Ufugaji wa Nguruwe ni kati ya shughuli zinazokuwa haraka katika Afrika Mashariki na ya Kusini. Ukuaji wa miji na ongezeko la watu kumeendana na ongezeko kubwa la mahitaji ya protini ya wanyama. Uwezo wa kukua haraka, ubora wa nyama kiafya na ladha nzuri inatoa nafasi kubwa ya maendeleo ya ufugaji wa nguruwe kama chanzo cha kipato kwa mfugaji. Chakulacom tutakupa mwongozo kuhusu mahitaji muhimu ya ufugaji nguruwe, mbinu za kuboresha uzalishaji, kudhibiti magonjwa na pia mwongozo wa kujali haki za nguruwe kama kiumbe hai kinachoweza kusikia maumivu kisipotendewa kinavyostahili. Nguruwe ana gharama ndogo za matunzo, anatoa mafuta, huleta kipato cha pesa, hutoa mbolea ya mimea. Faida ya ufugaji nguruwe hutegemea zaidi ubora wa matunzo. Vile vile kumbuka kutumia vyanzo nafuu vya chakula na kujengea miudombinu.
Ukweli kuhusu Nguruwe
Nguruwe ni mnyama msafi sana na mwenye akili. Akipewa banda lenye nafasi ya kutosha huweza kuchagua sehemu ya kulala, kujisaidia na akauweka mwili wake katika hali ya usafi sana. Usafi wa banda na mazingira utakuhakikishia nguruwe wasafi bila uchafuzi wa mazingira kama tunavyoona kwa wafugaji wengi mijini na vijijini. Tenga mavazi na viatu maalumu kwa ajili ya kazi za nguruwe na oga vizuri baada ya kufanya kazi kwenye mabanda ya nguruwe kwa muda mrefu.
Nyumba ya nguruwe
Kwa ujumla nyumba za aina mbili huhitajika katika ufugaji wa nguruwe
Nyumba za kukuzia na kunenepesha nguruwe wa kuchinja
Nyumba za nguruwe wazazi
Sifa za msingi za nyumba bora ya nguruwe
• yumba ijengwe eneo lenye kivuli cha kutosha
• yumba iwe na nafasi ya kutosha
• Ijengwe sehemu yenye mwinuko kiasi iii kuwezesha maji kuondoka kwa urahisi
• Iwe na chombo/kihori cha kuweka chakula na kingine chakuweka maji
• Iwe na sakafu imara iliyotengenezwa kwa saruji, mabanzi, miti na isiwe na unyevu
• Sakafu ya saruji iwe na mteremko (slope) inayoweza kuondoa uchafu kwa urahisi ndani ya banda.
• Sakafu ya mabanzi, mbao au miti iwe inatoa nafasi ya kuondoa uchafu kama kinyesi ndani ya banda.
• Iwe na mtaro wa kuondolea maji, mkojo na kinyesi hadi shimo la kutunzia
• Kuta za mabanda ya nguruwe zinatakiwa kuwa imara, ziwe na uwezo wa kuwasitiri nguruwe wasitoke nje.
• Iweze kuingiza hewa ya kutosha ndani ya banda hasa kama ukuta umezibwa (solid walls)
• Paa linaweza kupauliwa vizuri kwa nyasi, makuti, bati n.k
No comments:
Post a Comment