Tuesday, 9 October 2018

JINSI YA KUTENGENEZA VILEJA VYA JAM

VILEJA VYA JAM

Siagi nusu kikombe

Unga Vikombe 2 kasorobo

Yai 1

Vanilla

Sukari kikombe kasorobo

Jam kiasi

NAMNA YA KUFANYA

Saga sukari na siagi mpaka ichanganyike tia yai, vanilla, mwisho malizia na Unga unaweza kuongezea arki unazopenda. Ufanye donge Unga uufunike plastic film uweke kwenye frige kama nusu saa hivi halafu utoe sukuma kwenye kibao kata shape hiyo kama uwa halafu tia katika tray ya mini MUFFINS isukume kwa ndani kidogo kidogo ifanye kishimo halafu tia jam. Choma mpaka uone vinaanza kuwa rangi ya gold toa wacha vipoe halafu vitoe panga kwenye sahani tayari kuliwa. Tahadhari Unga wake unakuwa rahisi kukatika inabidi ufanye kidogo kidogo visivunjike wakati wa kutia kwenye tray. Mmmm Yummy 😋😋

No comments:

Post a Comment

COMMENTS/MAONI AU USHAURI

MATANGAZO