Biriani ya Ng'ombe
Mahitaji
Nyama nusu
Chumvi kiasi
Mafuta 1 Kikombe
Vitunguu maji 3 vikubwa
Nyanya 3 kubwa
Nyanya kopo
Thomu 1 table spoon
Tangawazi 1 table spoon
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 tea spoon
Kotmiri (giligilani) iliyokatwa 2 Vijiko vya chakula
Viazi 6
Uzile wa unga 1table spoon
Mtindi ¼ Kikombe cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA KUPIKA
1. Kwenye karai au (sufuria) mimina mafuta Yakishapata moto mimina vitunguu vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi. Vitowe viweke pembeni.
2. Kaanga viazi na viweke pembeni.
3. Chukua sufuria tia nyama, thomu, tangawizi, pilipili, nyanya, nyanya ya kopo, mtindi. Chemsha mpaka iive.
4. Tia vile vitungu ulioyovikaanga, tia viazi, uzile, kotmiri na yale mafuta uliokaangia vitunguu kama ¼ kikombe, acha moto mdogo mdogo kama ¼ saa, epua weka pembeni.
VIPIMO VYA WALI
Mchele kg 1
Mdalasini mzima wa vijiti
Zafarani ½ kijiko cha chai
Rangi ya biriani ¼ Kijiko cha chai
Mafuta yaliyokaangiwa vitunguu ½ Kikombe
Chumvi kiasi
Zabibu kavu.
Roweka zafarani na rangi kwenye kikombe na ¼ kikombe cha maji. Roweka kabla ya robo saa.
NAMNA YA KUTAYARISHA
1. Osha mchele uroweke kwenye maji muda wa dakika 20.
2. Chemsha maji kwenye sufuria kama magi 10.
3. Tia mdalasini.
4. Yakishachemka unatia mchele,chemsha usiive sana, unamwaga maji.
5. Unamimina tena ule mchele ½ yake kwenye sufuria, unatia rangi na zafrani kidogo na zabibu halafu unamimina mchele uliyobakia unatia rangi iliyobakia.
6. Mafuta yake unayachemsha mpaka yachemke unamimina juu ya mchele, unarudisha motoni unaweka moto mdogo ukisha kuiva, tayari kupakuliwa.
7. Unapakuwa wali unaweka chini kwenye sahani na juu yake rojo ya nyama.
Pishi lako lipo tayari kuliwa.
#Twende_Nalo
No comments:
Post a Comment