Tuesday, 16 October 2018

JINSI YA KUPIKA MKATE WA NGANO ISIOKOBOLEWA (ATTA)

MKATE WA NGANO ISOKOBOLEWA ( ATTA) :

Mahitaji:-

🔸Unga wa ngano isokobolewa(atta) vikombe 3
🔸Hamira vijiko 2 1/4 vya chai
🔸Maji ya vugu vugu kikombe 1  1/4 au zaidi
🔸Maziwa ya unga kijiko 1 cha chakula(sio lazima, yanaleta harufu na radha nzuri)
🔸Chumvi kijiko 1 1/4 cha chai
🔸Asali 1/3 kikombe
🔸Mafuta 1/2 kikombe
🔸Mdalasini wa unga 1/4 kijiko cha chai

NAMNA YA KUPIKA:

1. Tia maji vugu vugu, hamira na sukari katika bakuli , koroga vizuri kisha acha kwa muda wa dk 5 hamira ifure

2. Tia mahitaji yalobaki kisha  katika bakuli kisha changanya vizuri hadi ufanye donge, Kanda donge lako hadi liwe laini. Kama unga mkavu ongeza maji kidogo kidogo

Unga unatakiwa uvutike vizuri usinate ndio utapata mkate mzuri wa kuchambuka

3. Tia unga wako katika bakuli ulopaka mafuta kisha funika acha ufure hadi ujae mara mbili, sukuma na sokota kufanya umbo la mkate(loaf). (Unaweza fanya bhanzi pia kwa kipimo hiki)

4. Tia katika chombo cha mkate ulichopaka mafuta, funika acha ufure hadi ujae vizuri.

5. Oka katika oven ya moto joto 190°C hadi upate rangi na kuiva.

4. Utoe mkate wako katika chombo chake ,tumia kitambaa safi kuepuka kuungua kisha acha mkate upoe kabisa kabla ya kuukata.

5. Mkate tayari kwa kula. Mkate huu ni very healthy na unapendeza zaidi kwa chai ya maziwa au ilochemshwa kwa viungo vizuri.

Kipimo hiki utapata mikate miwili

No comments:

Post a Comment

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO