Monday, 29 October 2018

HAKUNA KUWAI WALA KUCHELEWA KAYIKA MAFANIKIO NA MAHISHA

Tanzania  iko Mbele Lisaa 1 zidi ya Congo... lakini hii haimaanishi Tanzania inaenda Mbio sana au labda Congo iko taratibu sana.. Zote ziko sawa isipokuwa kila moja ina TIME ZONE yake.

Kuna mtu yuko Single sasa hivi..
Kuna mtu Ameolewa na kusubiri Miaka 10 kabla ya kupata mtoto..
Wakati kuna mtu amepata Mtoto ndani ya mwaka wa kwanza wa Ndoa.

Au, kuna mtu amemaliza Degree akiwa na miaka 22, lakini akasubiri miaka 5 kabla ya kupata kazi,
Wakati kuna mwingine amemaliza Degree akiwa na miaka 27  na akapata kazi mwaka huo huo.

Kuna mtu kawa Mkurugenzi akiwa na miaka 25 na Kufariki akiwa na Umri wa miaka 50 ,
wakati mwingine amepata Ukurugenzi akiwa na miaka 50 na kuishi mpaka miaka 90

Kila mmoja anaishi kulinga na TIME ZONE yake.

RAFIKI ZAKO au
NDUGU ZAKO AU
WADOGO ZAKO WANAWEZA KUONEKANA MBELE YAKO , AU
WENGINE NYUMA YAKO
KILA MMOJA HAPA DUNIANI ANATEMBEA au KUISHI KWENYE BARABARA YAKE PEKE YAKE YA MUDA..
MUNGU Anampango TOFAUTI kwakila BINADAMU.. TOFAUTI NI MUDA TU..

Tazama , Obama amestaafu Urais akiwa na miaka 55, Trump ameanza Urais akiwa na Miaka 70.  YOTE HAYA NI TIME ZONE

Usimwonee WIVU mtu,
Wala USIMLAUMU mtu,
KILA MMOJA NA TIMEZONE YAKE.

Endelea KUJIAMINI, na amini KILA KITU Kitakua SAWA kulingana na TIME ZONE yako.

HAUJAWAHI WALA HAUJACHELEWA.. issue ni TIME ZONE YAKO TU.

Usiumizwe sana KICHWA KWAMBA ..
Mbona mwenzangu KAJENGA mimi BADO,
Mbona ana GARI Mimi sina,
Mbona KAOLEWA ila mimi BADO..
Mbona KAOA ila mimi BADO....
Mbona Ana Mtoto mimi Sina mpaka sasa.. N.K

CHAPA KAZI KWA BIDII,HUKU UKISUBIRIA MUDA WAKO..
MUOMBE MUNGU ATAKUBARIKI NA UMTEGEMEE YEYE...
KILA UFANYALO FANYA KWA IMANI KUWA SIKU ITAFIKA MUNGU ATAKUPA🙏🙏🙏.

MKATE WA MCHELE/MKATE WA KUMIMINA

MKATE WA MCHELE/MKATE WA KUMIMINA

Mahitaji
1.Unga wa mchele (rice flour 2
vikombe vya chai)
2.Sukari (sugar 3/4 ya kikombe cha
chai)
3.Hamira (dried yeast 3/4 kijiko cha
chakula)
4.Hiliki (cardamon powder 1/2 kijiko
cha chai)
5.Ute wa yai 1(egg white)
6.Tui la nazi (coconut milk kikombe
1 na 1/2 cha chai)
7.Mafuta (vegetable oil)
MATAYARISHO:-
Changanya unga wa mchele, hamira, hiliki na tui
la nazi pamoja katika bakuli la plastic kisha
koroga vizuri. Ufunike na uwache katika sehemu
ya joto mpaka uumuke.(ambayo inaweza
kuchukua kama dakika 30-45. Ukisha umuka tia
sukari na ute wa yai kisha ukoroge vizuri. Baada
ya hapo washa oven katika moto wa 200°C
kisha chukua chombo cha kuokea na ukipake
mafuta na umimine mchanganyiko. Kisha utie
katika oven na uoke kwa muda wa dakika 40.
Hakikisha unaiva na kuwa rangi yabrown juu na
chini. Na hapo mkate utakuwa tayari kuliwa pamoja na chai ya maziwa au ya rangi au hata juice.
NB:-KAMA HAUNA UNGA WA MCHELE WAWEZA CHUKUA MCHELE WAKO NA UKAULOWEKA KATIKA MAJI USIKU MZIMA KISHA UKAUSAGA KATIKA BLENDA NA MKATE WAKO UKATOKA VIZURI PIA.NA KAMA HAUNA OVEN YA KISASA BASI WAWEZA TUMIA JIKO LA MKAA KUOKEA.

KUTENGENEZA WA DAWA YA KUONDOA MADOA KWENYE VIATU

Utengenezaji wa dawa ya kuondoa madoa kwenye viatu

Mahitaji

1*limao

2*magadi soda

3*kaustiki

   Uandaaji

1*kamua limao kupata juice yake

2* loweka kaustiki kilo moja kwa maji Lita 5

Utengenezaji

Andaa ndoo Lita 10 weka maji ya kaustiki Lita 1

Kisha weka magadi soda vijiko 5 vya chakula

Kisha weka maji ya limao robo Lita kisha koroga kwa dakika 3

Baada ya hapo tayar kwa matumizi

  Matumizi

Kusafishia viatu

Kusafishia sinki iliokua na uchafu usio toka

Ukitaka kunipa ushauri nitafute innocence kesho. Kama mnanijali naweza hata kujiua

UTENGENEZAJI WA MISHUMAA

*MISHUMAA*

Malighafi na Vifaa

*Mafuta ya taa waxi/ Nta (Paraffin wax)*

*Asidi boriki na Stearine*

*Rangi (ukipenda)*

*Pafyumu (ukipenda)*

*Utambi / uzi*

*Umbo (mould) ya mshumaa*

*Jiko  la  mafuta  ya  taa/ mkaa na sufuria na vijiko vya chakula*

*Vifungashio vyenye lebo*

*Utengenezaji*

Utambi
Changanya asidi boriki vijiko 5 vya chakula na maji vijiko 4 vya chakula
Koroga kwa dakika 5
Tumbukiza utambi ukae kwa dakika 5
Anika ukauke
Mshumaa
Andaa maumbo  ya mshumaa

Weka utambi katikati ya chombo kwa kushikiza na ute wa mshumaa na funga utambi

Weka sufuria jikoni, changanya nta kilo 1, stearine vijiko 4, chemsha  
Changanya rangi, parfyumu, asidi na koroga hadi mchanganyiko uyeyuke
Epua, mimina mchanganyiko kwenye maumbo na weka kwenye kivuli hadi mchanganyiko unaganda
Ondoa mshumaa taratibu kutoka kwenye maumbo

Vifungashio na lebo
Fungasha mishumaa kwenye chombo kitakachomvutia mteja aweze kununua

*Bandika lebo kwenye chombo kuhusu bidhaa*

Aina, mchanganyiko wa malighafi, uzito au idadi, maelekezo ya matumizi na uhifadhi,
jina na anwani ya mtengenezaji, namba ya simu na barua pepe
Onyesha nembo za ubora kamaTBS na GS1 (Barcode)

Fuata maelekezo na taratibu za TBS

Hati na vibali
Onana na mamlaka husika kupata vibali na vyeti:

TBS and GS1
Pata hati ya TCCIA kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi

Fuata taratibu za uuzaji bidhaa nje ya nchi

JINSI YA KUTENGENEZA MAFUTA YA MGANDO

*JINSI YA KUTENGENEZA MAFUTA YA MGANDO*.

*tujifunze namna Kutengeneza mafuta ya mgando(meupe)*

*Mahitaji*

Micro wax kilo moja
White oil Lita mbili
Perfume vijiko viwili
Kutengeneza
Chukua sufuria kavu bandika jikoni weka micro wax kilo moja
Kisha white oil Lita mbili iache mpaka ichemke kwa muda mfupi utaweka perfume vijiko viwili mimina humo
Baada ya hapo utaiacha ichemke kidogo kisha isikae sana ichemke mana italipuka kwahyo wakati unaipika moto uwe wa wastani kisha acha ipoe ibakie ya uvuguvugu
Mpaka hapo itakua imekamilika mgando wako weka lebo

Thursday, 25 October 2018

JINSI YA KUPAKA MAKE UP USONI

*JINSI YA KUPAKA MAKE UP USONI*

Tunapenda sana urembo hasa wa uso lakini kuna mambo muhimu ya kuzingatia ili kupendezesha uso wako na kuonekana unavutia zaidi popote utakapotokelezea na watu wakasema waoohh you look gorgeous.
Sasa leo nimekuja na TIPS chache za kukufanya wewe uonekane mrembo zaidi kila wakati .

*1. USO*

osha uso wako kwa maji ya uvuguvugu na sabuni. kausha vzuri na kitaulo laini.
kama unatumia cleanser yoyote ni vizuri zaidi kuondoa uchafu kwenye uso wako kwa kutumia pamba na baada ya hapo osha tena uso wako kwa maji tuu ya uvuguvugu na ujikaushe.

*3. POWDER*

Paka powder inayoendana na ngozi yako juu ya foundation,hakikisha unasambaza uso wako wote pamoja na sehemu za shingo ili rangi iwe sawa na uso. kwa kutumia spounge au brush inayohusika.

*4 MACHO*

uso wako ukiwa tayari ,andaa vifaa kwa ajili ya macho yako na nysi zako ambazo zitakua tayari zimechongwa vizuri,hapa inahitajika wanja brown/ mweusi ,eyeliner na eye shadows chagua rangi ianyoendana na ngozi yako au inayoendana na nguo utakazovaa ili kuleta maana.

chora vizuri nyusi zako kwa wanja wa brown , na upake eyeliner juu ya kope zako ili kuzipa rangi,then ndo unakuja kuweka eyeshadows ,ni vizuri kupaka eyeshadow za unga kuliko za maji .yani namaanisha kavu au za vumbi.

*5.LIPS*

kama ni mpenzi wa lipstic za mafuta anza kwa kupaka lipshine ili uweze kulainisha lips zako then paka lipstick yako kulingana na rangi ulioichagua then paka na lipliner pembezoni mwa lips zako ili kuwekea ukingo.na kama ni mpenzi wa lipstick kavu haina haja ya kupaka lipshine paka lipliner yako then paka lipstick yako rangi uipendayo .

*LIPSTICK KAVU*

Baada ya kufuata hatua hizo tano hapo juu mdau wangu utakua tayari kwa mtoko wako

*ZINGATIO*

Katika upakaji wa foundation na Powder unatakiwa uzingatie mda sababu kuna foundation nyingine ni kwa ajili ya mchana na nyingine ni kwaajili ya mitoko ya usiku hivyo basi ni muhimu kuzingatia na kuwa na make up ya mchana  na ya usiku kuepuka mchanganyiko.
NB  baada ya kumaliza shughuli zako hakikisha hulali na makeup yani wakati wa kulala hakikisha unanawa uso wako vizuri au unaweza futa kwa kutumia make up remova

‬: *NJIA FUPI YA RAHISI YA UPAKAJI WA MAKEUP*

ni concealer hiyo unaipaka usoni huku ukizungurushia kwenye weusi wa machoni na ule wa madoa ya chunusi .


ni foundation hiyo unaipaka uso wote hii inaziba zile alama nyeusi na kuonekana una rangi moja bila madoa kuonekana.


ni powder tumia brush kupaka powder yako utapata muonekano mzuri
hakikisha unachagua makeup inayoendana na ngozi yako maana wengine huwa wanakosea makeup ya mweupe anapaka mweusi na ukiwa wapaka makeup unatazama na shingo yako kama rangi ya usoni na shingoni ni sawa.wengine wanakoleza makeup usoni wanasahau shingo zao.

Kabla hujaanza kujihusisha na mambo ya makeup ni vitu vingi sana unakuwa hujui na nadhani kuwa bado wapo wale wasiojua utaratibu wa makeup vizuri, kama vile makeup products au makeup tools..na hivyo kuna wengine bado wanatumia wanja wa kawaida kujazia/kuchorea nyusi zao, hiyo pia ni sawa lakini brow powder ndio better zaidi.

*Jinsi ya kujaziliza*

kuchora nyusi zako.
Uwe na wanja wa powder au wa jel, eyebrow brush na concealer ( hii ya mwisho sio lazima maana mimi siitumii natumia foundation na wanja wangu unakaa vizuri tuu).

Anza kwa kuzichana nyusi zako kwa kutumia brush au kitana kidogo sana ili nyusi zikae kwenye mpangilio mzuri, then chukua brow brush yako na uchukulie wanja wako wa powder kisha uanze kupaka.
Kama haupo vizuri katika kupaka unaweza kutumia eyebrow shaper na uchore shape inayokufaa

Halafu chukua foundation yako ili usawazishe ile iliyotokeza/kunyoosha ule brow powder. Tumia concealer brush kupaka mstari mwembamba ulionyooka ukifuatisha uliyochora au kujaziliza nyusi zako. Fanya hivi kwa juu na chini kisha sawazisha vizuri.

Hapa chini ni njinsi ambavyo unaweza kuchora mistari ya namna unavyotaka wanja wako uwe. Mimi kwenye kuchora hiyo mistari huwa natumia wanja wa kawaida huu wa penseli halafu katikati humo ndo naweka wanja wangu wa poda au jel.

Hapa kuna wanja wa poda na wanja wa jel
Mimi natumia zote mbili kutegemea na sehemu ninayoenda na event husika. Wanja wa jel unakaa sana kuliko wa poda. Huo wa jel hata ukitokwa jasho wenyewe hautoki mpaka utakaponawa uso na sabuni

Hii ndio eyebrow shaper. zinakuwa 3 ndani ya pakti yake na zinakuwa za shape tofauti. Kwahiyo wewe mwenyewe utachagua shape unayoipenda kutumia.

DAWA YA VIDONDA VYA TUMBO

*Dawa ya vidonda vya tumbo (gastric and duodenal ulcers)*

*Matango*

Tengeneza juisi ya matango na kunywa kila kwenye mlo wako.

*Matumizi*

Glasi 1 kila siku kwa muda wa mwezi 1.

*Bilinganya*

Katakata bilinganya vipande vidogo vidogo, chemsha na tia chumvi kidogo.

*Matumizi*
Kula mara 2 kila siku kwa muda wa mwezi 1.

*Kabichi*

Kabichi ½ kilo
Maji ½ lita
Katakata kabichi vipande vidogovidogo, tia maji na chemsha hadi maji yawe ¼ lita tu.

*Matumizi*
Kunywa maji yote baada ya kupoa, mara 2 kila siku kwa mwezi 1.

*Ndizi*

Ndizi 2 za kupika na maziwa glasi 1 mara 4 kama chakula pekee kwa muda wa siku 14.

*KUMBUKA*

Kabichi lina kemikali inayosaidia kuondoa vidonda vya tumbo

Asali na mdalasini inatibu maumivu ya tumbo pia hutibu vidonda vya tumbo kwenye shina la vidonda
Ili kupunguza makali au kujiepusha kabisa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo,

unapaswa kujiepusha na tabia ya kula na kushiba kupita kiasi, kwa sababu kushiba sana huchochea uzalishaji wa asidi nyingi wakati wa usagaji chakula tumboni.

Mbali na hilo, vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi na vyenye kiwango kidogo sana cha kamba lishe, imethibitika kuwa husababisha madhara mengi tumboni.

Hebu tuangalie aina ya vyakula anavyopaswa kula au kuviepuka mgonjwa ili kupata nafuu na kuishi bila kusumbuliwa nao:

*VYAKULA VYENYE VIUNGO VINGI*

Epuka ulaji wa vyakula vilivyopikwa na kuungwa viungo vingi vya aina mbalimbali, kama vile pilipili kali za aina zote na viungo vingine vyenye ladha ya ukali ambavyo hutiwa ndani ya mboga ama chakula ili kuongeza ladha.

*POMBE NA KAHAWA*

Pombe na kahawa au vinywaji vingine vyenye caffeine', vinaweza kuleta matatizo kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na kwa mtu asiye navyo anaweza kupatwa na tatizo, hivyo ni vyema kuepuka au kutumia kwa kiasi kidogo vinywaji hivi. Kimsingi vinywaji hivi huongeza asidi tumboni na hivyo vinaweza kusababisha vidonda au kuzidisha maumivu kwa anayeumwa.

*ULAJI CHUMVI*

Utafiti uliowahi kufanywa nchini Marekani umeonesha kuwepo kwa uhusiano kati ya ulaji chumvi na vidonda vya tumbo. Mgonjwa anashauriwa kuepuka ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi, hususan vyakula vya kusindika ambavyo huwekwa chumvi nyingi ili visiharibike haraka. Pia jiepushe na kuongeza chumvi kwenye sahani wakati wa kula.

*MAFUTA YA SAMAKI*

Baadhi ya utafiti unashauri wagonjwa wa vidonda vya tumbo wale mafuta yatokanayo na samaki (Omega-3 fats) ambayo yameonekana kutoa ahueni kwa wagonjwa. Na kwa mtu ambaye si mgonjwa atakuwa anajiwekea kinga dhidi ya vidonda vya tumbo na magonjwa mengine ya tumbo.

*VITAMINI NA MADINI*

Ulaji wa vyakula vyenye madini na vitamini kwa wingi husaidia sana kuleta ahueni kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo na kutoa kinga kwa wale ambao hawajaathirika. Wataalamu wa lishe wanashauri kupenda kula matunda na mboga za majani kama vile karoti, juisi ya kabeji, ndizi mbivu, na matunda mengine yenye vitamin C, halikadhalika maziwa ya mbuzi, jibini na cream za maziwa huleta ahueni.

*STAILI YA MAISHA NA VIDONDA VYA TUMBO*

Licha ya kusabisha Saratani, uvutaji sigara pia huongeza hatari ya mtu kupatwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, hivyo ni sababu tosha ya kuacha uvutaji sigareti. Japo msongo wa mawazo unaweza kuwa vigumu kuuhusisha moja kwa moja na vidonda vya tumbo, lakini maisha ya wasiwasi, ukichangaya na ulaji mbovu, huweza kusababisha ugonjwa huu, hivyo kama unataka kujiepusha au kupunguza makali ya ugonjwa huu, ni muhimu kuzingatia ulaji sahihi na kuishi maisha ya furaha

Friday, 19 October 2018

CAGE ZA UZALISHAJI WA SAMAKI KATIKA GHUBA YA ZIWA VICTORIA

Maeneo ya Cage katika uzalishaji wa Ghuba ya L. Victoria, wawekezaji wa kirafiki kwenye utamaduni wa ngome wanakaribishwa katika miili ya maji ya Tanzania. Utafiti huu unaonyesha ramani ya haraka ya maeneo yote ya ngome yaliyo na uwezo katika ziwa huku ikilinganisha eneo la jumla la maeneo na kuweka mipaka ya matumizi ya kulisha halali kwa siku. Maeneo yaliyotambuliwa yenye makadirio ya eneo yanaweza kutangazwa ili kuvutia wawekezaji wanaofaa zaidi na wa kirafiki. Marejeleo ya Boyd CE (2007). Kuongezeka kwa uzalishaji wa maji katika Uganda.Dafu ya uvuvi na aquacultures Allied. Chuo Kikuu cha Auburn, Alabama, USA. FAO (2006) Mapitio ya kikoa juu ya maendeleo ya majini katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Mzunguko wa Uvuvi wa Fisheria No. 1017 / 4.Rome, Italia, 93pp. Heuch PA, Bjorn PA, Finstad B, JC Holst, Asplin L, Nilsen F. (2005). Mapitio ya Mpango wa Taifa wa Hifadhi ya Norway juu ya Salmon Lice kwenye Salmonids T: Matokeo ya salmonids ya mwitu. Ufugaji wa maji, 246: 79- 92. Hindar K, Fleming IA, McGinnity P, Diserud O. (2006). Madhara ya kiumbile na ya kiikolojia ya kilimo cha lax kwenye saum ya mwitu: mfano kutoka kwa matokeo ya majaribio. Jumuiya ya ICES ya Sayansi ya Marine, 63: 1234-1247. Kashindye BB, Nsinda P, Kayanda R, GW Ngupula, Mashafi CA, Ezekiel CN. (2015) Impact ya mazingira ya utamaduni wa ngome katika Ziwa Victoria: kesi ya Shirati Bay Sota, Tanzania. Springer Plus (2015) 4: 475. Krkosek M, Lewis MA, Volpe JP. (2005). Mienendo ya uhamisho wa panya ya baharini kutoka kwa shamba hadi saum ya mwitu. Mahakama ya Royal Society B, 272; 689-696. Ngupula GW, Kayanda R (2010) Benthicmacrofauna muundo wa jumuia, wingi na usambazaji katika maji ya Tanzania na Uganda ya pwani na pwani ya Ziwa Victoria. Afr. J. Aquat. Sci. 185-192 Ngupula GW, Ezekieli CN, Kimirei IA, Wafanyabiashara E, Kashindye BB (2012) Tabia ya kimwili na kemikali ya maji ya ndani ya Tanzania na Ziwa Victoria katika 2005-2008. Afr. J. Aquat. Sci. 37 (3): 339-345 Masser M (2008) Je, utamaduni wa ngome ni nini? Mchapishaji wa SRAC No. 16

Mbuga ya Cage katika Ghuba ya Mwanza ya L. Victoria Mradi huu una lengo la kuchunguza maeneo yanayofaa kwa ajili ya kilimo cha samaki katika ngome ya Mwanza ya maji ya Ziwa Victoria. Kwa mujibu wa Sheria ya Uvuvi Nambari ya 22 ya 2003 na Kanuni za 2009, maeneo ya Nyashishi Bay, Nyegezi Bay, Kasomeko Bay, Igalagala, Gabalema A na B, Saanane Island, Butimba Bay, Kasimiko Bay, Shady Bay na Nganza Bay katika Mkoa wa Mwanza ni alama kama makao muhimu kwa ajili ya kuzaliana na samaki kwa sababu ya watoto. Kwa hiyo katika utafiti huu, isipokuwa kukiondoa maeneo yenye matumizi yanayotofautiana ikiwa ni pamoja na maeneo ya pwani kwa madhumuni ya burudani; pia maeneo yaliyotaja hapo juu hayakufuatiwa kwa kusudi. Vigezo vya utaratibu wa uteuzi wa tovuti na tathmini Kwa upande wa uteuzi wa tovuti na tathmini, TAFIRI inaweka aina mbili za maeneo kwa ajili ya kilimo cha samaki ya ngome katika ziwa. Hiyo ni maeneo ya mitambo ndogo au ya kati ya ngome (mashamba madogo au ya kati) na maeneo ya mitambo kubwa ya ngome (mashamba makubwa). A. Maeneo yaliyowekwa kwa mashamba madogo au ya kati ni:  Maeneo karibu na bahari na umbali mdogo wa 300 m kutoka pwani. Hii ni kwa sababu maeneo yaliyo karibu na maeneo mengi na karibu sana na pwani ni muhimu kama misingi ya kitalu na kuzaliana kwa samaki wengi wa ndani.  Maeneo yenye kina cha chini cha 7.0 m kuruhusu kibali cha ardhi cha 3.0 m.  Maeneo yenye uonekano wa chini wa 1.2 (120cm) hadi 1.5 m (150cm) na kwa namna fulani kufunguliwa kwa maji ya maji (sawa na upepo uliopo) kusafirisha uchafu kutoka mabwawa. Hata hivyo, maeneo yaliyo wazi sana kwa mikondo ya maji si nzuri kwa ajili ya kukaa kwa mabwawa kama mabonde ya nguvu ya maji mengi ya kuondokana na mfumo wa ngome inayosababisha hasara kubwa.  Maeneo yenye oksijeni ya kiwango cha chini (DO) ya 5mg / l kwa maji ya chini.  Maeneo ya mbali na chanzo cha uchafuzi wa mazingira (takriban umbali wa kilomita 1000). B. Maeneo yaliyowekwa kwa mashamba makubwa ni:  Maeneo yenye kina cha chini cha 30.0 m  Maeneo yenye umbali mdogo wa 300 m kutoka pwani ili kuepuka kuingiliwa na shughuli za kitalu na uzalishaji wa samaki wengi wa ndani.  Maeneo yenye uonekano wa chini wa 2m (200cm), hata hivyo sio wazi sana kwa mikondo ya maji yenye nguvu kama miamba inaweza kuharibu mabwawa.  Maeneo yenye oksijeni ya kiwango cha chini (DO) ya 5mg / l kwa maji ya chini.  Maeneo ya mbali na chanzo cha uchafuzi wa mazingira (takriban umbali wa kilomita 1000). 2

imekuwa kutoa huduma za ugani kwa vikundi vyote vya wakulima wa samaki na wawekezaji binafsi (aina nyingine ya PPP). 5.4 Mari - Utamaduni Mari - utamaduni unahusisha hasa kilimo cha samaki. Mari - utamaduni ni mpya katika mazoezi katika Wilaya ya Bunda. Hadi sasa inafanyika tu na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) (Huduma ya Taifa) kambi ya Bulamba. Uzoefu wa Bulamba unaweza kupatikana katika vijiji vya Karukekere na Kasuguti na maeneo mengine. Kwa mfano, Karukekere ni eneo ambalo lina hali muhimu kama vile kuwepo kwa kizuizi cha upepo kinachopunguza dhiki kwa samaki, kina cha maji zaidi ya mita tano kina na huru kutoka kwenye njia za usafiri wa uvuvi. Uwezo wa uvuvi wa ngome ni mdogo katika kijiji hiki na kama jitihada hizo zinaendelea kufundisha walengwa. Ili kufikia mwisho huu, kujenga uwezo katika cage kufanya ni required ili kuhakikisha kuwa mabwawa ni ya viwango vinavyotakiwa (Bamba 5.2). Bonde la 5.2a: Ngome ya samaki Bulamba, Bonde la Wilaya ya Bunda 5.2b: Ngome ya samaki Mauritius Mabwawa ya mafua ni zaidi ya kupendezwa kwa sababu hakuna kusukuma maji. Mabwawa yanapaswa kuwekwa karibu mita 400-500 mbali na pwani na kina cha mita tano. Kuhifadhi dalili itategemea ubora wa maji (ni mazoezi ya kufanya maji ya majaribio juu ya uzazi wa asili wa mwili wa maji. Chakula cha samaki kinachotolewa katika mabwawa hutegemea uzito wa mwili wa samaki, na kama chakula cha ziada kinachohitajika. Wanapaswa kuzingatia aina ya ufugaji wa Cage Utamaduni unaofaa kwa uwekezaji wao .. Mbinu za utamaduni kulingana na wiani wa kuhifadhi, upatikanaji wa chakula cha asili katika maji na uwepo wa ugavi wa bandia ni kama ifuatavyo: • Utamaduni mkubwa wa ngome - kiwango cha hifadhi kitakuwa juu ya pcs 20 (samaki) kwa kila sq. M (hakuna chakula cha ziada kinachopewa); • Utamaduni wa ngome yenye nguvu sana - kiwango cha hifadhi itakuwa bout 50 - 80 kwa sq m, na feeds za ziada zinazotolewa [• Kiwango cha kuzalisha utamaduni wa ngome - kiwango cha kuhifadhiwa kitakuwa takribani 200-500 kwa kila sq m na vidonge vya ziada (pellets).

Tujifunze kuhusu ufugaji wa samaki wa kisasa ambao hufanyika kwenye mabwawa ya kuchimbwa au visima na vitu vingine vinavofanana na hivyo.

Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao wanaweza kufugika kwa urahisi au ugumu kidogo tu na aina hizo wapo wale ambao sio wa kuzaliana(monosexual) na wale wa kuzaliana(heterosexual)

Urahisi hapa uko zaidi kwenye kuwafuga wasiozaliana sababu hawaongezeki wakati wale wanaozaliana utakuwa na utaratibu wa kuhamisha fishling(vifaranga) sehemu nyingine.

Rasilimali muhimu za kuwa nazo ili kufanikisha shughuli hii ni eneo la ardhi,maji, rasilimali watu na rasilimali fedha.Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni kwa namna gani bwawa lako liwe,aidha la kujengea na cement,kutandika plastic au kuchimba na kulitumia hivyohivyo.Bwawa huchimbwa/kujengwa kwa kuwa na sakafu yenye ulalo kiasi(gentle slope/gradient)

Wapo samaki aina ya Sato(Tilapia),Kambale(African catfish) na wengine aina ya pangasius ambao hufugwa kwa wingi sana.
Unahitaji samaki 7-8 katika meter moja ya mraba(1m^2) ,kwa maana hiyo kama una meter za mraba 600 nasi unaweza kufuga samaki 4500.Haishauriwi kulundika samaki kwenye eneo dogo kwani itawasababishia ukosefu wa hewa(oxygen).Ingawa zipo njia za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa kwenye mabwawa.

Ukishachimba bwawa lako(aidha na kulijengea) unaingiza maji kwenye bwawa hakikisha yamekaribia futi 2.5 mpaka kujaa full.Itakubidi kufanya liming(kumwagia chokaa bwawa kabla ya kuweka maji ili kuua bacteria hatarishi kwa maisha na afya ya samaki wako) pia unahitajika kuyarutubisha hayo maji kwa kuchanganya na mbolea(kama ya ng'ombe na za viwandani pia ingawa haishauriwi sana) na kusubiria kwa muda usiopungua siku 21 au zaidi.Unafanya hivi ili kuweka mazingira ya chakula asili(natural foood) kwa ajili ya samaki kujitengeneza,vyakula hivo hua katika hali ya mimea na viumbe wadogo(microorganisms)

Upatikanaji wa vifaranga vya samaki,hapa inakubidi uwe makini sana kama umeamua kuzalisha sato,changamoto kubwa ya sato ni kupata mbegu ambayo under right conditions vifaranga vitaweza kua samaki wenye uzito wa kutosha(miezi 6 awe at least 500grams au zaidi).Mbegu ya sato hupatikana kwa bei rejareja ya sh 300 na kambale sh 500 kwa kifaranga kimoja.Wapo wazalishaji wengi wa mbegu za vifaranga wa ndani na nje ya nchi ila kwa Tanzania nimewakubali Tanzania Fisheries Research Institute(TAFIRI) Nyegezi,Mwanza(Nimefwatilia performance yao shambani).

Ulishaji wa vifaranga vyako ,chakula chao kinategemea na uzito wao mfano samaki hula 5% ya uzito wake wa mwili akiwa mdogo na 3% akiwa mkubwa.Hapa tunaongelea ulishaji wa chakula cha ziada(supplement food),sababu cha asili amekipata kwenye ile mbolea ulioweka.Kama una vifaranga 100 vyenye gram 10 kila kimoja basi utahitaji gram 50 kuwalisha.

Itakuchukua Miezi 6-9 kuanza kuvuna samaki wako ambao unaweza kuwauza kulingana na uzito au au njia utayoona inakufaa.Samaki wengi wa kwenye mabwawa wanavunwa kwa kutumia nyavu au kumwaga maji yote nje ya bwawa.Masoko yake haya samaki ni pamoja na supermarkets, wafanyabiashara sokoni na mitaani pamoja na watu binafsi.










 

yapatikane. Chanzo
chaweza kuwa mto au chemichemi. (Maji ya mvua hayaaminiki, wakati yale ya
bomba ni ya ghali sana kutokana na kuyalipia kwa mamlaka husika).

2. Udongo unaofaa ni ule unaotuamisha maji, kama vile wa mfinyanzi au mchanganyiko
wa mfinyanzi na tifutifu. Mchanga mtupu haufai kwani huruhusu maji kunywea
kirahisi.

3. Mteremko ni vema usiwe mkali sana, ila uwezeshe maji kutiririka kuingia na kutoka
bwawani. Eneo la tambarare kabisa si zuri sana, kwani utafanya uchimbaji wa bwawa
kuwa kama kisima na haitakuwa rahisi kuondoa maji toka bwawani itakapo hitajika
ambalo si zuri kwa ufugaji bora wa samaki.

4. Ni vizuri eneo liwe karibu na nyumbani ili kudhibiti wezi na maadui wa samaki, pia
huwezesha kutoa huduma kwa urahisi.

CHAGUO LA UMBO NA UKUBWA WA BWAWA

1. Umbo na ukubwa wa bwawa hutegemea sura na mwinuko wa eneo husika na eneo
alilonalo mfugaji.

2. Kwa kawaida umbo lolote hufaa kwa uchimbaji wa bwawa, lakini, ili kurahisisha
uvunaji, umbo mraba au mstatili upendekezwa zaidi.

3. Vile vile, ukubwa wa bwawa hutegemea ukubwa wa eneo husika, uwingi wa maji na
uwezo wa mkulima.

4. Bali, ili kupata pato la kuridhisha na kurahisisha utoaji huduma kama vile kulisha,
inapendekezwa kuwa ukubwa wa bwawa ni vema liwe na upana wa kati ya mita 10 na
mita 20 na urefu wa kati ya mita 20 na mita 30. Umbo la mraba au mstatili huvutuia
zaidi.

HATUA ZA MUHIMU KATIKA UCHIMBAJI WA BWAWA

Fyeka mahali pa kujenga bwawa.
Pima bwawa na weka mambo.
Ondoa udongo wa juu (mbolea, mchanga, mizizi n.k.) na weka pembeni.
Chimba msingi wa kuta; upana futi 1 na kina futi 1½.

Jaza huo msingi kwa udongo wa mfinyanzi na kuushindilia. Hii itasaidia kupunguza
kunywea kwa maji.
Anza kuchimba bwawa na kujenga kuta kwa kutumia udongo tu (bila mchanga,
mawe, miti, mizizi n.k.) ili kupunguza kunywea kwa maji kutoka bwawani baada ya
kulijaza.
Shindilia kikamilifu udongo unaowekwa kwenye kuta.
Jaribu kusawazisha juu ya kuta na chonga kuta ziwe na mtelemko wa kiasi, zisiwe
wima kwani zitamomonyoka kirahisi.
Chonga sakafu ya bwawa kwa kuiwekea mteremko wa kiasi kutoka upande wenye
kina kifupi kwenda upande wenye kina kirefu..
Weka bomba la kuingizia maji na bomba la kuondolea maji bwawani.
Rudishia udongo wa juu uliouondoa hapo awali kwenye kuta za bwawa.
Panda majani yanayotambaa kama mbudu ukutani kuzuia mmomonyoko.
Jenga wigo wa kuweka mbolea ya samadi au Mbuji ndani yake
Jenga uzio, seng’enge au panda miti yenye miba kuzunguka bwawa kuzuia maadui
wa samaki kuingia bwawani.
Tawanya mbolea na majivu chini ya bwawa ili kuua wadudu wanaoweza kuwamo
ndani ya bwawa kabla ya samaki kupandwa bwawani.
Baada ya hatua hizo kukamilika, sasa jaza maji bwawani.

MAJI

Maji ni moja ya kigezo kikubwa sana kwenye biashara ya ufugaji wa samaki.
tulibahatika kukutana na msemo mmoja kutoka kwa wataalamu wengi na wafugaji pia
kwamba maji ni kila kitu katika ufugaji wa samaki.
Yaani usipozingatia hapa basi ni ngumu kupata matokeo uliyoyatarajia.
itaendelea kesho na urutubishaji wa bwawa la samaki na njia mbalimbali za urutubishaji wa bwawa

UTUNZAJI WA NG'OMBE WAKUBWA

UTUNZAJI WA NG’OMBE WAKUBWA
Kundi hili linajumuisha ng’ombe wenye mimba, wanaokamuliwa na madume.  Mfugaji anapaswa kutunza vizuri ng’ombe wake wakubwa kwa lengo la kumpatia malisho bora na maji safi ya kutosha kila siku.  Mambo muhimu ya kuzingatia katika utunzaji wa ng’ombe wakubwa ni pamoja na:-
-           Ng’ombe apatiwe majani makavu (hei) wastani wa kilo 10 au majani mabichi kilo 40 kwa siku kutegemeana na uzito.  Iwapo malisho hayatoshi hususan wakati wa kiangazi apewe masalia ya mazao (viwandani na mashambani) kama molasisi, mabua, maharage, mpunga n.k
-          Ng’ombe apewe vyakula vya ziada (pumba, mashudu, madini mchanganyiko, unga wa mifupa na chokaa) kulingana na hatua na kiwango cha uzalishaji na
-          Ng’ombe apatiwe kinga na tiba ya magonjwa kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo.

UPANDISHAJI
Mfugaji anapaswa kumpandisha ng’ombe kwa umri na wakati muafaka ili kuepuka matatizo ya uzazi na pia kuhakikisha anapata ndama bora na maziwa mengi.  Mambo muhimu ya kuzingatia ni pamoja na
-           Mtamba apandishwe akiwa na umri wa miezi 17 -24 na uzito wa kilo 230 – 300 kwa ng’ombe wa kigeni na umri wa miezi 30 – 36 na uzito wa kilo 200 kwa ng’ombe wa asili. 
-          Ng’ombe aliyekwisha zaa apandishwe siku 60 baada ya kuzaa na
-          Siku 18 – 23 baada ya kupandishwa, ng’ombe achunguzwe kama ana dalili za joto ili apandishwe tena.  Iwapo ng’ombe ataendelea kuonyesha dalili za joto baada ya kupandishwa mara tatu mfugaji apate ushauri wa mtaalam wa mifugo.

  UMRI NA UZITO UNAOSHAURIWA KUPANDISHA MTAMBA
AINA YA NG’OMBE
UZITO (KG)
UMRI (MIEZI)
Friesian
240 – 300
18 – 24
Ayrshire
230 – 300
17 – 24
Jersey
200- 250
18 – 20
Mpwapwa
200 – 250
18 – 20
Chotara
230 – 250
18 – 24
Boran
200 – 250
24 - 36
Zebu
200
30 -36




DALILI ZA NG’OMBE ANAYEHITAJI KUPANDWA
Ni muhimu mfugaji akazitambua dalili za ng’ombe anayehitaji kupandwa ili aweze kumpandisha kwa wakati.  Dalili hizo ni pamoja na
§  Kupiga kelele mara kwa mara
§  Kutotulia/kuhangaika
§  Kutokwa na ute mweupe usiokatika ukeni
§  Kupenda kupanda wenzake na husimama akipandwa na wenzake na
§  Kunusanusa ng’ombe wengine
Ng’ombe akionyesha dalili za joto apandishwe baada ya masaa 12, kwa kuhimilisha au kwa kutumia dume bora (kwa mfano, akionyesha dalili asubuhi apandishwe jioni na akionyesha dalili jioni apandishwe asubuhi).

UHIMILISHAJI
Uhimilishaji ni njia ya kupandikiza mbegu kwa ng’ombe jike kwa kutumia mrija.  Faida za uhimilishaji ni pamoja na kusambaza mbegu bora kwa haraka na kwa gharama nafuu, kupunguza gharama za kutunza dume na kudhibiti magonjwa ya uzazi.

ILI MFUGAJI ANUFAIKE NA HUDUMA HII ANAPASWA KUFANYA YAFUATAYO:-
-           Kuchunguza kwa makini ng’ombe mwenye dalili za joto
-          Kumjulisha mtaalam wa uhimilishaji mapema ili kuwezesha zoezi hili kufanyika kwa wakati.
-          Kuchunguza kama ng’ombe atarudi kwenye joto siku ya 18 – 23 baada ya kupandishwa na
-          Ng’ombe aliyepandishwa apimwe mimba siku 60 hadi 90 baada ya kupandishwa.

MATUNZO YA NG’OMBE MWENYE MIMBA
Ng’ombe mwenye mimba huchukua miezi 9 hadi kuzaa.  Katika kipindi hicho chote anastahili kupatiwa lishe bora na maji ya kutosha ili akidhi mahitaji ya ndani aliye tumboni na kutoa maziwa mengi baada ya kuzaa.
Mambo ya kuzingatia ni pamoja na
-           Ng’ombe apewe lishe bora na maji ya kutosha kipindi chote cha mimba
-          Miezi 2 kabla ya kuzaa apewe kilo 2 za chakula cha ziada kwa siku
-          Apewe kinga dhidi ya maambukizi na tiba ya magonjwa
-          Ng’ombe anayekaribia kuzaa, hususani mtamba, azoeshwe kuingia kwenye sehemu ya kukamulia.

DALILI ZA NG’OMBE ANAYEKARIBIA KUZAA
Mfugaji anapaswa kufahamu dalili za ng’ombe anayekaribia kuzaa ili aweze kufanya maandalizi muhimu.  Dalili hizo ni pamoja na
       Kujitenda kutoka kwa wenzake
       Kiwele kuongezeka
       Chuchu kutoa maziwa zikikamuliwa
       Kutokwa na ute mwekundu na sehemu za uke kuvimba na kulegea
       Kuhangaika kulala chini na kusimama na
       Kati ya saa moja hadi mbili kabla ya kuzaa sehemu ya uke hutokwa na maji mengi ambayo husaidia kulainisha njia ya ndama kupita.

HUDUMA KWA NG’OMBE ANAYEZAA
Ng’ombe anayezaa anahitaji uangalizi wa karibu ili kuhakikisha usalama wa ng’ombe na ndama anaezaliwa.  Mambo ya kuzingatia ni pamoja na yafuatayo:-
-           Sehemu ya kuzalia ng’ombe iandaliwe kwa kuwekwa nyasi kavu na laini na iwe safi.
-          Ng’ombe ahamishwe sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuzaa mara baada ya dalili za kuzaa kuonekana na
-          Ng’ombe aachwe azae mwenyewe bifa usumbufu

MFUGAJI APATE USHAURI/HUDUMA KUTOKA KWA MTAALAM IWAPO MATATIZO YAFUATAYO YATAJITOKEZA:-
-           Ng’ombe kushindwa kuzaa kwa masaa mawili hadi matatu baada ya chupa kupasuka
-          Kondo la nyuma kushindwa kutoka masaa sita baada ya kuzaa
-          Kizazi kutoka nje na
-          Ng’ombe kushindwa kusimama baada ya kuzaa

MATUNZO YA NG’OMBE ANAYEKAMULIWA
Ng’ombe anayekamuliwa anahitaji kupata chakula kwa ajili ya kujikimu na cha ziada kwa ajili ya uzalishaji wa maziwa.  Ili kukidhi mahitaji ya uzalishaji wa maziwa ng’ombe
v  Apewe chakula cha ziada kwa kiwango cha kilo 1 kwa kila lita 2 – 3 za maziwa anayotoa.
v  Apewe madini na virutubisho vingine kulingan ana mahitaji
v  Apewe maji mengi kwa vile ni ya muhimu katika kutengeneza maziwa.
v  Aachwe kukamuliwa siku 60 kabla ya kuzaa.  Uachishwaji huu ufanywe taratibu ili ifikapo siku ya 60 kabla ya kuzaa ukamuaji usitishwe.
v  Baada ya kusitisha kukamuliwa apewe kilo 2 za chakula cha ziada kwa siku hadi atakapozaa na
v  Apatiwe kinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa na tiba kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo

KILIMO CHA MAHARAGE YA NJANO

KILIMO CHA MAHARAGE YA NJANO.

Kilimo cha maharage ni rahisi na kinalipa sana kikifanyika kwa utaalamu. Gharama nafuu na competion ya soko ni almost zero. Huhitaji kusafiri, kinachofanyika ni kuwaita wateja waje shamba watuniashane misuli mbele yako bila dalali kisha ww ndo una decide whom to trade with!

Ekari moja ya maharage ya njano unaweza pata gunia 20 - 30. na gunia moja kwa sasa ni shs 270,000.

Shamba la maharage kama unalima kwa kumwagilia unaweza lima mara tatu kwa mwaka . Hii ina maana ukilima ekari moja tu utakua na uhakika wa kipato cha Milioni 5.5 kila baada ya miezi minne, na kama ukilima ekari kumi basi wewe kila miezi minne utakua unaingiza milioni 55. Hata uwe mlevi vipi huwezi maliza hizo helaa na ni lazima baada ya mwaka mmoja tu mabenki yataanza kukuheshimu na status yako itabadilika for good. Sasa baada ya kukupagawisha na kukuchanganya juu ya mill 55 kila baada ye miezi minne ndugu mdau wa CHAKULACOM na mkulima mwenzangu sasa twende tukalichambue harage la limwa vipi

Maharage ni lishe ya pili kwa umuhimu nchini Tanzania baada ya mahindi. Maharage yanaweza kuliwa yakiwa
machanga/mateke (green/French beans) na yakiwa mabichi au yamekauka baada ya kukomaa.
Maharage ni chanzo muhimu cha protini kwa binadamu na husaidia udongo katika utengenezaji wa madini ya nitrogen
kutoka kwenye hewa kwa kupitia mizizi ya maharage ambayo husaidiana pamoja na rhizobium/ryzobium bacteria
kwenye udongo. Nitrogen ni muhimu kwa ukuaji na uzalishaji wa mahindi.
Kwa miaka mingi maharage yamekuwa yakilimwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani lakini hali inabadilika kwasababu
soko la maharage limekua, bei yake kuongezeka na mahitaji ya maharage yameongezeka. Hii imesababisha kuongezeka
kwa uzalishaji na biashara ya maharage nchini na nje ya nchi.
Matumizi ya Maharage
Maharage hutumika kama chakula cha binadamu na pia majani yake huweza kutumika kama chakula cha mifugo. Katika
chakula cha binadamu maharage hutumika kama kiambatanishi (mboga) cha vyakula vingine kama vile wali au ugali.
Faida za maharage
a) Mbegu
Mbegu za maharage zina viwango vingi vya protini ambavyo ni muhimu katika kujenga mwili kwa sbababu yanatoa
proein; hivyo hutumika badala ya nyama, madini ya magnesium husaidia katika afya na ukingaji wa moyo kutoka kwenye
maradhi, madini chuma husaidia kuupa mwili nguvu, Vitamin B1 (Thiamin) na Vitamin K huongeza uwezo wa
kumbukumbu hivyo kuwa muhimu kwa watu wenye matatizo ya kupoteza kumbukumbu.
Maharage ni chanzo kizuri cha kupunguza cholesterol mwilini, cholesterol nyingi mwilini ni chanzo cha magonjwa
mengi. Pia maharage husaidia kukinga viwango vya sukari kwenye damu kuongezeka ghafla baada ya mlo, hivyo ni
muhimu sana kwa watu wenye kisukari. Zaidi ya yote vyakula vya jamii ya maharage vimeonekana kupunguza
uwezekano wa kupata mshituko wa moyo. Tafiti za hivi karibuni zimegundua kuwa ulaji wa maharage hupunguza
uwezekano wa kupata saratani (cancer) tofauti na nyama ambayo huongeza uwezekano wa kapata saratani.

i) Majani na maua ii) Maharage iii) Maharage machanga
b) Majani
Majani ya maharage pia huweza kutumika kama mboga na katika baadhi ya jamii za watu nchini, majani mateke ya
maharage huchumwa na kukatwakatwa kisha kupikwa kama mchicha au mboga nyingine yoyote ya majani.
Upandaji wa Maharage
1.Mbegu
Upandaji wa maharage unatakiwa ufanyike katika muda muafaka kutokana na eneo ili kuweza kupata maji ya kutosha
(mvua) na wakati wa mavuno kunatakiwa kuwe na ukavu ili maharage yasiharibikie shambani. Maji mengi yaliyotuama
na ukame siyo nzuri kwa maharage na husababishia mmea magonjwa na kuoza au kukauka� Kuna aina nyingi za maharage ambazo zinaweza kupandwa kwa mfano (Rojo, Mshindi, Pesa, SUA 90 na Canadian
wonder) ambazo ni mbegu zilizoboreshwa, lakini pia kuna mbegu za kawaida zilizopo kwa wakulima ambazo huhimili
baadhi ya magonjwa na wadudu.
Inashauriwa kupanda maharage katika umbali wa (50×20) sentimita 50 (mstari kwa mstari) na sentimita 20 (mmea kwa
mmea), panda mbegu mbili za maharage katika shimo moja, mbegu zinaweza kupandwa katika umbali wa sentimita 3-6
kwenda chini. Kama mbegu moja moja katika kila shimo, nafasi itapungua. Kwa maharage yaliyokuwa vizuri kunatakiwa
kuwe na idadi ya mimea 150,000-200,000 kwa hekta (maharage mafupi), maharage yatambaayo idadi yake ni nusu ya
maharage mafupi kwa hecta. Hekta 1 = ekari 2.471.

2.Mbolea
Mimea huhitaji virutubisho kutoka kwenye udongo ili kuweza kukua na kuzalisha matunda yenye afya. Maharage huhitaji
madini ya phosphorous na potassium ambayo hupatikana kutoka kwenye mbolea hai kama vile samadi, mboji, majivu,
mkojo wa mifugo na mabaki ya mimea. Ni muhimu kufahamu udongo ambao unatarajia kupanda mimea yako ili
kutathmini viwango vya madini yaliyopungua ili kufanya juhudi za kuongeza.
Zaidi ya yote ni vizuri kutumia mbolea hai ambazo zinasaidia viumbe hai huweza kukua na kuendeleza kurutubisha
udongo, kwa mfano mizizi ya maharage husaidiana na viumbe hai (nitrogen fixing bacteria) waishio kwenye udongo
kutengeneza nitrogen. Mbolea za chumvichumvi huharibu na kufukuza viumbe hai kutoka kwenye udongo.
3.Magugu
Inashauriwa kupalilia mimea kabla haijatoa maua. Shughuli hii inatakiwa ifanywe kwa uangalifu ili kukinga mimea
isiharibike kwenye mizizi kwani uharibifu wa aina yoyote huweza kusababisha magonjwa kwa mmea. Inashauriwa
kupanda mimea kwa kuzunguka (crop rotation) ili kupunguza uwezekano wa magugu na mardhi kuweza kushambulia
mimea.
4.Wadudu na magonjwa
Maharage hushambuliwa na wadudu na magonjwa. Miongoni mwa njia
za kuzuia, kukinga na kufukuza wadudu ni kuhakikisha kuwa mimea
ipo katika hali nzuri (imepaliliwa, nafasi ya kutosha na haijaharibika).
Pia kubadilisha aina ya mimea inayopandwa kwenye shamba moja mara
kwa mara husaidia kupunguza uwezekano wa wadudu kuongezeka.
Kwa baadhi ya wadudu kama vile viwavi (African Ballworm) huweza
kufukuzwa kwa kutumia muarobaini au vitunguu saumu. Maji ya
muarobaini ni dawa nzuri sana kwaajili ya kufukuzia wadudu na haina
madhara yoyote kwa binadamu.
5.Kukomaa na Kuvuna
Maharage ya kijani yanatakiwa yavunwe kabla punje za maharage hazijakuwa sana. Hii ni kati ya wiki 7-8 baada ya
kupanda. Maharage makavu huvunwa mara tu kiasi cha kuridhisha cha kukomaa na kukauka kinapokuwa kimefikiwa.
Kwa mfano asilimia 80 ya maharage yakishakomaa na kuanza kubadilika rangi (kukauka) au kwa aina nyingine kusinyaa
yanakuwa tayari kwa mavuno.
Kwa kawaida mmea wote hung’olewa na kuwekwa juani ili uendelee kukauka kisha maharage hutolewa kutoka kwenye
mmea na kuendelea kukaushwa ili kupunguza matatizo wakati wa kuhifadhi. Baada ya kukauka hadi kufikia angalaua
asilimia 12 ya unyevu, maharage yanatakiwa yahifadhiwe kwenye chombo chenye mfuniko kama vile ndoo ya plastiki au
pipa na kuendelea kuyaangalia mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa wadudu hawajaingia na kisha kuyafunika tena.
6.Kilimo mchanganyiko
Ni vizuri sana na inashauriwa kupanda maharage pamoja na mimea ya jamii nyingine kama vile mahindi kwani husaidia
katika kusambaza madini ya nitrogen na kwa maharage yenye kutambaa, hupata sehemu ya kujishikilia au kutambalia.
Maharage yanaweza yakapandwa katikati ya mistari ya mahindi. Pia viazi huweza kupandwa pamoja na maharage.
Inashauriwa kutokupanda maharage pamoja na mimea mingine ya jamii ya maharage (leguminous) kwani husababisha
mimea isiweze kukua vizuri kwasababu ya kutokupata virutubisho vya kutosha na huweza kusababisha matatizo kama �ya wadudu kama nzi weupe.

Mbegu za maharage ya njano F1 za Muda wa siku 85 zinazohimili ukame

FAIDA ZA MKOJO WA SUNGURA NA NG'OMBE

MKOJO WA SUNGURA NA NG'OMBE

Mkojo wa sungura hutumika kama mbolea ya maji katika mimea na unasemekana kuwa na virutubisho vingi muhimu kwa ajili ya mimea hasa  katika mazao ya mbogamboga.
Pia, mkojo huo unatumika kama kiuatilifu asili kwa ajili ya kufukuza wadudu hatari kwa mazao.

Hivi sasa mabanda ya kisasa yanayojengwa  kwa ajili ya kufugia sungura, yamewekewa miundombinu mizuri kwa ajili ya kuvuna na kuhifadhi mkojo wa mnyama huyo.

Mkojo huo huweza kuhifadhiwa katika mapipa. Unaweza kuandaa keni au solo pia kwa ajili ya kumwagilia.

Jinsi ya kuandaa na kuutumia

Mkojo ukishapatikana huweza kuhifadhiwa katika solo na unakuwa tayari kwa matumizi. Kinachoweza kufanyika ni kuchuja mkojo huo na kuondoa uchafu, kisha unakuwa tayari kwa matumizi.

Mkulima atamwagilia maji asubuhi,  kisha kwenye saa tatu asubuhi atachukua mkojo huo na kuuweka katika solo tayari kwa kupiga kwenye mimea.

Atapiga katika maeneo yaliyoathirika au katika majani ya mmea husika, shina la mmea husika. Lakini pia katika udongo wa shamba husika.

Mkojo wa sungura unasifika kuongeza virutubisho kwa mmea lakini pia unasaidia  katika kuondoa wadudu hatari kama wadudu mafuta, inzi weupe, utitiri na kuukinga mmea na magonjwa ya fangasi na bacteria.

Majani ya mwarobaini na mkojo wa ng’ombe

Dawa nyingine ya asili ya kuua wadudu shambani ni mchanganyiko wa majani ya mwarobaini na mkojo wa ng’ombe. Mchanganyiko huu ni nzuri na una matokeo mazuri  katika kufukuza wadudu hatari shambani.

Jinsi ya kuandaa

1. Chukua majani ya mwarobaini kiasi cha kujaza ndoo nne.

2. Chukua mkojo wa ngombe kama lita 20

3. Tafuta kifaa maalumu cha kutwangia majani ya mwarobaini

4. Tafuta mifuko ya saflet inayohifadhia unga ya kilo 25 kisha andaa keni au solo kwa ajili ya kumwagilia kwenye mimea yako.

Baada ya maandalizi haya, chukua majani ya mwarobaini (weka mengi  kiasi cha kujaza ndoo nne za lita 20). Kisha yatwangwe mpaka yawe laini kabisa kiasi cha kutoa maji.

Baada ya hapo, weka majani hayo katika mifuko ya kilo 25 yakiwa yametwangwa vyema. Kisha mfuko huo ukiwa na majani yaliyotwangwa yatatumbukizwa katika ndoo yenye mkojo wa ngombe kama lita 20.

Utaacha kwa siku saba mfuko huo ndani ya mkojo huo, vyote vinaweza kukaa katika ndoo kubwa ya lita 20. Siku ya kutoa majani yatakuwa yamejichuja katika mkojo wa ngombe na kutengeneza harufu kali.

Hapo utachuja kama kuna baadhi majani yameingia katika mchanganyiko huo.

Kisha mchanganyiko unachanganywa na lita 20 za maji masafi tayari kwa matumizi.

Jinsi ya kutumia

Utaweka katika solo mchanganyiko huo kisha utamwagia katika shamba lako. Kama kwenye mmea palikuwa na wadudu utapiga hapo katika wadudu. Piga katika majani ya mmea, shina la mmea na katika udongo kwa ujumla.

Pia, ondoa majani yalioathirika katika mmea mara baada ya kupiga dawa husika.

USINDIKAJI WA NYANYA

*USINDIKAJI WA NYANYA*
(Chachandu ya Nyanya (Stewed tomato))

*USINDIKAJI WA NYANYA* (Chachandu ya Nyanya (Stewed tomato))
Wakulima hupata hasara kubwa sana inayotokana na mazao hayo kuharibika haraka kutokana na uhaba wa soko.

Uzalishaji wa mazao ya aina mbalimbali nchini Tanzania, na kwingineko, umeshika kasi sana kutokana na jitihada zinazofanywa na wakulima katika kuongeza uzalishaji huo.
Hili ni jambo muhimu sana kwa kuwa walaji wanatoshelezwa bila kupata taabu, huku wakulima nao wakipiga hatua kadhaa za kimaendeleo.

Juhudi hizi zinakatishwa tama na ukosefu wa soko la haraka la mboga mboga na matunda, huku wakulima wakiwa hawana namna ya kuhifadhi mazao hayo kwa lengo la kusubiri soko au kwa matumizi ya baadHii ni aina ya kiungo ambacho hutumika kuongeza ladha kwenye chakula, pamoja na hamu ya kula.ae. Wakulima huacha mazao hayo yakioza ovyo, na baada ya kuoza wakulima wanakata tamaa kwa kuwa hupata hasara kubwa kutokana na upotevu huo.

Ni muhimu kwa wakulima na Wajasiriamali kufahamu namna mbalimbali wanavyoweza kuhifadhi na kusindika mazao wanayozalisha, ili wasiingie katika hasara isiyokuwa ya lazima.

Kwa kufahamu hilo, nimewaletea somo la namna ya usindikaji waChachandu ya Nyanya (Stewed tomato))Hii ni aina ya kiungo ambacho hutumika kuongeza ladha kwenye chakula, pamoja na hamu ya kula.
 

*Namna ya kusindika chachandu ya nyanya*

*Dondoo Kiwango cha*
*mahitaji*

yatakayoainishwa hapo chini na maelezo yake ni kwa ajili ya kutengeneza na kupata kiasi cha chupa 12 za nusu (½) lita.

*Mahitaji*
Nyanya sadoline 2
Pilipili hoho kilo 2
Vitunguu maji kilo 1¼
Chumvi vijiko 2 vya chai
Namna ya kuandaa
Osha nyanya na pilipili hoho vizu kwa maji safi
Menya vitunguu vizuri
Katakata vyote kwa muundo wa viboksi vidogo vidogo
Weka kwenye sufuria
Bandika jikoni
Koroga taratibu kwa muda wa nusu saa ili mchanganyiko huo usiungue

*Ufungashaji*
Wakati mchanganyiko ukiendelea kuiva jikoni, hakikisha unaandaa vifungashio/chupa
Ni muhimu kuhakikisha kuwa chupa hizo zimeoshwa vizuri na kuwekwa kwenye chombo maalumu cha kuulia vimelea (Sterilizer)
Weka mchanganyiko wa chachandu kwenye vifungashio kulingana na ujazo unaohitaji ukiwa bado wa moto
Funga chupa/kifungashio kiasi
Rudisha kwenye chombo maalumu cha kuulia vimelea
Acha humo kwa muda wa dakika tano
Ondoa na ufunge vizuri
Pindua chupa/kifungashio mfuniko ukae chini. Hii itasaidia mfuniko kufunga vizuri
Weka nembo tayari kwa mauzo
Inashauriwa kuanza kuuza bidhaa hiyo baada ya wiki moja tangu siku ilipotengenezwa. Bidhaa hii inaweza kuwa salama kwa matumizi ya binadamu kwa kipindi cha miaka 2 tangu ilipotengenezwa.

*Soko*

Bidhaa hii inauzwa na kutumiwa na watu wa kada mbalimbali. Inaweza kuuzwa katika hoteli za kawaida na zile za kitalii, pamoja na maduka ya kawaida ya vyakula vya binadamu.

BIASHARA GANI NI ZURI AMBAYO INALIPA NAWEZA KUIFANYA KWA SASA?

BIASHARA GANI NI ZURI AMBAYO INALIPA NAWEZA KUIFANYA KWA SASA?

Kwa ufupi ni kwamba  Biashara nzuri ni ile unayoipenda na unayoiweza kuifanya vizuri na  kwa ubora tofauti na wengine lakini ni lazima uwe na muda Wa kuisimamia,vinginevyo itafeli.
Biashara nzuri zaidi ni Biashara inayohusika na kutatua matatizo ya watu katika eneo lako unapoishi au unapofanyia kazi. That's all about Business.

Ukitaka kufanikiwa ktk Biashara ni lazima
1.Uipende Biashara yako.
2. Uwe na muda Wa kuisimamia.
3. Uwe na uwezo Wa kuifanya na uifanye kwa uzuri na ubora Wa hali ya juu tofauti na washindani wako.
4.Uwe na Elimu au maarifa sahihi kuhusu Biashara unayotaka kuifanya.
5.Uwe na washauri wazuri ktk Biashara yako yaani Uwe na watu walioifanya na wanaoifanya Biashara hiyo na ambayo wamefanikiwa ktk hiyo biashara. Ni hatari kubwa kuwa na washauri ambao eidha walifeli ktk hiyo Biashara au wasiofanya hiyo Biashara wengi wao watakukatisha tamaa na kukuvunja moyo.

Huu ni mfano hai ambao Mimi Binafsi nauamimi na  nimenufaika nao sana. Nilipotaka kuoa niliwauliza watu ambao wameoa na wanaishi vizuri ktk ndoa zao,nilipotaka kusoma fani ya uinjinia niliwauliza watu waliosoma na kunufaika na Elimu hiyo, nilipotaka kujenga niliwauliza watu waliojenga na nilipotaka kufungua Biashara niliwauliza watu sahihi wanaofanya Biashara hiyo na kamwe sijawahi kujuta ktk maamuzi Yangu namshukuru Mungu kwa hilo.

Angalizo Akili ya kuambiwa changanya na yako. Sio kila ushauri utakufaa ila ni muhimu kutafuta ushauri then baada ya ushauri ukae chini mwenyewe utafakari na ujiridhishe kama ni sahihi ufanye na kama sio sahihi tafuta njia nyingine.

Utajuaje kama ushauri uliopewa na mentor wako kuwa ni sahihi ama sio sahihi?

Akili ya kuzaliwa na kujifunza inakuhusu. Huwezi kufanikiwa ktk jambo lolote kama huna maarifa au Elimu nacho. Tafuta maarifa na Elimu,jifunze ili uelewe vizuri juu ya kitu unataka kufanya kabla ya kufanya maamuzi yako. Hapa ndipo watu wengi hukosea na kutuja baadae. Huwachukia waliowashauri kwa kuwasababishia matatizo ktk Ndoa zao,Biashara zao na hata maisha yao kwa ujumla kwa sababu walichukua ushauri na kufanya walivyoambiwa bila kuchunguza au kutafakari kwanza.

Usikurupuke ktk maisha utajuta na kujilaumu au kuwalaumu wengine bure usipojiongeza.

Katika Maisha ya mafanikio hakuna njia ya mkato. Ukitaka shortcut lazima ujiandae kusubiri maumivu ya majuto baadae. Kutafuta shortcut ktk maisha ni kuogopa kulipa gharama Leo na kusubiri kuja kulipa baadae.

So ukitaka kufanikiwa ni lazima ufuate Sheria,kanuni na miiko ya Mafanikio otherwise usitafute Wa kumlaumu zaidi ya kujilaumu mwenyewe.

DAWA YA KUOTESHA NYWELE

Maligahafi
1* mafuta ya Mnyonyo
2*chumvi
3*yai la kuku wa kienyeji

Utengenezaji

Andaa bakuli safi kisha weka chumvi kijiko 1 cha chai alafu weka yai 1 la kuku wa kienyeji koroga kupata mchanganyiko sawa

Baada ya hapo weka mafuta ya Mnyonyo robo Lita kisha koroga kupata mchanganyiko laini kisha acha sehemu yenye ubaridi kwa muda wa dakika 30+(nusu Saa )
Dawa itakua tayari

     Matumizi

Nyoa kipara kichwa chote na upake kila unapo amka baada ya kuoga na acha mafuta kwa masaa 5 yakiwa kichwani umepaka

Fanya ivyo kwa muda wa siku 12 mfurulizo

UTENGENEZAJI WA DAWA YA KUKUZA NYWELE

Utengenezaji Wa dawa ya kukuza nywele

Mahitaji
1*mafuta ya mnyonyo
2*asali
3*maji ya limao
4*Unt bakteria

Utengenezaji

Andaa bakuli linalo endana na wingi Wa mahitaji yako kisha weka asali robo Lita kisha weka mafuta mnyonyo robo Lita kisha weka maji ya limao kiasi upendacho kisha koroga kupata mchanganyiko safi

Baada hapo anza kutumia

Paka kwa nywele zilizo na dawa na zisizowai kuwekwa dawa

Baada ya kupaka mfano wakati Wa kulala funga kwa kusokota (mabutu) kisha funika na mfuko Wa plastik asubuh fumua na uoshe Fanya ivyo kwa siku 3 au 4 uone maajabu ya hii dawa

JINSI YA KUTIBU UGONJWA WA VIDONDA KOONI NA MAFUA UKIWA NYUMBANI

*Jinsi ya kutibu ugonjwa wa vidonda kooni na mafua ukiwa nyumbani*

Ugonjwa wa uvimbe kooni mara nyingi husababishwa na kufungana mapua na makamasi yanapopita kooni Baridi kavu inaweza pia kufanya koo likauke na mtu ahisi likiwashawasha.Unaposhikwa na mafua, pia inaweza kusababisha kidonda kooni kinachoweza tu kutibiwa na dawa. 

*jinsi ya kutibu ugonjwa wa koo na mafua ukiwa nyumbani*

*1. Tumia Apple Cider vinegar* 

jinsi ya kutibu ugonjwa wa vindonda kooni na mafua ikiwa nyumbani Ili kupunguza makali ya ugonjwa wa vidonda kooni,changanya kijiko kimoja cha Apple Cider Vinegar na maji moto,kunywa mchanganyiko huo ambao utasaidia kuua vijidudu vinavyosababisha uvimbe kooni.

*2.Vitunguu saumu*

Jinsi ya kutibu ugonjwa wa vindonda kooni na mafua ikiwa nyumbani Chukua vitunguu saumu kiasi, viponde halafu uvimumunye vikiwa mbichi kwa muda wa dakika 15 Aidha,unaweza viponda,uvichanganye na asali, Olive oil au mboga za kienyeji ili kuifanye juisi yake ipate ladha kiasi.

*3. Asali*

Jinsi ya kutibu ugonjwa wa vindonda kooni na mafua ikiwa nyumbani Changanya asali kiasi unachotaka na maji moto,Olive Oli au na dawa yoyote ya miti shamba. Kwa mara nyingi asali hujulikana kutibu vindonda kooni na pia kikohozi

*4.Maji ya Chumvi*

Jinsi ya kutibu ugonjwa wa vindonda kooni na mafua ikiwa nyumbani Mbinu hii ya kutibu vidonda hutumika na watu wengi nyumbani,chemsha maji kikombe kimoja na uchanganye na kijiko kimoja cha chumvi kisha sukutua maji hayo kwenye koo. Habari Nyingine:

*4.Kunywa chai ya Chamomile*

Jinsi ya kutibu ugonjwa wa vindonda kooni na mafua ikiwa nyumbani Chai ya chamomile humaliza haraka maumivu ya ugonjwa wa vidonda kooni na pia inasemaka inasaidia kuzuia maradhi ya ugonjwa wa saratani.

*5.Maji ya Ndimu*

Jinsi ya kutibu ugonjwa wa vindonda kooni na mafua ikiwa nyumbani Maji ya ndimu hukausha vidonda kooni na pia yanajulika kwa kuzuia maradhi yoyote ya ugonjwa wa saratani. Unatakiwa kuchanganya ndimu na maji moto,uongeze asali au chumvi kisha uyanywe maji hayo

6. *Kunywa maji mengi*

Kunywa maji mengi husaidia kusafisha koo na kulizuia kukauka Vile vile maji husaidia kuepukana na saratani ya tumbo kwa sababu inasaidia katika usagaji wa vyakula

DAWA YA KUTIBU HOMA YA MATUMBO(TYPHOID)  DAWA YA TIBA ASILIA

*DAWA YA KUTIBU HOMA YA MATUMBO(TYPHOID)  DAWA YA TIBA ASILIA*

*FANYA HIVI*

: Chukuwa Glasi 4 za Maji tia ndani ya jagi la maji changanya na nusu kijiko kidogo cha chumvi ya unga. Kisha tia ndani yake vijiko 6 vidogo vya sukari, kisha koroga vizuri hayo maji.

*Matumizi yake*

kunywa asubuhi kabla ya kula kitu glasi 1 mchana glasi 1 Jioni Glasi 1na usiku glasi 1 kila siku dawa ikiisha tengeneza dawa ingine utumie hiyo dawa kwa siku 30 utaweza kupona.

*Hatua za kuzuia kupata homa hii*

Usafi wa mazingara na wa kibinafsi ni hatua bora ya kujikina kutokamana na ugonjwa huu.
Homa ya matumbo haiathiri wanyama kwa hivyo maambukizi ni kutoka kwa binadamu mmoja hadi mwingine.
Homa hii hueza kuenea kwenye mazingara ambayo kinyesi cha binadamu hutangamana na vyakula vyao. Upishi wa makini na uoshaji mikono ni kingo bora zaidi kwa kuzuia maradhi haya kuenea.

Chanjo ni za aina mbili: moja inayotiwa kwa njia ya mdomo iitwayo Ty21a (au Vivotif Berna) na nyingine ya sindano kwa majina Typhim Vi iliyotengenezwa na Sanofi Pasteur au Typherix iliyotengenezwa na GlaxoSmithKline.

Tuesday, 16 October 2018

MIKATE YA UFUTA

MIKATE YA UFUTA

MAHITAJI

Unga vijiko 3 vikubwa (mugs)

Tui la nazi au maziwa lita 2 na nusu

Hamira kijiko 1 cha supu

Chumvi kias

Yai 1

Ufuta kiasi

Mafuta au samli ya kupakia mkate kiasi

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

(@) CHANGANYA PAMOJA UNGA,NAZI,CHUMVI,HAMIRA,SUKARI NA YAI HAKIKISHA UNGA WOTE UMETOKA MADONGE NA UME VURUGIKA VIZURI UWE LAINI UWE MAJI MAJI KAMA WA KAIMATI LAKINI UNA KUWA MZITO KIDOGO KULIKO WA KAIMATI USUBIRI UUMUKE (UFURE)


JINSI YA KUCHOMA

1 Hakikisha chuma cha kuchomea kiwe kina gandisha vizur kisiwe (non_stick) napia kisiwe kilicho pikia mafuta

2  Weka chuma kwenye moto kikipata moto rushia maji ya chumvi kidogo halafu tia unga kiasi kama kiganja kimoja cha mkono utawanye vizuri kwa kidole alafu nyunyuzia ufuta juu yake.

3.  Ukianza kuwa mkavu nyanyua chuma kifunikize kwenye moto mpaka mkate wako uwe wa rangi ya dhahabu

4.  Toa  toa kwenye chuma kwakutumia kisu

5.   Paka samli au mafuta juu ya mkate kwaku tumia brash

6.  Endelea hivyo hivyo paka umalize mkate wote

MWISHO

mkate wako utakuwa tayar kwakuluwa



KEKI YA ZABIBU MBICHI NA MACHUNGWA

KEKI YA ZABIBU MBICHI NA MACHUNGWA :

Mahitaji:-

🔸Unga wa ngano vikombe 2
🔸Sukari kikombe 1 1/2
🔸Baking powder kijiko 1 chakula
🔸Chumvi 1/4 kijiko chai
🔸Zabibu mbichi kikombe 1-1/2 (osha vizuri kisha zikaushe kwa paper towel)
🔸Ganda la chungwa 1, lilokunwa, tumia grater
🔸Mayai 3
🔸Maji ya machungwa 3/4 kikombe
🔸Mafuta ya kula 1/2 kikombe

NAMNA YA KUOKA:-

1. Changanya unga, baking powder na chumvi katika bakuli . Weka pembeni

2. Tia zabibu na ganda la chungwa kisha koroga vizuri unga uenee katika zabibu zote.

3.  Katika bakuli nyingine ya kati piga mayai kisha tia maji ya machungwa na mafuta na koroga vizuri kuchanganya.

4. Mimina mchanganyiko huu wa mayai katika bakuli la unga kisha koroga taratibu hadi mahitaji yachanganyike vizuri.

5. Mimina katika chombo cha kuokea ulichopaka mafuta. Kisha oka katika oven lenye joto 180°C kwa muda wa dk 40 hadi saa 1 au hadi ukichoma kijiti kati kitoke safi.

6.Toa katika oven acha ipoe katika pan kwa muda wa dk 10 kisha itoe na weka katika wire ipoe kabisa. Enjoy

JINSI YA KUTENGENEZA ICE CREAM ,LAMBA LAMBA ZA NAZI NA LIMAO

LAMBA LAMBA ZA NAZI NA LIMAO

               * MAHITAJI*
1; TUI LA NAZI

2; LIMAO UTAKAVOPENDELEA

3; SUKAR KIAS CHAKO

4; CORN STARCH KIAS CHAKO USIFA NYE NZITO SANA

                * MAANDALIZ*
CHEMSHA VIT VYOTE KWA PAMOJA FUNGA NA UGANDISHE👌🏼😋

JINSI YA KUTENGENEZA ICE CREAM ,LAMBA LAMBA ZA CUSTURD NA MAZIWA

LAMBA LAMBA ZA CUSTURD NA MAZIWA🥛🥛🥛👌🏼😋

                  * MAHITAJI*
1; MAZIWA LITA 1

2; CUSTURD VIKOMBE 2

3; SUKAR KIAS CHAKO

4; MAJI LITA MOJA

              *MAANDALIZ*
1;  CHANGANYA VITU VYOTE KWA PAMOJA NA UCHEMSHE

2; IKICHEMKA VIZUR EPUA JAZA KWENYE VIFUNGASHIO NA UGANDISHE😋👌🏼

JINSI YA KUTENGENEZA DATE MILKSHAKE/MILKSHAKE,YA TENDE: JUICE YAKUONGEZA HAMU YA JIMAI KWA WANANDOWA

DATE MILKSHAKE/MILKSHAKE,YA TENDE:
JUICE YAKUONGEZA HAMU YA JIMAI KWA WANANDOWA
💞💞💞💞💞💞💞
Ingredients:-

⚪Tende zilizotolewa peke na kukatwa katwa kikombe 1
⚪Ndizi 1, ilokatwa katwa vipande na kugandishwa
⚪Vanilla  kijiko 1  cha chai
⚪Maziwa ya baridi vikombe 2 1/2 au zaidi
⚪Ice cream ya vanilla 1/2 kikombe
⚪Mdalasini wa unga 1/4 kijiko cha chai

NAMNA YA KUTAYARISHA:

1. Saga mahitaji yote katika blender hadi mchanganyiko uwe smooth. Enjoy!
Na bwana kwan  huongeza. Nguvu kwajimai

💞💞💞💞💞

JINSI YA KUPIKA MKATE WA NGANO ISIOKOBOLEWA (ATTA)

MKATE WA NGANO ISOKOBOLEWA ( ATTA) :

Mahitaji:-

🔸Unga wa ngano isokobolewa(atta) vikombe 3
🔸Hamira vijiko 2 1/4 vya chai
🔸Maji ya vugu vugu kikombe 1  1/4 au zaidi
🔸Maziwa ya unga kijiko 1 cha chakula(sio lazima, yanaleta harufu na radha nzuri)
🔸Chumvi kijiko 1 1/4 cha chai
🔸Asali 1/3 kikombe
🔸Mafuta 1/2 kikombe
🔸Mdalasini wa unga 1/4 kijiko cha chai

NAMNA YA KUPIKA:

1. Tia maji vugu vugu, hamira na sukari katika bakuli , koroga vizuri kisha acha kwa muda wa dk 5 hamira ifure

2. Tia mahitaji yalobaki kisha  katika bakuli kisha changanya vizuri hadi ufanye donge, Kanda donge lako hadi liwe laini. Kama unga mkavu ongeza maji kidogo kidogo

Unga unatakiwa uvutike vizuri usinate ndio utapata mkate mzuri wa kuchambuka

3. Tia unga wako katika bakuli ulopaka mafuta kisha funika acha ufure hadi ujae mara mbili, sukuma na sokota kufanya umbo la mkate(loaf). (Unaweza fanya bhanzi pia kwa kipimo hiki)

4. Tia katika chombo cha mkate ulichopaka mafuta, funika acha ufure hadi ujae vizuri.

5. Oka katika oven ya moto joto 190°C hadi upate rangi na kuiva.

4. Utoe mkate wako katika chombo chake ,tumia kitambaa safi kuepuka kuungua kisha acha mkate upoe kabisa kabla ya kuukata.

5. Mkate tayari kwa kula. Mkate huu ni very healthy na unapendeza zaidi kwa chai ya maziwa au ilochemshwa kwa viungo vizuri.

Kipimo hiki utapata mikate miwili

JINSI YA KUTENGENEZA JIKI

Jinsi ya kutengeneza jiki
Mahitaji
Jiki yenyewe ipo chengachenga nusu
Sodaash nusu
Maji lita kumi
Jinsi ya kutengeneza
Weka maji safi lita kumi  weka jiki kisha koroga hd chenga ziishe kisha weka sodaash korogo kisha funika hd kesho yake
Kesho yake ukifunua utaona maji yako juu ule weupe upo chini ww chukua maji yale meupe paki kwenye vifungashio peleka sokoni

Monday, 15 October 2018

JINSI YAKUTENGENEZA SABUNI YA KUNAWIA MIKONO NA YA KUSAFISHIA VYOO

Sabuni ya maji   sabuni ya kunawia mikono.   Kusafishia vyoo

Malighafi kuu ni

1*Sulphonic acid (salfoniki asidi)

2*silesi au ungaroli

3*chumvi

4*manukato

5*rangi ya sabuni

Malighafi za kawaida (hazina ulazima)

1*soda ash

2*griselin

3*formalin nk

Katika malighafi zote malighafi mama ni salfoniki na siles

Pia unaweza kutoa Sabin kwa kutumia sulphonic acid bila siles

Pia unaweza kutoa sabuni kwa kutumia siles bila sulphonic acid

👇🏽
Utengenezaji Wa sabuni

  Andaa ndoo ya Lita 20 weka maji Lita 10

Baada ya hapo anza kukoroga maji kuelekea upande mmoja

Kisha unakoroga mwengne aanze kumimina sulphonic acid nusu Lita

Baada ya hapo mimina siles nusu Lita

Baada ya hapo mimina rangi kiasi upendacho ww

Baada ya hapo mimina manukato kiasi upendacho ww

Kama ukiwa na haya material

Mimina soda ash vijiko viwili vya chakula

Kisha mimina griselin robo Lita

Kisha weka formalin vijiko 5 vya chakula

Kumbuka usiache kukoroga

Baada ya hapo weka chumvi viganja wivili vya mkono

Baada ya kumaliza kuchanganya malighafi zote endelea kukoroga kwa dakika 15

Baada ya dakika 15 sabuni itakua tayari

Nb malighafi za kwanza kuanza Nazi ni sulphonic au unagalor alafu zingne utakazo penda wewe ila chumvi iwe ya mwisho

JINSI YA KUTENGENEZA SHAMPOO

Jinsi ya kutengeneza shampoo
Malighafi
-sulphonic acid
-ciles
-rangi
-perfume
-chumvi
-CDE
-gycerine
-sodash

Jinsi ya kutengeneza
-andaa vyombo kuwa na mwiko wa kukorogea,ndoo,beseni na maji
-anza na sulphonic acid vijiko vi 3
-fuata na ciles changanya vijiko 41/2
-koroga kwa dakika 3

NB:TUNAKOROGA UPANDE MMOJA ILI SHAMPOO YAKO
ISIKATIKE

-Chukua sodash ichanganye na maji kidogo then ukoroge kwa dakika kadhaa hadi mchanganyiko ukae sawa.
-chukua mchanganyiko wako huo wa sodash mimina kwenye mchanganyiko wa kwanza koroga mpaka ilainike.
-mimina glycerine vijiko 2 then koroga
-mimina rangi kiasi
-mimina perfume
-weka CDE kichupa kizima mimina
-Unaweka maji yako lita kumi then koroga
-unamalizia na chumvi kilo 1 unakoroga mpaka ilainike
NOTE: Tunatumia chumvi ya mawe,na chumvi ni hatua ya mwisho kabisa katika utengenezaji wako.
-

URUTUBISHAJI WA BWAWA LA SAMAKI KWA MBOLEA NA (MAJIVU) PAMOJA NA USAFIRISHAJI WA VIFARANGA WA SAMAKI


URUTUBISHAJI WA BWAWA LA SAMAKI KWA MBOLEA NA (MAJIVU) PAMOJA NA USAFIRISHAJI WA VIFARANGA WA SAMAKI.

Kutegemea aina ya udongo, majivu ya moto huweza kutawanywa bwawani kabla ya kuingiza maji ili kupunguza Tindikali ya udongo na kuua baadhi ya wadudu walio maadui wa samaki waliopo katika eneo la bwawa.
Mbolea huweza kutawanywa bwawani kabla ya kuweka maji ili kusaidia kujenga mazingira ya maji kutuama (yaani Kushikamanisha udongo).
Vinginevyo, mbolea huwekwa eneo maalum (Uzio) mara baada ya maji kuingizwa bwawani ili kulirutubisha na Kuliwezesha liwe na vijimea na vijidudu vidogo vidogo vitakavyokuwa chakula cha awali cha samaki.
Dalili za kuwepo kwa vijimelea hivyo bwawani ni kugeuka rangi ya maji na kuwa ya kijani.
Aina ya mbolea hutegemea upatikanaji wake. Samadi ya ng’ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, kuku, bata na hata Majani mabichi yaozayo kirahisi na yasiyo sumu kwa wanyama na binadamu huweza kutumika.
Kiasi cha kuweka mbolea hutegemea sana ukubwa wa bwawa, aina ya samadi na idadi ya samaki waliomo.
Kipimo kizuri cha kiasi kinachotosha ni kuingiza mkono ndani ya maji hadi kufikia kwenye kiwiko, na usipoona Kiganja chako, basi simamisha uwekaji wa mbolea kwani vijimelea na vijidudu waliomo wanatosha kulisha samaki Waliomo kwenye bwawa kwa muda wa siku kadhaa.
Ukizidisha mbolea ni hatari kwa samaki, kwani wanaweza kufa kwa kukosa hewa ya oksijeni, hasa nyakati za usiku.

USAFIRISHAJI, UPANDAJI NA ULISHAJI WA VIFARANGA WA SAMAKI

USAFIRISHAJI WA VIFARANGA WA SAMAKI
Upatapo vifaranga, visafirishe wakati wa asubuhi kwa kutumia ndoo ya plastiki, chungu, maplastiki makubwa.

Weka kiasi cha vifaranga 200 katika ndoo moja. Ni vema mkulima kuwa na tabia ya kupunguza maji
kwenye ndoo yenye samaki na kuweka mengine afikapo eneo lenye maji.

Ufikapo bwawani, inamisha ndoo ili maji ya kwenye ndoo yaingiliane na yale ya bwawani.
Hii ni kuruhusu joto la maji na mazingira ya maji yaingiliane na kuwa sawa.

Waruhusu samaki watoke bwawani wenyewe bila ya kuwamwaga. Itachukuwa muda kabla ya vifaranga wote kuingia bwawani. Kwa kufanya hivyo, samaki hawatapata mshituko ambao wanaweza kupata kama
watamwagwa. Mshituko wa   ghafla huweza kusababisha vifo.

UPANDAJI WA VIFARANGA VYA SAMAKI.
Ubora wa samaki utakao wafuga utategemea sana ubora wa vifaranga utakaokuwa umepanda bwawani.

Chanzo chako cha vifaranga ni bora kiwe na vifaranga wenye umri mdogo na ambao hawajadumaa.

Kwa samaki aina ya Perege, panda vifaranga viwili (2) hadi watatu (3) kwa kila mita moja ya mraba.

Kwa sasa,  samaki aina ya Perege ndio wanaoshauriwa kufugwa na wafugaji wa maji baridi hapa nchini.

Kambale huweza kufugwa na mkulima mzoefu kwani huduma yake huitaji mtaji mkubwa katika
kuwalisha na Utaalam katika kuzalisha vifaranga vyake.

ULISHAJI WA SAMAKI.

Samaki, Kama walivyo wanyama wengine, wanahitaji kula.
Chakula cha samaki huweza kugawanywa katika makundi mawili:-
Cha asili kipatikanacho ndani ya bwawa kama vile vijimea, vijidudu na samaki wadogo.
Cha ziada ambacho huongezwa bwawani na mkulima.
Ili chakula cha asili kipatikane bwawani, ni vema bwawa liwe limerutubishwa vizuri, kwani vijimea vinavyotarajiwa humea palipo na rutuba.
Chakula za ziada huwekwa bwawani na mkulima mwenyewe. Aina ya chakula cha ziada hutegemea upatikanaji wake, gharama na aina na ukubwa wa samaki. Baadhi ya chakula cha ziada ni kama: pumba za mahindi, za mpunga, mashudu ya pamba na karanga, machicha ya pombe, ugali na masazo ya jikoni, baadhi ya majani pori, majani yatokayo bustanini.
Inashauriwa mfugaji alishe kila siku, kwa muda ule ule, saa ile ile na sehemu ile ile. Tabia hii hujenga mazoea ya samaki kula zaidi na kupunguza wingi wa chakula kinachopotea.
Usilishe chakula kingi zaidi ya mahitaji ya samaki kwa siku hiyo. Mfano, usiweke debe zima la pumba kwa mara   moja na kuacha kulisha kwa wiki nzima! Sehemu ya chakula kitakachosalia, kitaoza na baadhi ya siku samaki hawatakuwa na chakula, watashinda na kulala njaa!

Sunday, 14 October 2018

JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA NGURUWE


Jinsi ya kutengeneza chakula cha nguruwe

Wakati wa kutengeneza chakula cha nguruwe inabidi kuzingatia yafuatayo:
• Mchanganyiko wake uwe na viinilishe vinne vilivyotajwa hapo juu
• Chagua aina ya viinilishe vinavyoweza kupatikana kwa urahisi na bei nafuu kwenye mazingira yako
• Aina ya mchanganyiko wa chakula ni muhimu uzingatie mahitaji ya nguruwe kama umri (mfano: nguruwe wanaonyonya, waliochishwa kunyonya, wanaokua, na  wanaonyonyesha)

Mifano mbalimbali ya vyakula vya nguruwe.
1. Mchanganyiko namba 1: inapendekezwa kwa wafugaji walioko kwenye mazingira ambayo pumba za mahindi na mashudu ya alizeti yanapatikana kwa urahisi
2. Mchanganyiko namba 2: kwa wale ambao pumba za mahindi, za mpunga machicha ya pombe na mashudu ya alizeti yanapatikana kwa urahisi.
3. Mchanganyiko namba 3: kwa wale ambao pumba za mpunga na mahindi yanapatikana kwa urahisi.

. Kiasi na namna ya kulisha
• Nguruwe wanahitajika kulishwa aina hii ya chakula mara mbili (asubuhi na mchana) au zaidi kwa siku
• Kiwango/kiasi cha kulisha kwa nguruwe wa aina na rika tofauti .

• Pamoja na vyakula vilivyotajwa, wafugaji wanashauriwa kuwapatia nguruwe vyakula vyao vya kijadi karna vyakula vya ziada mfano, majani mabichi laini HYDROPONIC, majani ya maboga, mbogamboga, matunda kama maparachichi, majani ya viazi n.k.

Viwango vya kulisha nguruwe wa uzito mbalimbali
Na Wakati Uzito wa nguruwe (kilo) Kiasi cha chakula (kilo kwa siku)
1. Baada ya kuachishwa 10-17 0.75
kunyonya hadi uzito kiasi
2. Uzito uliozidi kiasi kidogo 18 - 29 1.00
3. Uzito wa kawaida 30- 40 1.50
4. Uzito mkubwa kiasi 41 - 60 2.00
5. Uzito mkubwa 61 - 80 2.5
6. Uzito mkubwa sana 81 - 100 3.00
7. Nguruwe anaye nyonyesha 120 - 150 6.00

Jinsi ya kulisha jike la nguruwe  kabla na baada ya  kuzaa
Kipindi cha mimba, kuzaa hadi kuachisha kunyoyesha
Kipindi cha miezi mitatu baada ya kupandishwa
•Apatiwe chakula kiasi karna kilo mbili kwa siku
•Kiasi hiki kiendelee hadi wiki 3 kabla ya kuzaa

Wiki tatu kabla ya kuzaa
•Ongeza chakula kufikia kilo mbili na nusu.

1.3 Wiki moja kabla ya kuzaa
• Anza kuopunguza chakula taratibu hasa vyakula vya nafaka (Concentrate rations).
• Ongeza vyakula vya   mbogamboga,  majani laini na matunda (laxative  meals).

Siku ya kuzaa
• Usimpe chakula chochote cha nafaka.
• Mpe vyakula vya mbogamboga,na vilaini kwa kiasi kidogo tu
• Mpatie maji ya kutosha.

Siku ya 1 -  2 baada ya kuzaa
• Mpe nusu kilo ya chakula kamilifu.

Siku ya 3 na kuendelea
• Ongeza chakula cha nafaka kwa kiasi cha kilo 1 kwa siku.
• Ongeza kufikia kiwango kinachohitajika kulingana na idadi ya watoto alionao mama nguruwe.

Zingatia
• Mama nguruwe anahitaji kilo 3 za chakula kwa matumizi yake ya kawaida.
• Atahitaji kiasi cha ziada cha theluthi moja (1/3) ya kilo ya chakula kwa kila mtoto aliyenae

Mfano: kama mama ana watoto 9 atahitaii kiasi  ani cha chakula?
Mahitaji mama peke yake Mahitaji kutokana na watoto Kiasi cha chakula kwa siku
3kg Theluthi moja x 9: (113    X   9 =
3 Kg) 3 kg + 3 kg = Kilo 6 kwa siku
Endelea kumpa kiwango hicho cha chakula mpaka ifikapo wik:i moja kabla ya kuwaachisha watoto kunyonya.
Wiki moja kabla ya kuwachisha punguza kiwango taratibu mpaka kufikia kilo 3 kwa siku

Baada ya kuachisha kunyonya
• Mama nguruwe wapatiwe chakula bora kilicho na kiwango kikubwa cha maclini na vitamini kiwango cha kilo 2 - 3 kwa siku.
• Hii itamsaidia kuivisha mayai, hivyo kumsaidia kupata joto mapema.

MAGONJWA YA MIFUNGO ,DALILI NA TIBA ZAKE

SABABU ZA KUVIMBEWA KWA NG’OMBE
                (BLOUTING)

Hili ni tatizo ambalo tumbo la mnyama hujaa gesi (carbon dioxide) ambayo husababishwa na sababu mbali mbali, Ambapo kujaa huku kwa hewa hiyo ya carbon dioxide hupelekea kutofanyika kwa mmng’enyo wa chakula kama inavyotakiwa, tatizo hili huweza pia sababisha vifo kwa asilimia 25 endapo huduma ya kusaidia mnyama hazitofanyika kwa wakati.

SABABU ZA NG’OMBE KUVIMBEWA.
- Kula majani ya jamii ya mikunde kwa wingi.
- Kula majani aina ya lusina kwa wingi.
- Kula nailoni (maliboro).
- Kula chakula kingi chenye kiasi kikubwa chawanga ikiwemo pumba na ugali.
- Kuvimba kwa tezi ambazo zipo katika eneo la mguu wa mbele.
- Wakati mwingine ni tatizo la kurithi.

DALILI ZA NG’OMBE KUVIMBEWA
- Ng’ombe kushidwa kujisaidia.
- Tumbo kuonekana limejaa muda wote.
- Ng’ombe kushindwa kula.
- Ng’ombe kuonekana mchovu muda wote.
- Ng’ombe hulala muda mwingi.
- Kuonekana kuwa mwenye msongo.
- Ng’ombe kubeuwa mara kwa mara.

NAMNA ZA KUMUHUDUMIA NG’OMBE.
Kuna namna nyingi sana za kumuhudumia ng’ombe kulingana na aina ya visababishi vya kuvimbewa.
Pia kuna njia nyingi ambazo unaweza tumia kama mfugaji makini.

KWA NJIA ZA ASILI/ KAWAIDA.
- Tumia mkaa (chukua kiasi chochote cha mkaa ponda ponda na changanya kisha mnyeshwe ng’ombe mdomoni kwa kiasi cha lita ) kwa kufanya hivi unaweza msaidia ng’ombe kucheua na kutoa gesi iliyopo tumboni.
- Tumia mafuta ya kula kiasi cha chupa ya soda moja hii pia itasaidida katika kuondoa gesi tumboni.
- Tumia parachichi, kata kata kiasi chochote cha parachichi kisha ponda na changanya na maji kupata uji uji na kisha mnyeshe ng’ombe wake.

NJIA ZA KITAALAMU.
- Njia hii huitaji utaalamu wa hali ya juu nap engine zoezi hili lifanyike na mtaalamu wa mifugo ambaye hataweza kutambua sehemu nzuri ya kuchoma vifaa (trocar and cannula). Na vifaa hivi huchomwa sehemu ya kushoto ya tumbo inayoitwa Paralamba fosa, sehemu hii inahitaji sana utaalamau kuhifahamu.

Njia hii ni ya haraka sana kuondoa gesi ndani ya tumbo.

- Tumia Ipson salt, Hii ni chumvi ambayo ni maalumu katika kuwahudumia ng’ombe ambao hupata shida ya kuvimbewa na njia ya haraka sana, mpatie kwa muda wa saa 24 kiasi cha kijiko kimoja cha chakula (mills 20) kwa lita moja ya maji safi na salama.

MAMBO YA KUZINGATIA KUZUIA TATIZO HILI.
- Epuka kuchunga wanyama wako kuzunguka maeneo yenye nailoni.
- Wape kwa kiasi kinachotakiwa cha pumba.
- Kwa watakao changanya majani ya lusina na pumba hakikisha lusina imekaushwa kwa muda wa siku mbili katika kivuli kuondoa sumu ya Memosine.

Tatizo hili pia  linasumbua wanyama kama MBUZI,KONDOO kwa hiyo tuzingatie pia.

NDIGANA BARIDI, UGONJWA HATARI KWA MIFUGO.

Ndigana baridi (Anaplasmosis) ni ugonjwa unaosababishwa na kupe, mbung'o na inzi aina ya Stomoxys kwa mifugo yako hasa ng'ombe, mbuzi na kondoo.
JINSI UGONJWA HUU UNAVYOAMBUKIZWA (Mode of transmission of the disease)

Ugonjwa wa ndigana baridi unaambukizwa kupitia kwenye ng'ombe mgonjwa baada ya kuumwa na kupe, mbung'o au inzi, aina ya ng'ombe, mbuzi au kondoo walio na afya nzuri ili kupata chakula yaani kunyonya damu wakati wananyonya damu pia ng'ombe asiye mgonjwa. Pia kwa njia ya kutumia vifaa vya kitaalamu ambavyo havikuchemshwa sawasawa kama sindano, vijidudu vya ugonjwa husambazwa kutoka mnyama mgonjwa kwenda mnyama mwenye afya kwa kutumia vifaa hivyo.

Hivyo uangalizi mkubwa unatakiwa wakati shughuli hizo za kuchoma sindano, kukata pembe n.k. zinapofanyika.

WANYAMA WANAOPATA UGONJWA WA NDIGANA BARIDI.
- Ng'ombe
- Mbuzi
- Kondoo

Ndama wadogo hawapatwi na ugonjwa huu.

DALILI KUU ZA UGONJWA.

Dalili kuu za ugonjwa huu ni:-
(i) Homa kali (40-41C).
(ii) Kinyesi kigumu sana na chenye utando mweupe juu yake.
(iii) Kupumua/kuhema kwa shida.
(iv) Mnyama kushindwa kucheua.
(v) Rangi ya njano mdomoni, puani na sehemu zilizo wazi za mnyama kama machoni n.k.
(vi) Kukosa hamu ya kula.
(vii) Kupunguza uzalishaji wa maziwa.
(viii) Kutokunywa kwa sababu ya omasum kutofanya kazi (constipation).

MAGONJWA MENGINE YANAYOFANANA NA NDIGANA BARIDI.

-Ndigana kali
-Kuvimbiwa (bloat)
-Kichomi

JINSI YA KUZUIA UGONJWA WA NDIGANA KALI.

-Hakikisha wanyama wako wanaogeshwa vizuri na dawa ya kuua kupe (Acarcides)
-Ogesha kwa kutumia dawa zinazozuia kupe na mbung'o mara 1 kwa wiki mfano Tristix, Tixfix, Ciberdip, Paranex, Alfanex, Steladone, Dominex n.k.
-Chunga mifugo yako katika mbuga zisizo na kupe au mbung'o.
-Ikiwezekana chunga/lisha kwa mzunguko (rotational grazing) katika mbuga zako ili kupunguza kuzaliana kwa kupe.

JINSI YA KUTIBU MNYAMA MWENYE NDIGANA BARIDI

-Watibiwe kwa kutumia dawa ya Oxytetracycline ya sindano 5-10mg/kg ya uzito a
-Wanyama waliofunga choo wanyweshwe mafuta ya kupikia ili kulainisha tumbo


NDIGANA KALI

Dalili zake

i. Homa kali hadi nyuzi joto 42c
ii. Povu kutoka mdomoni na puani
iii. Kuhara choo kilichochanganyikana na kamasi na damu
iv. Tezi kuvimba sana na zenye joto
v. Kuacha kula
vi. Ukungu kwenye macho
vii. Kifo baada ya wiki moja hadi mbili

Tiba
Butalex, Parvexon, tiba iambatane na sindano moja ya kuondoa uvimbe kwenye mapafu kama hali hiyo tayari imeshajitokeza.

Tumia Multivitamin ili kuongeza hamu ya kula na Raxis ili kuondoa maji kwenye mapafu.

Kinga/zuia
Zingatia uogeshaji sahihi na Chanjo ya ECF

NDIGANA MKOJO DAMU (Babesiosis) ugonjwa wa kukojoa damu

Dalili zake
i. Mkojo kuwa na rangi ya damu isiyokolea zambarau ii. Mkojo hutoka kidogo kidogo na kwa muda mrefu
iii. Homa hadi nyuzi joto 40C
iv. Kuacha kula
v. Choo kigumu au kuhara wakati mwingine
vi. Kifo baada ya wiki 1

Tiba
Berenil ikisaidiwa na antibiotics za sindano kama vile oxytetracycline (OTC) pia tumia Multivitamin kuongeza hamu ya kula.

Kinga
Zingatia uogeshaji sahihi

Saturday, 13 October 2018

UTUNZAJI WA VITOTO VYA NGURUWE

UTUNZAJI WA VITOTO VYA NGURUWE.

Ulishaji wa maziwa ya kwanza
Baada ya kuzaliwa na kusafishwa, hakikisha vitoto vinanyonyeshwa.Vitovu viwekewedawa (Iodine 5%) ili kuzuia magonjwa. Kama mama amefariki mara tu baada ya kuzaa na hakuna nguruwe mwingine anayeweza kunyonyesha; tumia maziwa ya ng'ombe. ongeza sukari na yai bichi koroga na uwanyonyeshe kwa kutumia chupa ya maziwa ya mtoto.

Joto
Vitoto vya nguruwe havizaliwi na manyoya na hawana mafuta mengi ya kutosha kuwaletea joto mwilini; hivyo ni rahisi kufa kwa baridi. Tumia taa ya stimu au chemli kuongeza joto.

Kuzuia upungufu wa damu
Maziwa ya nguruwe yana upungufu wa madini ya chuma yaongezayo damu. Hivyo baada ya majuma mawili au matatu watoto huanza udhoofu kwa kukosa madini hayo mwilini. Kuondoa tatizo hili inabidi vitoto vidungwe sindano ya madini kwenye misuli siku mbili au tatu tangu kuzaliwa. Kama sindano haipatikani njia nyingine za kuwapatia watoto madini hayo ni kwa kuwapa vidonge vya madini chuma, au kuwapa madini hayo kwenye   dimi zao au chuchu za mama yao siku mbila hadi tatu baada ya kuzaliwa.

Ukataji meno
Siku chache kabla ya kuzaliwa, meno yaliochongoka • Meno hayo humuumiza mama wakati watoto wanapo nyonya mama hupiga mateke. Hii husababisha vifo vya watoto kutokana na kuumia inabidi meno hayo yakatwe  na chombo kinachofanana kupunguza madhara hayo.

Kulisha chakula cha ziada

Chakula kigumu zaidi ya maziwa kianze kulishwa kidogo kidogo kuanzia siku ya kumi baada ya kuzaliwa, kwani wakati huu maziwa ya mama hayatoshelezi. Endelea kuwapa chakula hiki mpaka watakapo zoea kutokunywa maziwa ya mama yao tena. Chakula hiki kiwe na viini lishe  vya kujenga mwili, kuleta nguvu na kuzui maradhi. Nguruwe wapewe chakula hiki kwa wingi na maji ya kutosha.

Kuachisha kunyonyesha
• Viachishe vitoto kunyonya wakifikia umri wa miezi miwili wanapokuwa na uzito wa kilo 10.
• Siku ya kuachisha kunyoyesha muondoe mama nguruwe kwa watoto wake na kumuweka chumba kingine
• Mpe mama chakula cha kutosha

7. Vyakula na ulishaji
Chakula bora kwa nguruwe ni moja ya mahitaji muhimu sana kwenye dhana nzima ya ufugaji wa nguruwe wenye tija na faida kwa mfugaji. Chakula cha nguruwe kinagharimu yapata asilimia hamsini sabini ya gharama zote za ufugaji wa nguruwe. Kati ya matatizo mengi yanayosababisha tija  na ufanisi duni wa uzalishaji wa nguruwe yanatokana na lishe duni. Nguruwe wakipatiwa lishe bora, tija na ufanisi wa uzalishaji utakuwa mkubwa hivyo kuongeza faida kwa mfugaji.

Tukakushauri utumie *Hydroponic fodder* itakusaidia Sana wewe mfugaji kupunguza gharama za chakula pia ni lishe nzuri Sana itakayo wafanya Nguruwe wako waongezeke kilo kwa muda mfupi sana hasa wadogo.

Baadhi ya faida za lishe bora kwa nguruwe  ni:
1. Lishe bora huharakisha ukuaji wa haraka wa nguruwe na hivyo kupata uzito unaohitajika kwa kipindi kifupi .
2. Lishe bora hupunguza gharama za ufugaji na hivyo kuongeza faida kwa mfugaji kwa sababu nguruwe atahitaji kiasi kidogo tu cha chakula na atachukua muda mfupi kupata uzito mkubwa
3. Lishe bora itapunguza maambukizi ya magonjwa.
4. Lishe bora huongeza kiasi cha mayai yatakayoivi shwa na mama nguruwe na hivyo kuongeza idadi ya watoto watakaozaliwa
5. Lishe bora huongeza kiasi cha maziwa yatakayotengenezwa na mama nguruwe kwa ajili ya watoto hivyo kuwafanya wawe na afya bora itakayo wawezesha wakue haraka na kupunguza idadi ya vifo kwa watoto.
6. Lishe bora inaongeza ufanisi wa madume ya nguruwe na hivyo kuongeza uwezo wa kupanda

Viini lishe muhimu kwenye lishe ya nguruwe
Nguruwe wana uwezo wa kula aina nyingi za vyakula lakini vyenye uwezo wa kumeng'enywa kwa urahisi. Chakula cha nguruwe kilichokamilika kinahitaji kuwa na mchanganyiko wa viini lishe vitano, navyo ni
1. Vyakula vyenye kutia nguvu mwilini (kama pumba za mahindi, ngano, mchele)
2. Vyakula vya kujenga mwili (kama mashudu ya alizeti, pamba, unga wa dagaa)
3. Vyakula vya asili ya madini (kama chumvi, chokaa, mifupa iliosagwa)
4. Vyakula vya asili ya vitamini (kama majani mabichi Hydroponic, mbogamboga na matunda)
5. Maji

UFUNGAJI WA NGURUWE,NA JINSI YA KUWAPATA

Upate wapi Nguruwe wa Kufuga
Nunua nguruwe wa kufuga kutoka kwenye mashamba au watu binafsi wanaoaminika ukizingatia yafuatayo.
• Usizalishe nguruwe wanaotokana na ukoo mmoja yaani ndugu kama kaka na dada. Nunua dume najike toka mahali   tofauti.
• Tumia ushauri wa wataalamu kuchagua Nguruwe bora

Sifa za kuangalia kwa nguruwe bora wa mbegu:
• Nguruwe wa mbegu awe na sifa ya kukua haraka na asiwe na ulemavu wa aina yeyote, na hasa wa miguu kwa dume.
• Mama mzazi wa nguruwe awe na historia ya kuzaa watoto 10 hadi 12 kwa mzao mmoja
• Jike awe na chuchu zaidi ya 12.
• Dume awe na sehemu za kiume yaani korodani na uume unaoonekana sawa sawa. Pia awe na hamu ya kupanda majike

Mbinu za uzalishaji
Matunzo ya dome la uzalishaji
• Chagua dume la mbegu bora, lisilokuwa na kilema au ugonjwa wowote. Tenganisha dume na majike iii kuepusha kupandwa kusiko na kumbukumbu. Dume la nguruwe halipaswi kunenepa, kwa hiyo usimlishe chakula kingi na mpatie mazoezi ya kutosha asije akawa mvivu
• Nguruwe dume anaanza kupanda majike akiwa na umri wa miezi 4 hadi miezi 9. Dume liruhusiwe kupanda mara moja tu kwa kila juma. Anapofika miezi 10 anaweza kupanda mara mbili hadi mara tatu kwa wiki. Akiwa na mwaka mmoja na zaidi anaweza kupanda kila siku kwa majuma mawili hadi matatu, kisha apumzike kwa majuma mawili. Ni vizuri nguruwe dume mmoja apande majike 15 hadi 20 kwa mwaka.
• Madume madogo yapande majike madogo, dume kubwa likimpanda jike dogo anaweza akamletea maradhi ya mgongo. Ni muhimu kupandisha dume kabla hajala chakula, na asitumiwe mara tu baada ya chakula ili asiwe mvivu.

Utunzaji nguruwe mwenye mimba
• Mimba ya nguruwe huchukuwa miezi mitatu (3) wiki tatu(3) na siku tatu(3) yaani siku 114
• Nguruwe mwenye mimba apewe chakula cha kutosha kiongezwe polepole tokea posho ya kawaida hadi kilo 3 - 3.5 kwa siku.

Matayarisho ya nyumba kabla ya  kuzaa
• Osha banda la kuzalia kwa maji na kuliacha likauke
• Tandika nyasi kavu mara baada ya nyumba kukauka
• Ongeza taa ya chemli au umeme kama uko mikoa yenye baridi kwenye sehemu ya vitoto.
• Tengeneza sehemu ya kuzalia kwa mbao au mabomba

Kumuandaa nguruwe mama kabla ya  kuzaa
• Mpe  dawa ya minyoo siku 10 kabla ya kuzaa
• Mogeshe mama nguruwe kwa sabuni ya mkono na brashi
• Muhamishie katika churnba cha kuzalia siku 7 kabla hajazaa
• Mpunguzie lishe siku 2 kabla  ya kuzaa
• Siku ya kuzaa mpe nguruwe maji ya kunywa na chakula kidogo ili kuepusha kula watoto

Matunzo ya vitoto vya nguruwe
Vitoto vya nguruwe vinyonye maziwa ya mama siku zote hadi wakifikisha siku 56.

UKITAKA KUPIGA HATUA KIBIASHARA HASA MWANZO BASI ACHANA NA HELA ZA MAJIRANI ZAKO AU RAFIKI ZAKO AU NDUGU ZAKO

UKITAKA KUPIGA HATUA KIBIASHARA HASA MWANZO BASI ACHANA NA HELA ZA MAJIRANI ZAKO AU RAFIKI ZAKO AU NDUGU ZAKO

**[Nilisema hili mwezi April naomba nilirudie tena]**

Sikia..

Mzee Bakhressa anaishi Masaki lakini maji ya Uhai au lambalamba na chapati zake hauzii majirani zake. Au ulishaona vile vibaiskeli vya lambalamba za Azam vikizunguka Masaki nyumba kwa nyumba?

Mzee Mengi hauzi maji ya Kilimanjaro kwa ndugu zake au wakwe zake au jirani zake.

Shigongo hauzi magazeti kwa majirani zake maana unaweza kukuta majirani zake wanasoma Daily News na *The Citizen* na wasijue hata sura ya gazeti la Shigongo ipoje.

Dewji hauzi vitu vyake kwa classmate wake wa zamani au jirani zake.

Lakini wote hao niliowataja wamepiga hatua bila kujali jirani au ndugu au classmate zao wa zamani wananunua au la.
Hiyo ndo akili ya kibiashara.

Tatizo la watu wengi ni kudhani kuwa ukianza kitu chako mfano biashara au ujasiriamali basi ndugu zako na marafiki na majirani ndo wanapaswa kukusapoti. Wasipokusapoti *unanuna* na kuona hawakutakii mema. Unawasema na kulalamika.
Wewe kuna kitu hujajua bado ukikijua kwanza hutataka kuhangaika na makundi hayo ya watu kibiashara.

Kama upo hapo unawaza kuanza biashara na unafikiria kuwauzia jirani zako au ndugu zako basi kajipange upya kwanza. Utakuwa disappointed  na kuanza kulaumu watu bure. Ndiyo maana Mungu alikuumbia ndugu na marafiki wachache kuliko idadi ya watu usiowajua dunia hii.
Ukitaka kupiga hatua kibiashara achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako.

Diamond hauzi karanga kwa ndugu zake au majirani zake. No wateja wa karanga zake ni watu tofauti kabisa.  Majirani wanunue wasinunue no problem.
Wanaoshindana kuview nyimbo zake You Tube au kuzidownload wala wala siyo eti rafiki zake. Ni watu tofauti.

Vijana wengi wanaojifunza kwangu biashara huwa wananiuliza swali: *"SASA BRO NTAMUUZIA NANI MAANA HUKU NINAKOKAA DUH WATU NI WA HALI YA CHINI KWELI KWELI NA HATA RAFIKI ZANGU YANI BORA MIMI"*
Jibu ni moja tu hapa: Ukitaka kupiga hatua katika biashara *achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako*

Anayezalisha tissue papers au toilet papers anauzia rafiki zake? Wanaoanza kutengeneza furniture huwa wanauza kwa ndugu zao? Sasa why wewe unawaza jirani zako ndo wateja.
Unakuta mtu anataka kuanza kufuga kuku anataka majirani zake na wafanyakazi wenzake ndo wale kuku wake! Kwani wanaoshona nguo kwa *Sheria Ngowi* ni ndugu zake au eti jirani zake? No.
Ni watu wengine tofauti kabisa. Maana kwanza jirani ataanza kuleta ujirani kwenye biashara yako changa halafu mtaishia kugombana bila kutarajia.
Achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako.

Kakangu alinunua vitu kwangu miaka mitatu na nusu baada ya mimi kuanza biashara. Yaani wakati nimeshasimama na biashara. Tena alinunua vitu vingi hadi nikachekelea kwa kweli. Lakini huko nyuma kila nikimwambia eti "aniungishe" kumbe yeye anataka kujua ubora kwanza siyo kununua kwa vitu halafu asivitumie. But unaona sasa ningesubiri anunue ndo niendelee ningekuwa wapi? See, ukisubiri sapoti ya ndugu unaweza kuipata mwaka keshokutwa.
Sasa si utakufa masikini?

So we anza tu ndugu waje wasije isikukwaze. Kwani mwenye Facebook wewe umejiunga kwa kuwa mna undugu au eti unamsapoti? Kama vipi we acha kujiunga Facebook uone kama atakufa njaa kwa kuwa hutaki kumsapoti.

Kwani hiyo simu uliyonayo unadhani mwenye hiyo kampuni hana ndugu? Angesubiri ndugu zake au rafiki zake wamuuingishe si angeacha biashara kwa kukosa wateja? Maana wewe unatengeneza Tecno wakati ndugu zako wanachotamani ni iPhone hapo si utalaumu watu bure?

Mi nimeona jirani zangu wakija kuuza unga wa lishe. Lakini taste yetu kwenye hivyo vitu ni nyingine. Anasema "niungishe tu hata huu mfuko mmoja tu jirani" Sasa hapo mtu anauza kwa kuhurumiwa. Sasa utafanikiwa kweli? Nilipoanza biashara nilikuwa na list ya rafiki zangu ndugu zangu na majirani. Tena wenye uwezo mzuri. Kila niliyemshirikisha anakwambia tu *"TUPO PAMOJA"*. Hahaaaaaa.
Hawakununua. Nimekwambia hivi kakangu alinunua kwangu miaka mitatu na nusu toka nianze. Baada ya kuona naambiwa tu TUPO PAMOJA ndipo nilipostudy watu waliofanikiwa waliuzia nani vitu vyao. Nikapata jibu. Hebu jiulize.

Kwani anayejenga hoteli anawajengea rafiki zake au majirani? Nani akalale sehemu ambako anajulikana?  Sasa ukitaka ujenge mgahawa au saluni halafu rafiki zako ndo waje utakuwa hujajua kitu bado. Utaifunga tu hiyo saluni.

Cha msingi wewe tengeneza VALUE. Hilo ndo muhimu. Kisha wateja SAHIHI watakuja tena kutoka mbali kweli kweli. Ukiwaza  kufungua biashara huku unawaza mashosti sijui washkaji utaifunga siku si nyingi afu utasema eti wateja hakuna.
Kweli?
Yani katika nchi yenye watu karibu milioni 50 unaweza kukosa wateja kabisa kweli? Ulichokosa siyo wateja ni maarifa.  Knowledge.

Sasa kuna watu huwa wananiambia "Lakini kaka Andrea hata matajiri walianza na majirani na ndugu bana lazima mtu uanzie mahali ulipo"

Well huwa najiuliza huyu mtu anamaanisha tajiri gani alianza kwa kuuzia ndugu na majirani. Bill Gates au Jeff Bezos? Warren Buffet au Carlos Helu? Dewji au Rostam Aziz? Hata yeye anayesema hivyo hana jibu.

Eti, Joseph Kusaga alianza kuwasikilizisha redio majirani zake? Hata wanaouza vitu kama madawa ya kulevya wanauza mbali na wanakokaa toka mwanzo mpaka wanakuwa mamilionea. Mbali kabisa na familia.

Well.. ni kwamba hukatazwi kuanza kuwauzia majirani zako. Mimi natoa tu ushauri siyo lazima ufate. Ukitaka wewe kawauzie tu ndugu zako na majirani ila kitakachokukuta usije facebook kuanza kulia eti Watanzania hatupeani suppport komaa na majirani zako tu mpaka utoke. Sawa?

But the truth is ukitaka kufanikiwa katika biashara hasa mwanzo fanya kama vile huna ndugu wala majirani. Fanya kwa ajili ya watu wasiokujua. Achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako. Wakizileta well and good wasipoleta no problem.

Kwani mimi nimeandika makala ngapi hapa Fecebook? Nyingi kupita kiasi..Lakini huwa nasubiri ndugu waniambie kaka au uncle au binamu hongera sana makala yako nzuri? Nikisubiri comments za hivyo nitakuwa mjinga. Ndugu na marafiki wana nafasi yao. Lakini watu wasionijua kama wewe unayesoma hapa ndo wana mchango mkubwa mno katika mafanikio yangu katika kuboresha makala zangu zinazofuata. Mrejesho hutoka kwa watu wasio ndugu zangu wala marafiki wala majirani.

Reginald Mengi wakati anaanza kuuza maji ya chupa hakuwa anatafuta marafiki wa kuyanywa hayo maji. Au unadhani ndicho alichofanya? No. Maana unajua marafiki na ndugu nao huwa ni rahisi kwao kufikiri unawageuza ngazi ya kupandia. Wengi huanza kuona wivu kwa siri kuwa wewe utawazidi kimafanikio sasa kwa nini wakusapoti huku hawataki uwazidi.

Ndo maana nimesema wewe concentrate na VALUE. Dunia ya leo ni dunia ya VALUE. Value yako ikiwa nzuri wateja wako watatoka sehemu ambazo hukuwahi kufikiri kabisa. Kuna siku nimeitwa Oysterbay nyumba ya mtu mmoja mkubwa akihitaji huduma kutoka kwangu. Value. Lakini majirani zangu wala hawana habari. Wana taste nyingine. Value yangu huenda haijawagusa. So sikasiriki.
Achana na hela za majirani. Usizipigie hesabu kabisa. Ndo maana hakuna tajiri anayehangaika na jirani zake.

Umeelewa?

Au niendelee kidogo?😄 Okay... Jifunze kwa ma-MC hawa washereheshaji. Unakuta MC anaishi Kijitonyama lakini sherehe za Kijitonyama watu wanachukua MC wa Magomeni. Sherehe za Masaki watu wanachukua MC wa Mbezi. Wakati Masaki pia kuna ma MC wanaishi. Sherehe iko Mwanza watu wanaita MC kutoka Dar au Arusha. MC huyo huyo majirani zake wanasema *"aah huyu ana bei sana tuchukue fulani afu huyu siku hizi anajiona kweli wakati ni MC wa kawaida tu"*. Unaona sasa? Huyo MC angesubiri kusherehesha kwa majirani angesubiri mpaka azeeke.

Kitabu kinasema Nabii hupata heshima nje ya nyumbani. Ukisubiri watu wanaokuzunguka ndo wawe wateja hujajua vizuri maana ya neno MTEJA.

Huoni Bar iko Sinza lakini wadau wake ni watu wa *Tabataaaa!*
Majirani wanaokunywa pombe wanaoishi jirani na hiyo Bar wanaenda kunywea Kinondoni. Kwani mwenye Samaki Samaki hana majirani? Lakini hapo Samaki Samaki wanaokula na kunywa ni jirani zake? No! Wengi hata hawajui alikotokea. Kwani mwenye Shabiby Bus anasafirisha majirani zake. Alinunua basi ili aanze na majirani na rafiki zake?

Sasa kwa nini wewe unatengeneza sabuni ya maji unafikiri jirani zako ndo wateja? Wasiponunua unaona eti hawataki kukupa sapoti. Nimesema achana na hela za rafiki zako na jirani zako na ndugu zako. Utafika mbali sana. Yani ndugu watakuja huko mbele ya safari. Au utashangaa hawatakuja tu milele.

Nadhani sasa umeelewa vizuri japo ndo hivyo inauma kusikia lakini ndovile! 🤔

Achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako! Waheshimu tu lakini love them from a distance.

Ukifanya hivyo ndo utakuwa umeanza kuelewa shughuli hii ya biashara na ujasiriamali ilivyo. Na utaona amani wala hutakuwa na shida na mtu.

Nakubariki. Nakutakia mema!

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO