~BIRIANI YA KUKU~
1. Matayarisho ya KUKU
~ Mrowanishe kuku na viungo hivi kwa muda mdogo tu
~ Kuku (Mkate kate Vipande) - 4 LB
~ Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi - 2 Vijiko vya supu
~ Chumvi - kiasi
~ Pilipili nyekundu ya unga - 1 Kijiko cha supu
~ Bizari ya manjano (Haldi au Tumeric) - 1 Kijiko cha chai
~ Bizari ya pilau ya powder (Jeera) - 1 Kijiko cha chai
~ Gilgilani powder (Dania) - 1 Kijiko cha chai
~ Ndimu - 1 Kijiko cha supu
2. Mchele na vitu vya Masala:
~Mchele (Basmati mzuri) (rowanisha) - 7 cups
~Mafuta ya kupikia - kiasi
~Vitunguu Vilivyokatwa - 8
~Nyanya iliyokatwa katwa - 3
~Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi - 1 Kijiko cha supu
~Garam Masala -1 Kijiko cha supu
~Hiliki powder - ½ Kijiko cha chai
~Tomatoe paste - 1 Kijiko cha supu
~Pilipili mbichi zipasue katikati - 4
~Chumvi - kiasi
~Mtindi - 4 Vijiko vya supu
~Kotmiri iliokatwa (Chopped) - ½ Kikombe
~Mafuta ya kunyunyuzia katika wali - 3 Vijiko vya supu
~Zaafarani au rangi ya biriani - kiasi
3. Namna Ya Kutaarisha Na Kupika
~Weka kuku aliyerowanishwa na viungo vyake katika Foil tray au chombo chocote utakachomwagia wali humo humo na kupikia biriani, kisha mchome (Bake) mpaka awive na awe mkavu kiasi.
~Wakati kuku anapikika, kaanga vitunguu katika karai au sufuria mpaka viwe brown na epua nusu yake weka kando.
~Punguza mafuta yabakie kiasi tu, ongeza Thomu na tangawizi, na viungo vyote vya hapo juu isipokuwa Mtindi na kotmiri, endelea kukaanga hadi tomatoe zilainike.
~Ongeza chumvi, malizia mwisho kwa kutia mtindi, kotmiri na vile vitunguu ulivyoweka kando. Masala yako tayari.
~Mwagia masala juu ya kuku uliyekwishmpika changanya vizuri.
~Chemsha Mchele uwive nusu, chuja na mwagia juu ya masala.
~Nyunyiza mafuta kidogo juu ya mchele na zaafarani au rangi ya biriani.
~Bake katika moto wa 350 – 400 kwa muda wa 15 – 20 minutes. Biriyani imekuwa tayari kuliwa.
#Share
#TwendeNalo
No comments:
Post a Comment