Lakini muhimu sana sana kuilinda isiharibiwe na jua kwa kutumia cream maalum za kuzuia ngozi isiungue.

*4 NGOZI NYETI*

Kama ukipaka kitu chochote usoni unapata irritation,au ngozi yako huwa inawasha,wakati mwingine unaona wekundu kama kuungua basi wewe ngozi yako ni sensitive

Mtu mwenye ngozi hii anapaswa kuwa makini sana na aina ya bidhaa anazotumia

Usipende kubadili badili bidhaa, epuka kutumia bidhaa zenye chemikali na ni vizuri ukapata ushauri kwa mtaalam wa maswala ya ngozi kwanza.

*5 NGOZI MCHANGANYIKO*

Kuna watu ambao baadhi tu ya sehemu usoni ndipo anakuwa na mafuta,sehemu zingine mkavu,anapata pia chunusi japo si nyingi na ni sehemu zile zenye mafuta.

Tunaweza sema sehemu zile zenye mafuta uso unakuwa na tabia za ngozi ya mafuta wakati seheme zenye ukavu zinakuwa na tabia za ngozi kavu

Mtu huyu ngozi yake ni mchanganyiko au Combination Skin

NJIA ASILI ZA KUONDOA WEUSI KWAPANI NA MAPAJANI

➿➿➿➿➿➿➿➿➿➿



*🍇Njia asili za kuondoa weusi kwapani na mapajani🍇*

🍇Msuguano kati ya sehemu mbili kwa muda mrefu, unene kupita kiasi, matumizi ya deodorant, spray, matumizi ya dawa za kunyolea, matumizi ya vipodozi vikali na ugonjwa wa kisukari ni baadhi ya visababishi kwa maeneo kadhaa ya mwili kupata weusi hasa katika mapaja na kwapa.

🍇hii ni kwa wanaume na wanawake kwasababu matumizi ya vitu hivyo huchangia seli kufa kwa kiasi kikubwa na kutengeneza weusi.

🍇Ifahamike kwamba weusi mapajani au makwapani sio ugonjwa bali ni mabadiliko tu ya ngozi ambayo huwapata wengi na kuwafanya wasiwe na raha pindi wawapo na waume zao

🍇Zifuatazo ni baadhi ya njia za asili ambazo mhanga wa tatizo hili anaweza kuzitumia kuondokana nalo ambalo limekuwa changamoto kwa watu wengi

🍇2.Njia nyingine ni matumizi ya mafuta ya nazi, mafuta haya ni tib anzuri sana kutokana na uwepo wa vitamini E yansaidia kusafisha na Kung’arisha ngozi.

🍇Unachotakiwa kufanya ni kupaa mafuta hayo sehemu ya mwili iliyoathirikana weusi kwa muda wa dakika 10 hadi 20 kisha osha eneo hili kwa maji ya vuguvugu, fanya hivyo kila siku mpaka utapoona mabadiliko.

🍇3.Matumizi ya Tango pia ni muhimu kwa kusaidia kuondoa weusi sehemu za mapajani na kwapani.

🍇Unachotakiwa kufanya, kata vipande kadhaa vya tango jipake kwapani na mapajani au lisage kisha paka ukishapaka kaa kwa muda wa dakika 10 hadi 20.

🍇4.Majani ya Aloevera, chukua utomvu wa jani la Aloevera, Paka kwenye sehemu yenye weusi na kisha acha ule utomvu kwa muda takribani nusu nasaa kisha osha na maji ya uvugu vugu,  Fanya hivi mara moja hadi mbili kwa siku ili kuweza kupata matokeo haraka.

🍇5.Viazi ulaya/mbatata

menya viazi kata vipande jipake makwapani yale maji yake yakiingia kwenye ngozi yanatoa rangi nyeusi au unaweza kuponda kikiwa kibichi na kujipaka kwa dk 10-20 utanawa utafanya hivyo mara 2 kwa siku mpaka weusi utakapoisha

🍇6.Sukari -chukua brown sugar changanya na olive oil paka  badaa ya mda osha

🍇7.Baking soda-inasaidia kutoa dead cells kwa urahisi .

changanya baking soda na maji iwe nzito nzito paka kwapani acha kwa dk 10 osha na jikaushe fanya hivyo mar 2-3 kwa wiki ,endelea na zoezi mpaka utakaopona umeridhika na mabadiliko

🍇Zoezi hili linaweza chukua mda mchache ukaona mabadiliko makubwa au ikachukua mda mrefu kuona  mabadiliko inategemea kila mtu na ngozi yake .

🍇Zingatia kutumia dodoki la kuogea usugulie sehemu hizo husika na hakikisha hukai na nywele ndefu.

🍇Tumia hand shaver isiwe kiwembe, na iwapo umetumia njia hizi kwa miezi 1-2 na hakuna mabadiliko mwone daktari.

🍇Kuna baadhi ya creams au deudorants nazo zinasaidia kutoa weusi.

*Tutaishia hapa, ni matumaini yangu mmenufaika*

➿➿➿➿➿➿➿➿➿➿

Monday, 18 March 2019

MBAAZI ZA NAZI

MBAAZI ZA NAZI

Mbaazi kavu nusu kg
Kitunguu maji 1 kikubwa
Tomato fresh 1 kubwa au 2 za kiasi
Pilipili boga/cupsicum kiasi
Bizari nyembamb/cumin powder 1 tablespoon
Pilipili manga /black pepper 1 teaspoon
Kitunguu saum/garlic 1 tablespoon
Tangawizi mbichi 1 teaspoon
Chumvi
Vegetable maggi /kidonge cha supu 1 (sio lazima)
Tui la maji vikombe 5 (3 tui jepesi na 2 tui zito )
Bizari ya mchuzi/tumeric kiasi
Chemsha mbaazi kwa maji mpaka ziwive, zikauke maji au zibaki na maji kidogo sana, kata kata kitungu, tomato, pilipili boga ndogo ndogo na uweke kwenye sufuria ya mbaazi, add na vitu vyote vilobaki isipokua tui/nazi,
tia nazi/tui jepesi na uwache zichemke, tui jepesi litaivisha vitu vyote, vikishawiva na tui limekaribia kukauka, tia tui zito, funika wacha zichemke mpaka iwe size unayotaka, angalia chumvi na spices kama ziko epua na ENJOY kwa mikate maandazi au wali, zangu mm mekula na 

Bamia robo kg
Kitunguu maji 1 kikubwa
Kitunguu saum kijiko 1 cha chakula
Tangawizi mbichi kijiko 1 cha chai
Chumvi kiasi
Bizari nyembamba /cumin powder 1 tsp
Mafuta ya kupikia 3 tbsp
Pilipili manga kiasi
Tui/Nazi ya maji kikombe 1

Kosha bamia zikate kate ndogo ndogo, kata kata Kitunguu maji, changanya na bamia zisage, kama unatumia blender tia na tui la maji  nusu kikombe, saga pamoja mpaka zinakua laini kiasi, zitoe

Weka sufuria kwenye moto, tia mafuta ya kupikia, tia kitunguu saum, tangawizi, bizari nyembamba na pilipili manga, wacha zipate moto kidogo, tia ile bamia uliyoisaga na kitunguu, ipike kwa dakika 5 malizia tui nusu kikombe tia chumvi , wacha lichemke mpaka iwive pamoja na kitunguu,

Kama uliposaga ulitia tui ni sawa, kama uliposaga hukutia tui , vile linachemka litie tui lote kikombe 1,  wacha lichemke mpaka liwe zito na kila kitu kiwe kimewiva, unaweza kuweka pilipili ya kuwasha ukipenda.

PILAU YA SAUCE YA SOYA NA MBOGA

PILAU YA SAUCE YA SOYA NA MBOGA

VIPIMO

Kuku (mkate mkate vipande) 1

Mchele wa Basmati (rowanisha) magi 3

Mdalasini  mchi 1                     

Vitunguu maji (vilivyokatwa vyembamba) 6

Mchanganyiko wa mboga za barafu (karoti, mahindi, njegere) - Magi 1

Kabichi (iliyokatwa katwa nyembamba) magi 1

Pilipili mbichi (iliyosagwa) 3

Pilipili boga iliyokatwa vipande vidogo vidogo 1

Pilipili manga kijiko cha chakula 1

Chumvi kijiko cha chakula 1

Sosi ya soya (soy sauce) vijiko vya chakula 5

Kotmiri iliyokatwa katwa magi 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa vijiko vya chakula 2

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1.  Tia mafuta ndani ya karai. Yakipata moto kiasi, mimina vitunguu maji na mdalasini 1 mzima kaanga. Itachukua muda kidogo. Kaanga mpaka viwe rangi ya hudhurungi (brown). Viepue na uweke kando.

2.  Ndani ya sufuria kubwa, mimina kuku, chumvi, thomu na tangawizi, sosi ya soya, pilipili manga, pilipili mbichi, chemsha mpaka kuku awive na maji yakauke.

3.  Changanya vitunguu  ulivyokaanga, kabichi, pilipili, mboga, kotmiri, mchanganyiko wa mboga za barafu na weka kwa muda wa dakika tano au kumi. Tia na mafuta kidogo uliyokaangia vitunguu .

4.  Chemsha mchele na chumvi uwive kama kawaida ya kupika wali wa kuchuja. Ukishauchuja umwagie katika masala ya kuku.

5.  Nyunyizia mafuta kidogo uliokaangia vitunguu.

6.  Weka moto mdogo mpaka wali ukishawiva.  Uchanganye ukiwa tayari kwa kuliwa.

KIDOKEZO:

Unaweza kuupika wali huo ndani ya jiko, yaani badala ya kutia masala kwenye sufuria ukayatia katika bakuli au treya ya jiko (oven), kisha ukamwagia wali uliouchuja humo na kuupika kaitka moto wa 400-450 Deg kwa muda wa dakika 15-20.

Enjoy!

COCONUT HALWA / HALUA YA NAZI

COCONUT HALWA / HALUA YA NAZI :

Mahitaji:

Tui zito –kikombe  1+1/4
Maziwa – 2/3 kikombe
Sukari – 2/3 kikombe
Nazi ilokunwa  – 1/4 kikombe
Siagi isokuwa na chumvi – vjk 2 vya kula
Lozi na Pistachios – kiganja kwajili ya kupambia

Maelekezo:

1. Bandika sufuria jikoni moto wa kiasi.
2. Tia tui zito na maziwa.
3. Acha ichemke.
4. Tia sukari na nazi ilokunwa.
5. Koroga hadi ishikane.
6. Tia siagi, koroga kisha epua.
7. Tandaza kwenye sahani ilopakwa mafuta ipate kupoa.
8. Mwagilia lozi na pistachios ukipenda.
9. Kabla haijapoa kabisa kata vipande.
10. Andaa.

Thursday, 14 March 2019

UTENGENEZAJI WA MISHUMAA YA KUUA MBU

*UTENGENEZAJI WA MISHUMAA YA KUUA MBU*

*MALIGHAFI*
1.PARAFFIN WAX
2.STERINE
3.BORIC ASID
4.MOULD(MAUMBO)
5.UZI (UTAMBI)
6.RANGI KAMA UKIPENDA
7.JIKO
8.SUFURIA

*MAANDALIZI*
andaa maumbo ya mshumaa kwa Jinsi unavopenda unaweza kutumia bati

andaa utambi kwa kuchukua boric asid vijiko vitano vya chakula changanya Na maji vijiko vinne vya chakula ,koroga kwa muda wa dakika tano, KISHA toa Na ANDIKA ili ukauke,sababu ya kufanya hivi ili utambi usiishe haraka wala kutoa moshi. Na hii ndio Kazi kubwa ya boric asid

*UANDAAJI WA MSHUMAA*

baadavya kuwa umeandaa maumbo Yako ya mshumaa chukua utambi wako Na uweke katikati ya mould Yako KISHA funga utambi wako juu ya chombo chako kwa kushikiza Na kijiti .kijiti kitakusaidia ili utambi usikae pembeni

Washa jiko Lako Na weka sufuria Yako jikoni chukua paraffin wax kilo moja ,sterine vijiko vinne,rangi kijiko kimoja cha chai, perfume kama ukipenda kijiko kimoja cha chai

wakati mchanganyiko wako unayeyuka koroga taratibu mpaka uchanganyike vizuri

Epua mchanganyiko wako Na anza kuweka kwenye maumbo Yako uliyoandaa kwa kuweka utambi ndani yake

weka sehemu ya kivuli ili mshumaa wako upate kuganda kwa urahisi ukisha ganda utoe taratibu kutoka katika hayo maumbo yake *BAADA YA HAPO MSHUMAA UTAKUWA TAYARI KWA MAUZO NA MATUMIZI YA NYUMBANI*

*NB:* SIMPRONELLA/CITRONELLA hii ni perfume Na pia ni dawa ya kuua mbu ko kama ukipenda mshumaa wa kuua mbu basi sehemu ya kuweka perfume weka aina hii

Saturday, 9 March 2019

UJASIRIAMALI* YATAKAYOKUWEZESHA KUJIAJIRI MWENYEWE NA KUTIMIZA NDOTO ZAKO.                                              *Masomo 80

*UJASIRIAMALI* YATAKAYOKUWEZESHA KUJIAJIRI MWENYEWE NA KUTIMIZA NDOTO ZAKO.
                                             *Masomo 80
1:SABUNI YA MAJI NZITO(AINA NNE)
2:SABUNI YA MKAA- CHUNUSI.
3:SABUNI YA MCHELE - USOFT
4:SABUNI YA NYANYA.
5:SABUNI YA MAZIWA & ASALI.
6:SABUNI YA KIAZI- MAKOVU.
7: *JIKI.*
8:SHAMPOO.
9:LEMON SOAP.
10:MANJANO SOAP.
11:MISHUMAA/CANDLES.
12: *CHAKI/CHALKS.*
13:SABUNI YA MCHE/LAUNDRY BAR SOAP.
14: *SABUNI YA MAGADI.*
15:SABUNI YA MLONGE.
16:SABUNI YA TANGO.
17:SABUNI YA ALOVERA.
18:SABUNI YA MAJIVU.
19:SABUNI YA UKWAJU
20:SABUNI YA PAPAI.
21:SABUNI YA SULFUR/ NGOZI YA MAFUTA NA CHUNUSI.
22:TILES) SINK CLEANER.
23:SABUNI YA MWAROBAINI.
24:SABUNI YA KUNAWIA MIKONO.
25:MAZULIA/CARPETS.
26:SHAMPOO YA ALOVERA.
27:SHAMPOO YA TANGO.
28:SABUNI YA TANGAWIZI.
29:SABUNI YA  MAWESE NA ASALI.
30:SABUNI YA  CHUNGWA.
31:MITO/PILLOWS.
32:BATIKI TIE & DIE  TONE LA MAJI.
33:BATIKI YA MUHURI.
34:MASHUKA/BEDSHEETS.
35:BATIKI TIE & DIE  CRANCKE. PARTERN.
36:BATIKI YA CHAPA{printing}
37:BATIKI YA KUCHUBUA{Bleach.}
38: *VIATU*
39:BATIKI PUBBLE PRISM.
40:BATIKI TIE & DIE NYOTA.
41:BATIKI TIE & DIE UPINDE  WA MVUA.
42:BATIKI TIE & DIE  DOUBLE SPYRAL.
43:BATIKI ZA MSHUMAA.
44: *MIKOBA/HANDBAGS*
45:MAZIWA YA SOYA.
46:SOYA MASALA.
47:SIAGI YA KARANGA.
48:MAZULIA/CARPETS.
49:CRIPS ZA VIAZI.
50:JUISI YA DUKANI.
51:KARANGA ZA MAYAI.
52:TOMATO SAUCE.
53:CHILI SAUCE.
54:UBUYU WA VIMTO.
55:UFUTA
56:KASHATA ZA KARANGA.
57:ICE CREAM ZA UBUYU.
58:MKAA.
59:UNGA WA LISHE.
60:VIBANIO VYA MAPAZIA.                                                                                                                                                 61: *KEKI NA UPAMBAJI WAKE.*
62:MAFUTA YA KAROTI.
62:AIR FRESHENER.
63:DAWA YA KUUA WADUDU.
64:ICE CREAM YA MAZIWA.
65:LEMON ICE CREAM.
66:BISKUTI.
67:FUDGE AINA ZOTE.
68: *UPAMBAJI WAKUMBI ZA SHEREHE.*
69: MAFUTA YA MNYONYO{Castor oil}
70: *ANTI AGING LOTION*
71:HAND WASHING GEL.
72:MAFUTA YA NAZI.
MAFUTA YA MGANDO.
73:MAFUTA YA NGOZI{MAKUNYANZI}
74:JUISI ZA MATUNDA.
75:SABUNI YA
78: *LEMON OIL.*
79:ALOE VERA GEL.
80:SABUNI YA UNGA

Tuesday, 5 March 2019

JINSI YA KUTENGENEZA MASK KWA AJILI YA NGOZI ZA AINA ZOTE

*JINSI YA KUTENGENEZA MASK KWA AJILI YA NGOZI ZA AINA ZOTE*

*NGOZI YENYE CHUNUSI*

*Mahitaji*

🍇Kungumanga🌰
🍇Asali🍯
🍇Maziwa 🥛

*Jinsi ya kufanya*

Changanya mahitaji yote kwenye bakuli safi mpaka uhakikishe umepata mchanganyiko mzuri

Safisha uso kisha paka na ukae nayo kwa muda wa nusu saa kisha osha vizuri na maji ya uvugu kisha malizia na maji baridi

Futa na taulo laini uso wako kisha jipe unyevu kama kawaida

*NGOZI YA MAFUTA*

*Mahitaji*

🍇Unga wa ngano🍚
🍇Mtindi 🥛
🍇Manjano

*Jinsi ya kufanya*

Changanya mahitaji yote mpaka uhakikishe imechanganyika vizuri

Safisha uso kisha paka paste yako na uiache kwa muda wa nusu saa kisha osha kwa maji ya uvugu ukifuatisha na maji baridi

Futa uso kwa taulo safi kisha paka moisturizer kama kawaida

*NGOZI YENYE MIKUNJO*

*Mahitaji*

🍇Aloe vera gel🌿
🍇Asali 🍯
🍇Mafuta ya nazi

*JINSI YA KUFANYA*

Changanya mahitaji yote mpaka uhakikishe imechanganyika vizuri

Safisha uso kisha paka paste yako na uiache kwa muda wa nusu saa kisha osha kwa maji ya uvugu ukifuatisha na maji baridi

Futa uso kwa taulo safi kisha paka moisturizer kama kawaida

*NGOZI KAVU*

*Mahitaji*

🍇Ndizi mbivu🍌
🍇Asali🍯

*JINSI YA KUFANYA*

Changanya mahitaji yote mpaka uhakikishe imechanganyika vizuri

Safisha uso kisha paka paste yako na uiache kwa muda wa nusu saa kisha osha kwa maji ya uvugu ukifuatisha na maji baridi

Futa uso kwa taulo safi kisha paka moisturizer kama kawaida

JINSI YA KUTENGENEZA COFFEE SCRUB

*JINSI YA KUTENGENEZA COFFEE SCRUB*

*Mahitaji*

🍇¼ kikombe ya kahawa iliyosagwa

🍇½ kikombe ya mafuta ya nazi/olive oil extra virgin

🍇2 Tbs ya mdalasini wa unga au manjano

*JINSI YA KUFANYA*

Changanya mahitaji yote kwenye bakuli safi.

Osha mwili wako kwanza ili kuondoa uchafu kwenye ngozi kisha jikaushe na taulo

Sugua ukitumia scrub yako kwa kufuata mduara

Iache kwa dakika 15 kisha osha vizuri

Kama una sensitive skin hakikisha unasugua taratibu sana

Coffe ni kama exfoliator ambayo inasaidia kuondoa dead cells na itaiacha ngozi yako ikiwa laini ya kupendeza...

Mafuta ya nazi /olive yataipa unyevu ngozi yako na kuiacha ikiwa na afya na yenye mng'ao

Manjano na mdalasini vitaondoa bacteria wanaosababisha chunusi na kuiacha ngozi yako na ikipendeza zaid

JINSI YA KUTENGENEZA LOTION ASILIA KWA NGOZI NYORORO YENYE MNG'AO (NATURAL)

*JINSI YA KUTENGENEZA LOTION ASILIA KWA NGOZI NYORORO YENYE MNG'AO  (NATURAL)*

*Chagua moja kati ya lotion zifuatazo*

*Mahitaji*

🍇Vitamin c powder/unga1 Tbs

🍇Vitamin e Capsule/oil matone 5

🍇Rose water 1Tbs🌹

🍇Glycerin 1 Tsp

🍇Shea butter au Vaseline lotion/Lotion yoyote uipendayo 100ml

*Jinsi ya kufanya*

Tia rose water kwenye bakuli safi kisha tia kijiko kimoja cha unga wa vitamin C

Changanya vizuri na ukoroge kwa muda wa dakika 5 mpk vitamin c iyeyuke kabisa kisha ongezea glycerin na vitamin e na uchanganye vizuri

Tia lotion yako ya vaseline ujazo wa ml 100 ama shea butter ama cream yoyote uipendayo mwenyewe kisha changanya vizuri hadi ichanganyike

Weka kwenye chupa safi tayari kwa matumizi

Hii itafanya ngozi yako kua laini na kuondoa ukavu wa ngozi pamoja na kuiacha ikipendeza zaidi na zaidi

Unaweza kupaka kwenye mwili hata usoni na ni salama kabisa haina sumu

Lotion ya pili

*Mahitaji*

🍇Mafuta ya nazi
🍇Aloe Vera gel
🍇Rose water
🍇Glycerin
🍇Vitamin e Capsule/oil

*Jinsi ya kufanya*

Weka kwenye bakuli safi kijiko kimoja cha chakula cha aloe vera gel (ya dukani iwe 100% natural)

Ongeza kijiko kimoja cha chakula cha mafuta ya nazi pamoja na glycerin na rose water kisha ongezea na vitamin e kama ngozi yako ya mafuta tumia capsule kama kavu unaweza kutumia vitamin e oil

Changanya vizuri mpaka ichanganyike na uone imekua na rangi ya kupendeza na ipo laini kisha hifadhi kwenye kichupa safi tayari kwa matumizi

DAWA YA KUKUZA NA KUNYOOSHA NYWELE,KUONDOA WEUSI MAKAPANI,VIDOLENI,MAGOTI

Utengenezaji  dawa ya kukuza nywele/kuondoa michirizi kwapani,vidole,magoti,kunyoosha nywele

      Mahitaji

1*mafuta ya mzaituni

2*mdalasini ya unga

3*asali

Uandaaji

Andaa sefuria jikon na acha ipate moto

Baada ya kupata moto weka mafuta ya mzaituni nusu Lita acha yachemke (kupata moto )

Baada ya kupata moto weka mdalasini kijae kikombe kimoja cha chupa ya chai acha jikon ukiwa unakoroga

Koroga hadi kuona inaacha kuchemka yani kupata moto sana maana haichemki kama mboga😁

Acha usikoroge na kusubiri hadi ibadirike rangi na kua kahawia nyeusi ipua na subiri kupoa

Baada ya kupoa weka asali vijiko 10 vya chakula kisha koroga tena

Baada ya kuweka asali na kukoroga mafuta yapo tayar kwa matumizi

Matumizi

Paka kichwa kuanzia kwenye ngoz ya kichwa (utosi) hadi juu ya nywele

Nb isikae kichwani zaidi ya robo Saa (dakika 15 )

🍉🍅na kuondoa weusi makwapani,vidoleni na magotini🍒
changanya mchuzi wa limao au ndimu ,na asali au sukari alafu jisugue sehemu husika kila siku kabla ya kuoga.baada ya kujisugua kaa dkk 10 then nawa au oga kama kawaida

♥DAWA YA MICHILIZI
🌷🌷@umbo_la_asili
Mahitaji⤵
🔹limao 1
🔹olive oil vijiko 5
🔹kahawa vijiko 4
🔹sukari vijiko 2

♥♥NJIA♥♥♥
Weka kahawa ktk bakuri ongeza mafuta ya olive oil  vijiko 5 pamoja na sukari vijiko 2
Koroga ongeza na limao ktk mchanganyiko
Paka sehemu za michirizi km unasugua.fanya hiv kwa mda km dkk mbili.acha kusugua kaa kidogo km dkk 20
Baada ya hapo kaoge kisha paka mafuta ya nazi hasa mafuta ya naz ya minara.🌷🌷🌷🌷🌷♥♥♥♥♥♥♥
@umbo_la_asili

KUNYONYOKA KWA  NYWELE
wale walio na tatizo la kunyonyoka kwa nywele,wanaweza kupaka kichwani uji wenye mchanganyiko wa mafuta ya mzeituni yaani olive oil,asali kijiko kimoja cha chakula,mdalsini kijiko kimoja cha chai kabla ya kuoga na kuuacha kichwani kwa muda wa dk 15 na kisha kuosha kichwa.hii husaidia kurudisha nywele

Thursday, 28 February 2019

JINSI YA KUTENGENEZA PIPI TOFI (TOFFEE)

*JINSI YA KUTENGENEZA PIPI TOFI (TOFFEE)*

1/2 kikombe unsalted butter- siagi (ambayo haina chumvi)
1 kikombe sukari
1/2 kijiko cha chai Chumvi
1/4 Kikombe maji au maziwa
1 kijiko cha chakula vanilla au radha yoyote ile
100g Cooking Chocolate (sio lazima)

Zabibu zilizokaushwa, vipande vya Lozi, korosho au karanga

Namna:

Paka siagi sinia yako weka pembeni.
Ktk sufuri weka sukari, siagi, chumvi na maji-maziwa. Chemsha kwa moto mdogo kwa dakika 8 (angalia usiunguze), huku unakoroga utaona inaaza kubadilika rangi kuwa kahawia. Hakikisha mchanganyiko wako unaaza kuwa mzito sana. Weka lozi au karanga ktk mchanganyiko wako koroga.

Yeyusha cooking chocolate kwa mvuke au microwave weka pembeni.

Mwagia tofi ktk sinia ulikwisha tayarisha, tandaza acha ipoe kidogo. Halafu mwagia ila cooking chocolate juu ya tofi acha ipoa kiasi, kata tofi ktk vipande. Tayari kuliwa.

Kikombe kilichotumika ni ´measuring cups´.

Wednesday, 27 February 2019

DAWA YA KUONDOA MICHIRIZI YA UNENE AU MISTARI YA UZAZI

Dawa ya kuondoa michirizi ya unene au mistari ya uzazi

Mahitaji

1*magadi soda

2*limao

   Matumizi

Anda bakuli la kawaida kisha weka magadi soda vijiko 2

Baada ya hapo kata limao utoe vipande 2 kisha chukua kipande kimoja chovya katika bakuli la magadi soda na usugue sehem ya mistari

Tumia hadi kupata matokeo

Monday, 25 February 2019

WHAT IS YOUR REASONS TO LIVE??.

WHAT IS YOUR REASONS TO LIVE??.

"Your reasons to live, gives you the reasons to die".......Katika uumbaji wa Mungu kila kitu na kila mtu alimuumba kwa sababu maalum.....Ile sababu ambayo ilimfanya Mungu akuumbe ndiyo inatakiwa iwe sababu yako ya kukufanya uishi na iwe ndo sababu ya kukufanya uwe tayari kufa kwa ajili ya hiyo.

Miongoni mwa kitu kitakachkokufanya ufanikiwe kirahisi kwenye maisha yako ni kuitafuta sababu ya wewe kuishi na ambayo utakuwa tayari kufa kwa ajili ya hiyo pia.

Kila mtu aliyefanikiwa kuipata sababu muhimu ya kumfanya aendelee kuishi na ambayo alikuwa tayari kufa kwa ajili ya hiyo basi alifanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu sana na watu wa aina hii waliacha alama kubwa duniani ambazo zimefanya ulimwengu usiwasahau!!

Martin Luther King Jr aliwahi kusema “If you haven’t found something worth dying for, you aren’t fit to be living.”.....Alimaanisha kuwa "Kama hujapata sababu ambayo uko tayari kufa kwa ajili ya hiyo basi hustahili kuendelea kuishi".

Martin Luther King Jr alishafariki miaka mingi iliyopita lakini bado anaishi kutokana na mambo aliyoyafanya enzi za uhai wake, kutokana na uthamani wa maisha aliyoishi, kutokana na sababu iliyokuwa inamfanya awe tayari kufa. JE SABABU YAKO YA KUISHI NI NINI?? NA JE UPO TAYARI KUFA KWA AJILI YA HIYO??

Inatakiwa ifike hatua uishi ukiwa na STRONG REASON ya kuishi kiasi kwamba hata kama Mungu akiamua kupunguza watu wanaoishi maisha ya ilimradi akiisikia Sababu yako awe na kila sababu za kukuacha uendelee kuishi!! JE, MUNGU AKIAMUA KUWAONDOA WATU WASIO NA SABABU MUHIMU ZA KUISHI, WEWE UTAKUWA KUNDI GANI??

Fid Q kwenye moja kati ya nyimbo zake aliwahi kusema "JE, UNAISHI ILI ULE AU UNAKULA ILI UISHI??".

Kama Unaishi Ili ule, uwe na Magari au na Majumba au tajiri BASI NAKUPA POLE SANA NA NAKUONEA HURUMA SANA KWANI HUJAJUA NI KWA KIASI GANI UNAMHUZUNISHA ALIYEKUUMBA!!

Na kama UNAKULA ILI UISHI, Basi kuna Sentensi mbele unatakiwa kuimalizia " UISHI ILI UFANYE NINI??".....Kama jibu lako linaishia kwenye "KULA ILI UISHI TU" basi hauna utofauti na yule mtu wa kwanza ambaye ANAISHI ILI ALE!!

Ungana na kundi la watu ambao wamejitoa kuifanya dunia kuwa sehemu nzuri kuishi, Ishi kufanya kile Mungu alikuumba kufanya, Ishi kuweka thamani kwenye maisha ya wengine.

Dr. Myles Munroe alikuwa anapenda kusema "DON'T JUST MAKE A LIVING, BUT LIVE TO MAKE A DIFFERENCE"

Ukifika hatua ukapata kitu ambacho utakuwa tayari kufa kwa ajili ya hicho basi jua kuwa itakuwa ndo mwanzo wako wa kufanya mambo ya ajabu duniani na utafanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu and you will be UNSTOPPABLE!!

JE UPO TAYARI KUFA KWA AJILI YA NDOTO YAKO?? Kama Jibu ni HAPANA basi jua kuwa HAUNA PASSION NA NDOTO YAKO NA JUA KUWA HILO ENEO SIYO ENEO LAKO SAHIHI.
"Ndoto ya kweli ni ile ambayo upo tayari kufa kwa ajili ya hiyo".......Maranyingi huwaga nasema " Ili ufanikiwe ni lazima ukubali kuingia kwenye mapambano ya kufa na kupona" Sasa huwezi kufanya mapambano ya kufa na kupona kwenye ndoto yako kama haupo TAYARI KUFA KWA AJILI YA NDOTO YAKO!!

"FIND YOUR REASON TO DIE THAT WILL GIVE YOU THE REASON TO LIVE"
Martin Luther King Jr alipata sababu ya kupinga ubaguzi wa rangi   ambayo alikuwa tayari kufa kwa ajili ya hiyo,.... Mwalimu Julius Nyerere alipinga ukoloni na alikuwa tayari kufa kwa ajili ya kupambana dhidi ya ukoloni.....Nelson Mandela alipingana na ukoloni na ubaguzi kiasi kwamba ilimpelekea kukaa jera miaka 27 alikataa kila ofa ya cheo, pesa, magari na kila kitu cha kumfanya ayafurahie maisha, alikubali kuendelea kuteseka kwenye chumba ambacho kilikuwa kifupi kuliko yeye ili tu asimamie Kusudi lake na sababu yake ya kuishi......Mahatma Gandhi aliwaambia Wakoloni wakizungu kuwa hatakula chakula wala kunywa maji mpaka afe kama hawatawaachia wananchi wake, WHAT A SPIRIT??

Unaikumbuka Sababu iliyompleta YESU duniani?? Na Je, Unakumbuka Sababu iliyomfanya auawe??
TAFUTA SABABU YAKO YA KUISHI!!

Live Your Dream!!

HAKIKISHA MAPAMBANO YAKO YANAENDANA NA NDOTO YAKO

HAKIKISHA MAPAMBANO YAKO YANAENDANA NA NDOTO YAKO.

Kuna msemo mmoja unasema "The big the dream, the higher the grinding"...... Yaani "Ndoto inapokuwa kubwa basi lazima mapambano yawe makubwa".

Ili malengo yaitwe malengo na ndoto iitwe ndoto ni lazima sifa ya kwanza kabisa malengo au ndoto iwe ni kubwa kuliko level uliyopo sasa na kiwe ni kitu ambacho kita ku-challenge.....Sasa kitu unachotakiwa kukijua ni kuwa kadri unavokuwa na ndoto kubwa au malengo makubwa ndivyo ambavyo mapambano yako ni lazima yawe makubwa zaidi.....Kwa mfano: Mwamafunzi kwenye malengo ya kupata Division One, hawezi kupiga msuli sawa na mwanafunzi mwenye malengo ya kupata Division Three, Mwenye Malengo ya Division One lazima akubali kuumia zaidi ya mwenye malengo ya Division Three....AU, Mtu mwenye ndoto za kuwa Rais ni lazima akubali kuumia sana na zaidi kuliko kijana mwenye malengo ya kuwa Diwani.

Sasa Miongoni mwa swali unalotakiwa kujiuliza mara kwa mara ni hili "JE, MAPAMBANO YANGU YANAENDANA NA NDOTO AU MALENGO YANGU??"........Kama Jibu ni YES basi keep grinding, yaani endelea na Mapambano kwa style hiyohiyo bila kupunguza.....Lakini kama jibu ni NO basi unatakiwa kuongeza Mapambano.

Sasa ili kijiweka kwenye level ya Mapambano kuendana na ndoto au malengo yako basi ni lazima uzingatie na uhakikishe unajifanyia self assessment kwenye maeneo yafuatayo:

Je, Unautumia muda wako sawa na ukubwa wa ndoto yako??

Je, Discipline yako na Commitment na Bidii yako inaendana na ukubwa wa ndoto yako??

Je, Tabia zako za kila zinaendana na ukubwa wa ndoto yako??

Je, Marafiki Unaoambatana wanaendana na ukubwa wa ndoto yako??

Je, kiwango cha Maarifa Uliyonayo sasa yanaendana na ukubwa na ndoto yako na Je, speed yako ya kutafuta Maarifa yakukupeleka kwenye ndoto yako inaendana na ukubwa wa ndoto yako??

Je, Maamuzi unayoyafanya kila siku kwenye maisha yako yanakupeleka kwenye ndoto yako kubwa??

Kimsingi ni kuwa kama una ndoto kubwa lazima na standards zako ziwe kubwa kwenye kila eneo......Eneo muhimu kabisa kupima kiwango cha mapambano yako ni kujiangalia kiwango cha discipline, commitments, hard working yako,marafiki unaoambatana nao, kiwango cha Maarifa Uliyonayo na mambo mengine mengi, kwenye maeneo haya ni lazima uhakikishe standards zako zinakuwa kubwa kama ndoto yako ni kubwa.....Lakini pia ni muhimu ukajua kuwa haya mambo yote kama vile Discipline, Hard working, kiwango cha Maarifa, Marafiki vimejikita kwenye namna unavotumia muda wako...... Kama unatumia muda mwingi Kufanya mambo ambayo hayahusiani na ndoto yako basi jua kuwa mapambano yako hayaendani na ndoto yako, hapa kama kweli upo serious na ndoto yako basi ni lazima ubadili style...... Kumbuka kuwa you are not alone mwenye ndoto kama yako, kuna wengine wana  ndoto ya kuwa Rais kama wewe, kuna wengine wana ndoto ya kuwa best singer in Tanzania kama wewe, kuna wengine wana ndoto ya kuwa wanasiasa mashuhuri kama wewe...... Sasa input ndogo unayoiweka usidhanie hata siku moja kama utashindana na mtu ambaye 24/7 anapambana dhidi ya ndoto yake na ameweka standards za hali ya juu kwenye ndoto yake, ambaye muda wote anajifua ili kuwa bora zaidi na kujiweka sehemu nzuri zaidi ya kutimiza ndoto yake......Yaani haijalishi umejaaliwa uwezo au kipaji kikubwa kiasi gani kama wenzako wenye ndoto kama yako wanafanya zaidi ya wewe unavofanya na wanapambana zaidi yako basi jua kuwa utashika mkia na utaishia level za wakaida sana!!
KUMBUKA YOU ARE IN THE RACE....YOU ARE IN THE COMPETITION!! HAUPO PEKEYAKO UNAYEKITAKA HICHO KITU!! RAISE YOUR STANDARDS!!

Live Your Dream!!

Friday, 22 February 2019

JINSI YA KUTENGENEZA MISHUMAA

*JINSI YA KUTENGENEZA MISHUMAA*

*Malighafi na Vifaa*

Mafuta ya taa waxi/ Nta (Paraffin wax)
Asidi boriki na Stearine
Rangi (ukipenda)
Pafyumu (ukipenda)
Utambi / uzi
Umbo (mould) ya mshumaa
Jiko  la  mafuta  ya  taa/ mkaa na sufuria na vijiko vya chakula
Vifungashio vyenye lebo

*Utengenezaji*

Utambi
Changanya asidi boriki vijiko 5 vya chakula na maji vijiko 4 vya chakula
Koroga kwa dakika 5
Tumbukiza utambi ukae kwa dakika 5
Anika ukauke
Mshumaa
Andaa maumbo  ya mshumaa
Weka utambi katikati ya chombo kwa kushikiza na ute wa mshumaa na funga utambi
Weka sufuria jikoni, changanya nta kilo 1, stearine vijiko 4, chemsha  
Changanya rangi, parfyumu, asidi na koroga hadi mchanganyiko uyeyuke
Epua, mimina mchanganyiko kwenye maumbo na weka kwenye kivuli hadi mchanganyiko unaganda
Ondoa mshumaa taratibu kutoka kwenye maumbo

*Vifungashio na lebo*

Fungasha mishumaa kwenye chombo kitakachomvutia mteja aweze kununua

Bandika lebo kwenye chombo kuhusu bidhaa: Aina, mchanganyiko wa malighafi, uzito au idadi, maelekezo ya matumizi na uhifadhi, jina na anwani ya mtengenezaji, namba ya simu na barua pepe

Onyesha nembo za ubora kamaTBS na GS1 (Barcode)
Fuata maelekezo na taratibu za TBS
Hati na vibali
Onana na mamlaka husika kupata vibali na vyeti: TBS and GS1
Pata hati ya TCCIA kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi
Fuata taratibu za uuzaji bidhaa nje ya nchi

MADE DEODORANT / JINSI YA KUTENGENEZA DEODORANT NYUMBANI

MADE DEODORANT / JINSI YA KUTENGENEZA DEODORANT NYUMBANI :

Mahitaji :

3/4 kikombe mafuta ya nazi safi

1/2 kikombe corn starch au corn flour

1/2 kikombe baking soda  (BICARBONATE OF SODA )

Maelezo :

Changanya mahitaji yote kwa pamoja katika  bakuli. Kisha mimina katika kikopo kisafi na kikavu na weka sehemu yenye ubaridi au katika fridge ili igande. Unatumia kama deodorant zingine.
Inaondoa weusi katika makwapa na kukata harufu mbaya ya kwapa na kupunguza kwa jasho kutoka kwa wingi.
Hata kama haijaganda ni sawa tu. Tumia hivyo hivyo.

Unatumia tu kama deodorant za madukani.

Saturday, 16 February 2019

VITU VIKUU VITATU VILIVYOBEBA TOFAUTI KATI YA WATU WALIOFANIKIWA NA FAILURES

VITU VIKUU VITATU VILIVYOBEBA TOFAUTI KATI YA WATU WALIOFANIKIWA NA FAILURES

Wote tunakuja duniani baada ya kuwa washindi katika mapambano makubwa yanayohusisha mabilioni ya washiriki.....Wote tunakaa mapumzikoni miezi tisa tukijaandaa na pambano lingine.....Wote tunakuja duniani tukiwa full packed na vitu muhimu vya kukusaidia kushinda mapambano mengine ya hapa duniani, ambapo Mungu humpa kila mtu vitu sahihi anavovihitaji kuendana na aina ya pambano lake.....Yaani tunapewa vitu kama vile Passion, talents, core abilities, potential, akili, nguvu, viungo kutokana na kuendana na aina ya mapambano unayoyaendea.......SWALI NI JE, NINI KINASABABISHA WENGINE WASHINDE MAPAMBANO YA HAPA DUNIANI NA WENGINE WASHINDWE ILI HALI WE ARE ALL WINNERS??.......Utofauti huanza kuonekana kutokana na;

1. Kutotumia nyenzo za Mapambano tulizopewa na Mungu.

Kila mtu amezawadia na Mungu vitu maalum vya kumsadia kwenye mapambano....Na kwa bahati nzuri ni kuwa yeyote anayeamua kuzitumia nyenzo hizi ni lazima awe mshindi kwenye hayo mapambano.

Na tofauti ya watu wanaofanikiwa na wasiofanikiwa huanza pale ambapo wengine wanaamua kuzitumia nyenzo hizi wengine wanapuuzia kuzitumia...... Am totally convinced kwamba "Kila mtu ana kipaji/ Uwezo fulani wa kipekee aliopewa na Mungu" ambao ndiyo nyenzo kuu kwake kwa mafanikio....... Kuna watu wamepewa kuchora, wengine kuimba, wengine kufundisha, wengine udaktari, wengine uhandisi, wengine uongozi, wengine Technology, wengine uvumbuzi wa vitu, wengine biashara na ujasiliamali, wengine kishauri, wengine utunzi, wengine habari, wengine ujeshi, wengine michezo etc......Vitu hivi vyote na vingine vingi Mungu ameweka ndani yetu kama Primary weapon ya kutusaidia kufanikiwa.... Tatizo ni kuwa kutokana na Malezi na kukua tukitamani maisha ya watu wengine waliotutangulia kutokana na kuangalia mahali panapoonekana panalipa kwa macho ya kibinadamu basi wengi wameiga na kijikuta wamekaa maeneo ambayo siyo ya kwao......Mtu alitakiwa kuwa daktari amekaa kwenye uhandisi, aliyetakiwa kuwa mwana michezo yupo kwenye udaktari, mwanajeshi yupo kufundisha watoto kama mwalimu, mchoraji yupo polisi, aliyeumbwa kuwa mwanasheria yupo hospitali kama daktari na aliyetakiwa kuwa mchungaji kanisani yupo kwenye siasa.....Yaani ni vururu vururu kila mtu amekaa mahali pasipo pake na hivyo kutotenda kwa viwango vikubwa vya hali ya juu na hivyo siyo rahisi kufanikiwa eneo ambalo siyo eneo lako sahihi. Kwani mtu aliyekaa kwenye eneo lake sahihi kuwa na uwezo wa tofauti na wengine kwenye eneo hilo na anaweza kuona zaidi ya wengine wanavyoona kwenye hilo eneo na pia huwa mbunifu na mvumbuzi wa mambo kwenye hilo eneo.....Sasa wachache waliofanikiwa kukaa kwenye maeneo yao sahihi ndilo kundi la watu waliofanikiwa sana na sisi tunawashangaa na kuwaona kuwa hawa watu wa maakili mengi lakini kumbe hata siyo akili bali ni kutambua eneo lao sahihi na kuamua kukaa hapo.

Watu waliokaa kwenye maeneo yao sahihi ni wabunifu, wavumbuzi wa vitu vipya, wanafanya kwa ubora kwani wao kwao ni kama hobby, wanajituma bila kuambiwa kwani wanaenjoy kufanya hata bila malipo wapo tayari kufanya.

Siyo rahisi kufanikiwa eneo ambalo siyo eneo lako sahihi...... Ukikaa eneo ambalo siyo eneo lako sahihi utaonekana kilaza tuu.....Nyani hakuumbwa akae majini hivyo kama akiwekwa majini utamcheka sana na kumuona hana uwezo.....Samaki hakuumbwa akae nchi kavu bali majini, ukimpleka samaki nchi kavu utamuona kilaza.....simba hakuumbwa kupanda miti, ukimshindanisha na nyani eneo hilo basi lazima simba ainekane mbumbumbu..... Hivyo ndivyo binadamu tumekosea kutokukaa maeneo yetu sahihi.... Leo ukimuona Diamond Platnums anafanikiwa ni kwa sababu yupo eneo lake sahihi, Mbwana Samatta anazidi kuchanja mbuga ni kwa sababu yupo eneo lake sahihi etc.....JITAFUTE, TAFUTA ENEO LAKO SAHIHI, THEN KAA HAPO KWANI NDIPO PENYE MAFANIKIO YAKO!!

2. Tabia zinazoongoza maisha yetu ya kila siku (HABITS).

Mafanikio ni muunganiko wa tabia mbalimbali zinazoleta mafanikio, na uzuri ni kuwa tabia ni kitu ambacho kila mtu anaweza kujifunza.....Ukimuona leo mtu ni Drug addict basi jua hakuzaliwa anatumia madawa ya kulevya bali ni tabia tu alianza kujifunza taratibu, na inawezekana alianza na pafu moja ya bangi na badae akazoea na kuona kuwa bangi hazina stimu za kutosha na kuamua kuanza na unga kidogo then finally addiction.....Tambua kuwa tofauti kubwa iliyopo kati ya watu waliofanikiwa na watu failures siyo akili wala mazingira bali ni tabia zao zinazoongoza maisha yao ya kila siku......Tofauti iliyopo kati ya masikini na tajiri siyo pesa bali ni tabia, kwani huyu ambaye anaonekana masikini leo kama akiamua kuishi kwa tabia za watu matajiri naye baada muda fulani atakuwa tajiri tu.

Kitu chochote ukikifanya maranyingi na kila siku huwa kinakuwa tabia.

Tabia za uvivu, uongo, kuto kujituma, ni miongoni mwa tabia zinazoleta umasikini na kufeli kwenye maisha....Lakini kujituma, ukweli, uaminifu, kumcha Mungu, ni tabia zinazoleta mafanikio.

Tabia ni kitu unaweza kujifunza, Anza leo kujijengea utaratibu wa kujijengea tabia zinazoleta mafanikio.... Kitu chochote ukikifanya kwa mfululizo kwa siku 21 huwa kinabadilika na kuwa tabia.....Na kikifika level ya kuwa tabia maana yake utakuwa unaifanya automatically bila kutumia nguvu.!!
AMUA KUUNGANA NA WASHINDI KWA KUJIJENGEA TABIA ZA MAFANIKIO!!

3. Maamuzi na Chaguzi Tunazozifanya Kila Siku (Decisions and Choices).

Maamuzi unayoyafanya  ndo kitu kinabeba Destiny yako......Unaamua uishi vipi, unaamua kuwa na tabia za aina gani, wewe ndo unaamua kuambatana na watu wa aina gani, wewe ndo unaamua ufuatilie habari za aina gani, wewe ndo unaamua ujaze vitu vya aina gani na taarifa za aina gani kichwani mwako kama ni udaku au skendo za wasanii au movies za kikorea au vitabu na maarifa chanya, Wewe ndo unaamua na kuchagua namna ya kuutumia muda wako na siku yako, wewe ndo unaamua utumiaje pesa unazozipata, wewe ndo unaamua uwe na mahusiano ya aina gani, wewe ndo unaamua uwe mvivu au uwe mtu wa kujituma, wewe ndo unaamua uwe mcha Mungu au mtu dhambi, wewe ndo unaamua kuwa mlevi au la, wewe ndo unaamua na kuchagua uwe kicheche au mwaminifu..... Chaguzi zako na maamuzi unayoyafanya kila siku kwenye vitu mbalimbali kuhusu maisha yako ndivyo vinaamua kama utafanikiwa ama la??!!

Kwenye huu ulimwengu Mungu ametuwekea Uhuru wa kuchagua tunachokitaka na kuamua tunavotaka.....Na bahati nzuri ni kuwa Mungu anatamani kila mtu afanikiwe kwa kiwango cha hali ya juu na ni hasara kubwa sana kwa Mungu kukuona wewe ukiwa failure kwenye maisha yako kwani amekuwekea vitu vingi kwa ajili ya kuwafaa wengine ambavyo ndivyo vingekupa mafanikio makubwa lakini kutokana na uhuru wa kuchagua na kuamua aliotupa wanadamu ndio maana anakuacha uamue wewe Na uchague wewe aina ya maisha unayotaka kuyaishi, Ukichagua kufanikiwa yupo pamoja nawe, ukiamua kufeli anaumia lakini hana namna ya kukulazimisha kufanikiwa.

Maamuzi yoyote na chaguzi ya aina yoyote ile huwa ina kuwa na matokea ndani yake, hivyo kila unapochagua au kuamua kufanya jambo linalokuangamiza na kukudidimiza jua kuwa matokeo yake yatakuwa saw a kabisa na vile ulivoamua au kuchagua..... Kumbuka Bible inavosema " ....Mungu hadhihakiwi, apandacho mtu hakika ndicho avunacho"......Unapofanya maamuzi ya kuvuta sigara jua kuwa matokeo yake ni Kansa ya mapafu, Unapochagua kuwa mzinzi jua kuwa matokeo yake ni HIV/ AIDS, Unapochagua kuwa Mvivu na kujionea huruma na kutoumiza kichwa jua kuwa matokeo yake ni umasikini wa kutupwa.....Lakini pia jua kuwa unapoaamua na kuchagua kujituma, bidii, kumcha Mungu, Uaminifu, maarifa na kutembea na washindi na watu positive jua kuwa matokeo yake ni Mafanikio makubwa.

Maamuzi haya na Chaguzi hizi zinapoendelea kwa muda mrefu huleta matokeo makubwa......Unavoamua na kuchagua leo, kesho na keshokutwa ndivyo vitakavyoleta matokea kuhusu future yako......Ukiamua kama watu waliofanikiwa wanavoamua na kuchagua basi nawe ni lazima utafanikiwa vinginevyo utajiunga na failures.

Dr. Myles Munroe huwa anasema "SUCCESS IS PREDICTABLE".....Unaweza kujua mtu kama atafanikiwa au hatafanikiwa kwa kuangalia kama je anajua anachokitafuta duniani, Tabia zinazoongoza maisha yake (Habits) na Chaguzi zake za Lea na Maamuzi anayoyafanya leo.
JIWEKE KWENYE KUNDI LA WATU AMBAO MAFANIKIO KWAO NI LAZIMA KWA KUTAMBUA ENEO LAKO SAHIHI, KUWA NA TABIA ZA WASHINDI NA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI!!

Live Your Dream!!

Monday, 11 February 2019

UTENGENEZAJI WA MAFUTA YA ALOVERA

Utengenezaji wa mafuta ya alovera

Mahitaji
1*alovera

2*mafuta ya Nazi au mzaituni

    Utengenezaji

Andaa alovera na ukwangue na uweke kwenye blenda na usage usiweke maji

Baada ya kusaga ipua juice ya alovera kisha  weka katika sefuria na uchanganye na mafuta nusu Lita endapo ukipata juice ya alovera robo Lita

Weka jikoni na acha ichemke kwa muda ukiwa unakora

Koroga hadi karibu kuauka utaona imebadirka rangi na kua ya kahawia

Hapo ipua na weka katika chombo kingne ukiwa unachuja

Baada ya kuchuja hapo mafuta yatakua tayar

KASHATA ZA MAYAI

KASHATA ZA MAYAI

Mahitaji:
1. Sukari nusu kg,
2. Samli (aseel ) nusu kg,
3. Mayai 15 mpaka 16,
4. Maziwa mazito ya sona,
5. Iliki kijiko kimoja cha chai,
6. Arki ya vanilla Na rose kijiko kimoja chai. 

Namna ya kupika:
Yeyusha samli yako iwe liquid, iache ipoe kdg isiwe moto sana. Then kwenye bakuli safi weka samli yako, sukari Na mayai yako. Piga au changanya kwa mchapo mpaka vichanganyike vizuri. Then minina mchanganyiko wako kwenye sufuria ya kiasi ambayo haitokupa tabu kukoroga then weka kwenye jiko lako kwa ajili ya kuanza mapishi. Moto usiwe mkali sana wala mdogo sana. 

Anza kukoroga kwa mwiko usiachie mkono ili isigande kwenye sufuria au kuungua kabla kuwiva. 

Endelea kukoroga itaanza kuwa nzito kama crumble eggs, Endelea kukoroga itaanza kubadilika rangi taratibu from white to brown light. Ikianza kuwa brown light weka iliki Na arki zako huku bado unaendelea kukoroga. 

Ikianza kukoza brown minina maziwa ya sona kiasi nusu kikopo. Then koroga koroga kdg tu kiasi maziwa yachanganyike then epua. 

NB: maziwa ya sona unaweka karibia kuepua)
Vile vile usiache kuwa brown dark itakuwa haina test nzuri.

Tunaendelea: ukisha epua sufuria mimina mchanganyiko wako kwenye sinia ya kiasi yenye nafasi nzuri. Unapomimina, mimina upande mmoja kwa sababu samli huwa inabaki nyingi so utapata kuinua sinia yako upande Na kuitoa samli yote. Ukiacha sinia ikalala Kashata zako zitakua Na samli nyingi Na zitakuwa Si nzuri. Kata kata kashata zako vi square wakati bado haijapoa. 

Iegemeze sinia yako sehemu ili samli itiririke upande mmoja Upate uitoe kwa kijiko.

Ukisha hakikisha samli haiteremki tena laza sinia yako usubiri kashata zigande. Inachukua masaa kadhaa kuganda so make sure huzibandui kashata mpaka zigande vizuri.

Zikisha kuganda vizuri bandua uweke kwenye bakuli zipate kuhifadhika vizuri. Kashata zako tayari, Ni nzuri kula kwa gahwa. 

Sunday, 10 February 2019

TIBA YA FANGASI ZA KWENYE KUCHA

Ukiwa na zile fangasi za kwenye kucha ambazo wengi zinaletwa na kufua Chukua jani la hilo uwa huwa linautovu weka pembeni ya kucha ilioharibika  acha usishike maji kwa muda huo iliingie kwenye ile sehemu iliyoharibika * Hapo ikiwa inaingia utasikia maumivu kiukweli nimakali kwani inakusanya usaha  sasa kidole Kitavimba kidogo kamuaa usaha wote utatoka na damu ukikamua maumivu yataisha maana yanaletwa na usaha kitabaki kidonda unaweza tumia dawa yyte ya hosp ilikipone basi kucha lililooza na fangas litakuwa linapanda juu kutoka na kucha zuri litafuata na hautapata tena fangas kwenye kucha hilo

TIBA YA KUKOSA CHOO (CONSTIPATION)

*MARADHI YA KUTOPATA CHOO (CONSTIPATION):*

Haya ni maradhi ambayo mgonjwa huwa hapati choo kwa wepesi. Haja kubwa inaweza kutoka baada ya siku moja au mbili au zaidi na ikitoka huwa ni kigumu na hutoka kwa shida na wakati mwingine huwa kama cha mbuzi. Wagonjwa wengine hupata maumivu wakati wa kwenda haja kubwa. Mtu mwenye afya nzuri hupata haja kubwa kwa kiwango cha chini mara moja kwa siku. Na choo huwa laini na hutoka bila matatizo.

*SABABU ZA MARADHI HUSIKA:*

(1) Upungufu wa vitamini mwilini hasa vitamin B.
(2) Maradhi ndani ya utumbo mpana.
(3) Kula vitu vigumu na vikavu kama vile vyakula vya ngano.
(4) Upungufu wa ulaji matunda na mboga.
(5) Kutokunywa maji ya kutosha.
(6) Upungufu wa fibre kwenye chakula zinazopatikana kwenye maganda ya mahindi.
(7) Ukosefu wa kufanya mazoezi ya viungo.

*TIBA*

Chukua glasi moja ya
maziwa freshi baridi uchanganye na vijiko viwili vikubwa vya Asali na kijiko kimoja kidogo cha mafuta ya habitsoda. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Dawa hii hufanya choo kuwa laini na kupata haja kubwa kwa wepesi.

*Tiba ya Pili*: Kunywa kwa wingi maji ya Uvugvugu ya kunywa ya kutosha na pia ule kwa wingi matunda na mboga za majani.

*Tiba ya Tatu*: Kula kila siku asubuhi tende saba kabla ya chakula cha asubuhi. Tende hufanya choo kuwa laini.

TIBA YA CHANGO


Chango

Huu ni ugonjwa uhusiano kwa wanawake upande Wa uzazi (chango ya uzazi)

Zipo aina nyingi za chango na mnaweza kua watu wa tano wa ugonjwa huu ila kula mmoja akawa na chango ya kipekee yake

Chango kikubwa hutokana na mwanamke kutoweza kushika mimba yani ovary kushindwa kufanya kazi  pia mwanamke huyu anaweza asiwe na siku za hatari na kama atakua nazo basi zitakuja bila mpangilio   aina hii tunasema ( ovelution disorder)

Matokeo yake nini
aina hii kuna hali mbili mayai huzalishwa lakin hayakomai au yanakomaa lakin hayasafirishwi kwenda kwenye mirija ya uzazi

Chanzo chake hua ni kisayansi zaidi nikieleza nitajichosha pia hatutaelewana tuangalie dalili 👇🏽

Kuna dalili nyingi ila kwa uchache ni hizi

1*kua na mzunguko wa hedhi kwa muda mrefu

2*kua na siku zisizo na mpangilio

3*kukosa hedhi kabisa

4*kuumwa tumbo chini ya kitovu wakati wa hedhi au tendo la ndoa

5*kutoshika ujauzito kwa kipindi kirefu

Tiba mbadara 👇🏽

Hakuna tiba ya moja kwa moja hospital isipokua huangalia chanzo na kurekebisha

Mfano .
Kama kuna uvimbe hutibu uvimbe

Kama tatzo la kihomoni hurekebisha homoni na hua hakuna tiba ya moja kwa moja wakati mungu ametupa vitu vya asili tena dawa kubwa na nzur

Utengenezaji wa dawa

Mahitaji

1*papai

2*mbegu za mlonge

3*tangawizi

Utengenezaji

Tumia tangawizi ya unga vijiko viwili vya chakula weka katika blenda

Kisha chukua na papai moja likate kipande 1

Kisha weka unga wa mbegu za mlonge zilizokomaa na kavu kikombe kidogo cha chai

Kisha Saga kwa kuchanganya na maji kidogo

Baada ya hapo acha kwenye friji ipate ubaridi kwa nusu Saa yani dakika 30 kama hauna friji acha kwenye sehem ya usalama yenye ubarido

Uwe unakunywa mchanganyiko huo kwa muda wa mzunguko wako wote wa hedhi utakua umepona kwa uwezo wa mungu

TIBA YA MATATIZO YA MACHO ;KONJACTIVA (CONJUCTIVITS)

*MATATIZO YA MACHO: KONJACTIVA (CONJUCTIVITS):*

Ni maradhi ya macho sehemu ya utando au ute sehemu ya conjuctiva, ambayo inaunganisha sehemu ya ndani ya jicho na kope.

*SABABU:*

Yanaweza kusababishwa na vumbi, moshi, upepo ulio na ubaridi, kuweza kutumia macho kwa muda mrefu kutizama kwa mfano kusoma, kukaa katika mwanga mkali wa jua, upepo wenye ukavu na ujoto wenye hali ya umoto, mvuke, gesi, moto, kemikali, n.k.

*DALILI:*

Kujikuna, kuvimba macho, macho kuwa mekundu, macho kutoa maji au machozi, kuhisi kuna mchanga ndani ya macho, kuogopa mwanga mkali, n.k.

*TIBA:*

Weka macho yawe safi na uyakoshe kwa maji ya baridi. Epusha macho kutokana na joto, baridi, moshi, vumbi, macho yasitumie nguvu sana kama vile kusoma sana.

Tumia dawa za kulainisha choo ikiwa hupati choo vizuri kwa sababu pia huchangia katika maumivu ya kichwa na macho

TIBA YA KUTOA MBA MWILINI

TIBA YA KUTOA MBA MWILINI
Chukua vidonge vya seprini kama vitano (5)
Chukua mafuta ya mgando hata baby care
NJIA YA KUFANYA
Saga vidonge vyote vitanokisha ukipata unga laini changanya kwenye mafuta yako ulioandaa ya mgando anza kutumia dawa hiyo paka sehemu zilizoathirika na mbaa wiki mbili iliikupe matokeo mazuri dawa hii imesaidia wengi karibuni

Saturday, 9 February 2019

BIHASHARA UPANDE WA NEMBO,UJAZO,PICHA YA BIDHAA

Jambo la 3 katika somo la biashara au nembo  nitaelezea kwa juu juu vitu muhimu

1* anuani yako au nambali ya simu

Hii husaidia mteja anapotaka kuchukua bidhaa yako kwenye kampuni au kiwandani ata fata anauni na njia peke ya kumuelekeza ni bara bara kuu na kisha ndipo unaweka namba yako au barua pepe

Picha nzur ya biashara

Hii husaidia kumshawishi na kumvutia mnunuzi au hata kama hajui kusoma lakin anaelewa lengo la bidhaa mfano shampoo kuweka picha ya mtu mwenye nywele ndefu na nzuri

Malighafi na kiasi

Huu husaidia mteja kujua ni vitu gan vimewekwa na kwa kiasi gan cha kumuaminisha ubora wa bidhaa yako

Mfano maji utaona

Magnesium 05
Sulphet 0.1
Calciaum 0.5
Potassium 4.0 nk haya ni malighafi za kuhifadhia maji

Ujazo

Lazima umwambie ni kiasi gan umetumua hata kampuni pekee hawasemi wametengeneza na nini ni kampuni za koka na Pepsi lakin ujazo wanasema

Kwahy lazima uweleze kama kilo sema kilo 1 au moja na nusu basi 1.5 nk na kama haijafika kilo basi itakua gram andaka g 1 nk na kama nusu ni g 500 robo g250 nk

Kama kimiminika ni Lita yani Lita moja utaandika l 1  nk kama haijafika Lita ni ml

Hayo machache katika muhimu

JINSI YA KUPUNGUZA TUMBO NA NYAMA UZEMBE KWA SIKU TATU

JINSI YA KUPUNGUZA TUMBO NA NYAMA UZEMBE KWA SIKU 3 TU .
💫hii pia ni kiboko ya vitambi na nyama  uzembe mrembo .
MAHITAJI
a) unga wa manjano 5 tsp
b) asali 5 tsp
JINSI YA KUTUMIA .
💫chukua manjano changanya na asali koroga vizuri hadi kila kitu kimechanganyikana  vizuri .
💫tumia kijiko 1 tu kunywa kwenye maji ya moto asbh kabla ya kula chochote ,mchana na usiku .
💫tumia siku 3 kwa USAHIHI kabisa utaona matokeo mazuri .

💫💫KUMBUKA
JUHUDI ZAKO MAFANIKIO YAKO .

💫💫UNAWEZA TENGENEZA MCHANGANYIKO MWINGI UKATUNZA KWENYE FRIJI UNADUMU WIKI 2

JINA LA BIHASHARA

1* jina la biashara

Biashara yeyote lazima iyundwe kwa jina tena sio jina tu jina zuri la biashara

Ninaposema biashara hata iwe kampuni au kitu gani lazima uweke jina

Na jina linatokana na mambo 3

1* jina lako wewe au ukoo
  
Hapa unaweza kutumia jina lako au ukoo wako kukutamburisha kupata jina la biashara yako na kukuza jina lako pia na kama jina lako yupo mfanya biashara analitumia sababu ya kufanana basi nenda kwenye ukoo
       Pia kama una jina refu au haliendani na biashara fupisha

        Mfano Muhammad (mo) utapata mo cola nk

Fatma (fetty)
             Fetty unga lishe

Hadija (dija ) dijja or d liquid soap nk

2* jina linalotokana na mahali ulipo au chanzo cha biashara yako

Unaweza kupata jina zuri la biashara kwa kuangalia mazingira ya mahali ulipo sababu chimbuko lako au biashara yako

Mfano bwana mengi kutumia maji ya Kilimanjaro sababu ya kwako pia chimbuko la biashara husika

Tanga fresh huzalishwa dar lakin muazirishi kwao tanga

Dar fresh

Ndanda  maji hutoka mlima ndanda

Udzungwa maji nk

Pia unaweza kutumia jina lililo kupa nguvu au msaada

Mfano umesaidiwa na mtu unaweza kutumia

Mfano serikali kutumia majina ya eneo lilopewa msaada kama daraja fulan lina jina la kiongozi au muasisi Fulani

   Au mmetengeneza kikundi mkaita tupendane hata bidhaa mtakazo tengeneza mfano sabani ya unga mtaita (t detergent) 

Au bakhresa kutumia jina la azam

3* jina linaloendana na biashara

Mfn unazarisha sabuni ya maji unaweza kutumia takasa kwa maana mtu akisikia ajue kua hii inasafisha au ina takasa ndio maana ikaitwa ivyo

Mfano vinywaji kupewa majina ya  energy.  Mo faya nk

Au vituo vya habari kama magazeti kuitwa nipashe tiba mbadara nk

Hii sehem ya kwanza katika kutafuta jina la biashara yako

DAWA YA KUKUZA MAZIWA

Utengenezaji wa dawa ya kukuza maziwa

Mahitaji

1*unga wa uwatu

2*sukari

3*unga Wa ngano

4* papai

Utengenezaji

Saga papai kwa kutumia maji moto kwenye blenda

Baada ya kusaga weka kwenye robo Lita kisha changanya na sukari vijiko 2

Kisha weka na unga wa ngano vijiko  3 vya chakula

Kisha weka na unga Wa uwatu vijiko 3 vya chakula koroga kupata mchanganyiko

Kisha unaweza kutumia kwa siku 10 tu utaona mabadiriko

Sunday, 3 February 2019

UTENGENEZAJI WA SABUNI YA KUKUFANYA UWE MWEUPE KUTUMIA KEMIKALI

Utengenezaji Wa sabuni ya kukufanya uwe mweupe kutumia kemikali 1

  Mahitaji

1*siles (ungaroli)

2*asali

3*limao

4*chumvi

5*rangi

6*manukato

Utengenezaji

Andaa ndoo Lita 20 kisha weka maji Lita 10

Anza kukoroga hayo maji kuelekea upande 1 kwa dakika moja

Baada ya dakika moja mimina silesi(unga roli) Lita moja anza kukoroga kwa dakika 3

Baada ya dakika 3 weka chumvi ya mawe mikono (viganja) viwili  endelea kukoroga kwa kuelekea upande mmoja kwa dakika 15

Baada ya kukoroga kwa dakika 15 sasa weka asali nusu Lita koroga kwa dakika 1

Baada ya dakika moja weka maji ya limao (juice ya kikao) nusu Lita koroga kwa dakika 1

Baada ya dakika moja weka rangi pamoja na manukato kiasi upendacho kisha endelea kukoroga kwa dakika 5

Baada ya dakika 5 sabuni  tayar  kwa matumizi

Matumizi

Kuogea au kunawia uso au sehemu ya ngozi yenye madoa

Saturday, 2 February 2019

CHAMOMILE(CAMOMILE

*CHAMOMILE(CAMOMILE*

Huu ni mmea tiba unaotoa maua,kuna ambao unatoa maua yenye njano na nyeupe na kuna unaotoa maua ya blue na njano

Mafuta ya huu mmea chamomile essential oil ni karibia sh milion 3 kwa lita,
pia maua yaliyokaushwa ya chamomile kwa kg moja ni sh karibia sh 50,000/=.

Huu ni moja ya mimea yenye thamani ya juu sana duniani kutokana na faida ya maua ya huu mmea  kwenye afya na muonekano wa binadamu

FAIDA ZA MAUA YA CHAMOMILE(CANONILE)
NA MAUA UTUMIKA ZAIDI KUTENGENEZA CHAI,.KAMA CHAI

A).FAIDA  ZA KIAFYA

-Inatibu  maumivu ya misuli
-Inatibu maumivu ya hendi
-Inatibu maumivu ya vidonda vya tumbo
-Inapandisha kinga ya mwili
-Inabalance kiwango cha sukari mwilini
-Inatibu  bawasiri(uvimbe  kwenye njia ya haja kubwa)
-Inatibu allegies na vipele
-Inatibu maumivu ya kichwa
-inasaidia kufanya ulale na upate usingizi vizuri

B).KWENYE  NGOZI
chai ya maua ya chamomile

-Inasafisha ngozi
-Inasaidia matibabu ya matatizo yote ya ngozi
-Inafanya ngozi iwe nyeupe(natural skin bleacher)
-inatibu muwasho wa ngozi
-inatibu  chunusi
-Inafanya ngozi isizeeka mapema
-Ni scrub ya asili
-Inafanya ngozi kuwa nyevuu

C) KWENYE  NYWELE
- Inaimarisha rangi ya nywele
-Inazuia mba
-Inakuza nywele

JINSI YA KUPANDA HUU MMEA
(AGORA TUNAPROGRAM YA
(PANDA MIMEA TIBA USIPANDE MAUA AMBAYO HAYANA TIJA)

Mmea wa  chamomile unapandwa kwenye hali ya hewa yoyote
ila kwenye barufu haistawi vizuri,ila kwa hali ya hewa kama ya nchi ya Tanzania huu mmea unastawi cha msingi kuwe na rutuba nzuri

Panda kwenye chungu cha maua,au dishi au sehemu yoyote iwe kama urembo wa nyumba pia tiba asilia

Ukitaka kulima kwa biashara wasiliana na agora team kwa elimu
vitu vichache ni kwamba

=Ekari moja inachukua miche 85,000/=.
Inapadwa kama inavyopanda ni cm 25 kati ya mmea na mmea na cm 30 kati ya mstari
=Na uvunaga unafanyika  ni msimu kama mahindi
=ukitaka kulima herbs lazima uwe na shamba lako
=usipo tumia chemical unafanya mmea uwe vizuri zaidi ki afya
=Mbegu ya agora ya  chamomile kwa wastani kwa akari unavuna
majani makavu ni kg 364.

Mche wa agora wa chamomile herbs unauzwa sh 1000/=

Tuesday, 29 January 2019

EGG CHOP ZA NYAMA YA KUSAGAA

EGG CHOP ZA NYAMA YAKUSAGAA

Mahitaji

1. Nyama yakusaga

2. Thomu Na tangawizi ilosagwa

3. Mikate ya slice ulo sagwa / bread crumbs

4. Pilipili manga Ya unga na nyekumdu

5. Uzile / bizari nyembaba

6. Mayayi yaku chemsha

7. Mayayi yaku changanyia nyama

8. Mayayi yaku chomea

9. Cotmiri / coriander / daniya

10. Blender / food processor

Jinsi yakutayarisha na kupika

0. Mchemsha mayayi kiasi Chako weka pembeni

1. Kausha nyama yakusaga na viungo ikole kisawa
sawa.

1.1 Nyama ikisha poa tia kwenye blender na isage kidogo sio sanaa yote. Mimi hutia kwenye food processor

2. Kwenye hiyo nyama yakusaga tia ile mikate ulo sagaa tia na mayayi kama 2 lakini ina tegemia nakiasi cha nyama yako tia na cotmiri

3. Sasa chukua yayi 1 badaa ya 1 na lizonge kwenye ile nyama yakusaga yote.

4. Sasa piga mayayi mengine tia egg chop na choma kama katlesi kata kati tayari

PIZZA YENYE TOPPING YA KUKU NA CHEESE

Pizza yenye topping ya kuku na cheese

Pizza, chakula rahisi kuandaa unachoweza kula wakati wowote - asubuhi, mchana au usiku. Ni vizuri kuandaa siku unayotaka kula chakula na kupumzika vizuri ukiwa unaongea na familia, marafiki au wengine Ni chakula chepesi, chenye virutubisho vingi na pia ni kitamu sana. Unaweza kuongeza vitu unavyopenda kuipendezesha pizza yako. Mapishi haya yameandaliwa na nnjosie, asante kwa kutushirikisha kwenye kujiramba na utamu wa misosi.

Kuandaa: dakika 75
Mapishi: dakika 35

Mahitaji
Kwa ajili ya unga:

Vijiko 2 vya chai vya hamira (yeast)
Vikombe 1 ¾ vya unga wa ngano. Tenganisha, weka kidogo pembeni
¾ ya kikombe cha maji ya uvuguvugu
Chumvi kijiko 1 cha chai
½ kijiko cha mafuta ya Olive (Mafuta ya mizeituni)
Kwa ajili ya topping:

Minofu ya kuku
Mixed  herbs vijiko 2 vya chakula
Nyanya 2 kubwa
Pilipili hoho 1 na nusu
Mozzarella cheese
Kitunguu saumu vijiko 3 vya chakula vilivyosagwa
Butter vijiko 2 vya chakula
Pilipili manga kijiko 1 cha chai

Mapishi haya ya pizza unayoweza kuandaa kirahisi nyumbani yameandaliwa na nnjosie. Kwa ujumla pizza hii imeandaliwa kwa kufuata maelezo kama ilivyoandikwa hapa, lakini imetumia topping ya kuku, butter, mozarella na pilipili manga.

Andaa pizza kama ilivyoezwa hapa.
Pasha oven nyuzi joto 350°F (180°C). Bandika minofu ya kuku jikoni, acha ichemke kwa dakika 15. Weka pembeni ipoe.
Kwenye kikango, weka butter acha iyeyuke, kisha weka kitunguu saumu kijiko 1, mixed herbs na pilipili manga. Epua acha ipoe weka kwenye friji kwa muda.
Sambaza butter iliyotoka kwenye friji juu ya pizza kwa tumia kijiko. Weka kuku, nyanya, pilipili hoho kisha nyunyizia kitunguu saumu. Weka mozzarella cheese na nyunyizia mixed herbs. Oka Pizza kwa dakika 15 mpaka 20.
Epua. Jirambe.

CHAPATI ZA VEGETABLES

CHAPATI ZA VEGETABLE.....

Mahitaji..

1. unga 4 cups (ngano)
2. hamira vjk 2 vya chai
3. chumvi kjk 1 cha chai
4. bicarbonate of soda 1/2 kjk cha chai
5. pilipili hoho 1, kitunguu maji kimoja, karot 1. ( katakata vyote vipande vidogo vidogo na carrots kwangua )
6. samli vjk 2 vya chai
7 .maji ya kukandia mug 1{yabaridi}

JINSI YA KUTENGENEZA :

1. changanya kila kitu katika unga mpk viwe sawa, kisha anza kuweka maji kdg kdg mpk upate donge. endelea kukanda mpk unga uwe laini.
2. kata madonge 12 kisha sukuma na zungusha km chapati za kawaida, acha ziumuke kwa nusu saa.
3. ikishaumuka, anza kusukuma km chapati lkn isiwe nyembamba, iwe nene kdg. kisha choma km chapati.
~~ ENJOY ~~~

JINSI YA KUTENGENEZA CHILL SAUCE

*KUTENGENEZA CHILL SAUCE*

*Mahitaji*

Ø Pilipili mbuzi nyekundu kilo 1

Ø Nyanya zilizoiva kilo 2

Ø Vitunguu swaumu
viwili vya wastani

Ø Sukari (kama unapenda) vijiko viwili

Ø Maji ya uvuguvugu kikombe cha chai kimoja

Ø Mafuta ya kula vijiko 6 vya chakula

*Jinsi ya kutengeneza*

Menya nyanya, toa mbegu, kata kata kisha weka kwenye blenda. Kata pilipili, toa mbegu weka kwenye blenda.

Menya vitunguu swaum, weka kwenye blenda kisha Weka maji ya uvuguvugu, kisha saga vyote kwa pamoja.

Chukua mkorogo wako, weka kwenye kikaango chenye mafuta kama tufanyavyo katika utengenezaji wa tomato sauce.

Hapo itakuwa tayari kwa matumizi.

Kumbuka: hatuweki vinegar kwa sababu chill sauce haiharibiki kwa kuwa ina pilipili.

KASHATA ZA NAZI

Kashata za nazi
Nazi  iliyokunwa mmoja kubwa
Jelly kiasi
Sukari robo
Maziwa ya unga 3tspoon
Hiliki chembe 5
Maji kiasi
Food colour

Chukua bakulia kavu weka nazi uliyoikuna tia hiliki na maziwa changanya uzuri mpk uwe kitu kimoja weka pembeni chukua sufuria tia maji weka jikoni subir yachemke weka sukari suburi mpk ifanye povu zito chota kwa mwiko halafu gusa na vidole ukiona inanata snaa km gundi weka nazi yako  n'a jelly changanya uzuri mpk mchanganyiko uwe kitu kimoja,mimina ktk kibao cha mkate ulichoweka mafuta ukimaliza sukuma na kifimbo ulichokipaka mafuta ukimaliza wacha ipoe halafu aaza kukata shepu uipendayo,andaa n'a kahawa Kula.

Wengi zinawapa tabu hizi kashata kwa sababu nazi inakuwa maji maji ukitaka uweze ikune mapema ukimaliza chukua sahani kubwa
zitandaze weka juani kidogo halafu ndoo upike n'a sio lazima kuweka jelly mm nimeweka km urembo tu.
  👩‍🍳 mapishi bora 👩‍🍳

JINSI YA KUTENGENEZA CHOCOLATE

JINSI YA KUTENGENEZA CHOCOLATE
Unaweza kutengeneza chocolate nyumbani kwa kutumia vifaa vya nyumbani na ingredients zinazo patikana madukani.

MAHITAJI KWA AJILI YA CHOCOLATE.
-Siagi kikombe kimoja
-Cocoa powder kikombe 1
-Icing sugar/Sukari iliyosagwa au asali kikombe 1/2
-Maji 1/2 kikombe
-Vanilla ya maji kijiko 1 ccha chai
-Chumvi tone

MAELEKEZO
1)Pima Sukari na Cocoa powder kwenye sufuria size ya kati.
2. Ongeza maji kwenye mchanganyiko wa sukari na cocoa poda.

3)Weka maji kwenye sufuria kubwa yajae 1/4 kisha weka kwenye moto mdogo.
4)Weka sufuria ya size ya kati iliyo na cocoa poda+sukari+maji juu ya sufuria kubwa(double boiler).

5)Wakati maji ya sufuria kubwa yanachemka, koroga mchanganyiko wako wa cocoa poda taratibu, kwa dk 15 mpaka iwe nyepesi kama uji.
6)Ondoa sufuria ya mchanganyiko wa chocolate kwenye moto, kisha ongeza  siagi iyeyukie, ongeza fleva kama vanila.

7)Blend mchanganyiko wako, tumia blender au hand mixer,lengo la kublend ni kufanya chocolate yake iwe smooth isiwe na mabuja.

8)Mimina chocolate mchanganyiko,kwenye ice cube tray,acha kidogo isawazike kwa dk2.
9)Weka ice cube tray iliyo na chocolate kwenye freezer, kwa masaa 1-2 au usiku kucha.
10)Waweza toa kwa lisaa limoja,kisha ukaweka juu ya chocolate karanga zilizosagwa,au peanut butter,au strawberry(Angalia pichani),kisha rudisha frijini kwa lisaa1.

-Chocolate tayari,toa tray, ondoa chocolate kwenye tray tayari kwa kuliwa.ENJOY
  👩‍🍳 mapishi bora 👩‍🍳

Monday, 14 January 2019

MALIGHAFI ZINAZO HITAJIKA WAKATI WA UTENGENEZAJI WA MISHUMAA

*Jinsi ya kutengeneza mishumaa*

*MALIGHAFI ZINAZO HITAJIKA WAKATI WA UTENGENEZAJI WA MISHUMAA*

1. Paraffin Wax
2. Utambi
3. Mould ( Umbo )
4. Stearine au mixture
5. Rangi
6. Jiko la mafuta ya taa au mkaa.
7. Sufuria.
8. Boric acid.

*VIDOKEZO MUHIMU*
1. Paraffin Wax :
Hii inatokana na nta na sega ya nyuki iliyo changanywa na mafuta ya taa. Ina rangi nyeupe na katika utengenezaji wa mishumaa ina ubora kuliko bee wax.

* Bee Wax : Inatokana na masega ya nyuki yaliyo changanywa na mafuta ya petroli na diesel na rangi yake ni ya njano.

2. STEARINE
Hii dawa maalumu inayo fanya mishumaa iungane ama ishikamane.

3. BORIC ACID :
Hii ni maalumu kwa ajili ya kuufanya utambi usiishe mapema na uwake bila kutoa moshi.

4. RANGI :
Rangi nzuri zinazo tumika katika utengenezaji mishumaa ni rangi za chakula na nyingi huwa ni za maji.

*JINSI YA KUTENGENEZA*

Andaa mould ( umbo lako ) utakalo litumia baada ya kuyeyusha ( paraffin wax ) na kuchanganya na michanganyo yote.

Kwa Mfano : ( Kipimo cha stearine )
1. Wax kilo moja - Stearine vijiko vinne vya chakula.
2. Wax nusu kilo - Stearine vijiko vinne vya chakula
3. Wax robo kilo - Stearine kijiko cha chakula.

Baada ya mould ( umbo ) kuwa tayari , chemsha wax mpaka iyeyuke na itoe kwenye vyombo ambavyo umetayarisha na usubiri ikauke ili uanze kutoa mishumaa

DAWA YA KUNG'ARISHA VIATU VYEUPE

Dawa ya kung'arisha Viatu vyeupe

Mahitaji

1*magadi soda

2*vinegar

3*maji

Utengenezaji..

Andaa bakuli lako linaloendana na wingi Wa mahitaji yako kisha weka magadi soda vijiko 5 vya chakula kisha weka vinegar vijiko 5 vya chakula kisha weka maji vijiko 5 vya chakula koroga

Hakika Viatu hata kama vilikua vimegandia uchafu sugu au kufubaa vitarudi katika hali yake ya zamani

Friday, 11 January 2019

UTENGENEZAJI WA SABUNI YA KUNAWIA MIKONO,KUSAFISHIA VIOO,

Utengenezaji Wa sabuni ya maji,_ shampoo, sabuni ya kunawia mikono   sabuni ya kusafishia vioo, dawa ya kusafishia choo   yote ndio hii

Tofauti unaweza kumbadirisha rangi tu na kumuwekea Vifungashio tofauti

Mahitaji

1* siles (ungaroli)

2*chumvi

3* rangi ya sabuni ya maji

4*manukato

Utengenezaji

Andaa ndoo Lita 20  kisha weka maji Lita 10 kisha weka siles (unga roli) Lita 2

Kisha koroga Kwa dakika 15  ila kila baada ya dakika 5 weka chumvi mikono (kiganja) kimoja kwahy hadi dakk 15  utakua umeweka chumvi viganja 3 

Baada ya kukoroga Kwa dakika 15 sasa weka manukato kiasi upendacho pamoja na rangi kiasi upendacho

Koroga tena kwa dakika 5  

Hapo utakua umekorga Mara   dakika 20 hadi kumalizika kwa sabuni

Na sabuni yako itakua tayar

Hakuna alie jaribu hii sabuni na sizani kama aliwai mtu kutengeneza ni nzito sana na malighafi chache

Tuesday, 8 January 2019

UTENGENEZAJI WA JAMU YA NANASI

*UTENGENEZAJI WA JAMU YA NANASI*

Jamu ya nanasi ni bidhaa inayotengenezwa kwa kutumia mchanganyiko wa mananasi yaliyosagwa (pulp) na kuchemshwa pamoja na sukari na acid. Ili kupata jamu yenye ubora mzuri ni sharti kuzingatia uwiano mzuri kati ya acid, sukari na pectin.


*Mahitaji/Viambaupishi*

Nanasi

Sukari

   
citric acid (Kutegemeana na aina ya matunda)

   *VIFAA*

SUFURIA

   KIJIKO CHA CHAI

  VISU

  KIPIMA JOTO (THERMOMETER)

   CHUJIO

   MWIKO

   NDOO

     SINIA
   REFRACTOMETER

  MZANI

MASHINE YA KUSAGA MATUNDA (BLENDER)AU ‘PULPER’


  UBAO WA KUKATIA MATUNDA

Hatua za uzalishaji

Osha matunda vizuri kwa maji safi na salama. Chagua matunda yalyoiva
Menya matunda na ondoa macho na moyo wa katikati, katakata vipande na uvizage.
Chemsha kupata pulp ya matunda

Weka

sukari
acid

Changanya vizuri, pika polepole ukikoroga hadi joto la kutosha litakapofikia.
Hakikisha jamu yako imeiva vizuri
Jaza kwenye chupa safi ikiwa bado ya moto.
Jamu tayari

JINSI YA KUTENGENEZA SHAMPOO

*JINSI YA KUTENGENEZA SHAMPOO*

shampoo zipo za aina nyingi inategemea virutubisho na kemikali zilizotengenezwa.kuna shampoo ambazo zina harufu nzuri .kwa mfano waweza tumia perform[harufu]kama havened lemon,jasmine,peach apples) na shampoo za virutubisho kama parachichi,karoti alovera,tango,mayai.

Mfano(i)
Kutengeneza shampoo (ambayo inatumia chemical)
zilizochanganywa harufu au perfume(vyote ni kuchanganya kwa pamoja
na kukoroga tu).

Mfano(ii)
malighafi za shampoo isiyo na virutubisho/shampoo hiyo
unaweza tengeneza kwa formula mbili
.    sulphonics Acid
.    soda ash
.    maji
.    sless
.    rangi
.    perfume
.    grycelin
.    chumvi.

*JINSI YA KUTENGENEZA*
*HATUA YA*

Kwanza tayarisha malighafi zote,ziwe juu ya meza utakayo fanyia kazi,vyombo vya kufanyia viwe visafi na kumbuka kusafisha kwa maji kila unachotumia.
Tayari vifaa vya  kufanyia kazi
Anza na sulphonic acid vijiko (4) vya chakula tumbukiza kwenye ndoo au mashine yako.

Fuatia na soda ash vijiko(2) vya chai lakini kumbuka kuchanganya na maji kidogo.
Koroga na mwiko au na mti baada ya mchanganyiko

Tia maji lita 4 nakuanzia hapo anza kukoroga kwa muda wa dakika kumi,kisha unafuatia malighafi zifuatazo
Strees-robo
Glycerine vijiko(3) vya chakula
Perfume-kijiko cha chai kimoja
Rangi-Kijiko cha chai kimoja.
Chumvi kijiko cha chai kimoja

   Usiweke kitu kingine na ukumbuke chumvi ni ya mwisho kama muda umefika ikiwa nzito kama uji/shampoo yako itakua tayari

YOUTH OPPORTUNITY

Please share these opportunities within your students and friends and networks👇

1. Australia Award  Scholarship (http://australiaawardsindo.or.id)
2. LPDP Scholarsh hip (http://www.beasiswalpdp.org/index.html)
3. DIKTI Scholarship a. Dalam Negeri (http://www.beasiswa.dikti.go.id/dn/)b. Luar Negeri (http://beasiswa.dikti.go.id/ln/)
4. Turkey Government Scholarship (http://www.turkiyeburslari.gov.tr/index.php/en)
5. General Cultural Scholarship India (http://www.iccrindia.net/gereralscheme.html)
6. USA Government Scholarship a. (http://www.aminef.or.id/index.php)b. (http://www.iief.or.id)
7. Netherland Government Scholarship (http://www.nesoindonesia.or.id/beasiswa)
8. Korean Government Scholarship (http://www.niied.go.kr/eng/contents.do…)
9. Belgium Government Scholarship (http://www.vliruos.be/4273.aspx)
10. Israel ... ... xxx
11. Sciences Po France (http://formation.sciences-po.fr/…/the-emile-boutmy-scholars…)
12. Utrecht University Netherland (http://www.uu.nl/…/grantsandscholarships/Pages/utrechtexcel…)
13. Prasetya Mulya Business School Indonesia (http://www.pmbs.ac.id/s2/scholarship.php?lang=ENG)
14. Brunei Darussalam Government Scholarship (http://www.mofat.gov.bn/index.php/announcement)
15. Monbugakusho Scholarship Japan (http://www.id.emb-japan.go.jp/sch.html)
16. Paramadin ba University Master Fellowship Indonesia (https://gradschool.paramadina.ac.id/…/paramadina-medco-fell…)
17. PPM School of Management Indonesia (http://ppm-manajemen.ac.id/beasiswa-penuh-s2-mm-reguler/)
18. University of Twente Netherland (http://www.utwente.nl/internationa…/scholarshipsandgrants/…/)
19. Sweden Government Scholarship (http://www.studyinsweden.se/Scholarships/)
20. Chinese Government Scholarship (http://www.csc.edu.cn/laihua/scholarshipdetailen.aspx…)
21. Taiwan Government Scholarship (http://www.studyintaiwan.org/taiwan_scholarships.html)
22. United Kingdom Government SCholarship (http://www.chevening.org/indonesia/)
23. Panasonic Scholarship Japan (http://panasonic.net/citizensh…/scholarships/…/requirements/)
24. Ancora Foundation Scholarship (http://ancorafoundation.com)
25. Asian Public Intellectuals Fellowship Japan (http://www.api-fellowships.org/body/)
26. AUN/SEED-Net Scholarship (http://www.seed-net.org/index.php)
27. Art Asia Major Scholarship Korea National University of Arts (http://eng.karts.ac.kr:81/karts/board/list.jsp…)
28. Ritsumeikan Asia Pacific University Japan (http://www.apu.ac.jp/home/life/index.php?content_i
d=30)
29. Seoul National University Korea (http://en.snu.ac.kr/…/gradu…/scholarships/before-application)
30. DIKTIS Overseas Scholarship (http://www.pendis.kemenag.go.id/beasiswaln/)
31. Honjo International Scholarship Foundation Japan (http://hisf.or.jp/english/sch-f/)
32. IDB Merit Scholarship Programme for High Technology (http://www.isdb.org/irj/portal/anonymous…)
33. International HIV & Drug Use Fellowship USA (http://www.iasociety.org/fellowship.aspx)
34. Nitori International Scholarship Foundation Japan (http://www.nitori-shougakuzaidan.com/en/)
35. School of Government and Public Policy Indonesia (http://sgpp.ac.id/pages/financial-conditions)
36. Inpex Scholarship Foundation Japan
37. Asia University Taiwan (http://ciae.asia.edu.tw/AdmissionsScholarship.html)
38. Macquaire University Australia (http://www.mq.edu.au/…/macquarie_university_international_…/ .

Please share for the benefit of our youth. You will be surprised with  the difference you can make.

Monday, 7 January 2019

HOMEMADE FONDANT ICING / NAMNA YA KUANDAA FONDANT KWA AJILI YA KEKI NYUMBANI

HOMEMADE FONDANT ICING / NAMNA YA KUANDAA FONDANT KWA AJILI YA KEKI NYUMBANI :

MAHITAJI

🔸Icing sugar, ilochekechwa vikombe 7 na  1/2
🔸Maji ya baridi 1/4 kikombe
🔸Unflavored gelatin kijiko 1 chakula (kwa waislam hakikisha ni halali gelatin) maana zingine zatengenezwa kwa mafuta ya nguruwe
🔸Glucose 1/2 kikombe
🔸Glycerine kijiko 1 1/2 chakula
🔸Vanilla kijiko 1
*NOTE*
GLYCERINE YA CAKE NA GLUCOSE YA CAKE. SIO VYA KUPAKIA MWILINI. NI VIFAA KWAJILI YA CAKE🎂

NAMNA YA KUTAYARISHA:-

1. Tia icing uliochekecha katika bakuli kubwa kisha weka kishimo kati

2. Katika kisufuria kidogo tia maji kisha nyunyiza gelatin juu acha ilainike kwa muda wa dk 5.

3. Ipashe moto gelatin ukiwa wakoroga hadi  iyeyuke yote , usiache *ikachemka.* Zima jiko kisha tia glucose na glycerine na koroga vizuri hadi vichanganyike.

4. Tia radha, kisha mimina katika kishimo ulichoweka karika icing yako na changanya hadi icing yote ichanganyike vizuri.

5. Kanda foundant yako katika sehemu ya kukandia au sinia hadi iwe smooth na soft, ukiona inanata ongeza icing kidogo.

6. Fanya duara kisha zungusha vizuri na plastic na tia katika container lenye mfuniko.

NOTE
Usiweke katika fridge tumia kwa muda wa wiki 2

Ni vyema uiache ikae kwa muda wa masaa 8 kabla ya matumizi

Mahitaji yanapatikana maduka ya vifaa vya keki,na supermarket.

Sunday, 6 January 2019

JINSI YA KUTENGENEZA MAFUTA YA MGANDO

*JINSI YA KUTENGENEZA MAFUTA YA MGANDO*.

*tujifunze namna Kutengeneza mafuta ya mgando(meupe)*

*Mahitaji*

Micro wax kilo moja
White oil Lita mbili
Perfume vijiko viwili
Kutengeneza
Chukua sufuria kavu bandika jikoni weka micro wax kilo moja
Kisha white oil Lita mbili iache mpaka ichemke kwa muda mfupi utaweka perfume vijiko viwili mimina humo
Baada ya hapo utaiacha ichemke kidogo kisha isikae sana ichemke mana italipuka kwahyo wakati unaipika moto uwe wa wastani kisha acha ipoe ibakie ya uvuguvugu
Mpaka hapo itakua imekamilika mgando wako weka lebo

SABUNI YA MAWESE NA ASALI

SABUNI YA MAWESE NA ASALI

MAHITAJI

ASALI PURE VIJIKO 10,

MAFUTA YA MAWESE MILS 200

OLIVE OIL VIJIKO 2

BASE SOAP GM 700

RANGI( UKIPENDA ) NJANO ROBO KIJIKO.

HATUA YA 01:

YEYUSHA BASE SOAP NDANI YA SUFURIA LA MAJI YA MVUKE( DOUBLES  BOILER)

IKISHAYEYUKA ONGEZA MAFUTA YA MAWESE , ONGEZA  OLIVE OIL, RANGI, KISHA KOROGA KUPATA UJI AMBAO UTAMIMINA KTK MOLD ULIYOANDAA.

SABUNI HII IPO TAYARI KWA MATUMIZI MARA TUU IKISHAPOA NA KUGANDA.

Saturday, 5 January 2019

PSYCHOLOGY: SAIKOLOJIA DALILI 7 KUWA MKEO ANAHITAJI UMSIKILIZE

PSYCHOLOGY: SAIKOLOJIA DALILI 7 KUWA MKEO ANAHITAJI UMSIKILIZE


PSYCHOLOGY: SAIKOLOJIA DALILI  7 KUWA MKEO ANAHITAJI UMSIKILIZE
Wakati fulani kitu pekee ambacho mwanamke anakihitaji ni mtu wa kumsikiliza. Njia maridhawa ya kumsaidia mkeo katika
matatizo yake, kwanza ni kumsikiliza na kumakinika kwa anachosema kisha utoe maoni yako juu ya suluhisho la tatizo husika iwapo ataomba ufanye hivyo.
Iwapo hutambui ujumbe ambao mkeo anajaribu kuutuma, basi Famasia ya Ndoa Maridhawa inakuletea ishara saba za wazi zinazoonesha kuwa mkeo anahitaji sana umsikilize:

1. ANAPOONESHA TABASAMU AMBALO SIO HALISI:
Mwanamke anayeweza kutabasamu hali ya kuwa hajisikii vizuri, basi huyo ni mwanamke madhubuti, lakini bado anahitaji faraja yako. Mkumbatie na umuombe afunguke.
2. IWAPO SIKU NZIMA ALIKUWA PEKE YAKE NA WATOTO
Anahitaji kupata mazungumzo ya mtu mzima. Kama ni mama wa nyumbani, bila shaka atakachokuwa akikisikia kwa siku nzima ni makelele ya watoto, vilio vyao na sauti za vipindi vya katuni. Unaporudi nyumbani muulize kuhusu siku yake ilivyokuwa ili kumpa mazungumzo ya kiutu-uzima ambayo alikuwa na shauku nayo kwa kutwa nzima.
3. ANAPOKUWA KIMYA KULIKO KAWAIDA
Anapokuwa na ukimya usiokuwa wa kawaida, anaweza kuwa na hasira au msongo. Mkumbatie na umuulize kinachoendelea akilini mwake.

4. ANAPOSEMA KWA HASIRA "SAWA"
Iwapo uko kwenye ndoa kwa muda mrefu au unazifahamu silika za wanawake, anaposema "sawa" yaweza kumaanisha "sio sawa". Yumkini tatizo lisionekane, lakini huhitaji kuchimbua kutafuta mzizi wa tatizo. Muulize tu mambo gani hayako sawa na namna unavyoweza kusaidia kuyaweka sawa. Atapenda sana kuona kuwa unajali sana hisia zake.

5. ANAPOKUWA KATIKA MOOD NZURI
Anataka umsikilize anapokuwa na furaha kwa kiwango kilekile anachotaka umsikilize anapokuwa na huzuni. Muulize kuhusu siku yake ilivyokuwa. Yumkini anatamani kukupa habari njema.

6. ANAPOCHOSHWA NA MAJUKUMU YA KUTWA NZIMA
Tengeneza utayari wa kumsikiliza pindi anapokuwa na siku iliyojaa majukumu kayaya. Mkumbushe namna unavyothamini yote anayoyafanya kwa ajili yako na familia yenu pia. Hatua hii maridhawa itamthibitishia kuwa yote anayoyafanya yanaonekana na kumpa hamasa ya kuendelea kufanya mambo mazuri na kujituma zaidi.

7. ANAPOJIANDAA KULALA
Tengenezeni mazingira na utaratibu wa kuzungumza kabla ya kulala. Mweleze namna siku yako ilivyokuwa na usikilize upande wake pia. Muda huu wa ukuruba huwaleta pamoja kihisia, na atafurahia kutumia dakika hizo za mwisho kuzungumza nawe.
Kaka yangu, zichunguze ishara zinazoonesha kuwa mke anahitaji umsikilize. Anahitaji uwe pembeni yake anapokuwa na msongo au anapokuwa na furaha. Aidha, kwa upande wako pia, kama unataka mkeo akusikilize, mwambie. Ndoa yenye afya huimarika zaidi pindi wanandoa wanapokuwa na uwazi, ukweli na wakawa tayari kusikiliza.

Friday, 4 January 2019

TENGENEZA ELA NYINGI KWA KUFUNGUA KIWANDA KWA MTAJI MDOGO

Tengeneza ela nyingi kwa kufungua kiwanda kwa mtaji mdogo na chini

1* sabuni ya maji Lita 10 kwa 12000

2*sabuni ya kipande miche 10 kwa 10000

3*sabuni ya unga kilo 3 kwa 9000

4*sabuni za urembo vipande 40 kwa 6000 unauza 500 au hata 1000 kila kipande

5*kiwanda cha rosheni kwa 12000

6*kiwanda cha chaki kwa 5000

7*kiwanda cha juice kwa 4000

8* kiwanda cha pili pili tomato au chills kwa 8000

9" kiwanda cha mikate kwa 40000

10*kiwanda cha mafuta ya mnyonyo. Buree

11*Kiwanda cha mafuta ya alizet kwa 30000

12*kiwanda cha unga Wa lishe kwa watoto na wanao nyonyesha Kwa 50000 ila kila mfuko 1 unauza 5000 una unapata mifuko si chini ya 30 inabust maziwa

13*Kiwanda cha batiki kwa 28000

14 .kiwanda cha maji 300,000

15*kiwanda cha Viatu Kwa 20,000

16*kiwanda cha viungo vya chakula Kwa  10,000

17*kiwanda cha kusafishia masink kwa 20000

18*kiwanda cha chakula cha kuku kwa 100,000

19,kiwanda cha pafyum kwa 12,000

20*kiwanda cha kusindika samaki kwa 200,000

Hivyo ni baadhi tu za viwanda unavyoweza mm na wewe hadi mwezi Wa 12 tukawa kivingne kila jengo limeanza na tofari 1 na kila safari imeanza na hatua 1

Ukianza juu utashuka chini

Ukianza chini utapanda juu

Wewe ni champion

Tuesday, 1 January 2019

UTENGENEZAJI WA SABUNI YA MAGADI/MAWINGU

Utengenezaji Wa sabuni ya magadi/mawingu

Mahitaji

1*kaustiki soda (kama chumvi)

2*maji

3*mafuta ya mise au Nazi

4*magadi soda

5*chumvi

6*sodium silket au cde kimoja wapo (kama mafuta)

Vifaa vya usalama

Grops za mikono

Mask kuziba pua  wakat Wa kukoroga kaustiki

Ndoo

Mti Wa kukoroga

Boksi za kawaida kwaajiri ya kufanya maumbo

Utengenezaji

Hatua ya kuanza

Andaa ndoo Lita 10 weka maji Lita 5

Baada ya kuweka maji weka magadi soda vijiko 3 vya chakula ..

Baada ya hapo mimina kaustiki soda kilo 1

Anza kukoroga Kwa dakik 5
Baada ya hapo acha kwa siku 3 uwe umefunika au umeacha wazi ni sawa

Maelezo

Wakati Wa kuweka kaustiki maji yatakua ya moto ndio hali yake ila utakiwi kuchezea kwa mikono

Hatua ya kumalizia

Baada ya siku 3 kaustiki itakua imepoa  kwahy tumeleweka kwenye maji ili isichubue mikono sabuni yetu

Sasa chukua ndoo yenye maji ya kaustiki anza kumimina malighafi zifuatazo

Sidiuom silket au c.d.e vijiko 3 vya chakula

Kama unayo soda ash unaweza kuweka vijiko 3 vya chakula kama hauna acha tu

Baada ya hapo chemsha mafuta yako yawe ya vugu vugu sababu yana asili ya kuganda kwahy lazima uyachemshe hata kama hayajaganda

Baada ya kuchemsha sasa utaangalia ukubwa Wa umbo lako

Mimi Nina boksi Dogo nimeomba dukani kwahy nitachota Yale maji ya kaustiki soda Lita 1  alafu nitaweka kwenye ndoo isiokua na kitu chochote alafu nitachanganya na mafuta Lita 2 nitakoroga kidogo Sana kama sekunde 20 alafu namimina kwenye boksi langu ili ikauke kisha nikate vipande

Ila wakat Wa kuandaa boksi kwa ndani nitaweka maironi ili sabuni ikikauka isinasie kwenye boksi

Pia ile naironi nitaitoboa vitobo kidogo ili kuna maji maji niyape nafasi ya kupita

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO