SABABU ZA KUVIMBEWA KWA NG’OMBE
(BLOUTING)
Hili ni tatizo ambalo tumbo la mnyama hujaa gesi (carbon dioxide) ambayo husababishwa na sababu mbali mbali, Ambapo kujaa huku kwa hewa hiyo ya carbon dioxide hupelekea kutofanyika kwa mmng’enyo wa chakula kama inavyotakiwa, tatizo hili huweza pia sababisha vifo kwa asilimia 25 endapo huduma ya kusaidia mnyama hazitofanyika kwa wakati.
SABABU ZA NG’OMBE KUVIMBEWA.
- Kula majani ya jamii ya mikunde kwa wingi.
- Kula majani aina ya lusina kwa wingi.
- Kula nailoni (maliboro).
- Kula chakula kingi chenye kiasi kikubwa chawanga ikiwemo pumba na ugali.
- Kuvimba kwa tezi ambazo zipo katika eneo la mguu wa mbele.
- Wakati mwingine ni tatizo la kurithi.
DALILI ZA NG’OMBE KUVIMBEWA
- Ng’ombe kushidwa kujisaidia.
- Tumbo kuonekana limejaa muda wote.
- Ng’ombe kushindwa kula.
- Ng’ombe kuonekana mchovu muda wote.
- Ng’ombe hulala muda mwingi.
- Kuonekana kuwa mwenye msongo.
- Ng’ombe kubeuwa mara kwa mara.
NAMNA ZA KUMUHUDUMIA NG’OMBE.
Kuna namna nyingi sana za kumuhudumia ng’ombe kulingana na aina ya visababishi vya kuvimbewa.
Pia kuna njia nyingi ambazo unaweza tumia kama mfugaji makini.
KWA NJIA ZA ASILI/ KAWAIDA.
- Tumia mkaa (chukua kiasi chochote cha mkaa ponda ponda na changanya kisha mnyeshwe ng’ombe mdomoni kwa kiasi cha lita ) kwa kufanya hivi unaweza msaidia ng’ombe kucheua na kutoa gesi iliyopo tumboni.
- Tumia mafuta ya kula kiasi cha chupa ya soda moja hii pia itasaidida katika kuondoa gesi tumboni.
- Tumia parachichi, kata kata kiasi chochote cha parachichi kisha ponda na changanya na maji kupata uji uji na kisha mnyeshe ng’ombe wake.
NJIA ZA KITAALAMU.
- Njia hii huitaji utaalamu wa hali ya juu nap engine zoezi hili lifanyike na mtaalamu wa mifugo ambaye hataweza kutambua sehemu nzuri ya kuchoma vifaa (trocar and cannula). Na vifaa hivi huchomwa sehemu ya kushoto ya tumbo inayoitwa Paralamba fosa, sehemu hii inahitaji sana utaalamau kuhifahamu.
Njia hii ni ya haraka sana kuondoa gesi ndani ya tumbo.
- Tumia Ipson salt, Hii ni chumvi ambayo ni maalumu katika kuwahudumia ng’ombe ambao hupata shida ya kuvimbewa na njia ya haraka sana, mpatie kwa muda wa saa 24 kiasi cha kijiko kimoja cha chakula (mills 20) kwa lita moja ya maji safi na salama.
MAMBO YA KUZINGATIA KUZUIA TATIZO HILI.
- Epuka kuchunga wanyama wako kuzunguka maeneo yenye nailoni.
- Wape kwa kiasi kinachotakiwa cha pumba.
- Kwa watakao changanya majani ya lusina na pumba hakikisha lusina imekaushwa kwa muda wa siku mbili katika kivuli kuondoa sumu ya Memosine.
Tatizo hili pia linasumbua wanyama kama MBUZI,KONDOO kwa hiyo tuzingatie pia.
NDIGANA BARIDI, UGONJWA HATARI KWA MIFUGO.
Ndigana baridi (Anaplasmosis) ni ugonjwa unaosababishwa na kupe, mbung'o na inzi aina ya Stomoxys kwa mifugo yako hasa ng'ombe, mbuzi na kondoo.
JINSI UGONJWA HUU UNAVYOAMBUKIZWA (Mode of transmission of the disease)
Ugonjwa wa ndigana baridi unaambukizwa kupitia kwenye ng'ombe mgonjwa baada ya kuumwa na kupe, mbung'o au inzi, aina ya ng'ombe, mbuzi au kondoo walio na afya nzuri ili kupata chakula yaani kunyonya damu wakati wananyonya damu pia ng'ombe asiye mgonjwa. Pia kwa njia ya kutumia vifaa vya kitaalamu ambavyo havikuchemshwa sawasawa kama sindano, vijidudu vya ugonjwa husambazwa kutoka mnyama mgonjwa kwenda mnyama mwenye afya kwa kutumia vifaa hivyo.
Hivyo uangalizi mkubwa unatakiwa wakati shughuli hizo za kuchoma sindano, kukata pembe n.k. zinapofanyika.
WANYAMA WANAOPATA UGONJWA WA NDIGANA BARIDI.
- Ng'ombe
- Mbuzi
- Kondoo
Ndama wadogo hawapatwi na ugonjwa huu.
DALILI KUU ZA UGONJWA.
Dalili kuu za ugonjwa huu ni:-
(i) Homa kali (40-41C).
(ii) Kinyesi kigumu sana na chenye utando mweupe juu yake.
(iii) Kupumua/kuhema kwa shida.
(iv) Mnyama kushindwa kucheua.
(v) Rangi ya njano mdomoni, puani na sehemu zilizo wazi za mnyama kama machoni n.k.
(vi) Kukosa hamu ya kula.
(vii) Kupunguza uzalishaji wa maziwa.
(viii) Kutokunywa kwa sababu ya omasum kutofanya kazi (constipation).
MAGONJWA MENGINE YANAYOFANANA NA NDIGANA BARIDI.
-Ndigana kali
-Kuvimbiwa (bloat)
-Kichomi
JINSI YA KUZUIA UGONJWA WA NDIGANA KALI.
-Hakikisha wanyama wako wanaogeshwa vizuri na dawa ya kuua kupe (Acarcides)
-Ogesha kwa kutumia dawa zinazozuia kupe na mbung'o mara 1 kwa wiki mfano Tristix, Tixfix, Ciberdip, Paranex, Alfanex, Steladone, Dominex n.k.
-Chunga mifugo yako katika mbuga zisizo na kupe au mbung'o.
-Ikiwezekana chunga/lisha kwa mzunguko (rotational grazing) katika mbuga zako ili kupunguza kuzaliana kwa kupe.
JINSI YA KUTIBU MNYAMA MWENYE NDIGANA BARIDI
-Watibiwe kwa kutumia dawa ya Oxytetracycline ya sindano 5-10mg/kg ya uzito a
-Wanyama waliofunga choo wanyweshwe mafuta ya kupikia ili kulainisha tumbo
NDIGANA KALI
Dalili zake
i. Homa kali hadi nyuzi joto 42c
ii. Povu kutoka mdomoni na puani
iii. Kuhara choo kilichochanganyikana na kamasi na damu
iv. Tezi kuvimba sana na zenye joto
v. Kuacha kula
vi. Ukungu kwenye macho
vii. Kifo baada ya wiki moja hadi mbili
Tiba
Butalex, Parvexon, tiba iambatane na sindano moja ya kuondoa uvimbe kwenye mapafu kama hali hiyo tayari imeshajitokeza.
Tumia Multivitamin ili kuongeza hamu ya kula na Raxis ili kuondoa maji kwenye mapafu.
Kinga/zuia
Zingatia uogeshaji sahihi na Chanjo ya ECF
NDIGANA MKOJO DAMU (Babesiosis) ugonjwa wa kukojoa damu
Dalili zake
i. Mkojo kuwa na rangi ya damu isiyokolea zambarau ii. Mkojo hutoka kidogo kidogo na kwa muda mrefu
iii. Homa hadi nyuzi joto 40C
iv. Kuacha kula
v. Choo kigumu au kuhara wakati mwingine
vi. Kifo baada ya wiki 1
Tiba
Berenil ikisaidiwa na antibiotics za sindano kama vile oxytetracycline (OTC) pia tumia Multivitamin kuongeza hamu ya kula.
Kinga
Zingatia uogeshaji sahihi
No comments:
Post a Comment